Mbali na kuvunja sheria,
Je kuna faida ya “Kujilipua”?

Ninamuheshimu sana Kadogoo kwa juhudi alizozifanya za kujiendeleleza tokea siku alipowasili UK miaka 15 iliyopita.
Ingawa kutokana na sheria za Uingereza njia ambazo amezitumia ni kinyume cha sheria na kama ukweli ukijulikana na taasisi fulani fulani Uingereza watamyanga’nya vifaa vyote ambavyo amevipata na ambavyo ni vigezo vya maendeleleo yake akiwa UK yeye na familia yake na hata atakaporudi nyumbani Tanzania.

Kadogoo ni mwenyeji wa Mashati mkoa wa Kilmanjaro. Wazazi wake sio watu waliojiweza kipesa lakini walijtahidi kumsomesha Kadogoo mpaka akamaliza form six huko huko Kilmanjaro. Alipomaliza form six alipata nafasi ya kwenda chuo cha ualimu na vile vile alipata nafasi ya kazi kwenye kiwanda fulani moshi mjini.
Kadogoo alichagua kufanya kazi ili aweze kuwasaidia wazazi wake ambao hali yao kimaisha haikuwa nzuri sana na pia kumsaidia mdogo wake ambaye ndio kwanza alikuwa primary school na ambaye angehitaji msaada ili naye aweze angalao kupata kiwango cha elimu ambacho amekipata Kadogoo.
Akiwa huko moshi mjini alipata kuunda urafiki na dada mmoja ambaye alikuwa anasoma Uingereza. Dada huyo alimsaidia Kadogoo kupata visa ya kutembea Uingereza. Miaka 15 iliyopita haikuwa ngumu kupata hiyo visa hasa kama unafanya kazi. Dada huyo alimueleza Kadogoo kwamba yeye ni mwanafunzi na hana uwezo sana, anachoweza kumsaidia ni mahali pakushukia tu kwa muda, alafu baadaye ajitafutie maisha yake.
Kadogoo alijitahidi akakusanya pesa ya tiketi ya ndege ya kwenda Uingereza. Alipofika UK alishukia kwa huyo dada aliyekuwa anakaa kwenye chumba chuoni kwake. Alikaa naye kwa muda wa week mbili kabla ya huyo dada kumwambia wakati umefika wa yeye kuondoka kwenda kujitafutia maisha (kwa wadau wa UK mnajua ni jinsi gani mtu hakai na mtu bila kuwa na kazi au uwezo wa kuchangia expenses). Ndipo Kadogoo alipoanza kuchakarika na maisha ya UK .

Alihamia mji mwingine mbali na London ambapo alipata kazi ya ku-pack vyakula kwenye kiwanda cha kupack vyakula (kwa wadau wa UK tafadhali sio Milton keynes/Beni Foods J). Kuhusu kibali cha kufanyia kazi, ilibidi atumie kibali cha rafiki yake kutoka Nigeria aliyejuana naye wakati akiwa London. Hii iliwezekana kwasababu kipindi cha miaka 15 iliyopita waingereza walikuwa bado hawajawa wakali sana kuhusu sheria za kufanyia kazi (kwa msemo mwingine ni kwamba walikuwa wanahadaika kirahisi).
Alijitafutia chumba kidogo (single bedroom) kwenye nyumba ambayo alikwa ana-share na watu sita kutoka mataifa mbalimbali. Baada ya miezi sita visa ya Kadogoo ya kutembea Uingereza ilikwisha, kwa hiyo alikuwa hana kibali cha kisheria kinachomruhusu kukaa Uingereza na kama angekamatwa na askari wa mambo ya uhamihaji angerudishwa Tanzania.
Alikutana na watu mbalimbali wa mataifa mbali mbali mbao walimfundisha ujanja wa kuyamudu maisha ya Uingereza na jinsi ya kuweza kupata documents za kuishi Uingireza kwa njia ambazo waswahili tunaita za mazabe (au njia laghai), ambapo Kadogoo alikwenda kwenye ofisi za uhamihaji London na kusema kuwa yeye ni mkimbizi kutoka Ruanda na jina lake la pili (sir name) akalibadilisha, lakini jina lake la mwanzo likabakia lile lile. Wadau wa UK tunaita “Kujilipua”. Alipatiwa kibali cha muda. Kipindi hicho pia idara ya uhamihaji ya Uingereza walikuwa wanadangaywa kirahisi na watu wengi kutoka mataifa mabalimbali walikuwa wanatumia njia hii laghai kupata documents za kuishi Uingereza. Usijaribu sasa hivi mambo yamebadilika J.
Baada ya miaka miwili alipatiwa kibali cha miaka minne (asylum status), ambapo baada ya miaka minne kama mienendo yako ni mizuri wanakupatia kibali cha moja kwa moja cha kukaa Uingereza (Indefinite leave to remain in the UK). Kadogoo alipopata kibali cha miaka minne kama mkimbizi aliruhusiwa kwenda shule/college za serikali ambazo zinatoa elimu ya kiwango cha secondary (O level and A level). Kwasababu hakuweza tena kutumia vyeti vyake vya form six vya Tanzania kwa sababu ya kujiita mkimbizi, Kadogoo alichukua nafasi hii akaenda tena shule (high school) kuchukua A levels.
Kwa hiyo alikuwa sasa anafanya kazi usiku ya ku-pack vyakula na mchana anakwenda shule. Baada ya miaka mitatu alimaliza A Levels na alipopata kibali cha kukaa Uingereza permanent aliruhusiwa kwenda university kwa kulipiwa na serikali. Kadogoo tena alichukua hii nafasi aka-apply kuchukua degree kwenye moja ya university kubwa London.
Alihamia tena London kwenye chumba kingine. Degree ilikuwa ya miaka mitatu. Safari hii alitafuta kazi mbili za part-time kwenye restaurants. Wakati akiwa anachukua hii first degree aliweza pia kumsaidia boyfriend wake (naye kutoka Mashati – Kilmanjaro) pesa ya tiketi ya kuja London kwa visa ya kutembea. Boyfriend wake alipofika London, ili na yeye aweze kupata kibali cha kukaa Uingereza ilibidi waoane mara moja kwa ndoa ndogo iliyohudhuriwa na marafiki zake wanne.
Kwa maana hiyo boyfriend aliweza kutafuta kazi kwani documents za ndoa zilimwezesha kufanya kazi bila kizingiti chochote.
Kwanza alianza na kazi ya kusafisha maofisi na baadaye akafanya kazi kama security guard kwenye supermakets(maduka ya vyakula) ambazo zinalipa vizuri kama unafanya masaa mengi, yani usiku na mchana. Kwa hiyo mume wake Kadogoo alikuwa sasa anamsaidia kifedha, ambapo Kadogoo aliweza kupunguza masaa aliyokuwa anafanya kazi na kuweza kuweka muda wake na juhudi zake kwenye degree yake.

Alipasi vizuri degree yake akapata kazi kwenye kampuni fulani London. Sasa ikawa zamu ya mume wake kwenda university. Kwa mume wake mambo yalikuwa rahisi sana kwenda university kwa sababu, kwanza alimaliza form six na division nzuri huko Kilmanjaro, na pili alikuwa na documents zote (kwa ajili ya ndoa) zilizomwezesha kusomeshwa na serikali ya Uingereza na pia kwasababu jina lake halikubadilika kwa hiyo aliweza kutumia vyeti vyake vya form six alivyotoka navyo Tanzania.
Mumewe naye alichukua degree yake kwa miaka mitatu London. Alipomaliza naye alipata kazi London. Wote walikuwa sasa wana kazi nzuri na kwasababu walikuwa bado wanakaa kwenye chumba kimoja waliweza kujilipia fees/ada ya master degrees ambazo wote walichukua kwa wakati mmoja. Serikali ya Uingereza huwa inatoa grants/funding kwa first degrees tu (undergraduate).
Kadogoo pia ilibidi aombe urahia wa Uingereza kwasababu hakuweza tena kutumia passport yake ya Tanzania. Haikuwa shida kupata urahia wa Uingereza kwa sababu tayari alikuwa na Indefinite leave to remain in the UK.
Kwa hiyo alipata urahia wa Uingereza na kupata British passport. Mume wake ambaye naye kutokana na ndoa alikuwa ameshapata kibali cha kukaa Uingereza moja kwa moja, hakutaka kubadili urahia wake. Hii inamaanisha kuwa Kadogoo anaweza tena baadaye kupata urahia wa Tanzania kwa kupitia kwa mume wake.
Sasa ni miaka 15 imepita tangu Kadogoo afike Uingereza, yeye na mume wake wana elimu ya juu, na wana-ducuments zote zinazowawawezesha kufaya kazi popote pale duniani. Kadogoo pia hana haja tena ya kutumia sir name ya ki-Ruanda kwani anatumia jina lake la ndoa ambalo ni la kichaga. Kwa sasa wote wame-apply kazi huko Tanzania na wanaweza kwenda wakati wowote kufanya huko.
Pia Kadogoo amepata grants (funding) ya kuchuka PHD kwenye university yake alikochukua first degree. Hiyo PHD ni research ambayo anaweza akafanya wakati wowote huku anafanya kazi. Kadogoo pia anampango wa kumsaidia mdogo wake aweze naye kupata degree Uingereza.

Wazazi wa Kadogoo hawakuwa watu wenye uwezo mkubwa, lakini asante kwa mfumo wa maombi ya ukimbizi (asylum application process) iliyokuwa Uingereza miaka 15 iliyopita sasa hivi Kadogoo na mume wake ni wasomi na ndugu zao pia hata jirani zao huko Mashati wanafaidika.
Kama Kadogoo akirudi Tanzania anaweza kupata tena uraia wake wa Tanzania na hapo baadaye anaweza hata kufanya kazi kwenye ngazi za juu serikalini na hata kuwa Waziri au Raisi wa nchi.
Je wadau ni vibaya kama mtu alipata documents kwa njia hii ya udanganyifu ili apate elimu, ambayo hivi sasa inatumika kusaidia watu wengine?

Enyi wadau wa UK mliojilipua, tafadhali tuelezeni, kuna faida nyingine ambayo imepatikana kwa kujilipua? zaidi ya kuweza kukaa UK bila matatizo ya vibali na kutuma pesa nyumbani?
(tafadhali hili ni swali tu, kama unaweza kuchangia tafadhali changia)
PS: Jina lilotumika kwenye hadithi hii ni la kutunga (Fictitious name)
Sehemu za Tanzania zilizotumika pia ni za kutunga

Kay siye Kadogoo
Kay
Brunel University – London
Email:
kaysulleiman@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. Nyie nyie nyie! Shauri yenu hivi mmesoma documentary au article ya Hashim Thabit mwandishi wake alvyorefer comments za kwenye blogu ya Michuzi? Mtu unavyouliza hayo maswali lengo lako ni nini haswa?

    ReplyDelete
  2. Katika maisha watu hufanya lolote lile ili mradi watoke!Nahuo ndio uchakarikaji.Lakini ukiliangalia suala zima la kujilipua hufanywa na watu wenye akili moja na upeo mwembamba sana wa kuona mambo.Hawa watu hushauri kila mtu ajilipue hata kama ana scholarship!!ila wengi wao wameishia kuwa frustrated na maisha kwani walivyotegeme sivyo.Kuwa na uraia sio passport ya kufikia mafanikio.Mafanikio ni mtu mwenyewe.Wengi wao wameishia kudhalilishwa na pesa za madirishani,neno ASYLUM seeker ni sawa na MBWA!!wazawa huwaita"fuckin asylum seekers!
    wakina dada hu force kupata mtoto ili wapate nyumba,ukiwaangalia wako depressed sana na matololi yao. vijana wameishia kuwa wachanjaji na wizi wa magari ila kwa sasa ni ngumu kidogo.

    ReplyDelete
  3. hadithi haieleweki,,,kama unataka kumrithi Ben Mtobwa hutoweza ni bora ungojee wachora vikatuni uwarithi ila kwa sasa hadithi huwezi,,,samahani lakini kama nimekuuzi dont take it personal maana hadith yako ni mbaya na haieleweki na kama una mke (dem) mhadithie yeye na sio umaa

    ReplyDelete
  4. Kay Seleman please go get a life.

    ReplyDelete
  5. Ukitaka kuuita kuwa ni udanganyifu au utapeli mimi nasema kadogoo ni smart. Kudos to yeye na mme wake. Ni sawa na kuiba biblia kutoka kanisani ili uijue. Kwa hiyo wamefanya safi kujilipua.

    ReplyDelete
  6. KAMA MTU HUNA CHA KUANDIKA SI UKAE KIMYA TU, UNAPOTEZA MUDA MWINGI KUANDIKA YASIYOKUHUSU, UMESHIKILIA KUJIRIPUA KUJIRIPUA, SASA UNAANDIKA KWA FAIDA YA NANI? MICHEZO YOTE INAYOFANYIKA DUNIANI WATU WANAIJUA HAKUNA JIPYA, HAIKUANZA LEO WALA HATOKWISHA LEO, KATIKA MAISHA KUNA MICHEZO MINGI YA HATARI INATEGEMEA TU HILO GEMU UNALICHEZA VIPI. MZEE WA BWAWA LA MAINI BARUA KAMA HIZI UNATAKIWA UZITIE KAPUNI KWANI HUMU NDANI HATUZIHITAJI HAZINA UJUMBE WOWOTE, NA UKUMBUKE HII GLOBU INAPITIWA NA WATU KIBAO MIONGONI MWAO HAO WAZEE WA NONDO AMBAO KISWAHILI SIO DILI TENA.
    ANDIKA ISHU NYINGINE MJOMBA WATU WAKUCHANGIE HOJA.
    MDAU WA DARAJANI.

    ReplyDelete
  7. MICHUZI SIO KILA ANAEOMBA MSAADA KWENYE TUTA UNAMTUNDIKA,HUYU JAMAA KAPOTEZA MUDA WAKE MWINGI KUANDIKA UONGO MIAKA KUMI NATANO ILIOPITA WATANZANIA HATUKUA NA VISA UK,TENA ANASISITIZA VISA YAKE KADOGO ILIPOISHA,PLEASE MICHU ITOE HIYO MADA LETE MADA ZENYE AKILI,HUYU MTOA MADA LAZIMA ATAKUWA NA KICHAA CHA ULAYA AU VIPI WADAU,

    ReplyDelete
  8. Mtunga hadith mnafiki, wivu na majungu. kama mafanikio ya kadogoo umeyaona sasa unataka kuchunguza watu wengine ya nini???? Wewe uliko na maisha yako si inatosha wewe ya watu yanakuhusu nini. Watu wanavyoishi ni akili yao na wala hawana muda wa kukuambia ohh sijui kujilipua faida zake ni hizi na zile.

    Sasa ukishasikia faida zake ndio iweje? Watu wote wajilipue? Hebu acheni hizo hadith zisizo na kichwa wala mgongo. badala ya kukaa kuwaza maisha yako na mambo ya maana ....umekaa ukafikiriiiiiii hivi na vile ....ahhhhhhGGGGHHHHH sigh!!!! Then unapublish kwenye blog ya watu wanayoijua kila kona

    Who cares....hao wabunge wote umesoma resume zao ukaona walivyopamba ....je na wao ni mbaya.....? get a life my dear

    ReplyDelete
  9. To each his/her own. You are a pathetic ding dong who just want an attention. Get a life dude, before you know you'd be on a walker/wheelchair with nothing in your pocket ending up being a burden to a society. People of your type are just polluting our world with CO2.

    ReplyDelete
  10. HE WEWE KAY?HE HUKO SHULE UNAKOSOMA,HAWAKUPI KAZI ZA KUTOSHA MPK UNAPOTEZA MUDA WAKO WOOOOOOOOOTE KUANDIKA 'KUJILIPUA'????....

    ASAVALI KM UNGEKUWA UMEANDIKA KITU AMBACHO WATU HAWAFAHAMU,...NINGESEMA WALAU UNA MOJA LA 'KUIFUNDISHA' JAMII....YAANI UMEANZIA MBAAAAAAAAAAAAAAALI ROMBO MASHATIIIIIIIIIIIIIIII.......TEH TEH KUANDIKA KITU AMBACHO KINAJULIKANA NA KILA MTU!KWELI WEWE JUHA?!
    BASI UNGEKUWA UNA MASWALI YA MSINGI,UMEULIZA UNATAKA UFAHAMISHWE,NOOOOO UNAONEKANA UNAJUA KILA KITU KUHUSU KUJILIPUA SASA NINI SHAUO????AAGH UMEBOA KWELI!

    ReplyDelete
  11. HE WEWE KAY?HE HUKO SHULE UNAKOSOMA,HAWAKUPI KAZI ZA KUTOSHA MPK UNAPOTEZA MUDA WAKO WOOOOOOOOOTE KUANDIKA 'KUJILIPUA'????....

    ASAVALI KM UNGEKUWA UMEANDIKA KITU AMBACHO WATU HAWAFAHAMU,...NINGESEMA WALAU UNA MOJA LA 'KUIFUNDISHA' JAMII....YAANI UMEANZIA MBAAAAAAAAAAAAAAALI ROMBO MASHATIIIIIIIIIIIIIIII.......TEH TEH KUANDIKA KITU AMBACHO KINAJULIKANA NA KILA MTU!KWELI WEWE JUHA?!
    BASI UNGEKUWA UNA MASWALI YA MSINGI,UMEULIZA UNATAKA UFAHAMISHWE,NOOOOO UNAONEKANA UNAJUA KILA KITU KUHUSU KUJILIPUA SASA NINI SHAUO????AAGH UMEBOA KWELI!

    ReplyDelete
  12. muone huyo anony wa pili...eti kuwa na uraia sio passport ya mafanikio....KALAGHABAHO WEWE!...wasingejilipua basi!na sio tu warombo mashati tu km kadogoo ndio 'wanaojilipua'...hata mataifa mengine....wazimbabwe,wanaijeria..karibia mataifa yote...yanafanya mchezo...huuu...wanajua wanachokitafuta!KM wewe ni mojawapo wa hao wazushi mnaongalia wenzenu wakichukua risk na kuona ni wapumbavu then shauri lako...ila 'wajanja' walishajuaga siku nyiiiiingi kuwa na 'papers' ni kuwa na uamuzi kuwa 'maskini' au 'tajiri' na habari ndio hiyoooo....!!!
    km umeoza na upo upoo tu,jamani kajaribu bahati yako...acheni na hao wapuuzi wanaolonga longa
    hapa...

    NEY-BHAM.

    ReplyDelete
  13. MICHUZI ALIPI HOTEL KWA SABABUYA SISI KUJILIPUA, HUNA HOJA WEWE KAKWANGUE SAMAKI MAGAMBA.

    ReplyDelete
  14. hiyo ndio reality yenyewe either you like or not i dont care. alivyosema huyu jamaa ni ukweli mtupu kwa hiyo waliojulipua tumieni chance zenu kwa maendeleo kama kadogoo alivyofanya. watu wamepata bahati ya kulipiwa shule , nyumba bure na pesa wanalipwa wanachosoma hakieleweki miaka inapita yupo hapo hapo hakuna progress MUNGU AKUPE NINI (KIDONDA). wanawake hao ndio usiseme wenyewe wanachofikiria kujaza ulimwengu kuzaa tu ili wapate ela za watoto na kujiita single mother kila mwaka unazaa. wanaume sio mbaya sana mbali na uchanjaji na sio wote. HAYA NDIO MAISHA YA WENGI WALIOJILIPUA UK

    ReplyDelete
  15. Michuzi nawe unatuzingua kama walivyosema wenzangu sio kila kitu utoe humu au Michuzi unampango wa kuja kujilipua nini?

    ReplyDelete
  16. rules of engagament, ukiwa vitani unatakiwa kufanya kila uwezacho ushinde. mimi nimekuja hapa Uk mwaka 2001. wazazi wangu sio mafisadi hivyo hawana uwezo wa kunisomesha. nia ya kuja huku ni kusoma lakini kama mnavyojua kujisomesha Uk ni ghali sana. Nilijilipua nikapata makaratasi, nikaenda university nimkamaliza degree ya kwanza. maisha yakawa stable nikapata kazi nzuri nikaweza kujisomesha degree ya pili.
    Cha msingi kuhusu kujilipua ni akili ya mtu, kuna wanaojilipua kwa sababu ya mambo muhimu, kuna wengine ni kwa sababu zao binafsi.
    Sasa nipo bongo nafanya kazi kwenye bank kubwa, na hicho kitabu cha mama sina mpango nacho, wala sihitaji kurudi huko.
    Hivyo watu wanaishi Uk kwa njia nyingi, kuna wanaoolewa wengine hata ndugu wanaoana ili kurekebisha paper. sioni ni kitu cha ajabu kila mataifa wanafanya hivyo ugenini, wahindi, wachina, wanaigeria, wazanzibar etc.
    Hata waingereza wanapokuja bongo kuna wanaowaoa/kuolewa dada zetu ili kupata makaratasi. Hii ndio dunia, unapokuwa vitani fuata "rule of engagement" ushinde, it doesnt matter you can win uggly or clean, win is a win.
    Thank you
    Kadogoo original

    ReplyDelete
  17. Mimi nawapongeza wote waliojilipua na kwenda shule, hicho ni cha msingi sababu najua sio wote ni watoto wa mafisadi hivyo kama unafanya chochote kupata elimu ni kitu cha msingi sana. Nawashauri watanzania wote wafanye wawezavyo kupata elimu yao...degree haiandikwi refugee na degree ya UK inatumika popote duniani.
    Hata wazungu walikuja africa kama wamissionari halafu wakatufanya watumwa. " cause can be changed for betterment". It happen everywhere in the World, watz tusilale na tuache majungu

    ReplyDelete
  18. Watu wa box msitu-boe hapa! Mnapiga story ndefu namna hiyo mnadhani nani atakaa kusoma habari za ku-stowaway!?!

    Rudini bongo, huku maisha bora kwa kila mtu. Kichwa chako tu. Ila kama akili yako imezibwa na ukungu wa kubeba box, kaa huko huko!

    ReplyDelete
  19. khaaa! Mi napoteza muda wangu kusoma kumbe ni stori ya kutunga.Nyambafu mkubwa wee ,acha kutoa siri za Gvt, YA KADOGOO mwachie KADOGOO mwenyewe

    ReplyDelete
  20. dah,kwani usipoongea ndio hao ndugu zako huko dutumi watajua kuwa ushadedi nn?

    ReplyDelete
  21. wewe ni mjinga si umeona faida aliopata kadogoo baada ya kuishi hapa uk sasa unauliza nini tena get a life!

    ReplyDelete
  22. Hehehe...
    wabeba boksi washaanza kuchonga, naona msela kawatachi.

    Well said SINA MAKOSA,mi sioni kosa la mwandishi kaamua kutuhabarisha sisi ambao tuko bongo mnayoyafanya huko ughaibuni.

    ReplyDelete
  23. that girl(kadogoo)she is a genius!shes the kind of few girl who are determined to pursue dreams,she went in uk to get education,and she got!that is the best whatever the way it cost to me she is my hero ,the issue of citizenship is solved since she married tanzanian kadogoo bravo!im generally i failed to understand the aim of the author of this article whats ur problems?those are personal issues,dontfumes its ur problems

    ReplyDelete
  24. benifood ya baba yako?

    ReplyDelete
  25. Nyerere alishajibu hili swali, fanya utakaloweza ujiendeleze ili mradi usisahau nyumbani.

    Mbona wapo wengi wanaokuja bongo kujilipua na tunatoa pasipoti kiubwete tu hilo ndio jambo la kujadili, na wengine ni viongozi.

    Unachozungumzia ni ukimbizi wa kiuchumi, si jambo geni na halikuanza leo wageni wanakuja kwetu wanachuma na sisi si vibaya tukatafuta njia za kurudisha pasenti kidogo nyumbani.

    Michuzi uwe unaangalia sisi unaotuchongea ndio tunaokuwa wenyeji wenu mkija vekesheni!

    ReplyDelete
  26. HUYU MTU ANAONEKANA KAJA JUZI TU U.K. NA AMEPATA HIZO STORY JUU JUU TU HUKO CHUONI ALIKOFIKIA/BRUNEL UNIVERSITY NA NAHISI YEYE ANATAKA KUFANYA HIVYO SASA ATAFUTA UHAKIKA WA KUFANYA HIVYO. KIFUPI HII NI HADITHI YA KUTUNGWA NA HAINA UKWELI ASILIMIA MIA MOJA, PAMOJA NA KWAMBA KUNA UKWELI WA MBALI. LAKINI HUO HAIFANYIKI HIVYO. KWANZA U.K. LEVEL YA UNIVCERSITY ELIMU SI BURE, LABDA PROFESSIONAL KAMA NURSE KWA KUWA WANAHITAJIKA SANA NA LAZIMA UWE RAIA LAKINI DEGREE ZOTE UNAPEWA MKOPO UKIMALIZA SHULE NA KUPATA KAZI YA KIPATO CHA ZAIDI YA £15,000. KWA MWAKA UNAANZA KULIPA, NA HAMNA GRANT MASTERS LEVEL FROM GOVERNMENT. KUPATA URAIA WA UK SI LAZIMA UJIFANYA MKIMBIZI ZAMA ZA YEYE ALIZOZISEMA UKIKAA MIAKA MITANO MFULULIZO ULIKUWA UNARUHUSIWA KUOMBA KUKAA MOJA KWA MOJA SIKU HIZI NI MIAKA 8, NA ZAMA HIZO HATA KAMA UMEINGIA KIJANJA NA HATA HUNA VALID VISA ULIKUWA UNARUHUSIWA KUOMBA KUKAA MOJA KWA MOJA BAADA YA MIAKA 8 NA SIKU HIZI NI 14 YEARS. HADITHI YAKE YOTE NI YA KUTUNGA TU. NA UTARATIBU NI KUWA UNATAKIWA KU-DECLARE KUWA WEWE NI MKIMBIZI MARA TU UNAPOSHUKA KWENYE NDEGE NA SI VINGINEVYO, HUWEZI KWENDA MJINI UKAKAA MIEZI SITA ALAFU UKAGEUKA NA KUSEMA WEWE NI MKIMBIZI, SIKU ZOTE HIZI ULIKUWA WAPI?

    ReplyDelete
  27. Jamani upumbavu ni ugonjwa na dawa haijapatikana, kwa hiyo tuwa samehe wale walio wapumbavu
    Huyu mtu ni mpumbavu na amekosa jinsi ya kujitafutia ummarufu, sasa anajaribu kujitangaza kwenye hivi web site vya akina michuzi

    Ndugu yetu maisha ni vita ,na vita hachagui silaha- chanzo cha watu kutafuta jinsi za kuingia na kutoka bila ya kuomba visa , ndiyo mwanzo mkuu wa kujilipua , malengo ya kujilipua yanatofautiana kutoka mtu hadi mtu,sasa hebu jiulize swali moja nchi kama Philipines inaendeshwa kwa remitances kutoka nje ya nchi yaani watu wanaofanya kazi nje wanawatumia ndugu na familia zao kipato vinginevyo maisha ya waphillipino yangekuwa mabaya sana -wamejaa arabuni na nchi zote za ulaya

    Kitu cha pili kijana mitaji inapatikana kwa njia mbalimbali kama unauwezo wa kuchuma paundi ukainvest tanzania na miradi ikaendelea na ukaajiri ndugu na jamaa kuna ubaya gani - hawa waingereza na wareno na wajerumani walikuja kwetu miaka karibu zaidi ya 100, wakachukua walivyo chukua -mfano hadi ziwa letu wakaliita jina la malkia wao eti ziwa victoria , sasa kuna tofauti gani ya mtanzania alikuja uingereza kutafuta maisha karne ya 21 na david Livingstone aliyekuja afrika miaka zaidi ya 100

    Kuzungumza kwako mambo yasiyo na maana wala mwelekeo ni ushahidi tosha kuwa wewe ni;
    a)Limbukeni wa maisha uliyekulia kijijini - ukafika Dar ukajiona umemaliza,ukarudia darasa la saba ukafaulu ukaenda tanbaza ama azania - mume wa shangazi yako kakutafutia kazi kwa marafiki zake sasa unafungua mdomo
    b)Kujakusoma kwa hela ya serikali ni bahati ukizingatia nchi ni masikini wewe uliyepata scholarship-usitukane wanaopigana kwa njia zingine -maliza kusoma ukawahi foleni ya ufisadi

    ReplyDelete
  28. duh kama ndio alikua anajifunza kuandika hadithi basi na mushushulio yote aliyopewa ataacha kabisa.

    Hadithi inatakiwa iwe inaentertain na pia iwe na maudhui. Hadithi yako imelucky both of these. Haichekeshi, haieleweki, na haina maudhui.

    Watu wamekuambia you need to get a life

    Na kaka yangu watch out sio kila unachopostiwa uweke huku. Au na wewe unabeef nini na wanaojilipua huko.

    ReplyDelete
  29. Michuzi pamoja na kuwa na uwazi na ukweli lakini hadithi hii haina busara ndani yake!unafahamu kuwa waliojilipua ni wengi, hakuna ukabila wala nini wote ni wabongo lakini shemeji zangu wa unguja na pemba asilimia kubwa wamejilipua. Habari kama hizi ni za kijinga muziki wake utashindwa kuucheza.

    ReplyDelete
  30. wee ng'ombe usiweke hadithi ambayo ulipewa uko ulimwengu gani?

    ReplyDelete
  31. Kichwa chako cha habari ni,

    Mbali na kuvunja sheria,
    Je kuna faida ya “Kujilipu"?

    Wataalamu wa tungo tayari tumeshaona kuwa hicho kichwa cha habari kimepinda. Uvunjaji wa sheria hauwezi kuwa katika upande mmoja wa mizani na 'kujilipua' tena sio "kujilipua" kama ulivyoandika.

    Hivyo sijasoma hilo gazeti uliloandika. Rekebisha kichwa cha habari ndipo tuteremke na chambuzi mwanana.

    ReplyDelete
  32. UKWELI UNAUMA, ANGALIA WADAU MLIVYOMSHUPALIA KADOGOO KWA KUANDIKA ANALOLIJUA.

    HONGERA BALOZI KWA KUWEKA MADA MCHANGANYIKO HUMU KWENYE BLOGU YA JAMII.

    NIMEKAA UK MWAKA WA 13 HUU...KUJILIPUA HAKUNA MAANA, MIFANO IPO MINGI TU HATA MKIPIGA KELELE HAPA.

    ReplyDelete
  33. Kay ameshindwa kufikisha kile alichokuwa anakusuduia.
    Kwa hadithi alivyo-i-present, anayo majibu yote yeye mwenyewe. Sasa anataka nini???
    Hii inatuonyesha wazi kuwa hana uhakika na mambo anayaongea, hii ni story aliyoisikia na anataka uthibitisho kama ni kweli. Muda wa kumjibu kama ni kweli au si kweli sina, namshauri aendelee kufanya research vizuri mwenyewe.
    Naweza kumsaidia kidogo asichoelewa yeye ni kuwa Kuna "Kujilipua na kuzamia"
    Kujilipua amesha eleza faida zake, kuzamia ndio hajui.
    Kuzamia ni kuendelea kukaa bila visa, na kuna hasara nyingi sana.Cha kusikitisha zaidi ni kuwa unapofiwa na mtoto wako, Mama, baba, ndugu huwezi rudi kwenu, la ukirudi basi ndio Marekani au Ulaya ndio basi tena.
    Kama nilivyosema sina muda wa kumfundisha huyu jamaa huyu maisha ya mzamiaji hivyo naishia hapa.
    Mdau
    Katambuga

    ReplyDelete
  34. ndo maana tunataka dual nationality. ili tusilazimike kuolewa kama kadogo. we miaka kumi hujaenda nyumbani umimport mchumba si unajitakia laana??

    ReplyDelete
  35. Mimi nasema kujilipua ni kuzuri kama una malengo yako, kama kusoma, kusomesha watoto wako au kusaidia watu wako, lakini kwa kifupi ukimbizi ni taabu sana , haswa siku hizi ndio taabu kabisaaa, kama mimi baada ya kuachana na mume wangu, nikaja UK nikajilipua, umri wangu ulikuwa umeshapita na kichwa changu kilikuwa na mambo mengi sana, kwetu mimi ndio super star, kwahiyo baada ya kujilipua nikaamua nianze kazi, nikaanza kuosha wazee, kuosha vyombo kwenye marestaurant nk. Baada miaka mitatu nikaweza kuwaleta watoto wangu wote wanne niliokuwa nao, nao walijilipua na sasa wana kwenda shule kama kawaida na wana fanya vizuri sana darasani,sasa wana inkam zao wenyewe, hivyo nikaamuwa kurudi nyumbani niko kariakoo nina duka langu lina nikeep bizy na kila mwezi watoto wananiletea chochote, kijijini kwetu nimejenga kisima watu hawataabiki tena kwenda mbali kufuata maji. kwangu mimi ukimbizi ni njia moja wapo yakutafuta maisha tu, ikukubali powa tu, kuna wanaojilipua, kuna wanao uza unga, kuna wanaoibia selikari, nk kwa hiyo mimi sioni kama ukimbizi una ubaya.Mimi sasa hivi kwa ukimbizi wangu kijijini nimekuwa Bush Queen

    ReplyDelete
  36. Kujilipua ni itu kizuri sana ukizingatia ni njia mojawapo ya kuutumia uchumi amabo mwingereza aliuiba kwetu. Watu wengi wanaoponda kujilipua ni wale ambao wanafanya kazi za "kea". Believe me, as far as a human dignity is concerned, ni bora kujilipua kuliko kunawa mavi ya wazungu

    ReplyDelete
  37. Mdau hapo juu umenikuna, sana. Eti watu wanataka kwenda ulaya kuosha vibibi na vibabu vya kizungu, kushika mavi yaoo, bull ...shiiiit. Ni bora asylum seeker, ambaye atakuja furahi baada ya muda na familia yake yote FOR GOOD. Kuliko kujidhalilisha na hizo CARE.

    ReplyDelete
  38. Huyu mtu aliyeandika hii message pia aliandika hadithi nyingine za ukimwi yeye na mume wake, halafu nyingine tena ya ukimwi yeye peke yake ambapo alimaua kuwa changudoa

    ReplyDelete
  39. Fact, hapa Uingereza watu weusi wote wana heshima inayofanana, uwe mmarekani mweusi, mjamaica, mwanafunzi mweusi, mwafrika au hata black british. Mwingereza mwenyewe "mzungu" watu wote hawa anawaweka katika kundi moja. Ingawa kutokana na "legal point of view" watu hawa wana "chances" tofauti. Wewe unayesema kuwa "asylum seekers" hawaheshimiwi hapa uingereza, Jee ni kweli wewe unaheshimiwa hapa kuliko "asylum seekers" mzungu aliyekimbizwa Zimbabwe? Mjadala kama huu ni mzuri sana kwa maana unaonyesha kiwango cha akili cha watu "wabongo". Believe me or not. Wa-Nigeria hata siku moja hawawezi kuzungumzia upuuzi kama huu.

    Kuhusu kuvunja sheria, kujilipua ni njia tuu ya uhamiaji na uhamiaji siyo kosa la jinai, na ndo maana asylum seekers hawafungwi.

    Kama wewe unafanya kazi na kujitegemea, good for you, but asylum seekers have a safety net in this country which oyhers do not have.

    Wivu. Watu wanaosomeshwa na wazazi wao, au kujisomesha kwa kufanya kazi sana, wanawaonea wivu wakimbizi kwamba wanaweza wakaamua kukaa nyumbani na kusoma tuu bila ya kufanya kazi.

    ReplyDelete
  40. HAHAHAHAHAAAAAAAAA
    JAMANI HII KALI YA MWAKA AISEEE

    ReplyDelete
  41. MTOTO ERIC ANACHEZEA CHELSEA AMECHUKULIWA MWAKA HUU HIYO NDIYO KAZI YA UKIMBIZI.WAZANZIBAR WANANUNUA NYUMBA ILALA,MAGOMENI NA SASA ZIMEFIKA HADI MILIONI MIA 200 HAO NDIO WALIOJILIPUA.
    TUENDEE KUSEMA KUWA KUJILIPUWA KUBAYA WAKATI IKISHUKA BRITISHI AIRWAY UNAKUTA KINA MAMA WA KIZANZIBAR WAMEJAA KIBAO.
    SUBIRINI KIZAZI CHAO IN TEN YEARS THEN UJE KUULIZA JEE KUJILIPUA KUZURI AU KUBAYA.
    WALIOJILIPUA KINA DODI AL FAYAD.UNASEMAJE?

    ReplyDelete
  42. mambo ya kizamani kun'gan'gania ulaya...rudini home BONGO kumekucha kila kitu kipo including good posh jobs...mnateseka nini huko nje?? Kama mnaweza kuzamia na kuishi maisha ya shida nje mtacope mara mia mkirudi na kuadjust maisha ya home. As for me in person huko naja kutembea tu-in fact the story told here is outdated!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...