JK akitoka nje ya ukumbi baada ya kushiriki katika mkutano wa pili wa tume ya afrika jijini addis ababa, ethiopia. kulia kwake ni naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa dk. asha-rose migiro na shoto kwake ni mfanyabiashara mo ibrahim, mwanzilishi wa celtel ambayo sasa ni zain.
angalia video ya JK alipoongea baada ya mkutano huo kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Jakaya tunakuomba uumalize mgogoro wa Zimbabwe,
    Sisi ndio tuliowapa hifadhi, mafunzo na uongozi wakati wa Uhuru na hivyo tusikae kimya pale tunapoona Mzee amepotea njia.
    Tanzania ndio yenye mamlaka ya kweli kati na kusini mwa Afrika hivyo ni wakati wewe uchukue jukumu la kushughulikia tatizo hili.
    Tumeshaona kuwa Afrika ya kusini hawawezi hivyo fanya kitanzania.
    Mzawa

    ReplyDelete
  2. Wadau,

    Hivi Mo Ibrahim ni mfanyabiashara, muhujumu au tapeli? Kwa sababu kampuni yake ya CELTEL ambayo sasa hivi ni Zain waliihujumu au waliitapeli Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL). Hujuma na utapeli ule hakuufanya pekee yake bali kwa kushirikiana na Watanzania wenye dhamana kubwa kubwa kwenye jamii ya Watanzania.

    Michuzi anamuita Mo Ibrahim mfanyabiashara lakini ukimtafuta Ndugu Mapunda aliyekuwa mkurugenzi wa TTCL nadhani atakuambia vinginevyo.

    Siku itakapobainika kama ni kweli CELTEL waliihujumu au kuitapeli TTCL naomba viongozi wa Afrika waiharamishe na kuigomea tuzo yake.

    ReplyDelete
  3. "Ngoja nishughulikie matatizo ya Afrika huku nitaonekana zaidi achana nao wabongo na bongo yao ....!!!!"


    Tehe tehe tehe tehe tehe tehe

    Kwani bila wabongo kukuchagua uwe Rais wao hao wengine wangekuonaje...

    tehe tehe tehe

    Solve matatizo ya nymbani kwako kwanza ...mtoto wako anaumwa unaenda kushughulikia watoto wa wengine

    Mambo mengine unaweza ukadelegate tu kakaaa

    ReplyDelete
  4. JK,,juzi ulikua uku,mara moro mara naskia tena arusha,,,
    aisee nyie watu wa protokali mtamzeesha kijana wetu,afu atachoka ashindwe waza jinsi ya kumkomboa m-Tz
    aisee,,,
    pole JK majukumu meeengi sana kijana wetu my presidaa
    natamani siku tuonane sura-sura japo nikushike mkono

    ReplyDelete
  5. Huyu Mo Ibrahim amechuma na kuwa bilionea kwa kutumia jasho na damu yetu sisi waafrika. Tulitegemea angerudisha fadhila kwa kutujengea shule, hospitali, barabara nk. Badala yake anatoa dola mil.5(zaidi ya sh.bilioni 5) kuwazawadia viongozi wa Afrika kwa 'utawala bora', hivi ni kiongozi gani wa Afrika yuko msafi kiasi hicho, tunajua viongozi wengi wa kiafrika wanavyojilimbikizia mabilioni kabla hawajastaafu. Hivi inastahili kweli kumpa raisi mstaafu wa Afrika anayepata pensheni ya sh. milioni 20 kwa mwezi(mfano Tz)kiasi hicho cha pesa! Mi nadhani angefikiria jinsi ya kutumia hizo pesa vizuri kwa africa. Ya celtel siyajui

    ReplyDelete
  6. Kwanza nahisi kitanda cha Rais Ikulu kina upupu maana huyu mheshimiwa halali kama hayupo mikoani anahaha nje au hiyo miguu ya kuku aliyokula kwa Mr Kipanya inamsumbua??!!
    Poterea mbali lakini yapo matatizo makubwa matatu ambayo yanatuhusu sisi watanzania na ambayo Bwana JMK anawajibu wa kuyashughulikia.

    1. Zimbabwe Sisi ndio tuliowapa jeki la kutosha wakapata uhuru na tunajua kabisa viongozi wote kusini mwa Afrika ukiondoa Bostwana na marehemu wa Zambia wanamgwaya Jogoo kongwe la Zimbabwe. Ila sisi tofauti wajeshi wote wakubwa wa zimbabwe tumewafundisha hapo Mtwara na JMK anawafahamu fika. Pili ni watu wa kulinda haki za binadamu hivyo hatuwezi kukaa kimya wakati Jogoo ameamua kuwa kaburu.
    Mwalimu alishasema "Kaburu ni Kaburu tu, hana rangi".
    Hivyo inabidi tutamke msimamo wetu kuhusu zimbabwe wazi na si kujificha nyuma ya SADC.
    Tena JMK ndio kinara wa Africa sasa hivi lakini kimyaaaaa yaani ananitia wasiwasi.

    2. DRC au Congo hili sasa linatuhusu kabisa maana Congo kibiashara ni muhimu sana kwetu na hivyo utulivu kule ni jambo linalotuhusu moja kwa moja wazungu wanasema (Strategic Importantance) linagusa Maslahi ya Taifa.
    Nasema hivi kwa sababu Utulivu wa Kongo unaweza kutufanya mauzo yetu ya nje yakaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50% ukitaka kujua ukweli wa hili fuatilia kipindi kile cha mwaka mmoja ambapo Laurent Kabila alikamata madaraka.
    Haiwezekani sisi tuzubae wakati Kenya, Angola wanachangamka wakati Kijana mwenyewe tumemsomesha hapo jitegemee na bado ana nyumba Mbezi beach!
    Na ili tuweze kufaidika na hili tuache mchezo au tuache KUSHOOIYA(sijui tafsiri ya hili neno muulize mchagga aliyekaribu nawe) na Reli ya kati. Reli hii ni muhimu sana kwa ajili ya nchi zote hizi Kongo, Rwanda, Burundi na Uganda. Na pia kesho ikitokea vita tutafikishaje vijana mpakani??? Tutawapitishia Nairobi???!!
    Hivyo tuwe mstari wa mbele kuhakikisha hizi nchi zinakuwa tulivu na tujiweke tayari basi kufaidika kiuchumi na sio kuchekacheka ovyo huku tukiomba misaada.

    3. Ni Zanzibar: hili Bomu la muda (Timebomb!) Tuache mchezo na tuache kuuahirisha tatizo. Bwana BWM aliahidi kulimaliza katika kipindi chake lakini wala hakujaribu. JMK nae hivyo hivyo lakini ilipofika wakati akagwaya. Si siri Zanzibar kuna mpasuko mkubwa kati ya unguja na Pemba na karibu nusu ya wapemba wako bara sasa tukiendelea kufunika chungu ipo siku kitalipuka.
    Inabidi kulivalia njuga hili swala wakalishwe chini Wazanzibari waweze kuongea hadi wakubaliane. Iwapo watu wa Ireland kaskazini wamefanya hivyo sioni kwa nini hawa washindwe. Wakalishwe chini waamue hatima yao na baada ya hapo wakeshakubaliana ndio tukae nao tukubaliane muungano wetu uweje. Hii kujifanya hamna tatizo ni kujindangaya maana wanaowekeza Tanzania wanalijua na huliweka katika kile kinachoitwa "Political Risk"

    Sasa wakati mheshimiwa JMK anazunguka huku na huko aelewe maslahi ya nchi yake yako wapi na asiyakimbie matatizo ayaface head on(kifua mbele). .... kwani yeye si mwanajeshi???? au??
    haya mimi nimetoa mawazo yangu.
    Wenu

    Mungu Ibariki Tanzania, Mungu iokoe Tanzania.
    Mzawa

    ReplyDelete
  7. Zimbabwe siyo Ngazija (Comoro). Kajaribuni kuingia muone joto aliyoonja Msumbiji chini ya Selous Scouts. Zimbabwe shughuli bado pevu. Kinachomsibu (suala la ardhi) Zimbabwe kinasubiriwa South Africa, Namibia na Kenya.

    Kwa upande wa Zimbabwe Watanzania tunawajibika moja kwa moja kwa sababu tulikuwa ndiyo vinara wa nchi zilizo Mstari wa Mbele wa Ukombozi Kusini mwa Afrika. Hivyo tulikuwa washauri wa ZANU na ZAPU-PF wakati wa mazungumzo ya Lancaster. Pamoja na yale ya kikao cha Nchi za Jumuiya ya Madola kilichofanyika Ndola, Zambia. Brigedia Hashim Mbita alikuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ndugu John Malecela alikuwa kwenye kundi la Seven Eminent Persons ambao pamoja na mambo mengine walifacilitate suala la uhuru wa Zimbabwe.

    Hivyo basi jitihada za Rais Kikwete zirejee historia ya husika ya nchi yetu kwenye suala zima Zimbabwe. Halafu Waziri wetu wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa apewe darasa kidogo zaidi juu ya suala hili ili kwamba aepukane na kauli zisizoshabihiana na historia ya husika yetu na hali ya sasa ya Zimbabwe.

    Tusikurupuke ili tusije kukupurushwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...