
msanii francia chengula akitoa burudani kwenye hafla hiyo ya uzinduzi

mwansilishi wa ATWID akitoa zawadi kwa mmoja wadau waliofanikisha shughuli hiyo

Balozi wetu Uingereza Mh. Mwanaidi Sinare Maajar akizindua rasmi Association of Tanzania Women in Diaspora (ATWID) tarehe 01/11/2008, katika ukumbi wa 79 London Road, Reading.

Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akikaribishwa kwenye sherehe na mama Kalinga

Mhe Balozi akikabidhiwa nakala ya risala ya ATWID na Susan Mzee, mwanzilishi wa chama hicho. Kati ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la London (UK), Mhe. Maina Owino

wanachama na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo

ukumbi ulijaa wageni waalikwa na wanachama

baadhi ya wageni waalikwa

Balozi Maajar akiwa na fulanazzz ya ATWID

baadhi ya wanachama wa ATWID wakila pozi

baadhi ya wanachama wa ATWID kwenye ngoma za asili

Mariam Kilumanga , Mwenyekiti wa Tanzania Women Association (TAWA), akiwa katika Picha ya Pamoja na Wanachama wa ATWID pamoja na Mhe Balozi na Mwenyekiti wa CCM London (UK)

Wanachama wa ATWID pamoja na Dada Francia wakiimba na kucheza pamoja kusherehekea uzinduzi wa ATWID
Hivi kumbe watu bado wanakumbatia CCM eh...! Huyo mh. sana msimtambulishe kwa cheo cha chama kwani ATWID ni moja ya jumuiya za sisiM wao...? maana pengine hajitambui kuwa anapakwa matope mbele ya wapenda maendeleo. Au mh. umeomba pengine au ndiye mwenyewe umepost photos hizi, kuwa tutakutambuaje?
ReplyDeleteNakusihi usome alama za nyakati hasa katika kipindi hiki cha mageuzi makubwa!! Ukizingatia kuna operation Sangara huko nyumbani.
Nanyi diaspora wanawake, nawasifu sana kwa kampeni zenu, japo nanyi mpate kuambulia hizo za EPA. Fungueni Account ya association yenu basi!.
Pengine niulize nini hatma ya Diaspora kubwa, na mara ya mwisho mmekutana na kuweka mikakati kibao, na kabla hata hatujaanza kuona utekelezaji wa mikakati hiyo mnaibuka na ya wanawake!!! mna agenda gani? OK, aah...ni kama nilivyodokeza hapo juu!.Kitaeleweka tu, ni suala la wakati.
Ahsanteni.