mkuu Michuzi ninayo hii story yangu naomba uianike kwenye blog yako nipate ushauri wa wadau katika hili.

Niko njia panda sana kipindi hiki.
ILA NINGEOMBA USITOE JINA AU UTAMBULISHO WANGU KWA HILI.
ASANTE KWA KUTUWAKILISHA MTANDAONI.

Wadau,ningeomba ushauri wenu katika hili,Nimekua na mpenzi wangu kwa zaidi ya miaka miwili ingawa alikua anaishi kwao lkn alikua akija kwangu na hata kushinda au kulala siku zingine.
Sasa hivi majuzi mdogo wangu wa kiume alihamia kwangu baada ya chuo chao kufungwa ghafla na hivyo tukawa tukiishi nae.Tatizo likaanzia hapo siku moja nikarudi nkampa mdogo wangu hela akanunue vitu kwa ajili ya kupika na mpenzi wangu huyu akaanza kulalamika sana mpaka sasa bado hatujapata mwafaka.
Zaidi anadai kua kuja kwake kwangu atasitisha kwani inaonekana amekua akikwaza ndugu zangu,na pia anadai kua huyu mdogo wangu hamrespect na pia anaona kama yeye anamzibia uhuru wa kukaa nami kama ndugu yake.
Nilipokaa na mdogo wangu kumwuliza yeye alikana kabisa/katu katu kwamba hana tatizo nae na pia anamheshim sana kama shemeji yake,kumweleza huyu mpenzi wangu akaruka akasema ni mnafiki na wala hamaanishi hivyo,cha ajabu nimemwambia niwakutanishe yeye na mdogo wangu amekataa akisema hawezi kukaa na kubishana shemeji yake yeye atakachokifanya ni kutokuja kwangu.
JE HAPO MIMI NIFANYEJE KWANI NIKO NJIA PANDA??
nafikiria niachane nae au la kwani simwelewi ananimaanishia nini.jana nikawa nimempa hatima kua kama hawezi kuishi na ndugu zangu kwa upendo kama anaonipa mimi basi sioni sababu ya kuwa nae akanitumia msg kua NITAFUTE ATAKAE WEZA WAPENDA NDG ZANGU.
Nimekua njia panda kwani kiukweli nlikua na malengo makubwa nae coz NILIMPENDA ila naona nashindwa.
Je nifanyeje?
Mdau alie njia panda!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Pole kaka, hiyo ndo mitihani ya dunia hii. uamuzi uliofikia mi naweza sema ni makburi kwa sababu moja kubwa. maisha ya ndoa ni maisha tofauti ya u-boy na u gal friend ni maisha ya kufa na kuzikana kwa wanaoelewa maana ya ndoa.Najua kupenda ni ugonjwa mkubwa lakini kuishi kwa mtu asiyetaka ndugu zako ni azabu ya maisha yako yote.Maisha ya ndoa ni ya kuondoa ule umimi ulionao/alionao ni maisha yasiyo hitaji makuu.wasiwasi wangu ni kwamba hapo tu bado hujamuoa ,ukisha muoa si atasema huyo mdogo wako amembaka. muombe mungu akupe mke mwema.....

    ReplyDelete
  2. dada pole kwa mkasa uliokupata.rakini ukae ukijuwa.uyo mwanaume akufai,kwa mtazamo wangu mimi mdogo wako anashidwa kukuambia.inawezakana alimtaka kamkataa,jaribu kumbana mdogo wako akufamishe ukweli,uyo jamaa anaonekana muhuni,kaa jifikilie

    ReplyDelete
  3. ndugu huyo demu mchoyo atakusumbua

    ReplyDelete
  4. Pole sana ndugu yangu, lakini nakushauri utafute blog ambazo ziko kimapenzi zaidi na si blog hii. Huko utapata msaada zaidi.Ni kwa uzuri tu,si kwa ubaya kaka yangu

    ReplyDelete
  5. Kidume kama mimi kwa kesi kama hizi sitafuti msaada, dem keshaanza kuonesha ni mbinafsi...piga chini, maana akiolewa huyo ndo utajua joto ya jiwe.

    ReplyDelete
  6. acha ujinga wewe, kwanza una umri gani? kama ataacha kija kwako muache,kama anakupenda atakuja tu,
    wewe na huyo msichana hovyoooooooooooooo.

    ReplyDelete
  7. KWANI HUYU ALIYEOMBA USHAURI NI MWANAMKE AU MWANAUME KWANI MLIOMSHAURI HAPO JUU MMETOFAUTIANA
    MWINGINE AMEMUITA KAKA NA MWINGINE AMEMUITA DADA
    WHICH IS WHICH!!!!!!!!!!!!!!!!
    AAAAAHHHH!!!!!

    ReplyDelete
  8. katika maisha ya leo kitu msimamo ni muhimu zaidi usikubali kuyumbishwa sasa maana baadae utazamishwa na kupotezwa kabisa, la msingi kama anashindwa kuelewa umuhimu wa ndugu na jinsi alivyokupa hayo majibu mwache aende asikuumize kichwa ,dunia bado ina watu kibao wenye uelewa.....

    ReplyDelete
  9. i think that lady is not willing to stay with your family and you are lucky to get that feedback on earlier stage,just let that girl go her way, to hell with her she doesnt love you at all.

    she just eating your money and misusing you, let her go----gooooooo

    regards prince charles

    ReplyDelete
  10. Kaka huyo demu hakufai, tafuta mwingine. Kwanza inaonekana hicho ni sababu ya kukuacha, ameshapata mwingine na alikuwa anashindwa jinsi ya kuchomoka. Tafuta mwingine achana nae kaka.

    Big Sam

    ReplyDelete
  11. haiwezekani from nowhere mtu abadilike lazima kuna kitu tu aidha mama kamzimia mdogo wako, au unamnyima haki ya msingi kwa kisingizio cha mdogo wako. Kama haji nyumbani je mikonooooz sehemu nyingine anatembelea? au chuo kilpofungwa mshikaji wake naye karudi- yaani ulikuwa mwizi bila kujua!! tuliaaaa...itajulikana tu.. kupanik hakusaidii..chunguza utupe jibu huyo siyo mama au dada yako pengine anafanya short listing na wewe ni out katika big sister yake.Lakini uhawala hauna talaka-subiri
    Chakupewa wa Manzese

    ReplyDelete
  12. Achana na huyo msichana utapata mwingine, mdogo wako anaambiwa kiburi na hapo bado hujamuoa, ukimuoa si atamwambia mama yako kuwa ni mwanga!

    ReplyDelete
  13. Kuna vitu vya kuomba ushauri na vingine vinahitaji maamuzi binafsi!Kifupi yaonesha hauna msimamo,ushaambiwa utafute mtu atayewapenda ndugu zako lakini bado wataka ushauri!wa nini?Msingi wa ndoa ni upendo na hasa kwa ndugu.unachotaka ni kupima kati ya huyo demu na nduguzo!Katika facts hizo utapata kitu!!

    ReplyDelete
  14. huyo mpenzi wako mchoyo.. achana naye.mtu gani hataki watu..ndo watu wanaoleta vurugu kwenye familia hao..kama unaongea naye haelewi ndugu mapema aanze

    ReplyDelete
  15. Don't waste your time and energy she is not serious in love. I will not be suprise kusikia ana mtu mwingine amepata sababu.

    ReplyDelete
  16. Pole brother, Mshukuru Mungu amekuonyesha mapema jinsi huyo gal friend wako alivyo mbinafsi. kifupi huyo hakufai, jipe moyo achana nae, Mwombe Mungu atakupatia binti wa kukufaa. Naona haelewi kuwa nyie kuwa pamoja ina maana kuna familia zenu zimeungana pia. Sasa km hataki nduguzo ina maana gani kumuendekeza?? Ni ngumu ila jipe moyo Bro! Miaka miwili si mchezo..

    ReplyDelete
  17. Rafiki, Dalili ya mvua ni mawingu. Huyo hakufai kuwa mwenza wa maisha yako, atakutesa na kukutenganisha na ndugu zako kwa mapenzi yake ya kinafiki.

    ReplyDelete
  18. Pole na yanayokusibu Kaka yangu. Binafsi naona kama Mwenyezi Mungu anakuepushia jambo fulani kutoka kwa huyo dada na imekuwa jambo jema kwa wewe kuelewa mwenendo mzima baada ya ndugu yako kuja kukaa hapo na umshukuru Mungu kwa hilo maana bila ya ndugu yako kuja hapo naamini usingelijua hilo. Mimi kama mimi nakushauri kwamba ingawa ni vigumu kutoa maamuzi ukizingatia ulimtunuku kwa Moyo mmoja, Jikaze KIUME kaza roho achana nae utampata wa maana na utampenda zaidi ya huyo. Uking'ang'ana utajuta sana. Kumbuka "MAJUTO NI MJUKUU" Hakufai hata kwa mbeleko. Kwanza anaonekana Mchoyo na Mnyanyasaji na Usipoangalia hata ww atakunyanyasa achilia ndugu zako na mtu asiyependa ndugu zako basi hata ww HAKUPENDI KABISAAAAAAAAAAAA.
    Ni hayo tu kaka yangu. Nakutakia kila la heri.

    Nawire

    ReplyDelete
  19. waswahili walisema riziki mafungu saba, hilo ni moja tu; sioni hapo kama kuna uhusiano ulio wa kweli, na damu nzito kuliko maji, pima ili upate jibu- MPEMBA

    ReplyDelete
  20. Huyo ambaye hata uhakika wa ndoa hana keshaanza kuonyesha makucha saa hizi hakufai, mke akipenda na kupendwa na ndugu hata wewe utaona raha ya ile ndoa. MWACHE, wako wengi wenye tabia njema, wenye kupenda na kujali ndugu wa mume, wenye utajiri wa roho, huyo ana umasikini na ulimbukeni wa maisha. Mungu anakuonyesha kungali asubuhi, usitafute kujuta baadae.

    ReplyDelete
  21. Mimi sielewi watu wengine kaka wengine dad kwani wewe hujasema ni mwanamke au mwanaume sasa huu ushauri tunakupaje ? kama wewe ni mwanamke huyo bwana achana nae hakufai kama hapendi ndugu zako hapo ndio mnadate je mkiwa wanandoa atapiga ndugu zako marifuku kuja kwako. Na kama wewe mwanaume kaa ujishauri huyo mdogo wako ni mtu wa namna gani na huyo girkfriend ni mtu wa namna gani ? jiulize ujitafakari labda wanatakana , na kam wanatakana I suspect kutokana na reaction ya mpenzi wako basi mdogo wako amtaka shemejie !! vyovyote vile pole sana kwa kuwa mtu kati na kila la kheri.

    ReplyDelete
  22. Mimi sielewi watu wengine kaka wengine dad kwani wewe hujasema ni mwanamke au mwanaume sasa huu ushauri tunakupaje ? kama wewe ni mwanamke huyo bwana achana nae hakufai kama hapendi ndugu zako hapo ndio mnadate je mkiwa wanandoa atapiga ndugu zako marifuku kuja kwako. Na kama wewe mwanaume kaa ujishauri huyo mdogo wako ni mtu wa namna gani na huyo girkfriend ni mtu wa namna gani ? jiulize ujitafakari labda wanatakana , na kam wanatakana I suspect kutokana na reaction ya mpenzi wako basi mdogo wako amtaka shemejie !! vyovyote vile pole sana kwa kuwa mtu kati na kila la kheri.

    ReplyDelete
  23. Kaka ebu angalia mazingira unayoishi vizuri. Inawezekana mpenzi wako hapati uhuru fulani. Mfano mdogo wako analala sebuleni halafu uani ni mpaka utoke nje ya nyumba. Kuna life fulani la usela unaweza ishi mfano vyumba viwli sebule na bed room(choo ndani ya bed room) sasa ebu niambie akija mtu wa tofauti na mpenzi wako itakuwaje.

    Wengi wamechangia mi nadhani angalia pia mazingira ya kuishi hapo kwako.

    ReplyDelete
  24. wewe umerishwa rimbwata au, mtu gani huelewi, mpaka uambiweje ndo ujue kwamba hakutaki

    ReplyDelete
  25. Pole sana ndugu yangu. Hilo ni jabo ambalo inabidi ulifanyie uchunguzi na maamuzi makini sana. Kuna baadhi ya ndoa badala ya kuunganisha familia mbili za bibi na bwana zinakuwa zinatenga familia hizo eti shemeji haelewani na mawifi hivyo wasije kumsalimia kaka yao. Hii ni kwa sababu huo mdogo wako amekuja muda mfupi tena kwa dharura baada ya chuo kufungwa na mpenzi wako ameanza kasheshe, sasa mkioana itakuwa je?

    ReplyDelete
  26. kwanza,meseji yako haijakamilika!fafanua-mpenzio alilalamikia nini?na kwa nini umtume mdogo wako wa kiume sokoni wakati "mkeo mtarajiwa"yupo?pia tupe umri wa mpenzio tupime uelewa wake!
    Mwisho naona ushatoa maoni yako kuwa ULIMPENDA!sasa wataka ushauri gani au watu-joke!!!hii inaonesha kwa hili humpendi tena...

    ReplyDelete
  27. penzi na ndugu haviendani. Mtu akikupenda wewe sio lazima ajumlishe na ndugu zako. So hilo ni tatizo lako nenda tafuta mwenzio atakayependa wewe na ukoo wenu wote na wewe upende yeye na ukoo wake wote halafu muanzishe kijiji chenu

    ReplyDelete
  28. We ushapata bahati ya kujua tabia ya mpenzi wako unataka kuichezea! Ushauri wa nini sasa unataka wakati inaonekana wazi kabisa. Wenzako hawajui hayo mpaka washafunga "pingu za maisha"

    Muoe uone cha moto

    ReplyDelete
  29. Huu ni ushauri kutoka kwa mzee mwenye uzoefu wa miaka mingi ya uplayer kwanza gal friend wako akianza ugonzi bila sababu jibu lake ni>>> kapata basha mwengine nina asilimia mia na sitini kwa uzoefu huo sasa kwa ufupi tu bila kupoteza muda mtose chunvini full stop

    ReplyDelete
  30. Nauliza tena WEWE UNAETAKA USHAURI NI MWANAMKE AU MWANAUME au kwa maana nyingine huyo mpenzi wako ni MWANAMKE AU MWANAMME ??

    ReplyDelete
  31. Hakuna kumlazimisha demu hata siku moja wewe kama huna sehemu nyingine ya kupata mbembeleze ila kama unajuwa utapata mwache huyo demu kama alivyo hana mpango wa nini ataishia hivyo hivyo na hato pata mwanaume na akiangalia age yake itakwenda hatoolewa nani atakubali kumuowa mzee????Wakati wanakwenda na wakati demu akilinga unapiga chini unatulia tu unamuangalia hamna kumuomba hivi na hivi

    ReplyDelete
  32. Huyo bado hajawa mke na ana act hivyo?????? je ukimuoa....!!!!!!! Mimi ni mwanamke lakini nakwamba ...dump her.

    Ndio tunajua ndugu wamezidi kwa kuhamia kwa kaka zao na dada zao na kuextend their welcome mfano wanyakyusa wakija kusalimu hawaondoki lakini huyo mdogo wako ni temporary thing na pia huyo mwanammke anayekuja kukaa over the weekend tu lakini hawawezi kukaa na ndugu yako jiulize akihamia hapo itakuaje?

    Mwamini mdogo wako kwa mara hii ya kwanza, lakini ukipata mwingine ukasikia na huyo anasema hivyo basi itakua mdogo wako ndio mmbaya lakini for now huyo mwanamke si ameshakupa ruhusa kutafuta mtu atakayependa ndugu zako. Go for it .....

    ReplyDelete
  33. Ndg ndg hawa Gozi gozi, wewe utakuwa humpi nafasi huyo mpenzi kama zamani, kwa hiyo anaona unamsahau, mpe hela mdogo wako akatembee mbali wakati mkiwa na mpenzi, arudi baadae, kwa hiyo mtakuwa na nafasi nyie wawili. Chuo kikifunguliwa basi mambo yatakuwa poa.JUA TATIZO KWANZA ILI UPATE DAWA.

    ReplyDelete
  34. Mie ndiye huyo dada anayedaiwa kutopenda ndugu wa mpenzi wake.Cha kusikitisha ni kwamba story nzima haijawekwa wazi,na ndio maana watu wametoa comments nsizostahili.
    Hilo suala lenyewe la kumwambia atafute mtu apendaye nduguze alisema yeye nami nikajibu kwamba kama anaona mie sifai labda atafute huyo anaefaa huku nikisisitiza kwamba mie ntakuwa namsubiri kwani bado nampenda.
    Najua kupata mwenza ni rahisi sana, lakini kumpata huyo mnayeshibana ni nadra hivyo ingawa sikutegemea kama nlipomwambia aombe ushauri angetumia globu hii imibidi nami niweke sawa baadhi ya mambo.
    Shemeji yangu haja wahi kunitongoza hata siku moja tena namtreat kama mdogo wangu,kwani nina mdogo kama yeye.Mara nyingi amekuwa akifanya vitu vya UCHONGANISHI,DHARAU au MAUDHI lakini nkawa namezea kwani nlijua kabisa mwisho wa siku ningeonekana mie mbaya.Siku ya tukio nimefika kwa mpenzi wangu nkamkuta shemeji akanigombeza kama mdogo wake kwamba mie naharibu pc ya kakake.UONGO MBAYA KUUNGANISHA NA HAYO MENGINE ILINTIA HASIRA BUT NKASEMA NTASHIT TENA KAMA SIKU NYINGNE.
    ILIJUWA MIDA YA LUNCH NKAONA NIMUULIZE MPENZI WANGU ATAKULA NINI KWANI ALIKUWA AMEOKA,HAKUJIBU NA ALIPORUDI AKAENDA STRAIGHT KWA MDOGO WAKE AKAANZA KUMPA MAAGIZO ANUNUNE NINI KWA KUPIKA.KWA KWELI KAMA MWANA MKE ,KWANGU NLIONA KAMA KANIDHARUA HASA UKIZINGATIA MDOGO WAKE NAE KATOKA KUNIUDI.KWA HASIRA TUKARUSHIANA MANENO.AKASEMA ANANIACHA ATAFUTE ANAYEPENDA NDUGUZE!
    sikutaka nikutanishwe na shem kwani sio hulka yangu kusutana hasa na ndugu ya mpenzi wangu mapema hivi!Kama anainsist basi ntafanya hivyo kwani inaudhi kutafsiriwa kamadada asiyependa mashemeji.
    TATIZO LANGU KUBWA NI HII BETRAYAL AMBAYO NAIONA KWAKE,INAONEKANA ANAMUAMINI MDOGO WAKE 100% HICHO NDICHO KILICHONIFANYA NIVULIE YOTE.HUYO SHEMEJI YANGU MWENYEWE SHAHIDI HATA ANIPE MANENO YAKUNIBORE VIPI HATA SIKU MOJA SIJAWAHI KUREACT!
    NIMESOMA COMMENTS NYINGI NADHANI WENGI WALIOZITUMA HAWAUJUI UKWELI HALISI NKAONA NI JUKUMU LANGU KUELEZEA UPANDE WANGU PIA.NASISITIZA BADO NAMPENDA HUYU KAKA INGAWA YEYE ANAONGELEA WAKATI ULIOPITA NA HAPO NDO NASHANGAA YOTE TULIYOPITIA KWAKE HAYANA UZITO.SIWEZI KUMFUNGA KAMBA ABAKI NAMI,SO NNACHOSEMA NI KWAMBA AENDE AKIJUAN HILO KAMA ANATAKA SHEM AWE CHANZO CHA SIE KUTENGANA.
    MIE SIO CHIZI AU PUNGUANI NKURUPUKE TU SIKU MOJA NIANZE KUBWATA

    ReplyDelete
  35. Pole dada, mapenzi Bongo ni magumu hasa inapokuja suala la extended family. Wenzetu wana swali moja zuri sana wanalopenda kuuliza unapoingia tu, "WHAT TIME ARE YOU LEAVING" Hata watoto watapenda kukuuliza maanake unawaharibia ustaarabu wao na jibu langu linakuwaga I moved In. Kuna kibarua kigumu mbele kinakuja maanake wifi, wakwe, babu, wajomba, shangazi, harusi na misiba, ngombe, mbuzi, kuku na mashamba. Ni kazi

    ReplyDelete
  36. pole sana kaka huyo hamta wezana kabisa muombe muumba wako akupe mke mwema.

    sweet
    Arusha

    ReplyDelete
  37. HABARI YAKO INAWEZA KUWA UMEFICHA MAMBO FULANI, HAWEZI KUKASIRIKA KWA WEWE KUMPA MDOGO WAKO PESA YA KUNUNUWA VITU VYA KUTUMIA HAPO NYUMBANI, WEWE NI MUONGO.

    ReplyDelete
  38. kaka.Wadem wengi ndivyo walivyo.kwa si wenye ndoa tunajua hilo.wanaona shida sana kukaa na ndugu zako ila kukaa na ndugu zake ni poa.wadau mtakubaliana na mimi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...