Brother Michuzi kwanza nikupe pole Mbili (2) moja ya kazi nzito unayoifanya ya huduma kwa jamii kupitia blog yako na POLE YA PILI NI KWA BWAWA LA MAINI KUKAUSHWA KWA MARA YA TENA NA SPURS JAMANI YULE NI REDD K SIO RAMOS BENITEZ ANAENDA TUUU HEAD HEAD..BWAWA LITAKAUKA KWELI!!!
ISSUE YANGU LEO NI TATIZO LA PARKING DAR NALOTAKA KUPATA MAWAZO YA WADAU NA IKIWEZEKANA NIFANYIE KAZI MAWAZO YAO. WAKATI KWA SASA DAR KUWA NA GARI LAKO BINAFSI SIO STAREHE TENA BALI NI NECESSITY LAKINI ON TOP OF FOLENI ZA BARABARANI KUNA JIKERO MOJA KUBWA LA PARKING MAENEO YA POSTA.
LAST TIME NILIZUNGUKA NA GARI ALMOST 35 MINUTES KABLA SIJAPATA PA KUIPACHIKA. MAENEO YA PARKING YANAYOKIDHI IDADI YA MAGARI YAINGIAYO KATIKATI YA JIJI NI HAKUNA KABISA. HATA HIVYO KERO YANGU KUBWA IMEKUWA HAO WAHUNI WA CITY (MGAMBO) WANAOFUNGA FUNGA MAGARI NA FAINI YAKE NI 65,000/=.
HILI LINANIKERA MNO KWA SABABU CITY INAFANYA KAZI KIWENDAWAZIMU.
HUWEZI HATA SIKU MOJA HUJATENGENEZA MIUNDOMBINU YA KUTOSHA KUKIDHI HAJA UKAINSTITUTE FAINI KUBWA KIASI HICHO. CITY HAIJATENGA MAENEO YA KUTOSHA YA PARKING MJINI ILI IFIKE HATUA MTU AKIPAKI SEHEMU FULANI IONEKANE NI MKOROFI LAKINI WALE SCARVENGERS WAKIKUTA GARI TU WANAFUNGA NA INAKUWA MBINDE KULICHOMOA CHUMA LAZIMA ZIKUTOKE.
LAKINI CHA KUSHANGAZA NA HAPA NILISHANGAZWA PALE AKIBA MBELE YA JENGO LA NSSF.
PALE KUNA PARKING BAY FULANI..OFCOURSE YA KITUO CHA MABASI LAKINI HAKUNA ALAMA INAYOONYESHA NI CHA MABASI BALI MTU ANAYEEFUATA ALAMA ATAJUA ANARUHUSIWA KUPAKI.
NILIWAHI KUPAKI BAADA YA KUKUTA MAGARI KAMA MATATU LAKINI NILIPOKUJA NIKAKUTA LANGU LIMEPIGWA PINI MENGINE YAKO HURU. KUULIZA ETI KUNA MTU KWENYE GARI NA MENGINE ETI NI YA WATU WA OFISI ZA HAPA WANAOJULIKANA. NIKAJIULIZA NI SHERIA YA WAPI YA KUBAGUA HIVYO??
PILI ETI KUKIWA NA MTU KWENYE GARI HAWAFUNGI!!!! SIELEWI LOGIC HAPA MANA YULE MTU ANAWEZA KUWA NI DEREVA NDO OFISI YAKE ILE GARI LIKASHINDA KUTWA NZIMA ...WEWE UKAEGESHA KUNUNUA VOCHA UONDOKE UKAKUTA CHUMA TAIRINI!
NAIROBI KUNA TATIZO PIA LAKINI ATLEAST WANA VIWANJA VIKUBWA KAMA JIMKANA FULANI WATU WANAPARK MAGARI. DAR CITY HAIJAONYESHA JUHUDI HATA MOJA INAKUJA NA FAINI KAMAMBE KAMA HIYO NA ADMINISTRATION YA FAINI YENYEWE NI YA KIBABE ISIYO TUMIA BUSARA HATA TONE.
MI NAWALIA TIMING KWA SABABU NINA UHAKIKA KWA HAKI INAYOTLOLEWA KATIKA MAHAKAMA ZETU SIKU HIZI LAZIMA CITY WATAKUJA KUNITAJIRISHA KWA KUTOTUMIA AKILI ZAO HASA HILI LA KUFUNGA GARI FULANI MENGINE HUFUNGI MANA KAMA ENEO SIO PARKING YA GARI NI SIYO PARKING YA GARI...THATS IT!
LAKINI PIA UKIMUULIZA HUYO MWANADAMU WANAYEMWITA MWANASHERIA WA JIJI ANAYESAIGN FAINI DAR KUNA MAGARI MANGAPI NA CITY IMETENGA PARKING SLOTS NGAPI HAJUI ANACHOJUA KUVAA KOTI JEUSI...WEZI TUU!!
MI NADHANI MKUU WA WILAYA UNA NAFASI YA KUWAELIMISHA HAWA JAMAA MANA WATU TUNAWAHI TUJE KUVINJARI BLOG YA JAMII KABLA MCHAKAMCHAKA WA KAZI HUJAANZA MARA MUDA WOTE UNAISHIA KUZUNGUKA KUTAFUTA PA KUEGESHA BAJAJ ZETU..NCHI ITAENDELEA KWELI WITH ALL THIS TIME LOST ON ROADS, SEARCHING FOR PARKING ETC??
NAWAKILISHA NA IKIKUPENDEZA IRUSHE KWA WADAU
MDAU WA EMIRATES
“THE HOME OF PARFECT FOOTBALLING”
E MAIL KAPUNI KAMA KAWAIDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. TUNAPOTEZA PESA NYINGI KWA KUTANGAZA UTARII,TUNASHINDWA KUELEWA KUA VITU KAMA VIVYO (PARK) UCHANGIA SANA KUTOKUKUZA BIASHARA.

    ReplyDelete
  2. MDAU WA EMIRATES HAYA MAMBO NDIO YANAYOFANYA NCHI ISIENDELEE KWA SABABU MIUNDOMBINU MIBOVU/HAKUNA KABISA, HIYO FAINI UNAYOLIPISHWA WANAKULA MAFARA FULANI WASIOTOSHEKA WAMEANZA KULA TANGU ENZI ZA TAA(TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION) MPAKA LEO. YAANI WANARITHISHANA BABA MTOTO MPAKA VITUKUU, NINA MAANA HUYU KIKONGWE ANAITWA KINGUNGE NGOMBALIMWILU NA UKOO WAKE WANARITHISHANA WIZI TU KUIBIA NCHI NA WANANCHI. KWA UFUPI HUYU BWANA NI KIKONGWE WA MAFISADI, LAKINI JK HATOTHUBUTU KUMGUSA KWANI NAE NI GODFATHERS WAKE. BONGO NDIO HIVYO TENA MZEE AKIWA NDANI YA MFUMO BASI DOGO KULA PANDE NI MAMBO YA KAWAIDA.
    MDAU WA DARAJANI.

    ReplyDelete
  3. Kwa heshima na taadhima nami naunga mkono mada hii, inabidi Jiji litafute sehemu za kutosha za maegesho, sio kukimbilia kukamata magari ya watu bila kuwa na njia mbadala ya kutatua tatizo. Watanzania tumechoka kuburuzwa, tengenezeni mazingira mazuri ndio mjue kudai faini na fedha za maegesho.

    ReplyDelete
  4. Hakika mdau umenifikisha mahali ambapo nina hasira napo.Mimi nilipaki gari kariakoo anbapo kulikuwa na magari kama manne yamepaki,ile kuteremka kwenda dukani kununua simu ilichukua kama dk 5 hivi nikakuta gari langu limewekewa machuma,magari niliyoyakuta yalikuwepo kama kawaida hayana machuma,kufuatilia kutokana na notice yao wakanidaka nisiende kulipa hiyo 65,000/ bali nitoe 45,000/=,tuliyumbishana sana.Nikatonywa city inapata hela kidogo sana kutokana na hiyo sheria yao,bali hela zote zinaishia kwa wanasheria na mgambo wao.Wanakuanbia ukienda kulipia ofisini 65,000/=,au 45,000/= ya mlangoni,chagua moja.
    Issue ni hivi hakuna sehemu yenye vibao specific vya kuonyesha parking na sehemu ya kutoparking.Nikatonywa tena hayo magari ni janja wayotumia ili mtu uingie mkenge ujue ni sehemu ya parking.halafu wanawalinda hao madereva.Kwa kweli bongo inachosha sana..,Njaa za watu zimezidi.MDAU SAJ.

    ReplyDelete
  5. WIZI MTUPU!!

    ReplyDelete
  6. Mkuu wa nanihii,pole na mihanjo ya hapa na pale.
    hili suala la parking linakera sana tena sana.
    jiji hawajawa na plan yoyote kuhusu tatizo hili,na mbaya zaidi hata hivyo vibaza wanavyosema ndo parking tupark na kuvilipia hela haiendi jiji ana kula mtu binafsi wao wameishia kuwatuma vijana(migambo)wao kujazifunga gari za watu na kuwatoza hiyo faini ambayo hatuoni inafanyiwa nini..!!

    Wale mgambo wanaofunga magari hayo huwa hawana ustaarabu hata kidogo.
    nimewahi kushuhudia mama mmoja kapaki gari na hapo alipokua kunajua alishindwa kukaa ndani akawa nje ya gari amejibanza katika kivuli huku akilinda gari lake,walipolifikia hawakuuliza mmiliki/dereva yuko wapi,walilifunga huku mama akijieleza nipo hapa,wala hawakumsikiliza.na mbaya zaidi wanamwambia nenda ukalipie ndio watalifungua gari.

    hii itatufanya tuanze kutembea na za kukatia vyuma,pale wakifunga gari lako kisa hujakuwepo ndani yake na lajirani yako halijafungwa,basi unaikata cheni nakuondoka na chumalote.

    Mdau wa Gunners, aka KISODA.

    ReplyDelete
  7. WIZI MTUPU HUU,WIZI KABISA
    YANI HII NI KESI KUBWA NA UKIUKWAJI WA TARATIBU KBS KTK JIJI LA DAR LENYE MATAPELI NA WATU WA KUPENDA FWEZA ZA SHORT-KAT.
    NAKIA NI MRADI WA MTU!! teh teh teh
    yan wee utamlipishaje mtu eti kapaki pasipo ilhali no parking lots??ilo jiji wamejenga lini izo?yan kampuni nk ndo wamenunua places zao private wapaki.
    siku tutafikishana tu mahakamani

    ReplyDelete
  8. Mdau nimefurahi sana kwamba tuko wengi tunaochukia huu uovu wa yale ma landrover ya JIJI. Hakuna kitu wanafanya lakini wanataka sisi tuwajibike. Na kwanza hizo pesa huwa wanazipeleka wapi????

    Kaka Gee, AR.

    ReplyDelete
  9. Naungana na wewe ndugu yangu. Na mimi nitakusaidia kwa kumtafuta Mkuu wa Wilaya Mhe. Ndugu Tsere ili alifuatilie suala hili. Ninavyomfahamu ni miongoni mwa serious DCs tulion nao nchini. Nina hakika suala hili atalivalia njumu haaswa.

    ReplyDelete
  10. Hapa kinachohitajika ni kusambaza huduma nje ya mji maeneo kama ya KITUNDA,MAJIMATITU,BOKO,MAKABE NK.Huko ziwekwe branch za mabank,maduka makubwa,office za kukodisha nk.itapunguza mrundikano wa watu wote kupata huduma sehemu moja,kwa Dar es salaam watu wanatoka waliko na kufuata huduma sehemu moja jambo ambalo nazani hata akija meja wa jiji la LONDONI mji utamshinda.

    ReplyDelete
  11. Wizi mtupu.Hao mgammbo wa jiji yaani wanakera kuliko maelezo.Car park hakuna bado wanapiga pigu tairi!Wizi mtupu.
    Hela za E.P.A zijenge car park

    ReplyDelete
  12. Viongozi wetu wa majiji, halmashauri za miji na hata serikali wanaongozana kwenda nje ya tanzania kujifunza, lakini kwa bahati mbaya sana akuna "changes". Parking fees ziko kila mahali lakini kabla ya "institute" hilo lazima ujenge mazingira ya kufanya watu kutoendesha magari kwenda mjini n.k. Sasa, ukiangalia DAR, hakuna reliable public transport ya kumfanya mtu kutumia badala ya kuendesha gari lake. Mradi huo wa mabasi uje haraka na waone kama watu watakuwa tayari kuendelea kutoa faini hizo ambazo kwa mawazo yangu zingelikuwa basi,zinatumika hata kufanya mabadiliko!

    ReplyDelete
  13. NCHI ZOTE DUNIANI NI KITU CHA KAWAIDA KULIPISHA MAGARI YANAPO-PARK, NI MOJA YA VYANZO VYA PESA VYA SERIKALI ZA MITAA, NCHI KAMA U.S.A NA U.K HUWA KUNA MACHINE ZA KULIPIA PESA YA PARKING MARA TU UNAPOSHUKA KWENYE GARI UNATAKIWA UKALIPE, WALA HAKUNA MTU ANAYEKULADHIMISHA KULIPA NA UTAMADUNI TU ULIOJENGEKA NA MAZOEA KUWA UNAPASHWA KULIPA PARKING FEES, NCHI KAMA U.K. KUNA NDIO PARKING SLOTS, LAKINI MENGI YA MAGARI HUWA YANAPARK BARABARANI TU NA HULIPIWA FEES, HATA NYUMBANI KWAKO KAMA UNAPARK GARI BARABARANI NA WENGI NDO HIVYO HUPARK BARABARANI HULIPA KWA SERIKALI YA JIJI PARKING FEES, CHA MSINGI NI UTARATIBU UBORESHWA NAMNA YA KUFANYA MALIPO NA WANANCHI WAELIMISHWA UMUHIMU WA HIYO KODI NA INAFANYA KAZI GANI, ISIJE IKAWA NA MRADI TU WA MAFISADI NA SEMINAR KUBWA KUBWA TU, PESA NYINGI ZA PARKING FEES NDIZO HIZO HUTUMIKA KWA AJILI YA RAPAIRS ZA BARABARA, SHULE, AFYA NA MAJI, TAA ZA BARABARANI NA HUDUMU NYINGI ZA JAMII KATIKA SERIKALI YA JAMII, THEY COLLECT THOSE KIND OF FEES FOR PUBLIC FINANCE PURPOSES. TUSAHAU KABISA MAMBO YA KUPARK BURE NI YA MWAKA 47, LOGIC HAPO NI WENYE KIPATO KIDOGO KUCHANGIA MAENDELEO YA JAMII.

    ReplyDelete
  14. mbona kupark na kupewa ticket ni kitu cha kawaida kwa nchi za ughaibuni? maeneo ya busy kama central London ambayo ni kama posta kwa nyumbani, huwa vigumu kupata parking na ukipark sehemu isiyoruhusiwa wanakupa fine na hata kulichukua gari na malipo yake ni kuanzia £60 mpaka £ 250 kutegemeana na eneo walilolikuta gari. Cha maana soma alama vizuri or else acha gari nje kidogo maana mjini kati siku zote parking ni shida hata kwa nchi zilizoendelea. Hivyo wapendwa hayo ndo maendeleo yenyewe. Annon wa kule juu ni kweli kuwa sheria hairuhusu ku-clump gari kama dereva yupo ndani na wewe kama unaweza uwe unatembea na mpambe ili umwache kwenye gari wakati unakimbilia dukani.

    ReplyDelete
  15. MDAU HAPO JUU ANONY 12:56, INAONEKANA HUJAELEWA LALAMIKO LA MDAU. TATIZO NI HAKUNA PARKING LOTS ZA KUTOSHA JIJINI DAR..NA SEHEMU AMBAZO HAZITAKIWA MAGARI KUPAKI HAMNA ALAMA YA KUASHIRIA HIVYO..HIYO 65,000 SIYO GHARAMA YA PARKING NI FAINI YA KUPAKI SEHEMU ISIYOTAKIWA AMBAPO VICTIM HAKUJUA KAMA HIYO SIYO SEHEMU YA PARKING KS YA KUKOSA ALAMA. SASA NDIO HAPA ANALALAMIKA WHY? BADALA YA JIJI KUTAFUTA NJIA MBADALA YA KUONGEZA SEHEMU ZA PARKING KULIKO KUVIZIA KUWATOZA WATU FAINI...NA HUO NDIO WIZI UNAOZUNGUMZIWA. PARKING LOTS ZA KULIPIA DAR PIA ZIPO SEMA HAZITOSH NA ZINASIMAMIWA NA WATU SIO MACHINE AMBAZO MTU UNALIPA MWENYEWE..ISITOSHE HIZO PARKING LOTS NI BIASHARA YA MTU...NA HAPO NDIO WIZI MWINGINE....

    ReplyDelete
  16. Mmiliki wa hii biashara ni Mzawa mwenzetu, angekuwa Mhindi ingekuwa rahisi sana kumwita mnyonya damu.

    ReplyDelete
  17. aaaaaaarg wabeba box wa uk na usa mshadandia treni kwa mbele?get a life dudes kila kitu hata huku usa hata huku uk what a louse example,bebeni box huko mtoke vibyongo,wadau kweli jamaa hawa wezi tu lazima zifanyike jitihada za makusudi kuikomesha hali hii

    ReplyDelete
  18. WEE mdau uneyesema TSERE atalivalia njuga akijulishwa, UMECHEMSHA BIG TIME!! kwani halijui hili tatizo?? Kwani limeanza Leo??? Wote hao ndio hao hao tu hakuna jipya usijipe matumaini hewa!!

    ReplyDelete
  19. I LOVE BONGO KWANI SHERIA ZAFUATWA KWA MANATI!

    ReplyDelete
  20. JEHANAMU IPO KWELI,,,,
    LAZIMA WATU WAFE WAUNGUE MOTO KWA DHAMBI IZI HAZISAMEEKI HAKIKA
    wizi mtupu,,,nyamafu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...