Wanafunzi kutoka Uingereza kwenye semina ya maadili katika mkahawa wa vitabu- SOMA
Richard Mabala na Demere Kitunga wakifuatilia mdahalo wa vijana katika uga wa mhahawa wa vitabu SOMA

Mwandishi na mchapishaji wa vitabu mkongwe hapa nchini Walter Bgoya (kulia) akiwa na mwandishi kutoka nchi ya Matenique wakiangalia vitabu ndani ya duka la vitabu la SOMA



Manager wa duka la vitabu katika mkahawa wa vitabu – SOMA Bwana Godfrey George Kioko akikwa ndani ya duka.


Washiriki wa semina ya maadili wakifuatilia maelezo ya mwezeshaji Bwana Godfrey George Kioko katika mkahawa wa vitabu – SOMA

Wanafunzi wa shule za sekondari wakifanya mdahalo katika kwenye uga ndani ya mkahawa wa vitabu SOMA



Watoto wakisoma vitabu katika tamasha la WATOTO NA VITABU ndani ya mkahawa wa vitabu wa SOMA


Msanii wa kikundi cha Parapanda akifanya vitu vyake katika uga wa SOMA.

Balozi wa nanihiiiiiiiiii….
nakusalimia na pia nakupa pongezi nyingi kwa kuwawezesha wananchi kupata habari sahihi na taarifa mbali mbali kupitia blogu yako hii ya jamii. Naomba kuwasilisha hii mpya kwa Tanzania wajua kuwa kuna mkahawa wa vitabu hapa Dar es salaam (Book Café) ya pekee nchini. Inaitwa SOMA BOOK CAFÉ (MKAHAWA WA VITABU SOMA).
Upo pale regent estate karibu na hospitali ya AAR na jirani kabisa na kituo cha WAMATA. Mkahawa wa Vitabu Soma, Mlingotini Close, Kitalu Na 53 Mtaa wa Regent.
S.L.P. 4460
Dar es Salaam
Simu: 022 2772759,
Pepe :info.soma@infinet.co.tz
Hili ni eneo la wananchi na kushiriki matamasha mbali mbali ni bure. Wape wana jamii picha mbali mbali za matukio ya matamasha yanayo fanyika kila jumamosi na jumapili. Ni mimi mwana jamii mkongwe
Godfrey George Kioko
Manager wa duka na mratibu
Mkahawa wa vitabu – SOMA
+255 787 77 14 14





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Parapanda ndo wanavaa hivi siku hizi? Utandawizi oyeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. EBU TOA MAELEZO YA KUELEWEKA, MGAHAWA WA VITABU SOMA MAANA YAKE NINI, TUNATAKA KUJUWA. NAONA HII HABARI IKO JUU JUU TU INAELEA, TUPE HABARI KWANZA NDO PICHA ZIFUATE.

    ReplyDelete
  3. hi! inafurahisha kuona wanafunzi wa mataifa mengine kuja tanzania kuangalia maendeleo yetu katika elimu. mimi nachouliza sasa hivi je, serikali haioni aibu kuwa na migomo mingi katika mashule na vyuo? leo unasikia wanafunzi wamegoma, kesho unasikia walimu wamegoma, je hiyo ratiba yao inamalizika vipi? je, kuna uwezekano kweli wa kuwa na wahitimu bora? wenzetu kuja kutembea hii inaonyesha jinsi serikali zao zinavyojali elimu!

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli abiria tukome sana kabisa kwa madereva. Inasemekana ajali ya basi iliyotokea huko Singida ingeweza kuepukika kabisa kabisa kama dereva asingeondoa gari. Dereva alilalamikia ubovu wa break lakini wanasema abiria walimkoromea sana kwamba wenyewe wanataka safari. Sasa wamefika! Mungu ailaze pema kama kuna roho za watoto humo

    ReplyDelete
  5. heee uyo ndio RICCO big brother africa au sioni jamani maana hatumuoni tunashaangaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  6. Huu mgahawa wa Vitabu upo mtaa gani dar es salaam, naomba kufahamishwa

    ReplyDelete
  7. JAMANI WATANZANIA WENZETU NIMEPITA SLOGHT HAPO NIMEKUTA MSIBA WA MWENZETU MZANZIBAR MWENZETU ANAITWA ABDULLAH,ALIKUJA SIKU NYINGI HUKU U.K MASKINI NI MMOJA WA WALE WALIOJILIPUA HAPO SASA SIJUI ITAKUWAJE.ALIKUWA MGONJWA.WANA NDUGU TUPENI DETAILS TUWEZE KUSAIDIANA

    ReplyDelete
  8. Mkahawa wa vitabu SOMA upo pale regent estate karibu na hospitali ya AAR. Ukifika pale AAR utaona bango letu limeandikwa SOMA then fuata maelekezo ya bango utafika.
    Anwani: SOMA - Kwa burudani, utamaduni na maarifa.
    Simu: 022 2772759
    Mob: 0787 771 414 au 0715 771 414
    Email: info.soma@infinet.co.tz
    Email: kioko.soma@infinet.co.tz
    Website: www.soma.or.tz

    Ratiba:
    Kila Ijumaa ni kongamano la waandishi na wasomaji.

    Kila Jumamosi ni Tamasha la watoto na vitabu

    Kila Jumapili ni Mijadala na midahalo ya vijana

    KARIBUNI WOOOOTE SOMA

    ReplyDelete
  9. Baba Brian umekua manager sikuhizi si mchezo!! Nitamleta mwanangu umsomeshe hapo Mgahawani kwako.

    ReplyDelete
  10. We would like to know the cost implication, if there is any!

    Cause siku hizi hata kama umezaliwa genius kama huna kitu husomi ati, inatisha sana.

    ReplyDelete
  11. Michuzi,

    Hii huduma safi sana. Naomba kufahamishwa kama hapo mahali, Book Cafe, wanatoa huduma gani zaidi. Kwa mfano, Ni sehemu ya malumbano tu au pia ni sehemu ya kujisomea vitabu? au kununua vitabu? Kuna sehemu ya kukaa na kujisomea hata kama sinunui kitabu?. Je vile vile nikija na notebook computer yangu, WiFi aliyekomaa yupo atakaye niwezesha kwenda mtandaoni na Je kuna sehemu ya kuegesha magari. Je kuna mufindi (kiyoyozi)?. Nashauri afisa mipango wa hii Book cafe aangalie haya yote kama hajayafanya anayafanye. Huu ni ushauri tu. Kama ana huduma hizo mimi binafsi nipo radhi kwa mfano kulipia parking na huduma nyingine ili nije hapo Book Cafe badala ya kwenda kujilisha minyama myekundu na mapombe sehemu ambazo wabongo wamezoea kwenda na baadaye wanajikuta muhimbili kama sio matumbo kufumuka.

    ReplyDelete
  12. saaafi sana lazima nifike,,,izi ndo sehemu zenye akili bwana nakubaliana na mdau wa bold letters.
    yan wapata mahali watumia kukaa na kusoma lots of vitabu vyenye akili na watoto wawaleta na kuwajengea mazingira km haya,,sio migemu weeee,matoy mwisho wakua mambumbu

    ReplyDelete
  13. hi
    kaka michuzi,samahani kwa usumbufu but is it possible kupata namba ya simu ya richard mabala coz nina shida nayo sana alinisahidia sana nilipokuwa mtoto, thank you

    ReplyDelete
  14. Wanao ulizia mkahawa uko wapi nimetoa maelekezo hapo juu na ratiba ya kila mwisho wa mwezi. Kwa wanao taka kuja kila siku, mkahawa uko wazi saa mbili asubuhi hadi saa mbili usiku kwa ajili ya wewe kukaa kwa usalama na kujisomea au kufanya shughuli yoyote. Parking ipo tena kubwa sana hata kama una train njoo tena kuna ulinzi wa kutosha. Kwa kweli pametulia si mchezo. THERE IS NO COST, IT IS FREE AT SOMA BOOK CAFE. KARIBUNI WOOOOOOOOOOOTE JAMANI MJIONEEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...