Kundi zima la Jahazi Modern taarab, linaondoka nchini siku ya Ijumaa asubuhi na ndege ya Shirika la Ndege la uingeleza "British Airways" kueleka Uingeleza tayari kwa shoo yake itakayofanyika siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Silverspoon, uliopo pembeni ya uwanja wa Wembley.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, kiongozi wa kundi hilo, Mzee Yusuph, alisema kundi zima linaondoka na wanatarajia kurudi Dar es salaam tarehe 24 tayari kwa safari ya mkoani Tanga siku ya mkesha wa sikukuu ya Krismass.
Mzee Yusuph alisema hadi sasa wanafahamu kuwa watafanya onesho moja, hadi hapo wenyeji wao kampuni ya Jambo Publication Limited itakapotoa mwongozo wa shoo nyingine,lakini hadi sasa tunachojua kuwakuwa na shoo hiyo ya kusheherekea sikukuu ya miaka 47 ya uhuru wa Tanzania.
"Tunatarajia kutoa burudani safi kwa mashabiki wetu wa London na vitongoji vyake, tunakwenda kuwapata 'two in one' yaanikusheherekea sikukuu ya Idd El Hajji na sikukuu ya Uhuru, lakini pia na sisi tutawapa zawadi ya wimbo wetu wa Two in One, " alisema Mzee Yusuph.
Mratibu wa kampuni ya Jambop Publications inayodhamini safari ya kundi hilo, Juma Mabakila alisema maandalizi yote ya onesho hilo yamekamilika na iliyobaki siku yenyewe kuwadia na kuwataka mashabiki kuwahi mapema kwani ukumbi mwisho kuchukua watu 600 tu.
"Tumepewa onyo na wamiliki wa ukumbi kuwa hakutakuwa na watu wa ziada baada ya kufikia watu 600, hiyo aliwataka wale wanaotoka mbali kupiga simu namba 02083265606-7 na kuorodhesha jina ili hata ukichelewa jina lako litakuwa mlangoni ili kuepuka usumbufu,"alisema Mabakila.
Alisema mipango ipo mbioni kuhakikisha kuwa kuwe na shoo nyingine mbali ya hii ya London na kama kuwatakuwa na shoo hizo basi zitatangazwa siku ya Jumamosi ili kutoa nafasi kwa watu wengine watakaokosa nafasi kuwaona Jahazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Correct me if I’m wrong! This is the same guy in his song ‘Una Nyodo’; he insulted his ‘fellow Tanzanians’ in UK, I could say.

    I quote few words from his song; “Wadanganye wasiyojua paundi siyo mchezo, weka hapa weka pale ndiyo mkono uende kinywani [‘kubeba box’]”. “Mara Msomali mara Mburundi hela iwe mkononi”. It goes on “Tuli nimetulia Mzanzibari halisi, sipokei kwa malikia, viporo mi-siviwezi”.

    If you want to hear the full version of this song, copy and paste this link into your internet browser: http://uk.youtube.com/watch?v=wNAEjGJnUuA&feature=related

    Any way, for his ‘ignorance’ and ‘arrogance’, he doesn’t know that majority of so called his ‘fans’, who could be there in Silverspoon are the ones he insulted in this song. In fact, they are the ones who would be paying for his return ticket as [well as few quids to buy] second-hand suits in charity shops in London streets. And don’t forget, these are the same guys who would invite him for dinner in their council flats and accommodating him after ‘long performing nights’ at Silverspoon or any other place’! I should remind him; all of these are ‘VIPORO’ from MALKIA as referred to his song.

    Yusuf, I know you know this; “Baniani Mbaya, Kiatu chake Dawa”. And this is what you are trying do here! Welcome to UK, though it bitterly cold but I hope your hosts would spare you with their heavy jackets!

    This guy can be ‘talented’ to some, but he should learn to think critically before coming up with 'stupid lines' in his songs!


    Mzee Wauyagauyaga

    ReplyDelete
  2. MZEE YUSUF ANAKUJA LONDON, WENYE WAKE ZENU WAFUNGIENI MAANA YULE NI KIWEMBE!

    ReplyDelete
  3. Mzee wa Uyagauyaga, if you look at all songs and relate them to you, especially taarabu songs, then you will find all or most of them insulting. I agree with what Mzee Yusuf sang and his lyrics, because I have experienced them from my own relatives and some (not all) folks especially when they go back home, 'Nyodo' disrespect, and feeling they are better than anybody else. Yaani utakuta most of them hawana kitu, ni hiyo pauni ya malkia ndio inawasaidia na vibarua vya hapa na pale, hawataki kusoma kujiendeleza hasa wanawake, wao ni kushindana nani ana makochi mazuri, nani ana screen kubwa ya TV sebuleni kwake, elimu aah, ya nini, na wengine hata kazi hawataki kufanya eti kazi za hovyo, wakati watanzania wanaosoma shahada mbali mbali hata za Masters na PhD wanafanya hizo kazi za hovyo hovyo kwa sababu hawawezi kupata hizo pauni za Malikia. Heri ukutane na Mtanzania anayesota huku anasoma atakuona wa maana kuliko ukutane na hao wanao kula pauni za malikia wana nyodo kweli kweli. Na hasa wakirudi nyumbani huchagua kuanzia maji mpaka chakula, wanasahau kuwa ugali na kismavu ndicho kilichowakuza, hiyo ni mbali na kudharau kila kitu na kila mtu. Sio wote lakini baadhi yao wana nyodo haswa. Na mpaka wimbo ukuudhi basi umekutouch! Sanaa ni kioo cha jamii!

    ReplyDelete
  4. Kwa kuchangia tu , nilikuwa napenda kumpa 5 mdau wa hapo juu ndugu Mzee wauyagauyaga kwa comment yake inayohusu ujio wa "Al-anisa" oopppss ustadh Yussuf.kwa kweli hilo ni jibu tosha la muungwana kwa mjinga kama Yussuf. hapo inaonyesha jinsi gani wengi wa wasanii wa bongo wasivyo na mtazamo wa mbele wanaweza mtukana mamba kabla hata hawajavuka mto.leo Yussuf huyo huyo anataka kuja kukomba viji 10 pound vyetu tulivyo pata baada ya kubeba mabox, bila aibu wala soni ama kweli baniani mbaya kiatu chake dawa.ilibidi nicheke niliposikia Mzanzibar halisi anakuja kutafuta rizki kwa wabeba maboksi. waungwana huwa hawana majibu , jibu lao ni kukukaribisha. karibu UK.
    Mdau Zee la kitaulo -Leicester

    ReplyDelete
  5. Mhhh,mie sina maneno.Kwani sijui nimuunge mkono yupi.

    ReplyDelete
  6. Jahazi Modern Taarab pamoja na Jambo Publication mapromota, Watembezeni Jahazi Modern Taarab mitaani jijini London sehemu iconic za jiji la London na wachukue clips nyingi za video ili kujipromoti kimataifa ktk Youtube website n.k

    Msiwe kama Twanga, walikuja Uingereza/Holland hata kuchukua video clips za wana twanga pepeta wakivinjari Uingereza walishindwa.

    Waangalieni kina Xplastaz(wabongo wenzetu), KandaBongoman, Yondo Sister, Mbilia Bel, Saki n.k nafasi kama hizo wanazitumia kwa sana kujipandisha chati kwa kuwa na video za sehemu mbalimbali za dunia walizotembelea, wakiganga kuwa watakubalika kimataifa na kweli wanakubalika kimataifa.
    Kazi kwenu Jahazi modern Taarab na pia Juma Pinto wa JamboPublication na kina 'Mstahiki Meya' wa London.
    Mdau
    Rocky

    ReplyDelete
  7. mwandishi wa habari hii kaandika uingeleza kila mara au ameondoka nyumbani siku nyingi? ilitakiwa UINGEREZA.
    TANZANIA SASA IMEPIGA HATUA KUBWA YAANI KILA MIEZI MITATU ANAKUJA MSAANI TOKA TZ KUTUBURUDISHA. ASANTE SANA NAONA NI MATUNDA YA MZEE MWINYI KUSEMA KUWA RUKSA VIJANA KUSAFIRI SOON UTASIKIA WATANZANIA WANACHEZEA TIMU ZA HAPA. TAYARI KUNA KINDA CHELSEA AMBAYE NI MZANZIBARI.MZEE YUSUPH WALIOJILIPUA NI WAJANJA KWANI WANARUDISHA PESA NYUMBANI.TIZAMA TEN YEARS GENERATION YAO.

    KWANI INATIA RAHA UNAPANDA QATAR AU BRITISH UNAKUTANA NA MABAIBUI YA WAPEMBA(MAYAHUDI WA TANZANIA) WANANUKIA UDI,MARASHI.
    KUJILIPUA NI UJANJA NA UJASIRI.

    MIE NIMEJILIPUA NANYONYA TU KWA MALKIA. KWANI WAO WALIKUJA AFRICA NA KUJILIPUA KAMA WAMISHIONARI.

    ReplyDelete
  8. sina pingamizi na wale wote walokuja uk au walokwenda nchi yeyote na kujiripua ni uamuzi wao na ni ujasiri wao kwani sio wote wanaofanikiwa kuna tele wako katika detention hadi leo. kinachonisikitisha na mara nyengine kunichafua moyo ni mentality ya baadhi yao pamoja na wale wanaopita kuiba iba kwa kuanzia kuchanja card na mengineyo, mentality zao ni kama huo mfano wa huyo hapo juu annon. wa december 07, 2008 9:36 pm

    ReplyDelete
  9. Wewe 12:37 ni mmoja wa hao hao ...comment yako ya kudhalilisha wanawake ukome kabisa...ati hasa wanawake...tembea uone.....hao ulionao kama una hasira nao basi usidhanie ni wanawake wote hawasomi.......Njoo USA ujionee....Wana makoshi mazuri, big screen tv's na bado vitabu wamepanga kichwani.

    ReplyDelete
  10. Nijuavyo mimi maisha mtu anaweza kuyatafuta kwa njia nyingi,ili mradi siyo wizi,au ulaghai wa aina yoyote, hiyo haifai,kwahiyo kama mtu kaja kajiripua na kafanikiwa basi vizuri maana hiyo pesa anayopata huipeleka nyumbani tanzania,ila kwa uzoefu wangu wa kuishi ulaya,namshukuru MUNGU nimeshi ulaya zaidi ya sita na hii uk ni ya saba,ukweli ni kwamba watanzania wanaishi uk tofauti sana ,sana sana,na ulaya zingine,hapa hujui mwanamke nani na mwanaume nani,muda mwingi sana huutumia kusengenyana hasa inapofika saa kumi na mbili jioni(free phone),nasikia miaka ya nyuma walikuwa wanachongeana sana mpaka baadhi ya wazanzibar walirudishwa nyumbani,ni hii inatokana wengi kuwa wavivu wanataka pesa za bure tu,hata kama watakuwa wakali ukweli ndiyo huo,na habari ndiyo hiyo

    ReplyDelete
  11. Dada unayedai kuwa comment yangu ya kudhalilisha wanawake, naona hujawahi kukaa UK wewe, huku ni tofauti sana na US, kama uko US jaribu siku moja uje utembelee wala hutakosa mahali pa kulala. Maana watanzania wako kibao. Tatizo sio kujilipua wala nini tatizo ni nyodo kama hizo zako sasa kimekuuma nini kusema ukweli kuwa wanawake wengi walioko huku hawasomi? Hivi unategemea mustakabali wao hapo siku za usoni utakuwa nini? Mbona nafasi za kusoma wanazo kibao ila ndio hivyo wao wanaona bora kutoka na vibaby pushers, kuzunguka madukani, kwenda parks, au kulala na kuamka saa tano ya asubuhi kwa kuwa tu wanapata pesa za kula kutokana na allowance za watoto? Hivi mtu unaenda nchi ya watu kula na kulala au kutafuta opportunities ili zikusaidie wewe na familia na taifa lako kwa ujumla.

    Njoo ujionee tena njoo na bwana wako maana watakuchukulia mchana kweupe, halafu ndio utaniambia ukome vizuri, kama hujui south london ni Kariakoo basi ndio utajua mwaka utakaokuja. Jaribu tu tafuta shoga, halafu utaona na hicho kisomo chako. Halafu nimeshangaa sijui umekasirika nini eti njoo ujionee US hapa tunazungumzia hali halisi ya UK na kama unabisha jaribu! Na kuisema hali hiyo pengine itasaidia kuongeza idadi ya wanawake wanaojitambua na kuona umuhimu wa kutafuta elimu! Eti makochi mazuri na vitabu kichwani naona kichwa chako vitabu vyake havijapangika sasa ishu hapa ni mashindano, fulani kanunua fenicha IKEA ngoja namimi nikanunue kushinda ile, na kusengenyana masaa mawili kwenye simu kama alivyosema dau hapo juu. Kama unaona kuwa kushindana kuhusu nani ana makochi mazuri na screen ya TV kubwa nyumbani kwake ni jambo sahihi basi nina mashaka na hivyo vitabu vilivyomo kichwani mwako!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...