Habari waungwana,
Michuzi kuna hili swali nimelikuta katika blogu ya
likiuliza
IS SITTING ALLOWANCE A FORM OF CORRUPTION?
Nadhani si mbaya kama wadau wakijiunga katika huo mjadala
Wako mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Bwana Michuzi, naomba nitoe maoni yangu katika hili suala la sitting allowance. Kwanzi niweke wazi kuwa mimi si mwandishi wa habari, ila ninapenda habari.

    Suala la hii kitu inaweza kuwa malipo sahihi au yasiwe sahihi kutoka na mazingira halisi ya tukio. Ili nieleweka natoa mfano ufuatao.

    mfano: City Council imeitisha kikao cha wadau mbalimbali ili kujadili masuala ya maendeleo ya jiji. Kati ya wadau walioalikwa ni waandishi wa habari kadhaa.

    Katika tukio kama hili, bila shaka kuna wanahabari watakaojitokeza kwenda kupata kitu cha kwa ajili ya habari.

    Kwa hiyo utakuta kunamakundi mawili ya wanahabari hapa. La kwanza ni waalikwa (wamekwenda kuungana na wadau wengine kujadili ajenda husika) pili ni wanahabari walioenda wenyewe kutafuta habari.

    Kwa mtazamo wangu, kundi la kwanza watapewa sitting allowance kama wahusika wengine wa warsha au mkutano husika. Kundi la pili hawastahili kupewa chochote na wakipewa yatakuwa si malipo halali.

    ReplyDelete
  2. Marahaba,

    Mada imetulia hii, na mchangiaji wa kwanza kanigusa hapo kwa allowance za waandishi ambao kawagawa katika makundi mawili; waalikwa na wasio waalikwa. Mwaka jana niliandika mchanganuo wa kuomba fedha kwa wazungu kwa ajili ya jambo la kijamii na ndani yake niliweka allowance (posho?) kwa waandishi wa habari. Jambo hili lilizua utata mkubwa, ambapo ilibidi nijibu kwa mapana na marefu, hatimaye haikukubalika.

    Lililojiri ni kwamba waandishi wanaenda kutimiza wajibu wao, na pale kilichotolewa ni habari. Kuna mmoja kati ya waliokuwa wanapitia proposal yangu alinitania kwani huwa Tanzania tunauza habari bei gani? Osama bin Laden nae akitaka kufanya mambo yake auze?

    Ukiwaza kwa makini utagundua kuwa allowance kwa mwandishi ni RUSHWA!

    Kwa upande mwingine, kama alivyosema mdau wa kwanza ni kwamba allowances sio rushwa, hasa pale inapokuwa ni nje ya 'mazingira' ya kazi. ILA endapo tutafanya mkutano ndani ya ofisi moja, pengine wa idara fulani tu, na mle mle tujilipe allowance hiyo sio rushwa tu bali ni ufisadi.

    Asante.

    ReplyDelete
  3. Sitting allowance mimi naona ni matumizi mabaya ya pesa za umma, nasema za umma kwa sababu hii kitu ipo kwenye shughuli za uuma tu kwa shuguli za makampuni binafsi hakipo kabisa kitu kama hiki, kipo kwenye shughuli za umma kwa sababu bado watanzania tunadhani mali ya umma si yetu ni ya serikali hivyo ni lazima tulipwe mbali ya mishahara yetu. Natoa mfano nilikuwa afanya kazi NBC HQ, wakati wa vikao vya board walikuwa wanalipana zaidi ya Ths 2000,000.00 kwa kikao cha siku moja, hilo tu si neno kwa vile walishahidhinisha iwe hivyo, baaya zaidi kuna wajumbe wangine walikuwa hawahudhuri kwa sababu moja ama nyingine lakini bado walikuwa wanachukuwa hiyo sitting allowance kama kawaida, sasa nini maana ya sitting allowance kama hu-sit kwenye kikao, ni aina tu ya ufujaji wa mali ya umma, kuna wengine walikuwa wanatoka Uganda Kampala, analipiwa ndege kwenda na kurudi, hotel, nights na bado atapewa sitting allowance, hii si sahihi kabisa. Jambo lingine ni hili la wabunge kupewa zaidi ya Tsh.80,000.00 kwa siku wakati wa vikao vya mbunge, mimi hili naliona si sahihi, inatubidi tubadilise mtindo wa bubge letu, liwe kama la KENYA, UK, USA amako wabunge wote hukaa makao makuu ya nchi na hukutana kwa vikao vya bunge kila wiki mara zaid ya mbili kwa wiki, huwa ni full-time job na office zao kabisa, na huwa hapo ndo kituo chao cha kazi hawalipwi night allowance yoyote, huenda majimboni mwao regularly kupata mawazo kutoka kwa wapiga kura wao, na kupata kero zao. Kwa Tanzania wanatakiwa kukaa Dodoma full-time and no allowance, hiyo ndo office yao ndo kazi yao. Ajira ya mbunge inatakiwa iwe tofauti kabisa na ajira zingine, ubunge ni uwakilishi si kazi ya kuajiriwa.

    ReplyDelete
  4. Kwanza namshukuru huyu aliyepata nafasi na maono ya kuleta topic hii ya maana sana.
    Kwa ufupi issue hii iko-complicated na haina jibu la haraka haraka. Ila kwa mawazo yangu sitting allowance itategemea zaidi hali ya mazingira ya kazi. Hapa ughaibuni ninapopiga kibarua hakuna sitting allowance. As an executive unapoenda kwenye mitukutano unalipiwa nauli, chakula na matumizi madogo madogo.

    Kwangu mimi hii ina-make sense saana kwasababu mkutano ni sehemu ya kazi yako na tayari unalipwa mshahara. Kuna mtu mmoja kutoka Tanzania aliwahi kuniambia hivi "We unafanya nini nje? njoo huku tunatengeneza hela nyingi sana." Nikamuuliza kwani unalipwa bei gani? akasema analipwa laki nne kwa mwezi Tshs. Ila tayari ana nyumba mbili ana magari matatu; nilivyomuuliza hela yote inatoka wapi? akasema anatengeneza hela nyingi kwenye sitting allowance. By then I didn't even know what sitting allowance is. Akasema anajitahidi ku-create mikutano mingi kadiri anavyoweza ambayou ni mbali na kituo cha kazi ili aweze kupata hela zaidi ya allowance.
    Sasa ndungu zangu hiyo ni kufanya kazi au ni kuwahibia walipa kodi???
    Ila kuna sitting allowance ambazo naziunga mkono, kama mtu ni expert na anaenda kwenye mkutano, ikiwa ni pamoja na kuchangia kwenye mkutano then anafaa kupata sitting allowance.
    Sitting allowance za wabungu nyumbani kwakweli ni wizi wizi wizi mtupu,, inanitia hasira

    ReplyDelete
  5. sitting allowance ndio nini? wengine hatuelewi Ungetueleza ni nini kwanza halafu tengeweza kuchangia mawazo yetu.

    Hao waliochangia wanajua maana yake lakini walivyoeleza maelezo mengi hata kusoma inakatisha tamaa na sijui ni mtu mmoja huyo na inaelekea anaimaster hiyo topic kweli

    ReplyDelete
  6. Simple and kilia, Sitting allowance ni wizi wa hela ya walipa kodi.

    Na kama unataka kujua nani wanatuibia sisi walipa kodi wa Tanzania basi wabunge wetu ambao kwangu mimi hakuna wanachofanya.

    Wanalipwa mamilioni ya sitting allowance wakati nchi inazidi kuharibika...this is bs

    ReplyDelete
  7. MIMI NINAFANYA KAZI KATIKA KAMPUNI MOJA YA KIMATAIFA HAPA TANZANIA, KAMPUNI HII INAYO BODI YA WAKURUGENZI LAKINI HAKUNA HATA SIKU MOJA BODI INAPEWA SITTING ALLOWANCE KATIKA VIKAO VYAKE. HII NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA TUNAOPENDA KUCHAGULIWA KWENYE BODI KWA AJILI YA ALLOWANCE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...