askari polisi wa doria wawili wamekufa na wanne wamejeruhiwa, mmoja vibaya sana, baada ya gari lao kugongwa na basi la abiria la upendo.
kwa mujibu wa kamanda wa usalama barabarani afande kombe, basi hilo liliichomekea Landrover 110 la polisi lililokuwa kwenye doria ya kuangalia mabasi ya abiria yasijaze abiria na yasiende mwendo wa kasi.
mmoja wa majeruhi amepelekwa hospitali ya muhimbili na dereva kishatiwa mbaroni
Kwa kuwa imepata ajali gari ya polisi ndo tayari derva wa basi amechomekea, ingekuwa hiyo 110 anaendesha mfuga kuku habari ingekuwa yeye ndo kachomeka? hivi hata we misupu kumbe ndo walele.
ReplyDeletePole kwa waliofiwa and R.I.P wote waliopoteza maisha. Lakini hapo kuna somo limetolewa kwa polisi wetu. Waache kuchukua kitu kidogo kwa madereva wasiozingatia sheria za barabara.Madhara yake hayaji kwa walala hoi tu, yanafika hata kwa polisi wenyewe. Tuache kuchukua kitu kidogo, tuwaelmishe madereva.Wale wanaoshindikana sheria ichukue mkondo wake
ReplyDeleteMdau
Cardiff
yaani we acha tu. mara ngapi wabunge wamepata ajali na hatujaambiwa kwamba mmoja wao alichomekea.
ReplyDeleteJana(18/12/08) mitaa ya kamaa saa nane mchana pale mitaa ya kinondoni--karibu kona ya mahakamani karandinga la kubeba mahabusu lilipata ajali. Cha kushangaza sio ajali hiyo bali ni kwamba, gari ilikuwa limelala upande--juwa linawaka-lakini mahabusu wale waliachwa kwenye gari hiyo huku trafiki wakiwa wanapima. Hii siubinadamu--kwanza hao jamaa hawajahukumiwa bado
ReplyDeleteulikuwa haujui misupu ni serikali hana lolote ukikosoa huwa harushi comment yako. yeye huwa anafadhiliwa na kj kinyume ndo maana ziara zote yumo
ReplyDeleteInawezekana polisi ndo waliivaa basi lakini wanageuza mambo!hizo gari ni za trip ndefu aidha iringa,mbeya au tunduma hivyo kuzighasi mapema huku kibaha sio vema sana.Ikague basi-kama ina kosa ishikirie au tatizo litatuliwe sio kuzighasi tu bila sababu.
ReplyDeleteAJALI NI AJALI TU HAIJALISHI KAMA KWAKUWA WAMEKUFA POLISI NDIO MAANA DEREVA AMEKAMATWA MAPEMA AU LA, MI NADHANI KUKAMATWA AMA KUTOKAMATWA MAPEMA KWA DEREVA ALIYESABABISHA AJALI KUNATEMEA SANA NA MAZINGIRA YA AJALI YENYEWE. sWALA LA KUCHOMEKEWA KWA TZR, LINWEZEKANA NA PIA HALIWEZEKANI, HII ITAJULIKANA TU PINDI UPELELEZI WA TUKIO UKIFANYIKA KWA KUWAHUSISHA MASHUHUDA WA AJALI HUSIKA. tAFADHALI MASHUHUDA TUTOE USHIRIKIANI JAMANI EEEEEEEEEH ILI KUKOMESHA VITENDI HIVI VIOVU. TUTAENDELEA KUPOTEZA WATU KWA AJALI ZA KIZEMBE HADI LINIIIIII???
ReplyDeleteAnon wa 2:54 unasema kweli. Inasikitisha sana kumbuka Michuzi alipewa wadhifa huko Tegeta. Hivyo ukimkosoa JK atakuvuta shati.
ReplyDeletePoleni sana kwa msiba wa ndugu zetu wanausalama barabarani!! Matukio kama haya ya ajali zisizo za lazima barabarani kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na POLISI wenyewe kwa kuendekeza njaa zao na kutoa leseni kwa watu wasiostahili kuwa madereva hata wa MAGUTA ya sokoni Buguruni. Nawajua madereva wengi tu ambao wana leseni toka mamlaka halali baada ya kujifunza kusogeza gari tu mradi mshiko upo.
ReplyDeleteSishangai sana ongezeko la ajali Tanzania kwani hatuna madareva, hizo ndio gharama tulipazo kwa kukubali uzembe na ubinafsi kutawala maisha yetu.
Tanzania itaendelea kupatwa na misiba isiyo ya lazima hadi pale tutakapoamua kwa makusudi kubadili mtazamo wetu wa kushughulikia masuala muhimu na yenye kuzingatia usalama wa Taifa.
Pole Tanzania uzembe utakuangamiza
WAACHE KUFUKUZIA RUSHWA, NI WAO WALIINGINZA GARI YAO KWA MBELE ILI KUMLAZIMSHA ASIMAME NAYE AKAWALAMBA, ABIRIA SI WAPO WATASEMA UKWELI DEREVA GANI KICHAA ACHOMEKEE GARI YA POLISI TANZANIA HAJITAKI?
ReplyDeleteUntil a day we start treating trafic cases as murder cases
ReplyDeleteNdugu zetu wa Usalama Barabarani mmezoea kula na madereva ndio maana hawaogopi.Madereva wa ruti hii ya Dar/Mbeya ni mguu mtu.Gari hizi za Scania zinapelekwa hadi 160km/hr.Polisi wanajua hili lakini wanakula pamoja.Leo wamefanyiziwa mkuki kwa nguruwe.
ReplyDeleteSomo hapa ni ukicheka na nyani utakula mabua....!
Ndugu zetu wa Usalama Barabarani mmezoea kula na madereva ndio maana hawaogopi.Madereva wa ruti hii ya Dar/Mbeya ni mguu mtu.Gari hizi za Scania zinapelekwa hadi 160km/hr.Polisi wanajua hili lakini wanakula pamoja.Leo wamefanyiziwa mkuki kwa nguruwe.
ReplyDeleteSomo hapa ni ukicheka na nyani utakula mabua....!
Kaka michuzi!
ReplyDeletePoleni sana kwa msiba huo, lakini ijumaa ya tarehe 12 nilikuwa huko nyumbani na nilipokuwa njiani kutoka dar kwenda morogoro gari hilo la upendo na najmunisa yalinifanyia kitu mbaya sana barabarani, na hiyo haikuwa mara moja. Nakumbuka niliripoti matukio hayo kwa polisi wa usalama barabarani toka maeneo ya mbezi mpaka kibaha maili moja, na wote walinitazama kama kinyesi.Na hakukuwa na jitihada zozote za kuwasimamisha, au kuwakanya, licha ya matrafiki wetu kuwa na radio call na kila aina ya uwezo wa kuzuia uhalifu huo. Leo mwenzao kawatoka sasa sijui watachukua hatua gani au watakaa kimya.
Inasikitisha sana, lakini huu ndio ukweli.
Mdau - Ukerewe