Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akifungua ofisi ya Chama cha wafanyabiashara wa mafuta nchini (TAOMAC) iliyopo katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Krishnaprasad Rai. Picha na Anna Nkinda wa Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Wapunguze bei za mafuta.

    ReplyDelete
  2. hiki chama kitawasidia kutetea maslahi yao kama kuongeza bei mafuta, kupiga chua (kuchanganya na kerosine)

    ReplyDelete
  3. Mi nadhani lengo Kuu la umoja huu ni kuhakikisha kwamba maslahi ya hawa mabepali wachache wanayalinda na inasikitisha kuona muheshimiwa waziri yupo bega kwa bega kuwasaidia.EWURA wako wapi, ushuru wanaochukua wa shs 7 kwa kila lita ya mafuta wanazitumia kwa kazi gani? Ushauri wangu wa bure ni hii EWURA ifutwe na badala yake kiundwe kitengo maalum chini ya Ofisi ya Rais kitakachoshughulikia bei za nishati mabambali nchini.

    Ahsante...

    ReplyDelete
  4. Tunashukuru sana make inaonekana kazi kubwa ya viongozi hapo bongo ni uzinduzi tu na baada ya uzinduzi hakuna ufuatiliaji wa walichokizindua. Sasa naomba tumkumbushe Ngereja awaambie waweke bayana majukumu yao ili tuweze kutathimini utendaji wao wa kazi hasa SUALA ZIMA LA KUPUNGUZA BEI YA MAFUTA.

    CHANGARAWE

    ReplyDelete
  5. Yaani hao jamaa pamoja na kutukamua wameamua waunde na umoja kabisa ili wamng'oe meno EWURA.
    Waache tamaa wawapunguzie wananchi machungu ya maisha

    Mdau Oslo Norway

    ReplyDelete
  6. hawa bei ya mafuta imeshuka toka 147USD per barell mpaka 49USD per barell wao wanapunguza bei kwa shillingi moja kwa lita!

    ReplyDelete
  7. mafuta kwenye soko la dunia yameshuka bei lakini hawa wafanyabiashara wanaouza bongo hawataki kushusha
    EWURA walitoa tamko la kuwataka washushe but utekelezaji ni zero. Kwanza EWURA wenyewe wanakula na hawa wafanyabiashara
    muhimu ni Serikali kuiruhusu TPDC kufanya biashara ya mafuta, kila siku nawasikia bingeni wakisema kuhusu suala hilo bt utekelezaji ni zero then waziri anaenda kufungua ofisi ya wasanii hao!!!!ujue hapo kishapewa bahasha ya khaki
    bongo kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  8. Ina maana huyu ndugu anahalalisha huu ukiritimba na unyonyaji wa hawa walanguzi wa mafuta?

    ReplyDelete
  9. Naamini hili la bei ya mafuta kuna wengi hata wanashindwa kunena kwa sababu ya hasira. Kwa kifupi bei ya mafuta ishushwe, na nauli za daladala zishushwe. Kwa nini maisha ya mtanzania yazidi kuwa magumu kila siku?

    ReplyDelete
  10. NAULI ZA DALADALA ZISHUSHWE! TUKIWAAMBIA MAFUTA YASHUSHWE HAMSIKII, MNAZIBA MASIKIO HATA PALE AMBAPO BEI KWENYE SOKO LA DUNIA IKO CHINI. ILIPOPANDA KWA ASILIMIA 5 MNAPANDISHA NAULI KWA ASILIMIA 19. HAYA NDIYO MAISHA BORA?EWURA IS JUST LIKE A BULLDOG WITH NO TEETH.

    ReplyDelete
  11. Hapo hakuna kitu, hawa jamaa wanaanzisha ka OPEC kao kadogo hapa TZ ili waendelee kutunyonya. mafuta yameshuka kutoka pipa dola 147 mpaka dola 47 wao wanatuuzia bei juu bado. yani mafuta marekani (wenye per capita income Usd 43,000) ni cheaper (sh.700 kwa lita)kuliko bongo(per capita usd 300)lita sh.1500. hii ni dhambi jamani.Ukiuliza eti walinunua zamani, je hao wamarekani walinunua lini???

    ReplyDelete
  12. kaaazi kweli-kweli
    sijui tuwe viongozi???yan apo keshabeba chake wengine wajiju
    end of movie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...