Na. M. M. Mwanakijij wa
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Balozi wa Kudumu wa Zain,
Nimesoma mada ya “Suti na Lebo yake” ya mdau mmoja hapa. Kwanza nikiri kwamba mimi ni mmojawapo wa wavaa suti na lebo yake! (Hili lisikutatize kwani mimi mwenyewe mshamba mshamba hivi!) Kilichonishangaza kwenye mada hiyo hasa siyo swali lenyewe bali ni jinsi gani watu wamekuwa wataalamu wa lebo!
Yaani nimecheka hadi kona za masikio zinauma majibu ya wataalamu wetu wa uvaaji nguo zenye lebo na zaidi hasa jinsi gani kuna watu ambao wamekuwa waamuzi wa mavazi ya suti. Naamini kuna kautalaamu ka aina fulani hivi! Mimi nimeshangazwa na jinsi watu wanaonekana kukerwa na suti yenye lebo yake!
Ni mdau aliyesema hivi ndiyo amenifanya niandike kwa kifupi: “Mdau nakushukuru sana kwa kunisaidia kupigana na hii kero. kuwa na lebel kwenye sleeve NI USHAMBA WA KUFA MTU!!!!!!
Nishawahi hata kuwatolea mifano mingi kuwa sio siri kuwa JK ni mtu wa pamba. Sasa huwa nawauliza hivi mshamuona hata siku moja akiwa na lebel? Maana siyo siri JK anajuwa kupiga pamba tena siyo mvivu wa kuchagua. Jamani tuache ushamba. ondoeni lebel hizo kwenye misuti yenu eebo!!”
Yaani mtu amekerwa na lebo! Kinachonishangaza ni kuwa wengi wetu hatukerwi na vitu vinavyotupasa kutukera na mara nyingi tumekuwa tukivufumbia macho vile vinastahili kutukera kweli.
Nitatolea mfano suala la ATCL. Hivi kwanini imechukua mwaka mzima kwa Serikali kuonesha kukerwa na ubovu na uozo huo uliodumu kwa karibu mwaka mzima? Hivi hii kero ya kina Mattaka na Nyang’anyi kwanini imefumbiwa macho na vyombo vyetu vya habari hadi imefumuka siku hizi chache!?
Kwanini hatujakerwa na mauaji ya Albino kiasi cha kuandamana kutaka wale waliopewa dhamana ya ulinzi wa taifa letu kuwajibika?
Hivi mnakumbuka jinsi yule “Sniper” na msaidizi wake walivyoitisha Marekani walipoanza kuwapopoa watu kwa risasi? Baada ya kosa kosa ya kumuua yule mtoto wa miaka 13 Iran Brown, Mkuu wa Polisi alisema kuwa sasa suala hilo limefikia “personal”.
Taifa zima lilikerwa na jambo hilo na nguvu zote za usalama zikaelekezwa kuwatafuta wauaji hao. Sisi leo zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine kujeruhiwa na bado tuna ujasiri wa kufuatilia malumbano ya mfanyabiashara na wanasiasa na kuyaandika kwa kirefu!
Tunajadiliana kukerwa na lebo!
Hivi unaposoma kuna shule ya Ufundi Moshi imelazimika kufungwa kwa sababu ya “kukosa chakula” Kwamba katika nchi yetu ambapo wapo wanaokula na kusasa, kuna mahali watu wanashindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa chakula!
Sisi tunakerwa na lebo na jinsi gani mtu amevaa suti aliyoinunua yeye mwenyewe au kuiazima! Mheshimiwa Mdau, inawezekana mambo “serious” hayana mvuto wa fikra zetu, na mambo muhimu na yenye kuhitaji kugonganisha vichwa (brain storming) yanawahusu wataalamu, wasomi na wanasiasa.
Yawezekana pia bulogu yetu ya jamii ni kwa ajili ya kurelieve stress za maisha ya kila siku! Kama hayo ni kweli siwezi kusema.
Lakini ukweli unaoonekana na kutukodolea macho kama panya aliyebanwa na mtego ni kuwa yanapokuja mambo ya kitaifa na ya msingi, Watanzania tuko kama tumerogwa hivi! Tunakaa pembeni na kuwaacha wanasiasa na makuwadi wa ufisadi watawale nchi yetu wapendavyo!
Hata leo akiibuka “Obama” wetu na kuja na maneno kuwa “Change is coming” na kuwa “Yes we Can” ataangaliwa kwa kejeli na kuulizwa kama suti yake ina lebo! Ni kweli tukerwe na vitu vidogo vidogo, na tukosoea na kujisokoa kwa vitu visivyo na msingi (trivial) kwani yote ni maisha lakini ni lazima tuweke kipaumbele cha kutovumilila kero kubwa kubwa au kuzifumbia macho kwa sababu zitafufanye tuonekane wanasiasa au watu wenye matamanio ya kisiasa au kuonekana tuna wivu kwa watu walioko madarakani!
Nikijibu swali la lebo, ni kuwa ni kuwa naendelea kuvaa suti na lebo yake kwa sababu tangu nianze kuvaa nguo za mzungu sijawahi kukaa chini na kuanza kunyofoa lebo. Sijatoa lebo ya kaptula, shati, suruali, n.k! Sasa iweje leo nianze kunyofoa lebo iliyowekwa hapo kwenye suti kwa kujiona mjuaji.
Kama ingekuwa ni zile stickers zinazoonesha ukubwa wa nguo tungekuwa na mjadala, lakini suala la lebo ambazo si za kunyofolewa kwanini tujione tumeendelea kwa kuzinyofoa!?
Isije kuwa washamba siyo wanaovaa suti zenye lebo zake!
Wataalmu wanasema kwamba pamoja na umasikini, watu weusi ndio dampo la materials and design things. Fast food, maduka makubwa makubwa weka kwa weusi kwani ndio wateja wakubwa. Wazungu hela zao wanaweka akiba na wanafikiria kesho.
ReplyDeleteHiyo tabia ipo pia kwa wabongo wengine ambapo ni kufikiria tu kujirusha, nani anamjua nani, nani kavaa nini, can not focus on your self kazi tu kufikiria watu.
Civilized people are liable to change when they see the truth. Please, give us more facts! Angalieni, msije kuambiwa kuchamba baada ya kufanya haja kubwa ni ustaarabu mkakataa eti kwa vile kuna watu hawakai kwenye madawati shuleni.
ReplyDeleteBabao
Watu wanaotaka kusoma mambo ya ATCL, Buzwagi, Richmond, EPA, na kero au siasa za chuki watakuja kwenye saiti yako. Saiti ya wakereketwa wa OIC mahakama ya kadhi na kadhalika kila saa. Huku kwenye blog ya jamii, tuachie sisi, wavivu wa kufikiri, au kama tuanvyokunukuu:
ReplyDelete'Hivi kweli tunakerwa na vitu vidogo vidogo, na tukosoea na kujisokoa kwa vitu visivyo na msingi (trivial) kwani yote ni maisha lakini ni lazima tuweke kipaumbele cha kutovumilila kero kubwa kubwa au kuzifumbia macho kwa sababu zitafufanye tuonekane wanasiasa au watu wenye matamanio ya kisiasa au kuonekana tuna wivu kwa watu walioko madarakani! '
Kuna blog elfu za mtazamo wako, pamoja na za kwako, hatuendi huko, pengie kwa sbabu ulizozisema lakini pia sio wajinga kiasi kuwa kila saa ni siasa tu za vyama au uadilifu wa serikali
pengine wewe ni msomi na mwansiasa, mwanaharakati na mpiganaji wa agenda ulizoziahagua. Hata sisi tukitaka kusoma agenda hizo kwa matzamo wako tutakuja huko kwako, jambo au jamii. Pia wewe huchangia katika magazeti zaidi ya 7 hapa Tanzania.
ReplyDeleteTunaipenda hii site au blog kwa sababu tuko huru kuzungumzia jambo lolote lile na hata katika hayo unayoona wewe ni trivial ua upuuzi kuna mantiki na hoja nzito.
Tuachie sisi tuzungumze juu ya taswirazzzz, lebozzzzzz, fulanazzzzzz, vikwapa, vichupi, tarabu na misaada ya kwenye tutazzz.
Katika blog zingine kuna ubaguzi na kuweka msingi ya chuki ambayo wewe huipendelea zaidi. Sio kila mtu anapendelea hivyo.
Fungua mijadala kwenye website zako juu ya kukosa chakula shuleni, usafiri wa wanafunzi, nauli za daladala, kukosekana maji, kufungwa kwa vyuo vikuu, kesi za Manji, Masha,Mengi, Yona, Mramba, Mgonja na ufisadi uliokithiri BOT, Madini, Ardhi, PSRC, nk
ReplyDeleteYatajadiliwa huko. Heshimu watu.
Mtu kavaa label ndani nje, chini juu inahusu nini upeku peku usio kuwa na kichwa wala miguu?
ReplyDeleteMbona vitu vingine ni personals haviwahusu, mtu hajakuomba pesa ya kununua suti yake, kavaa mwenyewe apendavyo bado mwataka kumpangia mnavyotaka nyie? Mwisho watu waataanza kupekuliwa mpaka nguo za ndani kisa fasheni! Fasheni ni kitu cha kupita tu, leo wanavaa na labels kesho watazua lingine.
Kama nyie kweli ni watu mnaojifanya mnajali uvaaji, mbona hamusemi vijana wenu wanaokwenda makalio wazi wanaonyesha nguo zao za ndani hadharani! Suruali inashuka wee mpaka inataka kufika magotini mbona hilo haliwakeri au kwa sababu wameiga kwa Wamarekani kutembea nguo za ndani zinaonekana wazi! Suruali mpaka zinataka kudondoka chini si za watoto wa kike wala wa kiume, na sijaona hata siku mmoja mtu akisema amekerwa!
Pilipili usoila inakuwashiani?
mdau wa 19/12-10:48pm nakubalian nawe kabisa na wazo lako.
ReplyDeleteMzungu hata akiendesha Ford Focus iwe A,B, au C Reg. hata hajali.
Wabongo na Wapopo bwana wasipoendesha ML, BMW X3-5, Lexus RX au gari yoyote ile ya thamani anajiona hajatimia.
Tumekuwa kama kina Papa siku hizi tutavaa Cavalli kulala kwenye sakafu na baridi hili tunaona tumeula kumbe tunapotea.
Mawazo mazuri lakini kama tujuavyo, AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE. NDIYO MAANA WATU WANAJIZOLEA MAMILIONI TU BILA HOFU KWA SABABU WANAJUA HAKUNA ATAKAEMSHTAKI.
HIVI MTU KAMA MRAMBA ALIYEKUWA SERIKALINI TANGU ENZI YA NYERERE HADI ALIPOKAMATWA HIVI MAJUZI, IWEJE AWE NA MALI INAYOFIKA BILIONI SITA HUKU AKIWA MTUMISHI WA SERIKALI?
HATA TONY BLAIR ALIPOINGIA MITINI, BADO ANAFUATILIWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA NA HUENDA AKASHTAKIWA MARA USHAHIDI NA VIELELEZO DHIDI YAKE VITAKAPOKAMILIKA.
HUYO NI MRAMBA! MKAPA ATAKUWA NA BILIONI NGAPI (DOLA) JAMANI?
YULE MSUKUMA ALIYEKUMBWA NA KASHFA YA KUWEKA MABILIONI YA FEDHA JERSEY AKADAI "VIJISENTI" NAYE AMEISHIA WAPI? TUAMKE SASA WAJAMANEI NCHI INANYONYWA KAMA ENZI YA UKOLONI!
BORA ZAMANI TULIKUWA TUNAFAHAMU, LAKINI SASA HIVI TUNANYONYWA NA VIONGOZI WANAOCHAGULIWA KUONDOA UMASKINI WA WANANCHI! BALAAA GANI HILI.
NILISOMA KWENYE GAZETI LA "THIS DAY" HIVI KARIBUNI NA KUNA SERIKALI IMEPOTEZA ZAIDI YA DOLA BILIONI 300 KWA KUTOKUSANYA KODI YA WACHIMBA MIGODI(TAX EXEMPTION).
HII HAIPO KATIKA ULIMWENGUNI KOTE. UK UNADAIWA KODI HATA KAMA UNAFANYA KAZI NDOGO YA KUJIINGIZIA KIPATO BAADA YA MUDA WAKO WA KAZI ZA KAWAIDA( WORK FROM HOME OR OUT OF WORK INCOMES).
KIPATO CHOCHOTE LAZIMA UFAHAMISHE IDARA YA MAPATO. WAO NDIYO WATAAMUA KAMA WAPUNGUZE KODI YAKO YA MWAKA AU WAONGEZE. LEO TUNASEMEHE KODI YA WACHIMBA MIGODI WANAOJIINGIZIA MAMILIONI! INAINGIA AKILINI KWELI.
KAMA HIZO $300 BILIONI ZINGEKUSANYWA, ZINGEWEZA KUSAIDIA KIASI GANI KUPUNGUZA UHABA WA MADAWA HOSPITALINI? KUSAIDIA ELIMU KWA WATOTO WA MSINGI?
HIVI IMEFIKIA WAKATI MTU WA KIPATO CHA CHINI HAWEZI KUMSOMESHA MWANAE MPAKA AWE NA MAMILIONI YA FEDHA?
NASIKIA UCHUNGU SANA HASA NIKIFIKIRIA ENZI ZANGU NILISOMA KWA MCHANGO WA UPE ILIYONIGHARIMU SHILINGI 20. TOKA LA KWANZA HADI LA SABA. SEKONDARI BURE KABISAAA. SASA VIJANA WETU, WATOTO WETU HAWASOMI SHULE ZA BURE KWA KUWA SERIKALI HAINA FEDHA. BAJETI INATENGA NINI KUSAIDIA WANANCHI?
I THINK IT'S TIME NOW WE MUST WAKE UP AND START HARRASSING THE SO CALLED POLITICIANS. THE PEOPLE WHO STAND THERE TO LOOK AFTER THEMSELVES. THEY 'RE NOT THERE FOR THE BENEFIT OF PUBLICS WHATSOEVER.
IF WE CAN MAKE MASSIVE SOLIDARITY LIKE THE ONE HAPPENED WHEN STARS CAME BACK FROM SUDAN, IT MAY HELP IN ONE WAY OR ANOTHER TO TELL THOSE PEOPLE "THEIR TIME IS UP. THEY HAVE TO CHOOSE EITHER TO HELP PUBLIC WHO SUFFER THE MOST OR STAND DOWN AND FACE THE CONCEQUENCES FOR LETTING US DOWN.
I HAVE A DREAM....THIS IS VERY VERY VERY SERIOUS.
I HAD A DREAM AND I WANT TO FULLFIL MY AMBITION.
I WANT TO COME BACK HOME AND STAND IN THE GENERAL ELECTION AS PRESIDENTIAL CANDIDATE AND WIN THAT ELECTION.
I PROMISE YOU GUYS. I 'LL NEVER EVER SLEEP OR EAT PROPERLY IF YOU PEOPLES ARE STRUGGLING EVEN TO FIND A ONE DAY FOOD TO FEED YOUSELF OR YOUR FAMILY.
WE HAVE TO BELIEVE FROM NOW. I KNOW I CAN DO IT. BUT NOT ON MY OWN. I NEED PEOPLE WHO KNOWS, PEOPLE WHO SUFFERED AND STRUGGLE IN THEIR LIFE TO HELP OTHERS. YOU EDUCATION IT MAY BE HELPFULL BUT I VE SEEN WELL EDUCATED PEOPLE AND THEY ARE OIN THE POWER, BUT THEY JUST HELP THEMSELVES.
I HAVE A DREAM...A DREAM TO REVOLUTIONISE MY PEOPLE. THE HOPE WHICH FALL IN MY HEART, IT'S BIGGER THAN WHAT YOU THINK. I'M COMING TO GET RID OF ALL 'EM AND TAKE MY COUNTRY TO THE NEXT LEVEL.
Kweli wewe mwanakijiji ni mshamba mshamba kama ulivyosema mwenyewe.
ReplyDeleteNa wewe anony hapo juu sijui unasema nini. Kama mtu hakuombi hela ya nini umpangie jinsi ya kutumia. Wabongo jirusheni mpaka Yesu arudi. Na sidhani kama kuna tatizo mtu kufikiria na kama mtu hufikiri kisayansi wewe ni mfu.
i am lost. are we talking about obama, ATCL or lebo. summarize mzee, the article is too long.
ReplyDeletewe mwanakijiji hizi hukusikia kama timu ya taifa ilishinda? kazi kulalamika tu.
ReplyDeleteMwanakijiji nakubaliana na wewe juu ya sisi kuzifanyia kazi kero muhimu hasa masuala yanayoihusu chi yetu na ningeshauri watu serious wavisit tovuti yako ya mwanakijiji.com . Kwa hilo tuanze na si tu kukemea ufisadi bali kuwaondoa madarakani kwani wanalindana kuanzia top.
ReplyDeleteKuhusu label, you're wrong brother! Tuwe tayari kujifunza kutoka kwa wanaojua. Nimeona mada hii ilipoanza hapo chini kuna watu wamesema hata kina Beckham, Rio na wanamuziki wa U.S wanavaa suti na label. Ukweli ni kuwa hata ughaibuni kuna washamba wa kuvaa nguo, some of them are big stars! Kuwa na hela pekee hakumbadilishi mtu uvaaji wake. Music stars wangapi hawaendi na wakati kifashion?!
Labels zinawekwa kwenye sleeves kusaidia customers kujua who tailored/designed the suits kiurahisi i.e huhitaji kuanza kuivuta suit kwenye hanger ili kuona the made by label inapokuwa dukani, kwani hivyo unaweza kuiharibu.
Wakati wa maonyesho, models wanavaa suits/blazers na labels zake ili ku promote the designers.
Unapoinunua inabidi uitoe label, kumbuka labels hizo, unlike the ones inside hazikushonewa with a normal stitch ambayo ingesumbua kutoa. Zimeshikishwa kiaina tu ili ilwe rahisi kutoa.
Hao wanamichezo au music stars, especially weusi, ni ushamba tu wa watu kutaka kuonyesha wanavaa designer gani. Pia ikumbukwe hawa watu wanapewaga hizi nguo bure na designers ili kuzipromote hivyo inawezekana wanapewa conditions kuzivaa na labels. Hii inaweza kuwa news kwa watu wengine, but it's a fact.
Acheni mambo ya kila mtu anaruhusiwa kuvaa anavyotaka, hayo ni katika mashati ya vitenge!
Suits ni utamaduni wa ki West, na kama tunazivaa, tuwaige wao. Hutamwona yoyote kati yao akivaa na labels. Angalia their Presidents, princes, actors na hata watu wa kawaida in their business or even evening suits.
Nimeona nyumbani TZ watu wanashona suits zikiwa na suruali pana kama za watu wa ndombolo, they don't look smart! Pia uvaaji wa makoti oversize ambo nafikiri ulianzia na black americans. Naelewa ulegezaji wa casual baggy pants wa siku hizi na historia yake, hapo kila mtu ana choice ya kuvaa or not. Lakini, suti ni suti mjomba, hata P Diddy amejifunza hili!
Kumalizia, kuna mtu kamsifia J.K kuwa mvaaji mzuri wa pamba. ushauri wangu ni atafute mtu anayejua haya mambo, so many times namuona rais wetu amevaa a wrong suit in an occasion. He should stick to business suits akiwa kazini na dark evening suits akiwa kwenye tafrija za jioni. aachane na fancy shirts au suti za mistari. Yeye ni rais!
Fungua macho.
Nimefurahishwa sana na mabishano yako juu ya LEBO, ni kweli LEBO/LEBAL haikuwekwa ili inyofolewe, mbona hatunyofowi zile za shati ama suruali zilizo kwa ndani! acheni mabishano yasiyo ya msingi kama hutaki suti yenye lebo nje usinunuwe, full stop, lakini uzimlazimshe mtu anayezitaka kunyofoa, eti JK ni mtu wa pamba, kwani yeye nani/ ana authority gani juu ya design za mavazi, ni mteja kama mteja mwingine tu hununuwa zile azipendazo tu, hivi wale waliokulia miaka ya 60,70 na 80 wamesahau lebo zilivyokuwa deal enzi hizo? watu walikuwa wakibandika wenyewe achilia mbali hizo toka kwa designer.
ReplyDeleteMdau wa mwanzo ka make point kila mtu anajuwa vaa vyovyote muhimu jiweke safi wa mwili na roho pia. navaa kwa heshima mwenyezimungu ndio anavyopenda, tizama waimbaji wanavaa bling bling ndio tunavyopenda sie? au rapa states kava bei gani? asilimia kubwa ni sie watu weusi ndio tuko hivyo wauzaji ndio wanafurahi wanakula pesa wanatizama familia zao sie hatufikirii kazi kutenda tu. Ndosi.
ReplyDeleteMwanakijiji naungana na wewe 100%, thanks for giving us something to ponder.
ReplyDeletewell said mwanakijiji.huwa nashangaa sana swala la kijinga huwa linapewa kipaumbele kuliko swala muhimu humu ndani.sina mengi ya kusema kwani umeyazungumza yote mwana kijiji na mdau wa december 20 1:13 am.
ReplyDeleteby mzawa
Tafuta jimbo ugombee ubunge. Utapata fursa ya kujadili hayo yanayokukera ATCL etc. Haya mengine tuachie!
ReplyDeleteKama utasoma maoni ya watanzania wenzangu hapo juu utaweza kugundua kama sisi mawazo yetu yanafikiri kwenda mbele au yanakimbia kwa kasi ya ajabu kurudi nyuma...
ReplyDeletemwanakijiji mambo yako ya siasa unayaleta huku kutafuta nini. unatuharibia ladha sisi wapenda udaku.
ReplyDeletemoshi tech imeingiaje mwanakijiji mambo ya umbea tuachie wenyewe. siyo kila mtu anapenda stress za siasa. kwa nini unatulazimisha mambo hayo. wewe si una tovuti yako ya kupigia kampeni. acha kutuboa
ReplyDeleteWabongo tunabishana mno! ebo! hatuna dogo? naungana na mwanakijiji kwa asilimia zote. Tangu lini mwaswala nyeti kama EPA, ATCL yakawa na wenyewe? Haya yanamhusu kila mTz, sikatai kufurahi na mambo ya jamii lakini malumbano mengine yakijamii ni kupoteza muda ambao ungeweza kuinua hali ya uchumi kidogo!Label kuwa nje ya suit ndivyo ilivyokuwa kusudi la aliye-design, kama hupendi za aina hiyo, kuna suti ambazo hazina label nje, nunua, vaa and shut up! kama kuna anayevaa suti yenye label nje, vaa tinted glass isikuchefue, mwe! Kuna mambo ya msingi ya kuyawazia ati, c'mon Tanzanians, get over that nonsense!
ReplyDeletehii aluta kontinyua ipeleke jamiiforum. kama mdau hapo juu alivyosema hii tovuti ya mithupu is designed kuondoa stress na kupashana khabari ndogo ndogo za hapa na pale, tusiigeuze ikawa kama jamiiforum maana ile tovuti utazania mko kwenye kampeni ya mrema
ReplyDeleteBADO WALE WANAOCHOMEKEA MAKOTI YA SUTI NA KUKUNJA MIKONO YAKE NA VILE VILE KUNA SHERIA ZA UVAAJI WA SUTI
ReplyDelete1.USICHEKE KWA SAUTI AU KUKENUA MENO
2.USIPANDE DALADALA ESPECIALLY VIPANY
3.USIBEBE PLASTIC BAG - RAMBO
4.USITEMBEE KWAMIGUU UBUNGO-POSTA
5.USIKIMBIE KIMBIE KUFUKUZIA DALADALA
6.USITAFUNE GUM CHWA CHWA CHWA
7.UKIIBIWA USIPIGE KELELE MWIIIZI MWIIZI JUST SAY IT EASY MWIZI MWIZI
8.USILIE KWA SAUTI HATA UKIFIWA NA MAMA YAKO
9.USICHOMEKEE KOTI PLEASE
10.USIVAEE SUTI NA BOOT VIATU VIKUBWA
Mwanakijiji naiunga mkono hoja yako ya kua kunamambo mengi muhimu yametokea na yanaendelea kutokea lakini hatuyapi uzito nabadala yake tunaendelea kujadili mambo mepesi ambayo nafasi yake katika kutatua matatizo ya jamii ni finyu.Si kweli kwamba watu haya mambo mazito watu hawayazungumzii watu wameyazungumzia na wanaendelea kuyazungumzia lakini hakuna matokeo au ufumbuzi wowote mbali ya mazingaombwe tunayoendelea kuyashuhudia.Kitendo cha watu kujadili mambo mepesi ka label za suti n.k.Ni dalili ya watu KUKATA TAMAA!Kitendo ambacho ni hatari.Kitendo hiki nakifananini sha na hadithi ya mtoto mtukutu mchunga mbuzi ambae alikua akiwasubua wanakijiji kwa kupiga kelele kwamba kuna mbwa mwitu anashambulia mbuzi na kuomba msaada baada ya wanakijiji kujitokeza kuja kutoa msaada wanakuta ya kua ni utani kijana huyo baada ya kurudia vitendo hivyo mara kwa mara ikatokea kweli mbwa mwitu kavamia mifugo kijana huyo alipopiga kelele kuomba msaada hakuna aliyetokea wanakijiji wakidhani kua ni utani madhala yake yalikua makubwa!TUSIKATE TAMAA MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteNdugu yangu mwanakijiji na mambo yako ya KLH NEWS NA CHECHE ZA FIKIRA,Naomba uelewe kitu kimoja muhimu sana watu wamegawanyika,na kuna watu awana fikila kama zako kuna watu leo hii awajui hata kama kuna EPA UFISADI NA ATCL kunani huko,lakini pia ujue kuna watu awajui hapa TZ.kuwa Mbilia beli kaja kutumbuiza,hivyo usilazimishe watu kufuatilia wasiyopenda na si lazima watu wote wawe na uchungu wa kifo cha ATCL,Kuna watu wanaweza lia pale watakapo sikia BILLS CLUB imeungua HABARI NDO HIYO
ReplyDeleteMimi na ukoo wangu wote hatjuwahi kupanda ndege, wala hatujafaidi kodi inayotokana na ndege ya ATCL miaka yote. Ikiwepo, isi wepo hatuini faida yake. Wewe ndio unaona uchungu na labda unahisi ungekuwa Chairman au Meneja Mkuu wa hiyo ATCL. Sisi haturajii ajira huko hata za kupangusa vumbi hizo ndege.
ReplyDeleteUlikaa kiya wakati wa tenda ya kuwapa SAA, sasa huu mwaka ambapo ATCL imetoka huko na madeni kibao ndio unataka mjadala. Si mijadala ipo Jambo Forum, Cheche, KLHnews, raia mwema, Mtanzania Daima nk. ambako pia mnatumia lugha chafu na mwenzako Chinga. Haikutoshi kujadili huko mpaka uje huku kwa wadau ' trivial'....kwa kuwa mambo “serious” hayana mvuto wa fikra kama zako, na mambo muhimu na yenye kuhitaji kugonganisha vichwa (brain storming) kwa sababu sisis mbumbu na yanawahusu wataalamu, wasomi na wanasiasa kama wewe
Anae kutukana hakuchagulii tusi. Mungu atabainisha dhamira zako.
kweli wa tz tunahitaji kutibiwa ili kugundua udhaifu wetu, mtu anaongea mambo ya msingi watu wanaleta ujinga yaani jinsi watu walivyokua agaisnt hoja ya msingi 85% ndio namna ya kufikiri kwetu watz kulivyo, kamwe hatutaendelea, halafu tunataka tuishi kama watu wa dunia ya kwanza? itawezekana vipi kama mitizamo yetu na upeo wetu wa kufikiri ndio huu? hata kama watu wanapinga hoja ya jamaa ni sawa hakuna anae zuia mtu kutoa hoja zake lakini basi kuwe na point za msingi, sio mtu anasema kafungue blog yako,lakini wakiambiwa safari za kuja ulaya kila mtu anataka na kutamani, kwa nini tupende kukimbilia nchi za wenzetu? si kwa kuwa zina maendeleo? sasa kwa nini tusipevuke mawazo na kuwa na mtizamo wa mbele ili nasi tuweze kuendeleza nchi yetu? mmejengewa uwanja mzuri within hours watu wakauchafua kweli tutaendelea lini? unajua ndio maana hata watani wa jadi wanatudharau sana, kwa kuwa wanjua thinking capacity yetu ilivyo ndogo, angalia hata watz ambao wako nje ni wachache sana ambao utakuta wanaishi kama watu wenye akili timamu, kwa yeyote anaetaka kuwa na hoja za msingi asiwaze kuwa hoja zake zitatizamwa kama anavyofikiria, jaribu kuleta hoja za masengenyo uongo, ubi-show wa kipumbavu ndio utakuta kila mtu anatoa maoni yake kufwatana na hoja yenyewe jinsi ilivyo.
ReplyDeleteWabongo kiboko bwana!! ha aha ah leteni discussion za lebel bwana hizo siasa not now!!!! mtu gani kila wakati unaongea siasa? basi ukipenda waite watoto wako MMOJA EPA, mwingine ATCL, mwingine BOT, mwingine MEREMETA, mwingine BUZWAGI, mwingine AU UKIPATA MAPACHA TWIN TOWERS halafu yule first born mwite FISADI
ReplyDeleteUnajua tatizo lililopo sasa hivi kwenye blog na forum nyingine watu wanalazimishwa kuwa na mtazamo mmoja. Tuachieni blog yetu hii na nyie mka share frustrations zenu kwenye blog na forum zenu.
ReplyDeleteLabda tu ushauri mmoja wa ndugu yetu hapa mwanakijiji. Kubadilisha jina na websites zako mara kwa mara haisaidii kufanya watu wasoma mambo yako ubadilishe lengo kwenye makala zako. Maandiko yako yanaweza kuwa ya mvuto lakini mwisho mtu ukikaa chini ungaangalia umepata nini mara zote unakuja na jibu moja. Ni kama vile hotuba za Obama, zinavutia sana lakini akimaliza jaribu kuchukua kalamu na kalatasi jaribu kuandika chini mambo aliyosema kama yanaleta maana yoyote na unakubaliana nayo. Kuna kiongozi mmoja wa ma-gay alikuwa anahojiwa kwenye TV akawa anasema eti Obama amewageuka kuhusu gay-marriage. Alipoulizwa ni lini Obama ali-support gay-marriage alishindwa kujibu. You know why, Obama is too smart for most of us. Mara nyingi anapoanza hotuba zake alikuwa anawashukuru gays and lesbians lakini kwenye ujumbe ana support traditional marriages hapo nakuwa anakuwa ameua ndege wawili kwa jiwe moja. Sasa mtu unapokuja kugundua jinsi wanasiasa wanavyotaka kuchezea akili zetu unakuja kuamua "to hell with politics" ngoja tuongelee leboooz.
yeah, to hell with politics. mie madhumuni yangu ya kuingia kwa michuzi ni kupata habari live zenye mvuto, kama nikitaka siasa nitakuja huko kijijini. mie mwenyewe binafsi sijawahi hata kuipanda hiyo ATCL sasa kwa nini kiniume kama imeuzwa, hata nilikuwa sijui kama imeuzwa na wala siko interested kujua. KILA MTU ANA INTEREST YAKE JAMANI. kwa mfano mie interest yangu ni mambo ya biology the study of living things. najaribu kutafuta tiba ya cancer by studying cells. sasa wewe unavyofanya ni sawasawa na kuchanganya vodka na maziwa. ni sawa na sie tukulazimishe uwe mwana sayansi, utakubali?
ReplyDeleteLeo wadau tumepewa kisago cha kufungia mwaka:
ReplyDelete1.Hatuko “serious” na mambo ya msingi.
2. Tunachosoma au kujadili humu hakina mvuto wa fikra na (kwamba taahira wamejaa)wanashindwa kujadili mambo muhimu na yenye kuhitaji kugonganisha vichwa (brain storming).
3. Huenda kuna Vihiyo wengi humu ambao wanaona eti mambo kama ya ATCL yanawahusu wataalamu, wasomi na wanasiasa kama wao na kwanini yasijadiwe?
4. Hii blog ya jamii ni kwa ajili ya kurelieve stress za maisha ya kila siku! kujadili mambo ya kijinga tu.
5. Wadau muko kama panya aliyebanwa na mtego hasa yanapokuja mambo ya kitaifa na ya msingi.
6. Wadau humu kama mumerogwa hivi! kazi kujadiliana kukerwa na lebo na jinsi gani mtu amevaa suti !
7. kwa utaahaira wenu, hata leo akiibuka “Obama” wa Tz (jina tunalihifadhi) na kuja na maneno kuwa “Change is coming” na kuwa “Yes we Can” ataangaliwa kwa kejeli na kuulizwa kama pamba yake ya Kongo Street ina lebo?!
Ahsante kwa salam za lala salama
Kwa wale mnaosoma Daily News mtakubaliana na mimi kwamba kwa jinsi Michuzi anavyoandika kwenye Daily News ni tofauti kabisa na anavyoandika hapa. Ninamsifu kwa kuwa anaelewa ni nini watu wanataka hapa na nini nini wasomaji wa Daily News wanataka. Ndiyo maana hii blog ni "namba 1,2,3, na 4" na nyingine zinafuata. Sasa huyu anayetaka ku-define mambo ya msingi kwa mtizamo wake nadhani atafute kuwa namba 4 kwanza halafu aje hapa.
ReplyDeleteMwanakijiji ametudhalilisha..asusiwe au mnaonaje wadau.
ReplyDeleteASUSIWEEEE!!!!!
ReplyDeleteMimi nafikiri Mwanakijiji anapojadili mambo yake anasahau dhana kubwa na muhimu za fasihi "MUKTADHA" na HADHIRA.
ReplyDeleteNakubaliana na Mwanakijiji kuwa kuna umuhimu wa kujadili mambo ya nchi yetu lakini pia ni muhimu kukumbuka kuwa kuna platforms kwa ajili ya suala hilo.MUKTADHA wa MICHUZI si wa kujadili ATCL,EPA katika namna anayoifikiria Mwanakijiji.
Ikumbukwe kuwa MICHUZI amekuwa mstari wa mbele katika kuleta habari za mafisadi nchini na amekuwa anatuonesha jinsi watuhumiwa wa kesi za ufisadi wanavyofikishwa mahakamani na vitu vya namna hiyo na huo ni mchango katika kuwahabarisha Watanzania.Kwa ujumla watu wote wanaotembelea michuzi wanaipenda Tanzania.
Inapofika suala la kujadili masuala mengine ambayo yanafurahisha na kutu-amuse tuweze kusahau matatizo yetu na yanayotusibu ni vizuri watu wakapewa nafasi.
Kama alivyosema mchangiaji mmoja,suti si vazi la Tanzania.Tuna nafasi ya kujifunza toka kwa wenzetu wanaojua utamaduni wa suti.
mwanakijiji au benson mwakanjala anakata kutumia fursa hii ya michuzi kupata watu kwenye blog zake anazobadili majina kila siku.ama kweli usimtukane mamba kabla hujavuka mto alikuwa akiiikandia sana blog ya michuzi lakini leo hii yeye ndiye anajibanza humu kupenyeza sumu zake za uchadema.
ReplyDeletehapa tunajadili jamii tena umeiba jina la michuzi la blog ya jamii na kuamua kuiita blog yenu ya cahdema jamii forums ilitakiwa mumlipe mithupu mambo ya hati miliki.
mithupu naomba usimpe nafasi za uchochezi huyu mtu yeye yuko marekani anatufitinisha sisi tulioko Tz ili tupigane na kuuana yeye yuko kiguu juu kwa Obama. anatumia magazeti mengi kulaani serikali kila leo. au kuwakandia waislam kila mada iwe OIC au kadhi.
watanzania kuweni nae macho huyu mchochezi mwenye sumu za kidini. ukiandika against Chdema na Mbowe kule jamii forums unafungiwa na IP address zako anapewa Mbowe. jiulize huko jamii forums Mbowe.slaa ,mtei, mnyika wote wachangiaji.sababu ni blog inayomilikiwa na wao kama propaganda machine yao.
tunamshukuru na kumuombea mungu Mithupu aendee kuwepo ili sote tupate haki kuliko huko kwenye ubaguzi wa kidini na kikabila.
michuzi blog oyeeeeeeeee. hadi wanaomchukia mithupu wanaleta mambo yao humu.
ni mimi Mswahili.
Kama tatizo ni uchumi kwa nini tusimuajiri mchumi mmoja mzuri hata kama siyo raia awe kama rais atusaidie kutatua matatizo yetu. Hakuna lolote hapa ni uroho wa madaraka tu unaowafanya mtuingilie kwenye blog yetu ya jamii. Watu wanawakimbia kwenye hizo blog na forum zenu kwa sababu mna mawazo mgando ambayo haya make sense hata kwa mtoto mdogo na wewe mdau wa 85%uliyetutukana hapa "you got it right", 2010 tutampa Dr.JK 85% mpaka mjifunze kuomba kura kwa adabu.
ReplyDeleteMwanakijiji, Si umeshaandika makala ndefu juu ya ATCL kwenye tovuti yako na tayari wachangiaji wawili (ambao ni X na X) wamechangia maoni kukuunga mkono.
ReplyDeleteNi lazima ili tuwe serious tovuti zote na blog zotekwa wakati mwingi na lugha kali kali izungumzie jambo moja ndio ionekane kuwa tuko serious?
UJUMBE KWA MWANAKIJIJI
ReplyDelete1. ASANTE SANA KWA KUTUONA WAJINGA.
2. WEWE UMEWEKA LINI COMMENT YAKO TUKASHINDWA KUCHANGIA??
3. KWANINI UNAPANDA JUU YA MGONGO WA KERO NYINGINE KUWEKA YAKO?
4. JIFUNZE KUWEKA KERO KWA MPANGO WATU WASOME WAELEWE THEN WATACHANGIA.
Jamani mbona mwana kijiji anatutukana??????
ReplyDeleteAmetufuata mwenyewe nyumbani kwetu (hapa bloguni) na matusi.
wadau mnasemaje???
mwanakijiji nafikiri umefahamu sasa wachangiaji wa blog hii ni wa karba gani.Hii ni blog ya kada ya kawaida siyo ile ya kisomi na uchambuzi wa mambo kiyakinifu hapa tuambie mpira,n.k tutakuelewa lakini maendeleo hatutakuelewa.
ReplyDeleteKusema kila jambo lina nafasi yake na muda wake, ni vyema. Lakini kukiri na kusema kwa kukusudia kuwa katika blog hii watu hawataki kabisa kuzungumzia mambo ya maendeleo na matatizo ya nchi yetu ni UJINGA mtupu. Mbona mambo ya EAC yalitufanya wote tuandike kwa kirefu? Mwanakijiji labda amekosea ingawaje amechangia mawazo yake kuhusu lebozzz, turekebishaneni kwa amani na upendo. Sasa mbona wengine wana take it personal!!
ReplyDeleteEti kweli kaka Michuzi usingependa na wewe kujadili mambo muhimu humu kwenye globu ya jamii?
Fungua Macho!
Na wewe Mdau Fungua Macho huoni lugha uliyotumia hapo ni ya dharau na wakati huo huo unataka tukusikilize? Kutuambia sisi tufungue macho inamaanisha sisi ni vipofu au wajinga hatuoni mambo yanavyokwenda na wewe una akili sana? Au...
ReplyDeleteNa hili swali ulilomuuliza Michuzi kwa kuwa una akili sana ungeweza kusoma mambo Michuzi anayoachia yajadiliwe humu na ungepata majibu badala ya kumuuliza swali la uchokozi.
Mwanakijiji ni muumini wa mbowe, anamuona kama malaika hajawahi kumkosoa hata siku moja. mfano mbowe aliposema maneno ya fedhuli kuwa hawezi kufanya kazi na wangwe. mara mwanakjj akaja juu na kumsakama wangwe. bila kumohoji na mbowe. kwani waligombana wawili lakini yeye akaegemea kwa mfadhili wake(mbowe) nani hajui kuwa alipewa pesa na mbowe kufungua website zake?analipwa kuitukana serikali. ni mchochezi anayetumiwa kwa maslahi ya chadema.
ReplyDeleteKuna blog zaidi ya 100 za watz na 70% ni habari za siasa na upuuzi mwingine usio na maana.
ReplyDeleteKwa nini tusichangie maoni kwa michuzi ambaye anachanganya habari?
Wewe kama unauchungu sana na ATCL nenda jambo forum na utachangia maoni yako mpaka uchoke.
kwa kiinglishi wanasema "Opinion is like a butthole and everyone has his/her own." Wewe kama hii habari haijakufurahisha chagua sehemu/blog nyingine hii tuachie wenyewe.
asante.