Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya chapakazi ya nanihii na balozi maalum wa Zein,
Huku Ukerewe sijui umesikia yaliyotokea mchana wa leo jumapili?Lile daraja maarufu la pale katika kitongoji cha Stamford cha jiji la London nalo limekumbwa na balaa kama lililomkumba shetani mwekundu hivi karibuni kwa kubanjuliwa banjuliwa 1-2 nyumbani kwake, tukio lililotokea chini ya dakika nne za kipindi cha pili.
Tuseme kweli, kama ni kandanda hawa vijana wa Emirates hakuna awawezaye hapa Ukerewe, wanashindwa na mabavu tu na juju la kina Stoke city, Hull na Aston Villa.
Mlioliona pambano mtakubaliana nami kuwa Bwawa la maini ni asusa nyingine inayotusubiri, maana kwa futiboli tu Emirate kumekucha na hakuna katika timu nne za juu yenye mvuto na utaalamu pamoja na mbinu kama zile. Nani anabisha?
Jipatie kumbukumbu zako ndani ya ukurasa huu:
/leagues/premierleague/3536768/Arsenal
Mboni wadau rahaa!
Mdau Leicester

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...