Michuzi Kaka!
tafadhali naomba nitumie kama kuna web ya kuagalia tv za bongo live namiss home sana mimi niko usa. miaka 13.sasa naona kiswahili changu kinapotea na pia napenda kuona tv za nyumbani kwa habari zaidi asante.
Mdau Missouri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. sasa wewe unawachokoza waosha vinywa, kukaa miaka 13 usa haimaanishi kusahau luga yako uliozaliwa nayo, anyway ngoja niwasubiri waosha vinywa watakavyokupa msaada.

    ReplyDelete
  2. oya chungulia dullonet.com
    cku njema

    ReplyDelete
  3. Kinachokuzuia usiende nyumbani kwa muda wa miaka yote 13 ni nini?, au ndiyo nyie mlie ingia lakini hamuwezi kutoka mpaka siku ya kurudishwa na escort?. Pole sana.

    ReplyDelete
  4. eastafricantube.com

    ReplyDelete
  5. we mchangiaji uliopita hapo juu inaonekana hujawahi kusafiri basi hata kama ushasafiri basi hujawahi kukaa sehemu ambayo haizungumzi lugha yako native kw mda mrefu mimi naishi nci fulani lakini sio usa nimeishi hapa zaidi ya miaka minne lakini siku nilipo rudi bongo kiswahili changu cha kuongea kilikuwa cha kizushi kiaina sasa kwa mshikaji aliye kaa miaka kumi na tatu lazima asahau mimi najua hiyo kitu. basi ndo hayo mdau nataka kuku elewesha kama hujui.

    ReplyDelete
  6. Mimi namuunga mkono mtoa maoni wa mwanzo.kuishi miaka 13 huwezi kusahau lugha yako hata siku moja,labda uwe ume america tangu mdogo,lakini kama umekwenda umri kuanzia miaka 20 kwenda mbele sifikirii kama utasahau kiswahili.Mbona umekandika kiswahili vivuri tu,kwani kama lugha imeanza kukupotea hata kuiandika ungeiandika kimakosa,kwa hiyo usituzuge bwana.

    ReplyDelete
  7. wewe ulieuliza pamoja na mchangiaji wa nne nyooote ni waongo
    watu wako huku tangu miaka ya sitini na wanazungumza kiswahili safi tu na hata watoto wao waliozaa huku pia kiswahili chao safi tu sembuse wewe miaka minne na miaka 13 ndio mmeshaona ni miiiiiiiiiiiiingi sana ya kua huwezi kuzungumza vizuri sema tu kama ndio nyinyi mnaotupa jongoo na mti wake......usiache mbachao kwa mswala upitao

    ReplyDelete
  8. sasa wajemeni mimi nikitoka huku kijijini nienda darisalamu ambako hawaongei lugha yangu ya kijijini inamaana siwezi kuongea tena kimakonde, kinyakyusa kihehe kibena, kingoni, kikinga, kimasai, kisukuma, du basi hiyo kali. hebu niende nikafunge mbuzi wangu wasije wakatoroka
    asante sana
    ni mimi yule yule Mkulima

    ReplyDelete
  9. mnaojifanya kusahau kiswahili acheni uzushi.sehemu gani duniani hapa ambako hakuna wabongo????pumbavu sana.miaka 13 US ndo uogope kusahau lugha?wabongo wamejaa kila kona ya USA.ina maana wewe ni kipusa kiasi gani hadi ukose kuonana/kuongea na wabongo kwa style yoyote??eti kiswahili kinapotea.mbona umeandika kwa ufasaha kabisa.acha kuwa mbumbumbu wa kinywa!!!!!
    binafsi niko away from bongo for sometime na kila ninapopiga CM na kuongea na maskani wanashangaa jinsi ninavyo keep update na lugha yetu.m2 mzima,LKN Ovyooooooo!!!!!!

    ReplyDelete
  10. sasa kakuzuwia nani kurudi nyumbani ama ndio ukitoka kuingia tena unaishi kimazishi fanya uje usije ukakuta ukoo wako wote umekwisha

    ReplyDelete
  11. ACHA KUDANGANYA WEWE, WATU TUMEKUJA HUKU MIAKA 20 SASA NA WALA HATUKUTANI NA WASWAHILI NA BADO TUNAONGEA KISWAHILI.KISWAHILI AU LUGHA YEYOTE HAIPOTEI UNLESS UMEENDA SEHEMU UKIWA MDOGO BUT BY 16 YEARS OLD YOU SHOULD BE ABLE TO SPEAK YOUR LANGUAGE YOUR COGNITIVE FUNCTION IS MUTURE BY THAT TIME. KWAHIYO TUONDOLEE USHAMBA SASA HIVI , WEWE NDIO WALE WANAOJIDAI KUONGEA SLANG WITH ACCENT! AND IT SOUND SO BAD! GROW UP!!!!!!

    ReplyDelete
  12. jamani msimshambulie saana mtoa maada........lugha hukua na hufa,kuna maneno mapya kibao yakiswahili na kama mtu hupo pamoja na watu hom kwa miaaka basi siajabu kuuliza hivi neno fulani maana yake nini,yeye hakusema hajui kiswhili ila kinapotea na yawezekana kimtindo....by usinijue1

    ReplyDelete
  13. Nionavyo nyote; watoa maoni na aliyeko tutani, mko sahihi ila mnshindwa kupresent ideas zenu (kiswanglish hicho). Kimsingi, mwenzetu:
    1.anamisi kiswahili;
    2.anamisi matukio ya nyumbani;
    3.anatamani live-mishemishe za bongo;
    4.ANAMISI 'UPDATES' za lugha ya Kiswahili kwa kuwa
    a)Kiswahili kinakua kwani
    b)ni lugha pijimi,

    Kukaa miaka kumi na mitatu sio kwamba utasahau lugha yako bali utamisi updates na lafudhi itapwaya kiaina.

    KUHUSU TV ndugu yangu unachopaswa kufahamu ni kwamba kwa sasa tunajikongoja kutoka mifumo ya ANALOG kwenda DIGITAL. Wataalamu wa haya mambo wanaweza kukueleza zaidi ninachotaka kupresent. Tehehe!

    Mbarikiwa nyote,

    SAUTI ole NYIKANI

    ReplyDelete
  14. Heee watu wanamsupport huyu mtu kuwa ni kweli ameshahau kiswahili wote ni hao hao..

    MImi nipo hapa toka 5 yrs old. Na tunakoishi hakuna watu wengi wakiswahili. Na sas hivi niko in my early 40's. Kwenda Tanzania na kukaa sana ni 4 weeks tu, mara zingine zote ni week tatu au mbili. Na niliwahi somea form one and two kule. Lakini kiswahili changu hakitapotea.

    Na watoto wangu hata hawajakanyaga bado Tanzania na wanasikia lakini kujibu ndio hawawezi bado.

    Hawa watu wanaofanya hivyo nawaonaga wengi tu lakini rohoni naona ni kujidhalilisha na kukataa kwenu. Kama tena mtu umeondoka mkubwa kusahau lugha yako ni utumwa. Najua kuna slangs nyingi sitazielewa lakini kuongea kiswahili ati nimesahau nitakuwa muongo. Nakubali accent ni tofauti kidogo lakini naongea fluent and I am proud of it. Najuatia sana kuwa siwezi kuongea kichagga na kipare ambazo ni lugha za wazazi. Lakini Mtu akiongea nasikia pia.

    Wachina, wahindi watoto wao hata hawajui kwao lakini wanajua lugha yao.

    ReplyDelete
  15. Jamani mtu kaomba msaada mnamshambulia kama huwezi kumsaidia usimshutumu sisi hatujui mazingira anayoishi kiswahili bado anajua ndio maana akaandika ombi lake kwa kiswahili.

    ReplyDelete
  16. kimsingi haimaanishi kusahau kabisa, ila kiaina unakuwa unaingiza vitu visivyo .
    Hii inatokea hata kama ukiishi Dar miaka 13 bila kuongea lugha ya kijijni kwenu . ukirudi lazima utachapia kiaina , kweli sio kweli ?

    ReplyDelete
  17. Pole ndugu yangu! Kama ungeweka jina lako ningesema wewe u limbukeni lakini hukuweka jina naamini una shida ya dhati. Kuna wakati Star TV ilikuwa inapatikana kupitia mtandao fulani siukumbuki lakini kulikuwa na maelezo kuwa ni kulipia. Niliwahi kujaribu kulipia lakini sikufanikiwa na sikujaribu tena. Labda ujaribu kuingiza jina lao kama utaweza kufanikiwa!

    ReplyDelete
  18. nyamafu kabisa,,,ata uishi miaka 80 nje huwezi sahau lugha yenu tena kisw!!wazungu fulani wa scandinavia wanaongea kiswaili vizuri tu wala hawajawai ishi bongo toka vizazi,,,limbukeni kbs.wachina,wahidni,waarabu waliozaliwa miiida uropa hawasahau lugha yao kbs,,,haijalishi unaishi USA mtaa gan sijui usio na waswahili wezio ina mana una contacts na mswazi yoyote??
    fix tu na wataka watu tuongee tu!!!JAMANI UMASKINI WA FIKRA WA WATU WATOKAO NCHI MASKINI SANA ZA AFRIKA

    ReplyDelete
  19. KAMA NI HICHO KISWAHILI MBONA CHIBILITI ANAONGEA VIZURI TU...... NA TEMNA KARIBIA ATAMLETA OBAMA NA YEYE HUKO ITALI NA KISWAHILI ATAJUA

    ReplyDelete
  20. waosha vinywa bwana.. embu acheni kurarapa hapa,mtu kaulizia website,mpeni kama hamjui shut it and get to steppin.. SASA ANASAHAU KISWAHILI,UTAKE USITAKE HIYO NI SHIDA YAKO,YEYE HAIMWONGEZEI WALA KUMPUNGUZIA KITU.. MEDIA OF COMMUNICATION IN HIS HOUSE IS ENGLISH,AT WORK ENGLISH ETC.. ACHENI KUCHONGA TU

    ReplyDelete
  21. Acha makuzi dogo..! huku mbele tupo tunaishi na wazungu ambao walikuwa huko enzi za ukoloni miaka ya 50/60 na mpaka sasa bado wanapiga kiswahili fresh leo hii ndo ije wewe....! uliyezaliwa unaongea kiswahili usahau...

    ReplyDelete
  22. Hey,nyie wabongo vipi ??mbona mnapoteza point.....mtu kauliza wapi atapata ona tv. akiwa abroad, lakini miaka 13 mnafanya ishu ya msingi.asahau asisahau haiwahusu,ukikaa na wapanda ngamia lazima upande ngamia,ukikaa na Wadenish lazima uwe Mdenish,wabeoriginal lazima uwe ivo,wakerewe lazima uwe mkerewe.acheni hizo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...