Kijana Muafrika kushoto akitoa maelezo kwa Polisi baada ya kuwakimbiza na kuwanasa na kuwapa kichapo kikali sana vijana wawili wa kimalay ambao walijaribu kumuipora wallet yake ya pesa alipokuwa akitoka ATM maeneo ya Puchong huko Kuala Lumpur Malaysia juzi jumapili 16 Nov 2008.


Kijana huyu mwafrika alikurupushana na vibaka hao ambao walikwisha mpora pochi yake na kudandia pikipiki lakini mwanaume alikimbia na kuwadaka. Ni jambo la kawaida kwa vijana hawa ambao hutumia pikipiku kuwapora watu na kukimbia tabia ambayo Polisi wamesema imekuwa ikiongezeka kila kukicha. Mshkaji huyu aligoma kusema anatokea nchi gani ila alikuwa na lafudhi ya ki nigeria.


Pius wa Spoti na Starehe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Na jamaa alivojazia,wangemtambua kudaadeki..he he he,cheki mkono Nondo!!duh

    ReplyDelete
  2. Tayari polisi anataka passport ya mshikaji...angekuwa mzungu wala asingemuuliza hata jina!! huku ubaguzi kwa waafrika ni nje nje!!!

    ReplyDelete
  3. Du jamaa katoka nduki kuishinda motorbike na ana uchuchungu na uchache wake kesha wabana wamalei wanataka wamuibie tena lol may be wateja wake manake wapopo tena au kwa scam ndo wenye may be 411 kesha fanya hapo hizi malei kama scavenger hahah

    ReplyDelete
  4. hahaha Jibaba limeshiba sijui Waghasusu huyu limeshiba linauchungu hapo kawatandika vibaya saaana mbona wezi wamewaficha uso? alafu kama police amemkasirikia jamaa kuliko wezi? piga hao mikono laiiiiiiini kama amenawaaaaaaa hahaha kudadadeki. jibaba linapiga chuma zile za cimenti. Oganigweeee upo?

    ReplyDelete
  5. Nakuaminia mdau PUC aka Papaa Pius tuletee matukio mengi kama hayo kwani unao uzoefu na Malaysia kwa muda mrefu

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli hakuna vibaka kama huko! Wanakuja na pikipiki na ukizubaa wanakwapua kila kitu!

    ReplyDelete
  7. VIBAKA SIKUHIZI WANATUMIA VYOMBO VINAVYOELEWEKA BWANA WATU WAKO "HAI-TEKI" HATA HAPA BONGO MADAWA YA KULEVYA/MAJANI/WEZI WA SIMU/MIFUKONI, YANAFANYIWA MAMBO YA "HAI-TECH" NA "UNANDI" HAWAONI NDANI NA NDIO MAANA HAYATAISHA.

    ReplyDelete
  8. Kwahiyo huko kwa "WACHING-CHANG" Wewe ukiona pikipiki anza....!! Kimbia kama unafukuzwa na simba..Lol..!!
    KLS-USA

    ReplyDelete
  9. hahahaha,chakubanga kama vp chapa hadi hao mandata wasikuulize wakati umeshazinguliwa wasulubu tu

    ReplyDelete
  10. wewe anonymous wa November 19, 2008 4:53 PM ulikuwepo hapo? ulijuaje kama polisi alitaka kuona passpoti, wacha uzushi.

    ReplyDelete
  11. MIMI NI DENT MALAYSIA! NIMEFURAHI SANA KUPATA HIYO PICHA,KUNA WAHINDI WEUSI HUKU NA VIPIKIPIKI VICHECHE MBAYA, JUZI WAMETUFANYIA, STYLE YAO YA SASA HIVI WANAKURUSHIA MAWE MPK UWAACHIE VYAO HLF HAWANA NGUVU HATA KIDOGO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...