JK akimsabahi mtoto mwenye umri wa miaka minne Catherine Paul aliyelazwa katika taasisi ya MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo mapema wiki hii.Rais Kikwete alikwenda hospitalini hapo kupokea vifaa vya upasuaji mishipa na Ubongo vilivyo tolewa msaada na Kampuni ya Synthes Spine yenye makao yake makuu nchini Uswisi, kupitia hospitali ya Chuo Kikuu cha Weill Cornell kilichopo New York nchini Marekani.Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Daktari Bingwa wa Uapsuaji Mishipa na Ubongo Dr.Roger Hartl.
Dr.Roger Hartl(kushoto) ambaye ni Daktari Bingwa wa upasuaji Mishipa na Ubongo kutoka Hospitali ya chuo Kikuu cha Weill Cornell nchini Marekani akikabidhi kwa JK baadhi ya vifaa vya upasuaji ubongo na Mishipa leo katika taasisi ya MOI iliyopo katika hospitali ya taifa Muhimbili.Kulia niMkurugenzi mtendaji wa MOI Profesa Lawrence Museru.Vifaa hivyo vimetolewa kama msaada na kampuni ya Synthes Spine yenye makao yake nchini Uswisi na kuletwa Muhumbili kupitia cho kikuu cha Weill Cornell kilichopo New York,Nchini Marekani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. JK hili zengwe la walimu limekaa vibaya mwanangu wiki ijayo. Hebu Mkuu wape chao wanyamaze. Hata ukipunguza zile za EPA zinazorudishwa poa, au unasemaje mtu wangu?

    ReplyDelete
  2. Mpendwa JK,
    Nakuarifu kuwa nchi yetu hadi sasa haina mashine ya MRI hata hapo kwenye hospitali kuu ya rufaa Muhimbili. Hivi tatizo ni nini? Watu waendelee kuteseka kufuata kipimo hicho Nairobi hadi lini? Je, wale wasio na uwezo si ndio serikali imesha -sign death certificate yao? Jamani, mambo ya afya tuyape kipaumbele kuliko marupurupu na mashangingi ya wabunge! Naamini ujumbe huu utakufikia! We need the MRI machine ASAP! Ni aibu kwa nchi yenye wabunge wanaotembelea ma VX na ma LEXUS!

    ReplyDelete
  3. weill cornell??????????????????????
    Muhimbili-MOI????VIFAA VYA UTABIBU???
    SIAMINI ATA KIDOGO,,,duh awa jamaa siwawezi hahahaaaaaaaaaaaa
    wanablogu hii kali ya w.cornell

    ReplyDelete
  4. MRI inapatika Agha Khan Hospital. Japokuwa nakkunga mkono kwamba MNH inahitaji kuwa na hiyo mashine.

    ReplyDelete
  5. Tanzania kwa misaada hatujambo. hela walizorudisha za epa zingenunua vitu kibao bila masharti. Misaada haiji bure jamani

    ReplyDelete
  6. Haya mliokuwa mnakejeli safari za Rais nje ya nchi. Haya ndiyo matunda yenyewe. Acheni hizo aagh!!

    ReplyDelete
  7. hongera sana muheshimiwa raisi na wote walio fanikisha kupatikana kwa mashine hiyo,polepole ndio mwendo tutafika tu,matatizo yako mengi na serikali makini aiwezi kukurupuka ita yapangua moja baada ya lingine tusiwe na mawazo kama ya simba kocha akija jumatano jumamosi manazi wa simba wanataka icheze kama Arsenal.

    ReplyDelete
  8. Hongera JK!! kwanza nilipoona lile vazi juu ya mwili wake nikafikiria JK kavamia fani ya watu!!! (dRU)

    ReplyDelete
  9. ınapatıkana agakhan alokuwa hana uwezo wa kwenda aghakahan afe?

    jk naomba ulıpe kipao mbele hili suala la afya kama alivyosema mdau wa 4:58pm.

    MRI ni kifaa muhimu ktk kila hospitali ya rufaa

    ReplyDelete
  10. HİVYO VİFAA VİTATUMİKA WAPİ?MBONA KAMA NMESİKİA HAKUNA BRANCH YA BRAİN SURGERY BONGO?

    AU NDO İTAANZİSHWA?

    ReplyDelete
  11. Annon mmoja apo juu anasifia safari za JK majuu kwamba ndizo zinaleta hizi mashine za MOI.... Hivi waTZ tutakuwa mbumbumbu mpaka lini? Tujiulize; kwa nchi kama Malaysia, je Rais wao alifanya u-vasco da gama kwa saaaana ndipo nchi yao ikaendelea? Tufungukeni macho waTZ.

    ReplyDelete
  12. we michuzi umeibania comment yangu unamuogopa sana jk unaogopa kufungiwa hii blog nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...