Leo hii kampuni ya Simu ya mkononi ya Tigo tunajisikia faraja kuungana na Tanzania Mitindo House (TMH) kwa kudhamini onesho kubwa linalofanyika kila mwaka la Red Ribbon 2008 lenye dhamira ya kukusanya pesa kwaajili ya kusaidia kituo cha watoto yatima ambao wazazi wao wamepoteza maisha baada ya kuathirika na virusi vya ukimwi.
Dhamira ya Tigo kudhamini onesho hili ni kuwaunga mkono Tanzania Mitindo House na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye kituo chao cha Magomeni kupitia Onesho la Red Ribbon"
Tigo tumechangia shilingi milioni Tano kwa kutambua umuhimu mkubwa wa kusaidia jamii hii kwa kuwa ni njia mojawapo ya kurudisha kwa jamii kiasi cha faida tunayopata kutokana na ushirikiano mzuri kwenye biashara yetu hii ya mawasiliano kwa wateja wetu wa Tanzania.
Hivyo basi Tigo tunawapongeza waandaaji wa onesho hili na kuwashukuru wanamitindo waliojitokeza kuunga mkono wazo hili lenye dhamira nzuri ya kuimarisha ushikiano na undugu wa Watanzania kusaidiana ambao ni ROSE VALENTINE, ALLY REHMTULLAH, ROBBY MORO, ZAMDA GEORGE, FRANKO DESIGNS, KHADIJA MWANAMBOKA, ASIA IDAROUS, JAMILA SWAI, PAKA WEAR, AIDA SYKES, KIM DEAN, pamoja na JOHN KAVEKE kutoka Kenya na FAROUK ABDELA kutoka Zanzibar.
Bado Tigo tutaendelea na utaratibu wa kupokea na kusaidia michanganuo mingi nchini Tanzania inayoonyesha kuifaidisha jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Michezo, Elimu na mazingira ya jamii,
Hivyo tunawaomba watanzania kuiga mfano mzuri wa Tanzania Mitindo House kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi zao kuandaa matukio yenye lengo la kuileta burudani pamoja na kusaidia jamii nzima ili iweze kuwa na maisha bora zaidi.
i am suspecting the acrobates behind this big money handouts...lets wait and see...
ReplyDeleteJamani leo NBC nightly news wameonysha Anne Curry akipanda mlima kilimanjaro. Nadhani mnamfahamu yule mwanadada wa to catch a predator show. Basi ndio yeye. I was so happy ingawaje hakumaliza...Anyway wataonyesha tena kesho asubui katika today's show channel 4 NBC NY
ReplyDeleteDuh! Wengine mafisadi dada! Usicheke namna hiyo hadharani
ReplyDeleteJamani nakumbuka Joni Mashaka alilimwagilia miela milioni 12 hili taasisi la TMH. Zile hela ziliishia wapi kwa maana hawakutaka hata kumtaja huyo kaka kama ndiye aliyekuwa mdhamini wao tangu walipoanzisha NGO yao.
ReplyDeleteNiliwaona wakina khadija EATV wakisema kwamba walitoa misaada mingi kwenye jamii kutokana na udhamini kutoka nje ya nchi.
Waandishi hatukupewa hata senti tano wakati tunafukuziwa na huyu dada kuandika habari zake
Haya yasiwe ni ufisadi , kwa maana naona hesabu zenu ni kubwa ki dizaini. Mimi nanusa harufu ya ufisadi kusema kweli
Mwandishi, Mdhibit Ufisadi
Khadija aunty Mola akuzidishie kwa juhudi zako.Nilikuwa karibu sana na marehemu mama yako,Mola amueweke peponi wakati huo ulikuwa mdogo.Mie rafiki wa aunty Ashura bonto.Mola akupe nguvu uzima ueendelee na moyo wa kujitolea Amin.
ReplyDeleteWe annon Nov21: 3:29 acha ushamba wako hapa! Kama ulijuana na mama yake ku na sababu gani ya kusema hapa! Acha UFISADI wako wa kinamna ha
ReplyDelete