Miss Tz 2008 Nasreem karim bada ya kukabidhiwa bendera ya taifa
Waziri wa mambo ya ndani Mh. Lawrence Masha akimkabidhi Miss Tz 2008 Nasreem Karim bendera ya taifa katika kumuaga akashiriki vyema Miss World huko sauzi mwezi ujao. Kulia ni bosi wa masoko wa vodacom ephraim mafuru na shoto ni bosi wa vodacom foundation mwamvita makmba. Vodacom ndio wadhamini wakuu wa miss tz

waziri wa mambo ya ndani mh. lawrence masha (kulia) akiongozana na miss tz 2008 nasreem karim na mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji mh emmanuel ole naiko leo baada ya kumkabidhi bendera ya taifa tayari kwenda kutuwakilisha kwenye fainali za miss world baadaye mwezi huu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. ayy ayy ayy! hivi kweli tutaendelea jamani? viongozi wetu wa juu serikalini wanapoteza muda wao muhimu kuhudhuria hafla kama hizi. it can only happen in africa! it can only happen in tanzania!

    ndugu zangu mlio nchi mbali mbali hebu niambieni kama haya yanatendeka katika nchi mnakoishi!

    ReplyDelete
  2. Mh. mithupu tunaomba picha zaidi za tukio hili.
    Mdau numba 6

    ReplyDelete
  3. Thank you michu kwa kufuata ushauri wangu kuhusu kichwa cha habari. "Ni kukabidhiwa bendera" na "si kuagwa" kama ulivyotoa post ya awali.

    Tunamtakia uwakilishi mwema japo sina imani kama na yeye si wale kati ya wanaokabidhiwaga bendera kwenda kutalii kwa niaba ya taifa kila mwaka.

    ReplyDelete
  4. miss Bongo bomba lakini ana chicken leg hafiki popote huko anaenda vekesheni tu huo ndo utabiri wangu namuombea mungu ambariki japo awepo ktk mia bora

    ReplyDelete
  5. Kaka michu leo naomba nitoke nje ya topic kidogo, leo nilifurahi sana nilipokuwa saloon hapa rotterdam holland kusikia nyimbo ya ali kiba kwenye radio station ya kidutch, kwa kweli i must say it made my day kuona mbongo mwenzangu anasikika miles away from home, huwezi amini nilivyofurahi mpaka nikaomuomba dada mwenye saloon ambaye ni msurinam aongeze sauti. Yani kwakweli inaonyesha cinderella hata bila ya kujua maneno yanayoongelewa lakini nafikiri watu wanai feel. Hongera ali kiba kwani, he made my day

    ReplyDelete
  6. Uwezekano Upo Wa Kusimamisha Show Ya Nguvu Kama Odemba...Pamoja!
    BYABUSHA, Mwingine.

    ReplyDelete
  7. na weeee michu ovyooooo ndo nini unabania meseji??kwani nilitukana??mbona ilikua kawaida tu??
    kusema awa viongozi wa sirikali kazi kuongozana na vibinti vimiss ni kosa??maana lzm atafutwe apo baadae na "mzee" hahahahaaaaa
    BANIA NA HII

    ReplyDelete
  8. Aende bagamoyo akaage manake bila hivyo haendi mbali. Sio mrefu kabisa. Hebu angalia hapo na viatu virefu lakini hajawapita hao wanaume wawili na watu wote wanaomfuata nyuma wako almost the same height.


    Bongo tutajifunza lini. Kama tunataka kushiriki haya majambo kimataifa ni lazima tufuate sheria za kimataifa. Sisi urembo wetu bongo tunavyouona ni tofauti kabisa na jinsi hizi nchi zilizoanzisha haya majamboa wanavyouona.

    Kwa wao urefu ni muhimu sana na hipsi hawataki kabisa. msifikiri Flaviana alifika mbali vile kibahati au kwa vile alikua hana nywele ndefu ....Yule mdada urefu wake na figure yake ndio ilimfikisha mbali.....Huyu ni mzuri wa kwetu bongo....

    ReplyDelete
  9. Si mbaya kwa Serikali kuwasupport wanaoliwakilisha taifa katika nyanja yeyote Duniani. Kinachonisumbua ni Kuona kuwa "WAZIRI WA MAMBO YA NDANI" kufanya hivyo sasa hapo sijui anaiwakilisha serikali au yeye mwenyewe.
    Wadau hapo je;
    1. Anakosea kazi?!
    2. Anaingilia Kazi?! au
    3. Anajisahau?!!!
    Majambazi yatapungua kweli??!!
    Mmh

    Mzawa.

    ReplyDelete
  10. Mi staki Nasreen wala kimbaumbau chengine, Bi Mwamvita Makamba tu!...Hiyo Killa MegaWatt smile imeshanitoa roho. Duh kweli Mungu anajua kuumba, mtoto mzuli Halle Berry haoni ndani!!, hapo bila ya make ups! wala plastic surgery. Mwamvita, Im in love witchu baby...will U marry me?

    ReplyDelete
  11. Mi staki Bi Mwamvita Makamba wala kimbaumbau chengine, Bi Nasreen tu!...Hiyo Killa MegaWatt smile imeshanitoa roho. Duh kweli Mungu anajua kuumba, mtoto mzuli Halle Berry haoni ndani!!, hapo bila ya make ups! wala plastic surgery. Nasreen, Im in love witchu baby...will U marry me?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...