karen paul sabuni akifurahia baada ya kupata kipaimara hivi karibuni hapa dar. chini akiwa na wazazi wake na ndugu wakati wa sherehe



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Naomba kuuliza kwa kuwa sio Mkiristo. Kipaimara ni kubatizwa? Kuna mila kama hizi pia nchi za Marekani ya Kusini ambapo wasichana peke yao wanabatizwa wakiwa na umri wa miaka 15. Inaitwa "cinconiera" yaani 15.

    ReplyDelete
  2. Hapana. Kipaimara si ubatizo, bali ni kuukiri ubatizo (Mkristo anabatizwa akiwa mdogo, hivyo mdhamini anamsemea imani yake, ila anaithibitisha akiwa mtu mzima).

    Mila ya Amerika Kusini ni tofauti, ni kama kipaimara na kuwekwa mafundo/jando, ambapo hutokea wakati wa balehe. Mila hizi zilikuwepo kabla ya Ukristo (kama sisi tulivyokuwa na taratibu zetu), ila wakazi wa kule wakazichanganya na Ukristo na kuwa hiyo unayooiita "cinconiera". Nadhani umeelewa kidogo.

    ReplyDelete
  3. Kipaimara ndio nini tena, wa-jameni?

    ReplyDelete
  4. ukichunguza utakuta magharibi wanasherehekea haloween kama sherehe ya kidini na afrika hamna.

    Kwa hiyo watu huchukua mila zao na kuziweka kwenye dini.

    sidhani kama mila hizi hukubalika kwa Mungu (yaani kutekeleza mila hizi inaweza kuwa haina ujira kutoka kwa Mungu kwani hakuzianzisha).

    ReplyDelete
  5. Naona aliyeeleza hapo juu amesema sahii. Sasa kwa kidhungu ni confirmation. To confirm your faith.

    ReplyDelete
  6. Anony 6:37, ahsante kwa kunielimisha.

    Ni kweli kila pahali dini huwa zinachanganyika na mila za watu wao. Kwa mfano, mila za arabuni zinawabana sana wasichana wao na utaona wao ni wakali kufuata dini ya kiislamu ya kuvaa baibui na kuolewa mapema iwezakanavyo lakini waislamu wa Afrika tunaamini vile vile Kuran lakini wasichana wetu wengi hawavaii baibui na wanaruhusiwa kusoma na kuolewa baadae. Pia wengi hatufuati sheria za kidini (Sharia laws) na hatuwakati mikono wezi. Pia, nchi nyingi za Kiislamu za Afrika, tunaweza kununua bia kila kona.

    Ukiristo wa Ulaya pia umepoa ukali kuliko wa Afrika. Kuna wakikisto wachache wanaopinga mapadri wasiwe na mapenzi na wanaume wenzao lakini kitu ambacho Afrika bado hatukielewi kwa kuwa tunaamini biblia inakataza hilo jambo. Wakiristo wenye siasa kali ulaya sasa wanaungana na wenzao wa Afrika kupinga kuruhusiwa mapadri kuoa (wakatoliki)au kufanya mapenzi na wanaume wenzao (anglikani).

    Halloween sio kama inasheherekewa kama dini kama anony wa 9:58 anavyodai, ila ilianza wakati baadhi ya watu wao walikuwa wanaamini uchawi, moto, jua, na kadhalika. Siku hii ya haloween sasa ni biashara ya kuuza pipi kwa wafanyabiashara wao (dola bilioni 4 mwaka jana) na sio siku kuu ila watoto wanaenda kwenye nyumba za jirani na wanapewa pipi.

    India pia kuna watu wengi wanaamini jua na moto. Kuna nyumba moja karibu na ubalozi wa Palestina, Upanga, ambako watu wanakusanyika wanasheherekea hii dini Dar Es Salaam.

    Pia, kuna watu pia India ambao hawaziki wala kuchoma mwili, zoroastrian kama sikosei, ila wanaanika mwili katika jumba moja na kuwaachilia mwili uliwe na wadudu na ndege.

    Kwangu binafsi, imani ni baina yako na Mungu wako, ndio maana serikali imejitoa katika dini na inaheshimu dini zote. Mtu yoyote hana haki ya kusema dini yake ni bora kuliko yako au Mungu atakulani kama unafuata dini kadhaa na kadhalika. Hii inasababisha watu kutopendana na mwisho wake ni chuki na vita kama historia inavyotuonyesha.

    Ahsante kwa kunielimisha, nategemea pia nimewaelimisha wengine hapa pia.

    ReplyDelete
  7. Inaelekea we jamaa juu hapo wa 23/12/08 6:00 unaamini stereotypes. Kama tuanvyojuwa, hakuna msichana huolewa bila kupata muoaji dunia nzima. We unasema eti arabuni wanaolewa wadogo, kwani sheria ya bongo umeisoma? Halafu hebu nipe tofauti ya neno sharia na sheria, navyofahamu moja ni la kiarabu na lingine ni la kiswahili lenye asili ya kiarabu. Sijui kama ulikuwa unalenga Islamic Law?

    Ni kweli pia bongo hatukati mkono wezi ila twawavisha matairi na petroli na kupiga moto.

    ReplyDelete
  8. Asilimia 95 ya watanzania wanaishi vijijini, na wasichana vijijini wanaolewa wakiwa na umri wa 12, 13, 14, 15, n.k. Msichana wa umri wa miaka 18 kijijini anaonekana mzee, jinsi gani mtu anasema tanzania wasichana wanaolewa late?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...