Waziri wa Utalii Mh. Shamsa Mwangunga akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa London Tax 100 zinataokuwa na matangazo ya Tanzania kwa miezi sita. Kilemba cha njano ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, Bi Blandina Nyoni. Sherehe hizo zilifanyika katika sehemu ya watalii ya London Eye.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Peter Mwenguo kulia akiwa na Mkurugenzi wa masoko, Bw. Mcha katika picha ya pamoja huku nyuma likionekana tangazo la Tanzania lilolokuwa katika kituo hca treni cha Victoria, London.

Na Mwandishi Maalum
SERIKALI ya Tanzania imezindua kampeni kubwa ya matangazo ya utalii kwenye vituo vya treni ya chini ya ardhi na London tax nchini Uingereza yaligharimu Sh.milioni 800, yatatakayodumu kwa miezi sita.

Katika uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwanguga, katikati ya jiji la London katika sehemu ya maarufu ya watalii ya "London Eye" iliyopo karibu na ukumbi wa bunge la Ungereza.

Waziri Mwangunga alikata utepe kwenye tax mbili zenye matangazo hayo zilizokuwa katika eneo hilo, kuashilia kuzinduliwa rasmi kwa tangaz hilo na baada ya hapo na ujumbe wake walikwenda katika kituo kikubwa cha treni cha Victoria kuangalia moja ya matangazo ya vituo vya treni.

Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Publications, Bw.Juma Pinto iliyoratibu matangazo hayo alisema Serikali imelipia matangazo 25 tu kwenye vituo vya treni, lakini imepata matangazo ya ziada kwenye vituo vitano zaidi na kufanya matangazo hayo makubwa kufikia 30.

Bw. Pinto alisema kampuni ya CBS inayoratibu matangazo hayo ya vituo vya treni imetoa matangazo mengine 15 kwenye vituo vya treni ya DLR na matangazo 1,000 ndani ya treni.Matangazo hayo yote yatadumu kwa miezi mitatu.
Mkurugenzi huyo wa Jambo alisema matangazo mengine yaliyopo kwenye mkataba huo ni London Tax 100 "Black Cab" na matangazo 200 yatakakuwa ndani ya hizo tax yametolewa bure.Matangazo hayo ya London Tax yatadumu kwa miezi sita na yanatarajiwa kumalizika mwezi Mei mwakani.

Awali mwaka mwaka huu mwezi Machi, Tanzania iliweka matangazo 100 kwenye mabasi ya London na matangazo sita katika uwanja wa ndege wa Heathrow, lakini baadhi ya watu wakidai kuwa hakuna matangazo yoyote yaliwekwa London.

"Mimi nadhani wanasiasa walikuwa wanataka kucheza mchezo wao mchafu kwenye haya matangazo, jambo ambalo haliingi akilini kusema kuwa hakuna matangazo wakati hadi leo kuna matangazo yetu pale Heathrow," alisema Bw. Pinto.
Alisema mwezi mMachi mwaka huu Serikali ililipia matangazo manne na tukaongezewe mawili na kuwa sita pale sehemu ya kuchukulia mizigo termian 4, matangazo yale yalikuwa yaishe mwezi Julai mwaka huu, hadi leo matangazo yapo na ndio yaliyoghalimu pesa nyingi.

"Haya matangazo ya Tanzania tunayafanya kwa umakini mkubwa kama daktari anaemfanyia mgonjwa operasheni, lakini kila siku panapokuwa na ukweli uongo unajitenga, sisi tunaendelea na kazi na watafute lingine," alisema Bw. Pinto.
Akizungumza katika uzinduzi kampeni hiyo, Waziri shamsa alisema Serikali ilishaweka bajeti yake ya matangazo tangu mwaka uliopita wa fedha na sasa kinachofanyika ni utekelezaji.
Waziri shamsa alisema awali Serikali ilizindua kampeni kama hii kule Marekani mapema mwezi uliopita kwenye televisheni ya CNN, hivyo awamu iliyobaki ilikuwa ni Ulaya na kuichagua Uingereza.matunda ya matangazo hayo yameanza kuonekana baada ya Marekani sasa kuongoza kupeleka watalii badala ya uingereza.

Alisema hivi sasa Tanzania imeamua kujitangaza na kuvitangaza vivutio vyake katika kuhakikisha tunapata watalii wengi zaidi ili tuweze kuongeza pato la Taifa na pia matangazo kama haya yanatumika kuitangaza nchi pia.

"Kweli tunaishukuru sana kampuni ya Jambo Publications kwa kutufanyia kazi hii, kweli imefanyika kama sisi tulivyotaka na tuna imani hata huko siku za baadae tutaendelea kufanya nao kazi na hata kama kulikuwa na matatizo kidogo basi ya kibinadamu tu, alisema Waziri Shamsa.

Alisema Serikali inakusudia kuongeza matangazo zaidi ya utalii kwa duniani kwa sababu imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya pato la Taifa kutokana na watalii wengi sasa wanaongia nchini, hali inayofanya idadi yao kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Alitoa tathmini ya watalii wa Uingereza wanaotembelea Tanzania alisema mwaka 1997 walifika watalii 25,000 hadi 2006 walifika 69,160 na mwaka 2007 idadi hiyo iliongezeka na kuamini idadi hiyo itaongeza mwaka huu.

"Tutashilikiana na balozi zetu kuhakikisha tunafanya juhudi kubwa za kuhakikisha tunafanikiwa katika kuutangaza utalii na kuna mikakati mingi tumeifanya na sasa ni utekelezaji wake unaendelea," alisema Blandina Nyoni.

Alisema sasa wanaelekeza nguvu kwa nchi za Ulaya na hapa Uingereza ndiyo sehemu muhimu hapa Ulaya, kwani ndiyo nchi ambayo inapokea wageni wengi kuliko nchi nyingine yoyote hapa Ulaya, hivyo kujitangaza hapa ni sawa na kujitangaza duniani.

Awali Balozi wa Tanzania Uingereza, Mwanaidi Senare Maajar alisema tayari ubalozi wake umekuwa ukifanya kazi kwa karibu na wizara ya utalii tangu mwaka jana.Balozi Maajar alisema Uingereza ni ufunguo muhimu katika sekta ya utalii wa Tanzania, hivyo wameweka mikakati mikubwa ya kufanyia kazi soko la utalii ili kuongeza idadi ya watalii na pia lengo la pili ni kuitangaza Tanzania.

"Tanzania tuna vivutio vingi sana ambavyo vinahitajika kutangazwa,na haya yaliyotangazwa katika matangazo ya sasa ni vichache tu kati ya vivutio vingi,serikali yetu inafuata misingi ya demokrasia na hata hali ya kisiasa ni nzuri na wananchi wake wana upendo mkubwa sana," alisema Balozi Maajar.

Mbali na Waziri Shamsa,Balozi Maajr, wengine waliohudhulia uzinduzi huo ni Katika Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi Blandina Nyoni, Mkurugnezi Mkuu wa Bodi ya Utalii, Bw. Peter Mwenguo, Balozi Msaidizi,Bw.Chabaka Kilumanga,Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Bw.Gerald Bigurube wa Tanzania na kundi zima la utamaduni la sisi Tambala.

Baada ya shughuli hiyo ya uzinduzi, Bazozi Maajar aliandaa tafrija fupi ya chakula cha mchana ubalozini na baadae kutoa utambulisho kwa Waziri kwa wafanyakazi wa ubalozi na wale kampuni ya Jambo Publications na baadae Katibu mkuu, Blandina Nyoni kutoa utambulisho kwa msafara wa wizara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. I was very happy to see one of these adverts at Angel station last week; couldn't believe my eyes and guess what.... I was with my 2 friends who have already booked their holiday to Tanzania as they got motivated from the lion and masaai man on that ad; it works!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Tumechelewa sana. lakini kawia ufike. Anyway.

    ReplyDelete
  3. Mimi nina swali moja kwa wausika. Katika miaka hii tangu Mh. JK achukue madaraka tumeona new strategy katika sector ya utalii, nayo ni kunadi source zetu za utalii katika nchi za magharib.

    Miezi michache nikiwa kazini asubuhi niliona Tangazo la Tanzania kwenye CCM moring news with John Robert. Swali langu ni JEE HII MBINU INAFANYA KAZI? NAKAMA INAFANYA KAZI JEE WANANCHI TUNAWEZA KUONA VIPI KAMA INAFANYA KAZI? NA KAMA HAKUNA ANAEJUA KAMA INAFANYA KAZI AU LAA JEE KWA NINI TUNAENDELEA KUSUNK IN COST AMBAZO HATUWEZI KUZIRECOVER?

    Chumi wa Texas

    ReplyDelete
  4. HIYO PICHA YA CNINI YA VICTORIA NILIIONA JUZI BADO KIDOGO TU NIIPIGE PICHA NIKUTUMIE MISUPU LKN KUMBE NIMEWAHIWA

    ReplyDelete
  5. BIG UP SERIKALI NA NAOMBA KUISHAURI IFANYE MATANGAZO KWENYE CHANEL KAMA BBC WORLID NEWS MANAKE ILE INAONEKANA DUNIA NZIMA VILE VILE

    ReplyDelete
  6. We Chumi wa texas acha ushamba wako na box zako. Unataka uone kama inafanya kazi ili iwe nini?!! Hiyo ni advert kama zingine zote na zinafanya kazi sana. Mwaka jana tumewazidi kenya kwa watalii na kipato cha utalii. Moja ya indicators.

    Indicator nyingine wewe rudi bongo uombe kazi hoteli. Ziko za kumwaga

    ReplyDelete
  7. Hapo hamna lolote ni kuendeleza wimbi la epa tu hivi tumekuwa bora hata madudu tunatangaza utalii kwa gharama kubwa huku tunako waitia waje pakulala hapana miujiza wacha wachote tu wakikeseana watashikana uchawi na kujitia kufikishana mahakamani kisutu kama waloanza kufikishwa ni epa tu haman kitu hapo kuleni lakini muwakumbike na wenzenu huku mkiwanyima watakwenda kwa husea na kisha tuzungwe tunawafikisha mahakamani

    ReplyDelete
  8. Pamoja na kutoa pongezi kwa jitihada zote hizo lakini litakuwa jambo la maana zaidi kwa watanzania wote iwapo katika kutoa Taarifa za Kuongezeka kwa Idadi ya Watalii wanaokuja hapa nchini pia Watanzania watapenda kujulishwa Ni Mapato kiasi gani yaliyopatikana kutoka kwa watalii hao waliokuja nchini,watalii waliingiza kiasi gani katika Pato la taifa,watanzania wangapi walipata ajira katika sekta ya utalii,mahoteli mangapi ya kitalii ya kisasa yalijengwa(tourist hotels occupancy rate and bed capacity).Taarifa ya aina hiyo itatoa mwanga zaidi ya mwelekeo wa mafanikio ya sekta ya Utalii nchini.Vinginevyo,watalii wataongezeka kuja nchini,kumbe sehemu kubwa ya mapato yake yataishia mifukoni mwa wafanya biashara walioko nje ya nchi!Mimi ni mtazamaji mzuri sana wa CNN.Sijapata kuona hata siku moja tangazo la tanzania kuhusu utalii katika CNN INTERNATIONAL!kuna faida gani ya kuweka matangazo katika channel ya CNN ambayo huku nyumbani haionekani?Huu si ulaghai mtupu?Be more serious!Biashara ya Utalii ina ushindani sana kimataifa.Ile tabia yetu ya KISWAHILI ya yaani yaani haitakiwi katika Utalii!All the same I wish you all the Most of Success!

    ReplyDelete
  9. Ni hatua nzuri katika kunadi vyanzo vya utalii nchini.
    Majirani zetu wa Kenya na nchi za mbali kama Afrika Kusini wamekuwa wananadi vyanzo hivi kwa maslahi binafsi.
    Kinachotakiwa kufayika sasa ni kuboresha huduma za mahoteli, Tanzania ina hoteli chache sana. Kuboresha miundombinu na usafiri kufika katika mbuga zetu na mwisho kuwafundisha wazalendo jinsi ya kuendesha huduma ya utalii.
    Pole pole tutafika.
    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  10. Naipongeza wizara ya utalii ya Tanzania pamoja na wadau wote wanaofanikisha haya matangazo kwani hii itatusaidia sisi tuliopo nje kuifafanua tanzania pamoja na vivutio vyake.
    Pamoja na hayo ningewaomba waanze kuboresha utalii wa ndani nikiwa na maana watanzania wahamsishwe kutembelea vivutio vyetu kwani hii itasaidia sana ktk kuongeza mzunguko wa pesa katika maeneo ya vijijini pamoja na miji midogo na hivyo kuongeza vipato vya watu. Nasema hivyo kwa sababu watanzania wengi wanauwezo wa kusafiri kutoka mkoa 1 kwenda mwingine lakini wengi wetu utalii wetu ni kwenda Dar badala ya mikoa mingine. Mwisho kwa mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya nanihii, naomba ikiwezekana uanzishe mpango maalumu wa kuwahamasisha wadau wa blog hii kufanya utaliii(mfano unaweza kuruhusu mpambano wa picha za vivutio vya utalii kutoka mikoa, wilaya etc,....). Najua hii kazi unaifanya kila siku kwani picha zako za veksheni ni namna ya kutanga sehemu za vivutio, ila nakuomba wewe kama balozi wa nanii utumie mbinu zako za kibalozi ili tuwe na spidi kubwa ktk kuongeza mzungoko wa fedha ndani ya nchi na hivyo kushiriki ktk kupunguza umasikini

    ReplyDelete
  11. wakati kuna mchangiaji amesema rafiki zake wameshakata tiketi za kwenda tanzania, kwa upande wangu imekuwa kinyume. nilifurahi na kushangazwa kuona matangazo ya tanzania katika victoria underground, lakini sahib zangu wakaniambia hivi, the adverts haziwambii "why we have to go to tanzania" wakaendelea kuwa ikiwa kuona wanyama, kupanda milima na kuona mandhari unaweza kufanya yote hayo mahali popote pale, so why should we go to tanzania? hiyo ndio message ambayo wanataka to convey. whats special about tanzania?

    ReplyDelete
  12. Mi naona wizara ifanye kila njia angalau kuweka matangazo nchi nyingi za ulaya.Hawa jamaa wa kenya na Obama wao watatupiga bao sana kipindi hiki,maana watalii wengi watapenda kuiona nchi aliyotoka Obama ,hivyo tusitegemee labda watalii waende kenya halafu wapitie Tanzania,gharama ni kubwa si watalii wengi wanaomudu.Hivyo ni lazima tupambane na hawa jirani zetu maana tayari Obama kwao ni tangazo tosha.

    ReplyDelete
  13. HILO TANGAZO NIMELIONA KWENYE UNDEGROUND STATION LAKINI WAMEKOSEA SPELLING, WAMEANDIKA KILAMANJARO, YAANI A BIG MARKETING/ADVERTISING CAMPAIGN LIKE THAT WANASHINDWA KUFANYA SPELL CHECK KABLA YA KUPRINT FINAL DRAFT....

    ReplyDelete
  14. Michuzi,
    wizara ya utalii wanajitahidi sana lakini nadhani wanahitaji kuanza kuangalia masoko mapya. Miaka ya 90 na 80 ilikuwa vyema kama soko lako kuu ni ulaaya. Kama tanzania tunataka kufanikiwa na mambo ya utalii tuanze kuangalia uarabuni na china. tuna historia nzuri na waarabu (zanzibar) na china wanapenda mystical creatures like a lion. pia uchumi wa ulaya haundelei vizuri wakati kwa sas tuna ndege inaenda uarabuni kila siku na waarabu wamejaa mahela. tunaweza anzisha islamic toarism in pemba na unguja. (by the way mi ni mkristo na mchaga usidhani ni mshabiki wa seif). wachina wana hela kama twataka kufanikiwa ki biashara nao lazima waanze kuleta hela bongo kupitia utalii siyo sis tuwape raw material na wao watuuzie ndala. Mawazo kama haya siyo rahisi yapite wizarani kwani waamuzi ni wazee na mawazo yao bado ni ya miaka ya 70 kuwa kila kitu bora kinatoka ulaya!!!!

    ReplyDelete
  15. LAZIMA KUFANYIKE COST BENEFIT ANALYSIS YA HUO MKAKATI KILA MWAKA KUONA NI KIASI GANI TUMEFAIDIKA, NA IWE INAFAFANULIWA BUNGENI NA WAZIRI WA UTALII, PIA NI VIZURI SI KUOTOA MATANGAZO TU BALI PIA WAHUSIKA WASAFIRIKWENYE NJE ZILIZO MBELE KIUTALII, ILI WAKAONE WENZAO WANAFANYA NINI KUVUTIA WATALII, WAENDE KATIKA VISIWA VYA AMERIKA YA KATI - CARRIBEAN ISLANDS, SPAIN, FRANCE, ITALY, PORTGUESE, EGYPT, MORROCO, TUNISIA, SOUTH AFRICA, UK, CANADA, USA. NA UTALII SI MBUGA ZA WANYAMA TU HATA MIJI, FUKWE, MISITU. WATU HAPA ULAYA WANAENDA JAMAICA HAMNA WANYAMA, SPAIN HAMNA WANYAMA NA ILE RAHA YA KUWA KWENYE NCHI NGENI VIBRANT IN TERMS CLUBS, BAR, BEACH, SUN, GOOD PEOPLE, HAMNA, USALAMA, WANAENDA KUPUMZISHA AKILI ANGALAU KWA MWAKA MARA MOJA, NI UTAMADUNI WAO WAZUNGU KWENDA HOLIDAY HATA MARA MOJA KWA MWAKA HATA KWA WALE WASIO NA KAZI. TANZANIA TUNATAKIWA TUJITAHIDSI KATIKA USAFI, USALAMA, URAFIKI NA UKARIMU NA UPANUAJI WIGO WA UTALII SI MBUGA ZA WANYAMA TU, PIA BEI ZETU ZIWE COMPETITIVE ZA ZA KUWAKOMOA, BEACH ZETU ZIWE SAFI IKIWEZEKANA ZIWE ZINA WAFANYAKAZI WA KUFAGIA KILA SIKU, HILI LINAFANYIKA KATIKA NCHI ZINGINE, NENDA SOUTH EAST ASIA BEACH ZINAFAGILIWA KILA SIKU NA ZIKO SAFI SANA.

    ReplyDelete
  16. safi sana sirikali mambo ndio hayo pole pole tu mwisho kila kitu kitakuwa sawa hapo kilichobaki tu ni kuwadhibiti hawa wakenya wasilete watalii wao bongo kiujanjaujanja....hapo tutakuwa tumeweza.

    ReplyDelete
  17. nawapongeza kwa hili lakini pia sio matangazo tu ila na vivutio viwe vya aina nyingi. Nilikua naangalia jay leno siku si ningi nikamwona ellein aliyekua anacheza show ya seinfield anu siku hizi anacheza show inaitwa old christin. Alikua bongo summer hii kwa matembezi na familia yake. Lakini alivyokua anaongelea trip yake hakuonyesha ile raha sanaana ya kuwafanya watu watamani kwenda huko. Alisema "you watch all these elephant and then what,you know elephant they grow up too". Aliendelea kusema baada ya kuangalia wanyama then alikua bored.

    kwa hiyo mimi naona tungekua tunaengeza vitu vya kuwaonyesha hawa watu kuliko wakishawaona wanyama then wanaishia kukaa hotelini na kama weather ni ile ya mvua mvua miezi ya kwetu hawa watu wako so easy to get bored.

    ReplyDelete
  18. pongezi jambo publication kwa kazi nzuri ya kiitangaza nchi yetu nzuri ya tanzania msg from munira and iman

    ReplyDelete
  19. JAMANİ UATLİİ UNATANGAZWA KWA GHARAMA ZOTE,LAKİNİ CHA KUSHANGAZA KUNA SECTOR MUHİMU KWA AFYA ZA WANANCHİ KAMA MAJİ SAFİ,MAZİNGİRA MASAFİ,AFYA BORA(İ MEAN UHAKİKA WA MATİBABU).NAONA BADO HAZİJAPEWA KİPAO MBELE AU HİZİ Sİ MUHİMU KULİKO UTALİİ?
    KOZ HAO WATALİİ KABLA HAWAJAJA WANAANGALİA HİZİ SECTOR KAMA ZİNAPATİKANA AU LA!

    KAMA Sİ NZURİ WATAKUJA LKN WAKIRUDİ MAKWAO WANAANZA KUTUPAKA TOPE

    ReplyDelete
  20. Biashara ni matangazo, naamini kama yameandaliwa vyema yatazaa matunda, kufananisha na EPA kwani Mtanzania gani aliyesalama? Ukipiga kelele ni vile hatujasikia ya kwako au haupo kwenye position ya kuomba kitu kidogo.

    ReplyDelete
  21. Unajua waTZ tunachekesha sana. Shughuli kama hii ambayo ilihitaji kuwa outsourced completely na kufanywa na professionals kiasilimia mia moja sisi tunai-politicize.... What the hell!!!!.

    Ushauri wa bure ---- Tafuteni kampuni ya kimataifa itakayowafanyia kazi ya ku-advertise utalii wa TZ. Nchi nyingine duniani hazitumii mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wa idara za utalii katika kutangaza utalii. Kuna professionals ambao wanaweza kuifanya hii kazi kwa ukamilifu in a most efficient manner. Kukusanya timu nzima ya UTALII bongo na kuimwaga London kwa siku chache ni upotevu wa resources.

    Kuprove idea yangu ulizeni nchi kama South Africa wanafanyaje kutangaza utalii wao. Angalieni mashirika ya ndege kama Airfrance wanavyotengeneza classic adverts hapa US. Huwezi ona Managing Director wa Airfrance ama waziri wa utalii wa Sauzi wakitafuta per-diem London indirectly... They outsource vitu kama hivyo na matunda wanayaona.

    Wake up guys...

    ReplyDelete
  22. MIE NAOMBA KUFAHAMISHWA.UK KUNA TANZANIA TRADE CENTRE ILIANZISHWA KIPINDI CHA MZEE MWINYI KAZI ZAKE NI KUITANGAZA NCHI NJE.HII OFISI IPO NA IPO CHINI YA OFISI YA UTALII TANZANIA, NA INA WAFANYA KAZI WANALIPWA KWA KODI YA MTANZANIA.SASA KWANINI BLANDINA AWAPE TENDA WATU WA NJE WAKATI KITUO CHAKE KINA IDARA INAFANYA KAZI HIYO UK?

    BASI TANZANIA TRADE CENTRE IFUNGWE NA IACHWE JAMBO PUBLICATION KWANI KAZI ZAO ZINAFANANA. NAOMBA KUELIMISHWA?

    NA MATANGAZO SIO LONDON TU KWANI LONDON HAKUNA WATALII KUNA WANIGERIA,JAMAICA NA WEUSI WENGI KWANINI MSITANGAZE MANCHESTER AIRPORT,BIRMINGHAM AU STANSTEAD?
    NJE YA LONDON NDIKO KWENYE WAZUNGU WANAOTAKA KUTALII.
    MDAU COVENTRY.

    ReplyDelete
  23. Cost benefit analysis:
    Tshs 800 million kwa miezi sita ni sawa na £400,000 kwa miezi sita.

    John Terry wa Chelsea ana pato la £100,000 na ushee kwa wiki moja tu.

    Hivyo nchi yetu kutumia £400,000 kwa miezi sita ni sahihi kwani ndio 'dau' la kubandika matangazo sehemu ambazo idadi kubwa ya wakazi wa London hupitia. Tukumbuke kuwa maprofesa, ma-pilot, madaktari, plumbers, wabeba-box, wabeba-zege n.k wanatumia usafiri wa reli mijini na pia kipato chao na 'culture au way of life' yao 'holiday' nchi za ngambo ni kitu muhimu kwao na matangazo hayo watayaona wakiwa ktk mihangaiko yao ya kutafuta riziki kila siku.

    Tusiwe na 'roho au mahesabu ya kimasikini maana kuna pia watanzania wana vijisenti £600,000 ktk vijisiwa vya Uingereza hivyo 'big-up' kwa serikali yetu kutumia mbinu hii ya kukuza utalii kwa njia nzuri yaani kwa maneno mengine a good 'value for money concept.

    ReplyDelete
  24. We Jamaa ambae unaesema Trade Centre ipo kwa ajili ya utalii hapa, Trade Centre ipo chini ya wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya utalii wana utaratibu wake wa kutafuta agenty ambae atawafanyia kazi kama zilivyo katika nchi mbalimbali kama Ameriaca, Asia na Dubai.Katika kuondoa ukiritimba ndio maana serikali inatafuta watu wa kuifanya kazi hiyo.
    Hapo brother naona tatizo ni jambo kupewa kazi hiyo kwa sababu ya watanzania, lakini kumbuka kama kampuni inayo,milikiwa na waingeleza wangepata nafasi hiyo kwa matangazo hayo basi ingefika Bilioni mbili kwani hata hayo ya nyongeza jamaa wangepeleka invoice yake.
    Big up Jambo Pulbications kawape ushauri hao Tanzania Trade Centre wawe creative wa mambo kwani hakuna jipya ambalo wanalifanya wao ndio wanaokura pesa ya walipa kodi bure.Tanbgu hicho kituo kianze tuambieni kuna biashara gani ya Tanzania ambayo hapa Uingereza inafanyika succefully?
    Ngoja tujiandae na data tunakifutailia hicho kituo chenu.

    ReplyDelete
  25. It's stupid wrong timing!!siku zote walikuwa wapi?? sasa hivi Dunia ina face ECONOMY DOWNTURN.Watu hawasafiri kwasababu za kiuchumi,Travell companies na makampuni mengi yamekwenda Bust!!watu wengi wamekuwa victims of credit crunch!!Ni wehu huo na ufisadi.Huu ni muda serikali inatakiwa kujiandaa kikamilifu na hali mbaya ya kiuchumi iliyombeleni.Hawa wafadhili hawateweza`tena kutoa misaada kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayowakabili.

    ReplyDelete
  26. We annon November 16 5:52 acha ushamba wako. Nani amekwambia kuwa watu hawasafi? Ndege zote kuja Tanzania mwezi huu mpaka February ziko tele tele, I mean full booked! Usisikilize habari kwenye BBC au CNN ukabeba tu! Ni kweli uchumi wa duni unayumba lakini si kwa watu wote! Kuna watu wako fit mpaka uchumi uje collapse kabisa. Isitoshe, safari ya kitalii ya kuja bongo kwa wengi tu huko majuu ni mshahara wa mwezi mmoja unatosha! Middle class zinapta zaidi ya dola 4000 kwa mwezi, ukichukua nauli ET au Emirates 1200 London-Dar na booking ya room USD 60 pale Peacock na entrace ya PARK USD 350 tayari unakaa week nzima na kurudi kwenu na salio kwa mshahara wa 1 month!


    Tujitahidi tukisikia vitu tuwe analytical.

    ReplyDelete
  27. aaaaaaaaaaaah wabongo mtaumwa na dawa hakuna acheni vijiba ukiona mwenzio kapata basi jitaidi na wewe kufanya jitihata upate eti trade centre ndio ifanye kazi ya kutangaza utarii sasa walikuwa wapi siku,ongera sana jambo publication kwani kwa taarifa za juu juu tu inasemekana idadi ya watarii imeongezeka kwa kasi kubwa tanzania asanteni sana wausika mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...