Mh. Balozi na Mkuu wa Wilaya ya nanihino,

Nimesisimkwa sana na mdau wa dodoma anavyochangamsha globu ya jamii kwa kutukumbusha mambo mbalimbali ya zamani. mie nami natoa kamchango kango kwenye mada ya kumbukumbu kwa kuuliza wadau kama wanakumbuka novo za james hardley chase ambazo kwa kiwango kikubwa zilikuwa chachandu katika kuleta utamaduni wa kusoma na pia kupata mazoezi mazuri ya kiinglishi.

mie nilianza kusoma 'well now my pretty' nikafuatia na 'one bright summer morning' ambao baada ya hapo nikaja kusoma karibu vyote kama vile 'lay her among the lillies' , 'cade', 'the vulture is a patient bird' n.k. na hadisi zake nakumbuka hadi leo kwa jinsi zilivyokuwa tamu. wadau mnamkumbuka mark garland na yule adui silk?

haya mliosoma vitabu hivyo leteni uhondo hapa... sijui siku hizi vijana wanajisomea nini maana hapa nyumbani nakutaga marundo ya magazeti ya udaku tu. hata sijui kwa nini watu hawasomi siku hizi.
Mdau wa Newala
s

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. DU! Mdau unanikumbusha mbali sana, kwani baba yangu alikuwa mpenzi sana wa novel za James Hardley Chase. nakumbuka wakati huo (80s) nilikuwa mdogo, nilikuwa kiingereza bado sijui, nilipoanza kujua kiingereza nilisoma kama vitatu vinne hivi you you never know with women, Malory, lay her among the lilies, na kingine zikumbuki vizuri title yake..something..shroud

    Mpaka baba yangu alipofariki(1991) alikuwa navyo vitabu 16 vya chase.Ila niliambiwa jamaa alikuwa hatungi mwenyewe, wanatunga wengine wanatumia jina lake, je hiyo ni kweli?????

    UNAKUMBUKA vile vya Fredrick Forsth kama Alternative devil etc. Hivyo niliishia kusoma back cover tu, kwani jamaa kiingereza chake kilikuwa kigumu sana kwangu kwa wakati ule!!

    ASANTE

    ReplyDelete
  2. mmmh umenikumbusha mbali. Knock knock who is there, one bright summer morning, no orchids for miss Blandish, consider yourself dead, the dead stay dumb etc. Enzi hizo akifundisha mwalimu somo halipandi unakuwa na novel yako mapajani unateleza taratibu. Lakini zilisaidia sana ki English.

    ReplyDelete
  3. Du!! Mdau wa Newala, umenikumbusha 'Novo' ya James Hadley Chase kwa jina la 'You Have Yourself A Deal ' niliyoisoma nikiwa majeshi(JKT)mwaka 1983 Operation Safisha kule Itende. Yaani ilikuwa afande akisema tano bora basi mimi mkono unazama kwenye mfuko wa 'kombati' na ukitoa umeshikilia 'novo' na kuendelea 'kuila', nikiwa 'gadi' ndio nilikuwa najiachia kabisa...lakini SIYO ile 'gadi' ya 'AMARE'!!!, 'gadi' ninazosema mimi ni zile za bustani na ya kule chini kwenye mikahawa kuzuia 'raia' wasikatishe njia!! sijui kama bado ipo mpaka leo, ha ha haaa.

    Kwenye kitabu hicho nakumbuka kisa cha mmarekani Mark Girland wa CIA na hasimu wake wa kirusi Malik kutoka KGB walipokutana mitaa ya Paris kule Ufaransa kwenye kisa kilichomhusisha binti 'mblondi' aliyekutwa amezirai akiwa na alama takoni mwake za mwanasayansi wa kichina wa nguvu za atomiki. Kwa kifupi nakumbuka kazi ilikuwa Mark Girland(CIA) anamtaka binti huyo ili baadae akizinduka apamtie siri ya matengenezo ya silaha hizo, Malik(KGB) anamtaka pia kwa sababu hizo hizo, na kwa upande mwingine Wachina nao wanamtafuta binti huyo kwa udi na uvumba ili wamuue kabla hajatoa 'siri'..... yaani ni raha tupo. Vitabu hivyo vilisaidia mtu kuwa na hamu ya kusoma hadithi za kiingereza na hata kuongea; lakini siku hizi mmmh!! kama ulivyosema Mdau wa Newala vijana siku hizi hawasomi vitabu, wanasoma magazeti ya udaku tu kwa kwenda mbele na wale wa mijini wakishasoma wenye vijisenti vyao kidogo ndio wanakwenda kushinda internet cafe!!! Tutafika?

    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. Hehe balozi wa nani hii ilikuwa ni Mark Girland na Malik sio silk walikuwa wakipigiana mikwala kama 'Next time I meet you i will buy you a cup of coffee'. Nakumbuka the Whiff of money, sucker punch, i hold the four aces, gimme a favour drop dead, Hit and run, the world in my pocket, safer dead, an ear to the ground (al barney ' if you get time to eat, eat to the maximum coz you never know when the next meal is to come'), tell it to the birds akina Maddox, steve hamas watalamu wa insurance cases. Police mashuhuri 'Obrien'(he is cop cop all over his body).Mission to seana, mission to venice, the coffin from Hong kong (Fear is the key to open the wallet of the rich) , i would rather stay poor, duh nilisomaga nyingi mno sikumbuki kama kuna niliyoibakiza.

    ReplyDelete
  5. Kweli! Ukisoma moja, lazima utatafuta nyingine. Wakati huo hazipo kabisa mitaani. Unauliza kila mtu. Mimi nilikuwa napata kutoka kwa Padre mmoja pale Mbeya. Sasa hivi vimejaa mikononi mwa chingas pale Dar si mchezo!

    Kweli kiinglish changu kilinolewa sana wakati huo...

    ReplyDelete
  6. "The whiff of money","Come Easy,GO Easy",etc.

    ReplyDelete
  7. Meet Mark Girland,

    Knock Knock Who's There, Well Now My Pretty , Eve, Come Easy Go Easy, This Way For A shroud, Lady Here's Your Wreath. Get A Load of This, What's Better Than Money, You Have Yourself A Deal,Strictly For Cash. Never Trust A Woman,You Never Know With Women, In A Vain Shadow. The Things Men Do, Make The Corpse Walk, The Dead Stay Dumb, Just The Way It Is, Safer Dead, Figure it For Yourself, You're Lonely When You Are Dead. Lady. The Flesh Of The Orchid, No Business Of Mine, Just Another Sucker, Trusted Like The Fox, But A Short Time To Live. Why Pick n Me, The Double Shuffle, Ruthless, There's Always A Price Tag, You Find Him I'll Fix Him, Hit and Run, Shock Treatment, The Guilty Are Afraid. So What Happens To Me, I Would Rather Stay Poor. I Hold The Four Aces, An Ace Up My Sleeve, Three of Spades, The Joker in The Pack, I'll Bury My Dead, Not My Thing, Like A Hole in The Head, Want To Stay Alive?? Goldfish Have No Hiding Place, Just A Matter of Time. The Vulture is A Patient Bird, Believed Violent , An Ear to The Ground. Have This One On Me, Do Me A Favor Drop Dead , You are Dead Without Money.
    You Can Say That Again

    My Laugh Comes Last, Have A Nice Night

    Wasomaji wa hizo novel wataona ni jinsi gani zilinivyonitia uchizi mpaka kutunga story kwa kutumia title,

    Masud

    ReplyDelete
  8. Baada ya kuwa nimesoma novo karibu zote za Chase (Panther and Corgi) alikuja mwalimu wangu mmoja wa hisabati akiitwa Hans Liganger toka Norway na kutuambia kundini kwamba vitabu tunavyosoma (yaani Chase) ni, kwa maneno yake mwenyewe, "simple minded". Kwa umri wangu miaka ya mwisho ya sabini na themanini hapakuwa na novo bora zaidi ya hizo. Leo hii siwezi kukaa chini na kukisoma. Hukaa nikajiuliza yule mwalimu hakuwa anajua mienendo ya umri au ni kweli vitabu vile vilikuwa havina manufaa?

    Mbali ya yote yangu ya mwanzo ilikuwa Like a Hole in the Head ikifuatiwa (kama huyo mdau hapo juu) na One Bright Summer Morning. Mtakaokumbuka zile za kusisimua sana zilipewa majina yasiyosisimua kama vile The Way the Cookie Crumbles, This Way for a Shroud na Cade lakini mabomu yalipewa majina ya kuvutia kama You are Dead Without Money. Characters wakubwa walikuwa Poke Tohora (a Seminole - his formula was that fear is the key which opens the wallets and handbags of the rich...), Vitto Ferrari ambaye akikaa kitini miguu haigusi chini lakini akiua kuliko waliovamia Iraki. Of course nani atamsahau Mark Girland - kiboko ya Warusi na detective Lepsky toka Paradise City.

    Kwa undani na kumbukumbu zaidi wasiliana na rafiki yangu wa miaka hiyo - the Greek George Alexco Karras ambaye aliweza kusimulia mstari kwa mstari wa kila novo aloisoma - na, niamini, alizisoma zote. His sister Maria was just so cute with blue eyes.

    ReplyDelete
  9. Got this phrase from one of the chase baook 'when a man loves a woman nothing stands on his way..."
    or this one, got match on you buddy...

    ReplyDelete
  10. Hizo novo zilikuwa poa nakumbuka unamaliza unatafuta nyingine...kwa kuongezea tu..Mission to Sienna, mission to Venice..

    ReplyDelete
  11. AISEE WE ACHA TU MIMI NILIYESOMA JUZI JUZI 1991 NIKIWA FORM THREE NOVEL ZA CHASE ZILINISAIDIA SANA KUJIBU BARUA ZA MA BINTI WA KIFUNGILO KIINGEREZA CHAO KILISABABISHA WENGI TUJIFUNZE KI-ENGLISH KWA NGUVU LA SIVYO UTAISHIA KUSALIMIA TU!

    ReplyDelete
  12. Yeah ni mojawapo ya watunzi wa novel ambazo kwa kusema ukweli inaweza kumchukua msomaji kimawazo mpaka eneo la tukio analosoma, mara kwa mara miji ya vienna, paris, monaco, rome, geneva, newyork london huwa haikosi, kwa kweli James hardley Chase ametusaidia wengi kukuza ktk lugha ya wakoloni, Unakumbuka "No Orchid for Miss blandish" (mambo ya Magrison Gang), "I could rather stay poor", "you've got it coming", "The tortoise","An ace up on my sleeve", "I hold four aces", "Have a good night" na vingine vingi

    ReplyDelete
  13. Kwa taarifa ni kwamba James Hadley Chase japo alianza kama mwandishi hakuandika novo nyingi. Jina hilo lilikuja likawa ni brand tu ikitumiwa na waandishi walokiandika theme za crime/fiction baada ya mafanikio yake ya mwanzo huku yeye akiendelea kukatiwa chake. Wachapishaji wa Corgi na Panther ndo walionunua haki miliki ya jina.

    ReplyDelete
  14. Jamani nilikuwa nikishika novel ya chase naimaliza kwa siku moja tu, marafiki zangu wote walikuwa wanasoma "mills and boon", wakawa wananiambia ati nasoma novel za kiume, doubdle shuffle was my best, yule dada walisema alikuwa anapaka perfume ya "Joy", huwezi amini nimeitafuta sana hiyo perfume lakini sijaipata kwa jinsi ilivyosifiwa ktk hiyo novel, wangemtaja designer wake labda ningeipata..Anyway, Baada ya kuvisoma almost vyote na nilipoingia form 4 nikaanza kusoma vya Sidney Sheldon, nimevisoma navyo vyote, yaani kwa aliyekuwa anapenda Chase lazima ataenjoy Sydney Sheldon(RIP)
    Basi wale marafiki zangu waliokuwa wanasoma mills and boon wao wakahamia kwa "Danielle Steel"..hahahahah. mmenikumbusha mbali sana

    ReplyDelete
  15. Do you want to stay alive!

    ndio ninayo kumbuka

    na nakumbuka hii phrase

    poketoholo was a seminolo indian
    his invented a formula that fear is the key that unlock the pockets and the wallets of rich man

    but chuck a cop killer at eighteen didnt work to the fomula.....

    captain terell lumbered in....

    hiyo ilikuwa imeandikwa kwa nyuma ya novel
    huo ni mwaka 82...

    nilizisoma kama 56...
    nikandika summary zake

    good topic, good memory

    uzee noma

    masawe

    ReplyDelete
  16. James Hadley Chase ilikuwa ni "pen name" yake na alikuwa Mwingereza ingawa vitabu vyake vingi alivitunga kwa taswira za kimarekani. Kwa kweli kwa wakati huo wengi tulipokuwa sekondari miaka ya 70 na 80 ilikuwa ni must kusoma vitabu vyake. Vilikuwa ni "fast reading" na "simple minded" kama alivyosema mdau Al Musoma. Kwa upande wangu mbali na kumsoma Chase sana nilikuwa mpenzi sana wa vitabu vya Alistair Maclean ambaye vitabu vyake vingi vimechezwa sinema. Wadau mnakumbuka Where Eagles Dare, Ice Station Zebra, The Guns of Navarone n.k.

    ReplyDelete
  17. SIII MCHEZO,,,teh teh teh
    yan ulikua ugomvi home maana nikishika novo izo hakuna ata kutoka nje,kazi sifanyi wala nini!!yan waenda chooni mkuku urudi kusoma siku zima uko room wasoma,,
    bible ilikua haioni ndani yan,,,yan mama alikua nawaka ile mbaya kazi haziendi,no kusoma ila kiingereza kilipanda saaaana tu.duh siku nyingi sana now uwezo umepotea
    UGONJWA KABISA NOVO YAN UNAKUA OBSESSED COMPLETELY

    ReplyDelete
  18. Nikiwa darasa la saba 1985, nilisoma "Well Now, My Pretty ", Sikuwa naelewa hadithi kikamilifu, lakini nilisoma hadi kurasa ya mwisho bila kukata tamaa. Nikiwa kidato cha kwanza nilikisoma tena chote na kukifurahia mno. Kuanzia hapo mpaka jeshini, nadhani nimesoma Chase zaidi ya sitini, hivi navikumbuka; Lady Here's Your Wreath, He Won't Need It Now, The Dead Stay Dumb,Get A Load Of This,No Orchids For Miss Blandish,Just The Way It Is,Eve,I'll Get You For This,The Flesh Of The Orchid,Trusted Like The Fox,You're Lonely When You're Dead,The Paw In The Bottle,You Never Know With Women,Figure It Out For Yourself,Why Pick On Me,Strictly For Cash,But A Short Time To Live,In A Vain Shadow,The Double Shuffle, The Wary Transgressor,The Fast Buck,I'll Bury My Dead, The Things Men Do, This Way For A Shroud, Mission To Venice, Safer Dead, The Sucker Punch,Tiger By The Tail,You've Got It Coming, Mission To Siena,There's Always A Price Tag, You Find Him, I'll Fix Him, The Guilty Are Afraid,Not Safe To Be Free, Hit And Run, The World In My Pocket,Come Easy, Go Easy,What's Better Than Money, A Lotus For Miss Quon, Just Another Sucker, I Would Rather Stay Poor, A Coffin From Hong Kong,One Bright Summer Morning,The Way the Cookie Crumbles, This Is For Real, You Have Yourself A Deal,Cade,Well Now, My Pretty,Have This One On Me,Believed Violent,The Whiff Of Money, The Vulture Is A Patient Bird,There's A Hippie On The Highway,Like A Hole In The Head,An Ace Up My Sleeve,Just A Matter Of Time, You're Dead Without Money,Have A Change Of Scene, Knock, Knock! Who's There, So What Happens To Me,The Joker In The Pack,Believe This, You'll Believe Anything, Do Me A Favour, Drop Dead,I Hold The Four Aces, My Laugh Comes Last,Consider Yourself Dead,You Must Be Kidding,Hit Them Where It Hurts.

    Karibu kwa kila novel yake jamaa anajaribu kupata pesa kubwa kwa kufanya uhalifu, halafu mambo yanaenda kombo. Kwa kifupi vitabu vyake karibu vyote vilikuwa "unputdownable":-)

    ReplyDelete
  19. WooWoo wooo,sasa noma tunakumbushana enzi za 19makuti chase ndiye aliyenifanya nipasi kiingereza skuli,nimeviona hapo vingi vimetajwa,lakini I WILL BURY MY DEAD SIKIONI.

    RAS TAU

    ReplyDelete
  20. wadau msisahau marehemu mario puzzo, novel kama The corsican, the Sisily, Godfather nk. that was real life yaani kama huna tittle za kutosha kichwani kijiweni hapakaliki.

    ReplyDelete
  21. Ama kweli ya kale dhahabu! hebu kumbuka mstari huu 'women are wonderful animals that you never know with them'ndani ya you never know with women. Nilizisoma chache si haba maan upatikanaji wake ililkuwa kwa manati sana. Ila anon wa Nov 14 4:22 umenikuna sana na mambo ya sydeney sheldon, nilibahatika kusoma kitabu chake kimoja kinaitwa Master of the game nilisuuzika roho sana kwa kweli mambo ya Eve na pacha wake Alexandra, na picha aliyochezewa Eve na bwana wake Dr keith Webster, Tony blackwell na uchoraji wake bila kumsahau mkuu wa mipango Cathe blackwell,aah niseme nini ? Kama unajua mahali naweza kupata kitabu hicho kwa sasa tafadhali nijulishe kupia uwanja huu au mail kabelemtuta@hotmail.com Natanguliza shukurani za dhati.

    ReplyDelete
  22. ukivitaka online ktk pdf/rtf format ingia http://search.4shared.com/q/70/james%20hadley%20chase

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...