Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Neema Maunga (KUSHOTO) akibonyeza kitufe jana kwa ajili ya kumpata mshindi wa zawadi kubwa ya wiki ya droo ndogo ya Endesha Ndoto yako 2 kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania ambapo mshindi hujinyakulia muda wa maongezi wa shilingi laki moja. Wanaoshughudia wa pili kushoto ni Afisa Uhusiano wa kampuni ya Zain Celine Njuju na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini Sadiki Elimsu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania leo imechagua washindi wengine wa muda wa maongezi katika mfululizo wa draw zake za kila wiki za promosheni yake ya Endesha Ndoto Yako 2 ambapo mkazi wa Usangi Wilaya ya Mwanga. Omari Athumani, aimeibuka mshindi wa zawadi kubwa ya wiki ya muda wa maongezi wa Tshs 100,000.

Droo hiyo iliendeshwa na Ofisa Uhusiano wa Zain, Bi Celine Njuju mbele ya waandishi wa habari na msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ambapo wateja wapatao 1,101 wa Zain watawekewa muda wa maongezi wa thamani ya Tshs 7.6m ambapo mshindi huyo wa kwanza atawekewa muda wa maongezi wa Tsh 100,000, wateja mia muda wa maongezi wa Tshs 25,000 na wateja wengine 1000 muda wa maongezi wa Tshs 5000 .


Zain imeongeza draw za kila wiki katika promosheni yake ya Endesha Ndoto 2 wiki nne zilizopita ili kuongeza idadi ya washindi wa zawadi mbali mbali katika promosheni yake ya endesha ndoto 2. Zawadi za awali katika programu hiyo ni simu za mkononi aina ya Blackberry na Nokia zinazotelewa kwa washindi wa Ndoto Points na magari aina ya RAV 4 pamoja na zawadi kubwa ya Land Cruizer itakayotolewa mwezi Desemba.

‘’ Tunaomba wateja wetu waendelee kushiriki katika promosheni yetu ya ndoto ili waweze kujishindia zawadi hizi za muda wa maongezi na kunufaika kwa kuwa sehemu ya familia ya Zain,’’ alisema Njuju.

Njuju alisema zawadi hizo za muda wa maongezi ni utekelezaji wa matakwa ya wateja ambao waliomba zawadi ziongezwe katika promosheni ya Endesha Ndoto 2 ili watu wengi zaidi wanufaika.

‘’Siku zote Zain inawasikiliza wateja wetu ili kukidhi mahitaji yao na hilo ndilo limetufanya kuwa mtandao unaoongoza Tanzania.,’’ alisema na kuongeza kwamba Zain imezindua promosheni hiyo ya uaminifu ili kuwazawadia wateja wa Zain kwa kuwa katika mtandao wa Zain.

Hadi sasa Zain imetoa magari mapya aina ya RAV 4 nane. Zain itatoa jumla ya magari 11 mwaka huu ikiwemo gari aina ya Toyota Land Cruizer mwezi Desemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sadiki Elimsu tulikuwa pamoja pale "Kamandi" ya Tambaza Boyz.

    enzi hizo tukiwa chini ya uongozi shupavu wa Jenerali Mwalimu Felix Kulu-muna "father.

    Sadiki Elimsu alikuwa mkali wa Commerce na Bookeeping.

    ReplyDelete
  2. KAKA MICHUZI NAOMBA NITOE KERO YANGU NA TANGAZO ZA ZAIN LA "JAMES LEO MBONA UMENIPA MOJA...." JAMANI HALINA MAANA YOYOTE ILE TUNAOMBA LIONDOLEWE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...