Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italy ndugu Abdulrahaman A.Alli kwa masikitiko anawatangazia wazazi na watanzania wote Italy na popote anapofahamika marehemu kuwa: ABDALLAH MJUME aka DULLAH au Jr, (pichani) amefariki leo jumapili asubuhi katika nyumba aliyokuwa akiishi.
Sababu ya kifo chake bado haijajulikana,ila taarifa fupi kutoka kwa watu waliokuwa nae inasema kuwa Dullah alikuwa Disco kabla ya kufariki.
Wakati huo huo Katibu wa jumuiya ya watanzania anawatangazia watanzania wote wanaoishi Napoli kuwa kutakuwa na mkutano siku ya jumatatu saa kumi jioni kwa ajili ya taarifa kamili ya msiba na mipango ya mazishi,wote mnatakiwa kufika bila kukosa.
(INALILLAH WAINA ILAH-RAJ'UN)
RIP.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mungu aiweke roho yake pahala inapostahiki. Aamin.

    ReplyDelete
  2. R.I.P ABDALLA MJUME U'LL BE MISSED DEARLY BY UR FELLOW LOYOLITES AND ST. MARYS CREW! LOVE YOU ALWAYS! UR IN A BETTER PLACE NOW! MWAH

    XXX

    ReplyDelete
  3. ABDALLAh??DULLAH??siamini! nimesoma na wewe loyola ulikuwa mtu fresh sana abdallah we wil really miss u homie abdalah abdalah Mungu akulaze mahali pema abdalah jamani what happened to him?naombeni majibu siamini sitaki kuamini.. MUNGU AKULAZE mAHALI PEMA PEPONI.
    J!

    ReplyDelete
  4. Mwenyezi Mungu aliyemuumba ABDALLAH MJUME aka DULLAH au Jr, hatimaye amemrudisha kwake.
    Bwana alitoa, na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen

    ReplyDelete
  5. JAMANI,PAMOJA NA MSIKITIKO YENU,JAMAA WA ITALY WANATAFUTA WATU WANAOMJUA AU NDUGU ZAKE ILI WAWAPE TAARIFA,KAMA UNAJUA NDUGU ZAKE AU UMESOMA NAE MAJULISHENI BASI

    ReplyDelete
  6. mungu alize mahali pema peponi roho ya wajna wangu abdallah

    ReplyDelete
  7. Wow! Anony 1:15 Ina maana ndugu zao bado walikua hawajaambiwa???!!!!!

    Sasa kwanini walikimbiza matangazo kwenye blog? Yaani alifariki jumapili na jumapili wakaweka tangazo huku. Hii sio vyema kweli kama ingekua week kadhaa hawajapata ndugu zao ndio wangeweka huku. Just within few hours imagine huyo aliyeleta habari huku haraka haraka akipata habari msiba za ndugu zake kupitia kwa blog atajisikiaje?

    Kweli misiba inatufanya tuchanganyikiwe lakini wakati mwingine tunatakiwa kufikiria kabla ya kufanya kitu.

    RIP

    ReplyDelete
  8. Annon 1:46am kweli umenishangaza! Sasa tatizo liko wapi kuweka info humu kabla ya kuwafikia nyumbani?! hii ni Blog ya jamii na moja ya kazi za Blog kama hizi za Michuzi ni 'kutoa taarifa' kuna manufaa zaidi kutumia njia kama hizi kufikisha habari kila kona ya Dunia, meaning kama kwao walikuwa hawajui basi i am sure sasa wanajua na nina hakika kuwa haikuchukua muda mrefu kwa mtu kuwafikishia taarifa kuwa tumeona msiba online. NI njia ya taarifa tu, i dont understand why it should be a negative thing. Please step out of the box and appreciate the fast means of Technology that we have access to!! Its a sad situation however very necessary to get the message across.
    RIP Dullah, I knew you from Loyola, you were a cool guy.

    God Bless.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...