Bwana Michuzi;
Baada ya kuchoka kukimbia huku na huko mtandaoni kusaka nyimbo za dini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismasi na mwaka mpya (2009), nimeamua kuanza kuzikusanya na kuziweka nyimbo mbalimbali za dini katika blogu hii:
nyimbozadini.blogspot.com
Nachukua nafasi hii basi kuwakaribisha wadau wote wanaopenda kusikiliza nyimbo za dini kuitembelea blogu hiyo. Ni lazima niseme pia kwamba ndiyo tu nimeianzisha blogu hii na kutokana na pilipilika kuwa nyingi sijapata muda hasa wa kuishughulikia ipasavyo na kwa hivyo uchanga wake unaonekana wazi. Maoni ya jinsi ya kuiendeleza zaidi yanakaribishwa.
Blogu yangu ya kiuchambuzi wa kiundani kabisa wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi yetu inakuja hivi karibuni. Natanguliza shukrani zangu Mwalimu Masangu Matondo Nzuzullima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huyu jamaa namfahamu, very intelligent guy and world class linguist. Cha ajabu ni kwamba ukienda pale Mlimani Idara za Kiswahili na Isimu na Lugha za Kigeni hakuna walimu kabisa. Ninalotaka kufahamu ni kwamba kuna jambo lo lote ambalo serikali inalifanya kujaribu kuwafanya wataalamu wetu na hasa wale katika nyanja nyeti kama udaktari na uhandisi warudi nyumbani? Tungetenga fungu kidogo kutoka katika mabilioni yanayoibwa (na kurudishwa) na mafisadi tukawapa nyumba, magari na mishahara mizuri watalaamu wetu wangerudi. It makes me sad kuona watu wetu wenye akili namna hii wakizinufaisha nchi za nje wakati walisomeshwa kwa hela za wakulima...J.K. please jaribu kulitupia macho suala hili.

    ReplyDelete
  2. Sasa unatukaribisha wakati kazi bado? Subiri iishe kwanza then ndiyo utuambie tuaje kuangalia bwana.

    ReplyDelete
  3. We annon wa kwanza hapo juu ni lazima ufahamu kuwa University haziajiri mtu yoyote tu ati kwa sababu ni genious! Kuna qualities za kuwa mwalimu wa University.

    Madaktari sawa.

    ReplyDelete
  4. Niko pamoja na wewe Anonymous.Huyu Bwana kweli ni mataalam mzuri ni pia bado ni kijana kwa hiyo watu kama hawa tukiwatumia vizuri tutafaidika.Kwanza ni mtu wa dini,pili ana familiar yake,tatu hana makuu.He is very good and got good qualitys let JK focus on people like him.Hongera mzee Matondo.

    ReplyDelete
  5. naungana na mtoa maoni wa kwanza lakini huyo wa nne amechemsha...eti ni mtu wa dini na anafamilia yake,.....mafisadi wangapi ni watu wadini na wametoa michango mikubwa sana makanisani? na wote wanafamialia zao pia.

    Ukweli ni kuwa kama kuna serikali ikiwa serious itafaidiaka na watu wengi tu sana. Wako wabongo wengi tu huku wanacredantial nzuri sana ambazo zingesaidia sana maendeleo ya nchi yetu katika sekta nyingi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...