Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano yalipo makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam kuhusu mgomo wa walimu utakaoanza wiki ijayo. Aliyekaa upande wa kushoto ni naibu katibu mkuu wa chama hicho Bw. Ezekiah Oluoch.
---------------------------------------------------------------------
As teachers yesterday announced a countrywide strike starting next Monday, the government has said about half of their claims are not genuine.
The decision to call the strike was announced by the President of the Tanzania Teachers Union (TTU), Mr Gratian Mukoba, yesterday at a press conference in Dar es Salaam two days after the Court of Appeal had ruled in their favour.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Eee bwana eee duu, huyo oluoch nimekumbuka mbali sana.Huyo mwalimu alikuwa mnoko sana pale tambaza miaka ya 95-97 jamaa alikuwa anaonea mademu na watoto wa high school wakati watoto wa form 4 wanamtukana mbele ya pua yake na hafanyi kitu duu kweli dunia inazunguka.

    ReplyDelete
  2. waalimu wa nchi hii balaa,,,yan ukiwa mwl wee maskini wa kutupwa

    ReplyDelete
  3. Kha! Oluochu yopu hai kumbe?....haha! eti katoa pozi. Hicho chama cha walimu nacho kimeishiwa, Of all people!! Naibu?!!

    ReplyDelete
  4. THAT IS RIGHT, ENOUGH IS ENOUGH. WAO WANAKULA KUKU KWA MRIJA, NA MAISHA YAO LAINI KAMA VILE KUMSUKUMA TEMBO KWA UBUWA, UA KUMSUKUMA MLEVI KWA KIDOLE KIMOJA, WAKATI MAMILIONI YA WATANZANIA WANASHANGA FELI AU KWENYE MATAA YA FAYA. MAISHA BORA NI LAZIMA YA KWA WOTE SI KWA WATEULE WACHACHE TU, NINI SASA MAANA YA UHURU?

    ReplyDelete
  5. Oooooh shemeji......shemeji si ndivyo mlivyokuwa mnaimba nyie leo imekuwaje?!hamna jipya Tz yani badala ya kuendelea ndio inazidi kudidimia nakubali ule msemo wa Obama kipindi ya kampeni"You know you can put lipstick on a pig, but it's still a pig".Watanzania kazi tunayo

    ReplyDelete
  6. Kama wanaodai ni wakina Oluoch basi wasipewe kitu na kazi wafukuzwe kabisa. Mimi na akili zangu siwezi kumuunga mkono Oluoch kabisa labda wali ambao hawakusoma Tambaza.
    Na huyu Mukoba naona anatafuta uwaziri tu. Unajua wabongo huwa ni wepesi sana kusahau na kufikiri hawataki. Mnakumbuka Mama Sitta alikuwa rais wa chama cha walimu na alikuwa mstali wa mbele kudai haki za walimu. JK alipoingia madarakani akasema kwa kuwa yeye anatambua matatizo ya walimu basi atampa wizara ya elimu. Utumbo alioufanya huko Mungu anajua.

    ReplyDelete
  7. Ninachojua serikali kupitia Rais Kikwete iliishasema inashughulikia madai yao kwa kuhakiki. Sasa mgomo wa nini? Au wana agenda ya siasa? I hhope sewrikali itafanya haraka kuwalipa hawa walimu. Lakini na ile wizara ya Profesa Maghembe imeoza kweli inao watendaji walaji na wabinafsi. Masikini Tanzania nchi yangu. Iko kazi kweli.

    ReplyDelete
  8. Oluoch wee!Tunakumbuka enzi zako 1997 ulifuatilia watu waliokwenda kujirusha Bilicans.

    ReplyDelete
  9. Mimi siwaelewi kabisa walimu wakisema wanagoma. Wanagoma nini? Kama kufundisha hawafundishi, hata wakifundisha utumbo mtupu.

    ReplyDelete
  10. Viongozi Wanafanya nini hapo serekalini haswa Rais anaiharibu nchi tu,wenyewe wanaiba wanakimbilia nchi za watu halafu walimu wananyimwa posho zao,serekali ya tanzania haijali maisha ya wanachi wa kawaida,wanafunzi taifa la kesho wanafungiwa chuo ubabe ubabe tu au kwa vile kikwete mwanae anasoma ulaya basi wengine wastruggle tu,inatia aibu kwa kweli ila tusipoangalia tanzania kutakuwa na fujo kama ilivyotokea kenya kama hali hii ikiendelea

    ReplyDelete
  11. Jamani humo kwenye madai ya walimu kuna madili ya watu humo. Tena watu wenyewe wakubwa wala sio walimu wala hawana njaa wanashirikiana na baadhi ya wakuu wa walimu kuiba. Wanachogomea uhakiki ni nini? Mie nakumbuka kuna mama mmoja alishaacha ualimu wa msingi akawa anasoma zamani kidogo, basi alikuwa anapokea mshahara wakati na hiyo kazi keshaacha. Sasa watu walioko sasa hivi wanajua kuna vituko humo kwenye list yao, kuna walimu hewa, kuna waliokufa, kuna marisiti feki, sasa walipwe tu kwa kutishia kugoma? Hivi kugoma kwao kutaiumiza serikali au watoto wa maskini? Watoto wa vigogo wote na watoto wengi wa middle class wanasoma private school. Watoto wa hao walimu na watumishi wengine wa chini wa serikali wanasoma hizo shule za serikali.

    Halafu nimecheka kuna mtu katoa wazo eti wanagoma nini mbona hata kufundisha hawafundishi. Yaani kuna mtoto alikuwa anasoma Olimpio sijui Diamond, akirudi nyumbani hana hata homework, kumuuliza mbona huna homework anajibu mwalimu kasema mpaka mumpe hela! Kaazi kweli kweli.

    Hayo madai yako tangu enzi ya Nyerere mengine ndio yatalipwa yote leo kwa mkupuo? Kama sio mambo ya kisiasa ni ninina huyo Makoba msimpe hata ujumbe wa Nyumba kumi kumi, wameshaona kuwa huo ndio uchochoro!

    ReplyDelete
  12. Oluochi sijui Uleuchi, ( yule mnoko wa Tambaza miaka ya nyuma) whatever...asipewe kitu, tizama tumbo lilivyokuwa kubwa...ni ufisadi huo!.

    ReplyDelete
  13. Hapa Tanzania kuna mwalimu anayelipwa mshahara na marupurupu makubwa kuliko walimu na maprofesa wa vyuo vikuu vyote Tanzania. Hacheleweshewi mishahara yake. kapangiwa jumba la kifahari. Kapewa gari zuri. Anaalikwa kwenye dhifa kubwa kubwa za kiselikali na kibinafsi. Wanafunzi wake hawapasi mitihani wala hana vipimo vyovyote vya kudhibitisha uwezo wao wala uwezo wa mwalimu mwenyewe.

    Unamfahamu mwalimu huyo?

    Kama humfahamu ngoja nikufahamishe. Mwalimu huyo ni mwalimu wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Marcio Maximo.

    Ikiwa kama unafikiri haya niliyoandika ni uzushi tafuta data za mkataba wake; uone mshahara, marupurupu, bei ya pango (house rent), gari anayotumia na mengineyo. Halafu linganisha au wianisha na mikataba ya walimu na wahadhiri wa vyuo vyuo vikuu Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...