Hello Balozi
Please can you look at the link below and see if you can post it on our beloved blog to hear what will come out of Tanzanians
Taarifa kwamba viza za Watanzania wanaotaka kwenda Uingereza zitakuwa zinashughulikiwa nchini Kenya ili kupunguza gharama ni aibu kwa nchi kubwa kama hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya ubalozi wa nchi hiyo Tanzania iliyotolewa juzi, hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa nchi hiyo kupunguza gharama kwa kupunguza ofisi za viza kutoka 100 hadi 50 duniani kote.
Hivi sasa Mtanzania akitaka kwenda Uingereza anatakiwa kuomba viza wiki sita kabla halafu hati yake ya kusafiria na nyaraka nyingine zitapelekwa Kenya kushughulikiwa na ndipo zitarudishwa Dar es Salaam.
Ubalozi huo umesema zoezi la kupeleka taarifa za mtu Kenya litachukua takribani wiki tatu na kama zoezi litachelewa, mwombaji wa viza atajulishwa tarehe mpya ya kufuata viza.
Soma zaidi kwa kubofya linki hapa chini
http://www.habarileo.co.tz/uchambuzi/?id=13742
Please let me stay anonymous
Thanks
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Utoaji wa viza za Kiingereza ni uhuru wa serikali ya Uingereza. Kama wanataka iende Kenye kwanza au Hawaii kushughulikiwa, basi ni haki yao. Kusema kuwa ni aibu au kutoheshima Tanzania ni kutofahamu sheria za kimataifa. Uliza ufahamishwe mdau, hapa kwa Balozi elimu ni bure.

    ReplyDelete
  2. Ni rahisi tu kupatikana. Kama una genuine reason. Mbona ya Australi inaptikana Nairobi na mashrti ni hayo hayo na unapata muda mfupi tu. Pia ile ya New Zeland inapatikana South Africa na muda ni mfupi tu kuipata. Yangu ya Australia nilichukua siku 5 tu kuipata licha ya kuwa mahsrti ni replica ya ya hayo mapya ya UK.


    Issue hapa kwa zile akili za box! Wabeba box hapa hakuna ubabaishaji tena.

    Point hapa ni kuwa kwa kuvunja kile kitengo, watu kibao watakosa ajira pale kwenye kitengo. Wakosa ajira pia ni wapiga picha pale nje karibu na International house.

    Wewe mbeba box na comments zako utakoma. Baki hapa hapa

    ReplyDelete
  3. Na je kwanini embassy ya bongo uk iswafanyie na wao kama hivyo kwamba wakitaka kuja tz waje kwa visa kisha wakaifate hio visa russia ndio waweze kuja tz ,ebo!! tuna wanyama sie na ml kilimanjaro lazima watawashwa tu watake kuja,kwani wakisema hawaji wenzao hawatakuja?tujiamini na sie kidogo jamani

    ReplyDelete
  4. Hii ni foreign policy ya nchi we can not do anything about that, maybe what we can question why KENYA and not TANZANIA? the answer is very simple, KENYA is a proper former colony of UK and always they have a bigger Embassy there than Tanzania since ever, for that matter all facilities are there, and this is not just for us but for all east and central African countries, they wanna reduce costs, I think eventually they may close even the embasssy itself as well, as the cost is not on visas only but even on other administration costs. Do yu know that KENYATTA stayed in UK for long time and married a white woman and he had a children with her, do you know that there are still millions of English farmers in KENYA? Do you know many businesses in KENYA are owned by Britons. So Kenya is very close to UK than us (TANZANIA). WATANI WA JADI WAMETUPIGA BAO, GOAL LA KISIGINO HILO.

    ReplyDelete
  5. Mbona humu kuna watu ambao akili zao zimekwisha oshwa? Hivi wewe umeshajiuliza kwanini ubalozi uhamishe kitengo hicho Nairobi na vitengo vingine vibaki palepale? Hata kama ni uzalendo basi sasa huo wakwako uko wapi maana Nairobi ndio kuna wasafiri wengi? Wewe unafikiri Kenya hakuna wabeba box? Hata nchi za Europe kuna wanaokwenda UK kubeba box usiwe umetawaliwa na kasumba!
    Point ni kuwa nchi yetu imejaa wakina Yes Sir wengi sana hakuna hata kuuliza sababu ya maamuzi ama hata kujaribu majadiliano, kila kitu Yes Sir!

    ReplyDelete
  6. Huu ni ubabaishaji 2 wa kupotezeana muda na ndio maana apa Germany sasaivi wanaigeria nao kwa ujeuri wao wamewafanyia ivyoivyo wajerumani, coz Mjerumani akitaka Visa ya kwenda Nigeri inabidi apeleke maombi yake Ubalozi wa Nigeria apa Germany nao watamjibu ndani ya wiki 2 kama wampe au wasimpe sheennzzzii! na ole wako uende Nigeria ujifanye eti unachukulia Visa Airport, watakuweka ndani na kisha UNATOLEWA NDUKI kwenu bila kuuona hata mlango wa Airport; Ivyo nasi tuige ujasiri wa Kinaigeria jamani! BEN KINYAIYA; EATV:

    ReplyDelete
  7. kwa matazamo wangu sion problem kwenda kuchukulia Nairobi visa ila tatizo ni huo muda six weeks its a lot jaman ni muda mrefu sana

    ReplyDelete
  8. Jamani sisi watanzania tutaburuzwa mpaka lini? This is not wright. For some of us this six weeks period will ruin our business. Something has to be done about this RUBBISH!!

    ReplyDelete
  9. Tumeongea mengi sana hapa mengine yakiwa ni matamahuruku...point kubwa na yenye mantiki ni kutoka ka anony nov.17 1:49. Wiki sita ni nyingi sana wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa bkimataifa wana jukumu hapa la kujaribu kufanya majadiliano na wenzao wa Uk kupunguza hizi siku wengi huwa tunapata mialiko kwa kipindi kifupi hivyo tutashindwa kuhudhuria pia wafanyabiashara wa bongo watateseka sana hasa wanapokuwa wanahitaji kufuata bidhaa kwa ajiri ya biashara zao...MEMBE achana na OIC shughulikia hili la msingi zaidi.

    ReplyDelete
  10. 1. Tanzania na Nigeria ni nchi masikini.

    2. Usimpe viza mtalii wa Kijerumani, anakwenda nchi nyingine.

    3. Usimpe viza eapoti, anakwenda nchi nyingine.

    4. Nigeria ana mafuta kuliko nchi zote za Afrika. Ana fedha kuliko Tanzania.

    5. Je, tukose fedha za kujiendeleza kwa watalii au tujiheshimu na tuwabane kama wanavyotubana sisi?

    6. Wanapeleka pasi balozi zao jirani kubana matumizi, hali ya uchumi duniani kote ni mbaya. Usistuke kama nchi nyingine zitafunga ubalozi Bongo. Iraq, Algeria, Korea kaskazini, na Poland wameshahama zamani.

    ReplyDelete
  11. natafuta kazi office ya posta bongo ulaji huu unanukia.pobox....lol

    ReplyDelete
  12. Jamani.Sasa watanzania na umasikini tulio nao wanazidi kutuongezea gharama.Kutuma passport Kenya ama mtu kwenda Kenya ni cost hiyo.

    Na huo muda mrefu wa kungoja visa inakuwaje kwa watu wenye emergency.Mfano mama au baba anasikia mwanae anaugua mahututi UK je na wao watangoja hizo siku zote???

    Jamani jamani wazungu hawa wanatumaliza.

    ReplyDelete
  13. mwenye njaa hana decision, maamuzi yote anayo aliyeshiba!na mwenye uhakika wa chakula chake na chako , uongo?

    ReplyDelete
  14. Anony 1:18 hapo juu umesema la maana. Sisi tuna njaa na kufa, tunategemea misaada tangu tupate uhuru, halafu tunajidai kama tuwe na ubavu wa kuwabana wazungu na viza zetu (ingawa tuna balozi 20 tu nje).

    Uhuru wetu ni bandia, wazungu wanatuamulia bei za bidhaa zetu na tunawategemea wao watulishe, watusomeshe masomo ya juu na watutibu. Hata tukitaka kusafiri nchi zote za kitajiri, lazime tuwaombe ruhusa ya kusafiri miezi misita kabla na pengine tusipate ruhusa. Leo bajeti yetu, dola milioni 350 ni fedha za misaada. sasa huu ni uhuru au utumwa? Huo ubavu wanaodai baadhi ya wadau hapa uko wapi?

    ReplyDelete
  15. WANAPUNGUZA GHARAMA ZA UTENDAJI KWANI WALE WOTE WA KITENGO CHA VISA NGOMA INOGILE, SASA MTAKUBALIANA NA JOHN MASHAKA AS FAR AS WORLD CREDIT CRUNCH IS CONCERNED, MLIKUWA MNACHONGA MDOMO TU KUMPONDA JOHN MASHAKA.

    ReplyDelete
  16. WANAPUNGUZA GHARAMA ZA UTENDAJI KWANI WALE WOTE WA KITENGO CHA VISA NGOMA INOGILE, SASA MTAKUBALIANA NA JOHN MASHAKA AS FAR AS WORLD CREDIT CRUNCH IS CONCERNED, MLIKUWA MNACHONGA MDOMO TU KUMPONDA JOHN MASHAKA.

    ReplyDelete
  17. toba yalabi,,,kazi ipo apa bora twendege arabuni iraq,afghan no masharti ya dizaini izi,,,ndo mana waarabu wanatushangaaga why tunawaganda sana awa makolono??

    NYAMAFU KABISA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...