KUSITISHWA KWA UCHAGUZI WA WAJUMBE KUMI NA TANO (15) WA HALMASHAURI KUU - NGAZI YA TAWI LA CCM LONDON (UK)
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, Tawi la London (Uingereza)
Nachukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa uchaguzi wa viongozi wa kudumu wa Wajumbe Kumi na Tano (15) wa Halmashauri Kuu - ngazi ya Tawi la CCM London (UK), kama ulivyotangazwa awali kuwa ungefanyika pamoja Mkutano Mkuu wa Tawi huko London, Jumapili tarehe 16 Novemba 2008 umesitishwa (postponed), mpaka hapo tarehe mpya itakapotolewa.
Nachukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa uchaguzi wa viongozi wa kudumu wa Wajumbe Kumi na Tano (15) wa Halmashauri Kuu - ngazi ya Tawi la CCM London (UK), kama ulivyotangazwa awali kuwa ungefanyika pamoja Mkutano Mkuu wa Tawi huko London, Jumapili tarehe 16 Novemba 2008 umesitishwa (postponed), mpaka hapo tarehe mpya itakapotolewa.
Hii ni kutokana na sababu zilizoshindikana kupatiwa ufumbuzi wa haraka. Tutawajulisha mapema kuhusu tarehe mpya. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea, na pia tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Jamani, hebu fanyeni kazi zenye ulazima na zenye kuzaa matunda. Achaneni na huu uzugaji.Hivi ni kweli kuna haja ya "uchaguzi wa viongozi wa CCM" huko au mnafanya hivyo kwa kutumwa ? Ni kwa njia hii maendeleo ya Tanzania yatafikiwa ? Watanzania wenzangu tufanye kazi kwa bidii, huu uzugaji hautatufikisha popote pale.Leo hii tunasema Rwanda wanakuja juu,watatupita.Sisi baada ya kufanya mambo ya maana,tunabaki na huu ubabaishaji. We need to grow up,tumezidi!!
ReplyDeleteMimtu mingine utadhani imerogwa!
ReplyDeleteHivi lini tuttakuwa na akili ya kufikiria kufanya changes nyumbani?
Huo muda mnaopoteza kupena vyeo feki kwa nini msingeji-organize mkasaidia watu wa vijiji vyenu ambao watoto wao wanakufa kwa malaria kwa kukosa vyandarua au wale ambao wanasoma huku wamekaa chini kwa kukosa madawati?
Kuna mambo mengi ya maendeleo ambayo mnaweza kuyafanya katika jamii then mkaja kujitangaza hapa tukawaona kweli mna akili badala ya kuendeleza fikra ambazo hazisaidii kizazi kijacho.
Grow up you JUDAS!
Wadau naomba mnisaidie, mlio comment hapo juu nawapongeza kukosea kunakoleta maendeleo.
ReplyDeleteHawa jamaa hawana familia?hawasomeshi watoto? badala ya kuuendekeza upuuzi huu, ni bora muda huo wakatumie kusimamia watoto kufanya home-work zao, au ni bora mtu akae na mai waifu wake wapalilie ndoa yao. jema zaidi ni kuongeza muda wa kazi, kuongeza kipato zaidi. Haya mambo yatakuja kuwa-frustrate tu. Nyie ni watu wazima alaaaaaaa!!!
Na bado utabaki peke yako. hii aibu iliyopo huku home si mchezo. ww utaitishaje uchaguzi uk wakati hali ndani ya ccm ni tete!!.Tumia akili ya kawaida, soma alama za nyakati. wenzio wajanja wameshaanza kuliona hilo sasa wanakukacha, tafakari nawe uchukue hatua. achana na mambo yanayowachefua wanablog!! Pum......fu!!!
ReplyDeletemimi nadhani hawa mafedhuli wanapiga hesabu mbovu ambazo mlinganyo wake ni vichekesho. Wao walipoambiwa siasa ni kilimo, kilimo ndo uti wa mgongo wa nchi yetu( uhai wetu wa TZ), basi wakafanya hivi:-
ReplyDeleteSiasa=kilimo
Kilimo=Uhai
Therefore, Siasa ni uhai,
Teh, Teh, Teh he he heheeeeeeee!!
Nyie watu wa Ukerewe; acheni upuuzi, huo muda mnaopoteza kukaa vikao na kujipa vyeo hewa sijui wenzetu mnautoa wapi.Mwenzenu mpiga box natafuta muda wa angalau nipumzike siupati, nashangaa sana. Haya, watanzania tutafika tu.
Mpiga Box.
MIMI NATANGAZA KUWA MCHAKATO WA KUMPATA KIONGOZI MMOJA TU WA 'OPERATION SANGALA-DIASPORA' UNAENDELEA.
ReplyDeleteSHABAHA KUBWA NI KUPAMBANA NA MAFISADI POPOTE NA PIA KUHUBIRI INJILI YA MSIMAMO THABITI INAYOTUUNGANISHA WATANZANIA WOTE NA HATA IKALETA USHINDI KULE TARIME DHIDI YA WALE WANAOJIKWEZA PASIPO KIBALI CHA WANANCHI KAMA HAWA JAMAA WACHACHE WA UK!
We bwana michuzi usiache kuweka hii wadau wasome.CCM imejaa mafisadi wanaolindana. Kuna watu bado tunawasubiria tuwasikie kwenye sakata la EPA. Unabisha niwataje? najua nikiwataja hutaposti maoni yangu.ILa ROHO inaniuma nawataja na ukiacha kuposti nawe unasapoti ufisadi nao ni............................. Ros--tam,.. ....Ma--nji, niendee? we bwana michuzi huogopi?? Hata wadau wengine wa Kisiasa ila nawahifadhi kwa sasa.
ReplyDeleteHii inaonyesha jinsi gani watu wengine walivyofilisika kichwani, ingawa wakitembea barabarani wanaonekana ni watu wa maana. Bora mrudi nyumbani Bongo muisaidie hiyo CCM yenu maana iko hoi. Kuizungumzia na kutetea CCM kwa sasa huku nyumbani unaonekana kama mtu mwenye matatizo ya kufikiri
ReplyDeletejamani acheni u selfish,kila kitu mnataka mtafuniwe?wenzenu mpaka wamefika huko mnataka muangaliwe nyie tu,yaani watu hata wasichague shughuli za kufanya!mnawaza hela tu
ReplyDeletenilikuwa nagombea ujumbe na tayari nilishaanza kampeni za uchaguzi,je itakuwaje hizi gharama zangu?mtanirudishia au? next time naomba muwe na uhakika mnapotangaza mikutano yenu kwani watu tunaacha shughuli zetu zinazotupa ridhiki halafu mnatuyeyusha. au kama vipi basi wahusika wajiuzulu kwani ndio demokrasi.kidumu chama cha mapinduzi!!!!
ReplyDeleteMimi najiulixa wakishafungua haya matawi na kuchagua viongozi huko nje ya nchi faida yake ni nini?
ReplyDeleteHebu watupe katiba yao tuione basi?
Ndio maana USA tuliwakata kilimi. Sijui kile chama chao wanakifanyia chini ya mvungu.
Fanyeni yaliowapeleka huko mkirudi home basi mujiunge na huko. Manajidai wakereketwa wakati bongo mlikua hamna hata kadi.
Hebu mtwambie hivyo vingine vilivyofunguliwa toka miaka imepita wamefanya nini mpaka sasa au ni kushikilia tu title????
Vibaraka wa mafisadi. Kupitia serikali ya chama tawala mtu anakula bil. 42 wewe utakuwaje kiongozi wa hicho chama. Watu kama nyie mliopata nafasi ya kufanya uchambuzi with technology kama Internet halafu bado mnakuwa vibaraka mnasiitisha sana. Kujipendekeza labda mtapewa na vyeo
ReplyDeleteWe anon wa November 13, 2008 2:26 PM. big up sana. Una akili.
ReplyDeleteoperation saka mafisadi -diaspora inaendelea.
Balozi za Marekani, Canada, UK nk zimeshatangaza msimamo wake, kwamba wale wote wanaotuhumiwa na ufisadi ikiwa ni wao na familia zao, watoto wao na extended family zao kifupi wanaonufaika na fedha za ufisadi popote walipo. Hawatapatiwa VISA tena kuingia nchi hizo na endapo wapo ktk nchi hizo watarudishwa haraka sana bongo.
Ktk kuitekeleza operation saka mafisadi-Diaspora ikiwa ni pamoja na watoto wao, tunaomba majina ya vigogo na watoto wao wote walionufaika na fedha za wizi za walala hoi wa Tanzania, na Fedha za misaada iliyotoka kwa Wazungu waliolipa kodi zao.Tuwakilishe kwa FBI na CIA na Balozi hizi.Sasa
tufanye kazi kwa vitendo, tuache kuongea na kulalamika. Haya Sasa leteni majina ya hao mafisadi na ndugu zao popote pale walipo. kama michuzi atabana post hii, tutaanzisha blog maalum ya operation saka mafisadi-diaspora
nakuomba mzee michuzi usituwekee huu upuuzi!!!!!!!!!!111
ReplyDeleteCCM itakua UK ovyooooo si mrudi home mgombee huku wengine hata kusafiri kuja kupiga kura kunawashinda mnaishi kiukimbizi rudini huku kwetu tuwaone mashwaini hamna kazi nyie mnatia kichefuchefu.