maimatha wa jesse, mratibu wa usiku wa maraha uliondaliwa na mwanywele entertainment usiku wa kuamkia leo hoteli ya travertine, dar, akisherehesha katika onesho hilo liliofana sana ambalo lilidhaminiwa na tigo
mzee yusuf mfalme wa jahazi modern taarab akila sebene na wapenzi waliopagawa usiku wa maraha
wapenzi wa kila aina walikuwapo kuka maraha
tigo kama kawaida yao ya kuwafikia walaji wake walikuwepo kutoa huduma
safu ya waimbaji wa jahazi modern taarab ikighani kwa raha zake
hoteli ya travertine usiku kuamkia leo palikuwa hapatoshi wakati magwiji wa taarabu walipotumbuiza katika usiku wa raha

msumari huo....unachoma kote kote..... anaghani mzee yusuf mflame wa kundi la jahazi
mabaunsa ilibidi wafanye kazi ya ziada kudhibiti wapenzi wa taarab waliopagawa kwa maraha hoteli ya travertine, dar, usiku wa kuamkia leo. onesho lilidhaminiwa na tigo

safi sana maana naona watu wanajimwaga kwa raha zao, bora yule mbaya wa kuchukua picha za watu hayupo maana tulikuwa hadi tunaogopa kujimwaga tukienda mahali, safi sana tunapenda maendeleo kama haya na si ujinga na uzushi
ReplyDeleteHivi ni kwa nini waimbaji wa kike wa muziki wa taarab huwa wanakaa kwenye viti?
ReplyDeletePili Kwa nini wanawake wanaoimba Muziki huu huwa wanene?
Sijawahi kuona wananguaji katika muziki wa taarab.
Sina nia mbaya nataka kuelimishwa tu.
mzee yusuph anaposema msumari hasa anamaanisha nini? Na waimbaji wenzie wanaposema msumari unachoma kotekote ndio wanaponichanganya kabisaaa!!? Kwani huwa sielewi kinachoendelea kitu kinachosababisha nishinde `ku-enjoy` muziki wenyewe. Wajaribu kutokutufumba sana ili kutuvutia na sisi ambao bado hatujabobea kwenye aina hii ya muziki
ReplyDelete