Kaka Michuzi habari za leo.

Ni matumaini yangu kuwa u-mzima wa afya njema. Nakupa pongezi kwa kutupa habari. Mungu akulinde.


Naomba kuwasilisha kero yangu na wadau wengine wengi hapa nchini kuhusu uvaaji wa suti (hasa suti za kiume). Hapa chini ni ujumbe niliopata kwa njia ya sms naomba niuweke wazi;

"Hivi hii style ya kuvaa suit na label yake kwenye sleeve ni style ni ya wapi au ni ushamba wa Wabongo jamani!

I find it very weird! Hebu foward hii msg kwa wadau huenda tutapata jibu. Kama ni mmoja wao naomba unisamehe, ni vile sijaona wavaa suti kule zilikoanzia wakivaa na label". Mwisho wa kunukuu.

Hili tatizo limezidi kukua siku hadi siku hadi imefikia hata wanaopeleka suti kwa fundi hapa bongo anaomba fundi atafute label kwenye nguo nyingine na kubandika.

Sasa naomba urushe hii kero, ili tuweke wazi nini hasa kinatakiwa. Mimi naona ile label kwenye mkono(sleeve) inakusaidia unapochagua suti dukani usihangaike kuangalia kwenye kola tulikozoea label za nguo nyingi zimebandikwa, waligundua tatizo au ni fashion wakaona bora tuweke kwenye sleeve kurahisisha uchagua wa size, nk.

HIVYO BASI UNAPONUNUA SUTI ONDOA HIYO LABEL!!

UJUMBE
ATAKAYEONA MWENZIE OFISINI, KWENYE TAFRIJA NK AMEVAA SUIT NA LABEl KWENYE MKONO WA SUTI TAFADHALI MSAIDIE/MUELEZE AONDOE HARAKA SIO SAHIHI.

Naomba pia uweke picha hizi za suti dukani na picha ya mtu aliyevaa suti nimeambatanisha.
Mdau Mchukia Lebo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 78 mpaka sasa

  1. Kwa kawaida label inatakiwa itolewe ila hao labda wameazima sehemu hizi suti

    ReplyDelete
  2. KAMA LABEL UNAYOZUNGUMZIA NI HIYO HAPO YA MKONONI SI KWELI MAMENO YAKO NIMEONA WATU WENGI SANA WANAVAA SUTI NA LABEL HIYO IKIWEPO HASA HUKU ULAYA HASA U.K. PIA NIMEONA U.S.A. LAKINI NAKIRI SI SUTI ZA AINA ZOTE KUNA SUTI ZAKE HASA ZILE AMBAZO SURUALI MATERIAL INGINE NA KOTI MATERIAL INGINE HASA AMERICANS WANAFANYA HIVYON HASA VIJANA, NIMEONA BECKHAM, NIMEONA RIO FEDNAND, NIMEONA WANAMUSIKI WENGI TU, FOOTBALLER CWENGI TU WAKIVAA NA LABEL IKIWA IPO HAPO, PENGINE SI VIZURI KWA WATU WAZIMA LAKINI VIJANA NI WENGI TU WANAVAA HIVYO, NI SPECIAL DESIGN SI UKASHONESHE KARIAKOO ALAFU UKAOKOTE LABEL NA KUBANDIKA HATA HIVYO SI VIBAYA, NA MADHUMUNI YA LABEL REGARDLESS IMEBANDIKWA WAPI SI YA KUITOA UKISHA NUNUA NGUO NI YA KUBAKI HAPO ILIPO HIYO NI KAMA SIGNATURE YA MTENGENEZAJI WA NGUO HIYO. ILE INAYONING'INIA MARA NYINGI HUWA YA KARATASI KWA VYOVYOTE ITATOKA TU USITAKE UNATAKA. KWA MAANA HIYO BASI SIKUBALIANI NI CRITISISM ZAKO

    ReplyDelete
  3. Mimi ni mvaa suti za kila aina hasa ninapofundisha wanafunzi wangu hapa. Sijawahi kuona mtu akivaa suti pamoja na hiyo label yake. Lakini pilipili usiyokula inakuwashia nini. Kama watu wameamua kuvaa chupi kichwani na soksi mikononi wewe inakusumbua nini. Hii ni dunia yenye uhuru wa kufanya kitu mtu anachotaka na sio, na narudia, SIO kile KITU wewe mwandishi wa sononeko hili unachokitaka. Ukitaka anwani yangu na simu yangu nitakupatia lakini nafikiri haya yanakutosha. Wewe kutoka tu nyumbani unaona wale wanaobaki pale ni washamba? Ni wewe. Au tukuite wewe mshamba unayechangamkia bacon BILA kufikiri kwmaba hayo ni mabaki ya kiti MOTO? ha ha...

    ReplyDelete
  4. MIMI NINA SWALI KWANI HIZO LEBO ZINAKUWA ZIMEANDIKWA NINI?KAMA ZIMEANDIKWA MAELEZO YANAYOKUWA KWENYE LEBO ZA KWENYE KOLA BASI HAITAKIWI IWEPO,KWA UJUMLA MI NAONA NI USHAMBA ULIOPITA KIWANGO SIJAONA HAPA MAMTONI MTU ANAVAA HIVYO,AU STAILI YA BONGO?TATIZO LILILOPO DAR WAKULIMA NI WENGI MNO KUTOKA VIJIJINI,WATU WANA HELA LAKINI WASHAMBA.

    ReplyDelete
  5. Nahisi wewe ndiyo mshamba number moja, kama wewe huvai na label basi waache wengine wavae, Naamini uvaaji wa nguo ni uamuzi wa mtu binafsi hivyo kama haikufurahishi kaa kimya.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli, nilishangaa hata watu mashuhuri kama Mh. Temba na mpambe wake suti zao zilikuwa na label siku ya harusi yake!

    ReplyDelete
  7. HIYO LEBO NI KUONYESHA KAMA SUTI NI VERSACE, DONALD TRUMP, CALVIN KLEIN NK. SASA KAMA UKINUNUA YA MTUMBA AU YA WAL-MART UNABIDI UNAI-UPGRADE NA LEBO FULANI INAYOMAKE SENSE

    ReplyDelete
  8. Kama kuna watu wanaochefua ni pamoja na wabongo wanaojiita ako ughaibuni!!!!! they think they f**ken know everything!!!!! Eti sijaona huku zinakotoka wanavaa na lebo!!!!! Ishiii kwani lazima tuwe kama wao..acheni ushamba na ukasuku wa kudesa kila afanyacho mzungu you can o same thing differently.

    Nasema ni washamba coz pamoja na kwamba mimi sijawahi kuvaa suti mie uniulize jeans mpya ya Tommy, Kipanya,etc lakini suti spesheli zilikuwepo tangu huko nyuma. designers walikuwa hawaweki lebo. Siku hizi inawekwa lebo na inawekwa aesthetically ikiwa ni moja ya urembo wa suti. Tangu lini lebo ya nguo ikawekwa mkononi tena nje?? Lebo zinawekwa kwenye Kola na ubavuni tena ndani, inayowekwa nje ni urembo its not meant to be removed you naives. mbona wasiibandike mgongoni lakini constantly wameiweka mkononi??

    Mtakuja kutuambia na jeans tutoe gamba la kiunoni nyuma ati nayo lebo coz mmemwona mzungu katoa. Huyo aliyendika msg ni mshamba kama alivyo aliyetuma huu ujumbe.

    Kaka michu uwe unachuja hizi njumbe nyingine hazina tija na istoshe jamaa anakutusi huyu coz nishakuona umepiga yenye lebo mana zile ni suti expensive!

    ReplyDelete
  9. Mdau nakushukuru sana kwa kunisaidia kupigana na hii kero. kuwa na lebel kwenye sleeve NI USHAMBA WA KUFA MTU!!!!!! Nishawahi hata kuwatolea mifano mingi kuwa sio siri kuwa JK ni mtu wa pamba. Sasa huwa nawauliza hivi mshamuona hata siku moja akiwa na lebel? Maana siyo siri JK anajuwa kupiga pamba tena siyo mvivu wa kuchagua. Jamani tuache ushamba. ondoeni lebel hizo kwenye misuti yenu eebo!!

    ReplyDelete
  10. Nashukuru kwa hii kero. Ukweli ni kwamba suti haivaliwi na lebo wewe unaetetea samahani inaelekea wewe ni mvaaji namba moja.

    ReplyDelete
  11. UTETEZI WA KIJINGA
    SUTI HAIVALIWI NA LEBO NI KUTOJUA TU KWA WAVAAJI

    ReplyDelete
  12. kweli wadau hapo juu manatotetea suti na lebo unanichekesha sana.

    LEBO INAPASWA KUTOTOLEWA

    ReplyDelete
  13. hII POST IMENIFURAHISHA SANA BWANA MITHUPU LEBO ZINATIA KICHEFUCHEFU ANAYETETEA NINA HAKIKA NDO MVAAJI NA MOJA NAOMBA USIHARIBU WENZIO BAKI NA UJINGA WAKO

    ReplyDelete
  14. uvaaji wa suti zenye lebo; wengi wao ni wale wanaotangaza soko la kampuni husika mfano VERSACE .wachezaji na wanamuziki wengi hushiriki katika matangazo hayo.hivyo huvaa pamoja na lebo ili wewe uone amevaa suti iliyotengenezwa na kampuni flani ili nawe kama utaipenda ununue.Kwa ufupi kuvaa na lebo wakati umenunua suti hiyo ni kutangaza biashara ya mtu bila malipo.hivyo ni utashi wako kutoa au kutangaza biashara bure.mfano utakumbuka miaka ya nyuma kulikuja staili ya kuvaa suruali chupi inaonekana.hao walikuwa wanatangaza makampuni yanayotengeneza chupi,watu wakaiga.ni juu yako kuchagua kutangaza biashara au kuacha

    ReplyDelete
  15. Please tusijifaninishe na fulani yeye anavaa suti na LEBO hata siku moja. Lebo inapaswa kuondolewa

    ReplyDelete
  16. Michuzi leo ndo mara ya kwanza kufungua blog yako. Na duka la nguo hapa jiji na suti ni moja ya bidhaa zangu. Pia nimepata tenda sana ya kusambaza suti kwenye ofisi mbalimbali. Ukweli ni kwamba LEBO inapaswa kuondolewa kwenye suit mara unaponunua. huo ndio ukweli. Nikosa letu sisi wasambazaji wa hizi nguo kutoa aarifu wateja wetu mapema. Tusaidiane taratibu. LEBO inapaswa kutolewa

    ReplyDelete
  17. ULAYA NI ULAYA NA BONGO NI BONGO
    LEBO NI USHAMBA BWANA NAOMBA TUSIJIDI WAJUAJI WAKATI MWINGINE TUKUBALI KUWA BLOG ZINAREKEBISHA MATATIZO MADOGO MADOGO KAMA HAYA WEWE NENDA KATOE LEO HIYO LEBO

    ReplyDelete
  18. Do not please yourself eti fulani amevaa suti ya LEBO siku ya harusi yake. NENDA KATOE HIYO LEBO LEO

    ReplyDelete
  19. Tunajifunza kutokana na makosa na makosa mengi na ya kutojua hivyo basi ukweli ni kuwa unapaswa kuondoa label sio sahihi kuwepo mara unapoanza kuvaa. Asante mdau

    ReplyDelete
  20. SADIQ UMEZUNGUMZA KITU CHA KWELI KABISA LAKINI UMENIANGUSHA SIKUTOFAUTISHI NA YULE MJINGA ANAYE DAI WAZUNGU MBONA WANATOA LEBEL? NA WEWE UNARUDIA UTOTO ULEULE WA KUWAFANYA WANAUME WENZAKO NI BENCH MARK YA MAISHA YAKO FANYENI MAMBO ON YOUR OWN. ETI JK ANAPIGA PAMBA BILA LEBEL WEE LIKULIMA SANA KWA HIYO KILA ANACHOFANYA JK NI SAHIHI? UMENIKERA NDUGU YANGU HEBU FUATILIA MAMBO PERSONAL YA JK NAWEWE UYAFANYE, AKIZAA MTOTO NJE YA NDOA NAWEWE ZAA

    ReplyDelete
  21. Teh teh teh!! usitake nicheke mie. Mali ya yeye kampe yeye. Siri ya Ngedere aijuae Tumbili. Wote washamba tu. kwani M Bongo wa Ughaibuni au Bongo asili yao ni suti?? napenda suti za kimasai na Kibarabaig.

    ReplyDelete
  22. Kubali matokeo mshikaji SLEEVE LABELS LAZIMA ZITOKE

    ReplyDelete
  23. Hahahahhaha jamani katika kero hii funga mwaka I'm so happy..... 2009 NO LABEL KWENYE SUIT. hahahah Michuzi bwna sasa mbona ulikaa kimya muda wote huo

    ReplyDelete
  24. ANONY............WAFUATAO:

    December 19, 2008 4:54 AM
    December 19, 2008 5:21 AM
    December 19, 2008 6:39 AM
    December 19, 2008 7:08 AM
    December 19, 2008 7:32 AM

    MSIWADANGANYE WAVAO LEBO TAFADHALI
    turekebishane lebo kwenye suit ni ushamba ziondolewe

    ReplyDelete
  25. MIMI KWA UPANDE WANGU NAONA NI USHAMBA HATA KAMA BECKHAM ANAVAA HIVYO BASI NAE NI MSHAMBA TU KWANI MSHAMBA SIO LAZIMA AWE AMETOKA BONGO KILA NCHI INAWASHAMBA NA HATA WENYE PESA WAPO WENGI WASHASHAMBA KAMA JACK UNGUJA NI MSHAMBA WA KUMWAGA.
    MDAU
    KISIJU PWANI

    ReplyDelete
  26. nawalaumu wanaouza suti maana vijana wa benki lebo zimejaa sana

    ReplyDelete
  27. JE UKIVAA NA HIYO LABEL KUNA MASHTAKA YOYOTE AU UNAWEZA KUFILISIWA AU KITU GANI KITATOKEA? NADHANI NI UAMUZI WA MTU NA HAMNA MAHALI IMEANDIKWA ITOLEWE AU ISITOLEWE. NI UELEWA WA WATU TU NA UJUAJI KWA SANA NDO UNALETA MIJADALA MINGI. NA KINGINE "USHAMBA SI MZIGO KILA MTU ANAO........."

    mdauzi

    ReplyDelete
  28. Inasikitisha kuona jinsi wadau wengine wanajigaragaza kwenye harakati ya kuutangaza ushamba wao.

    Hizo label za mkononi mwa suti zinawekwa ili tu mtengenezaji aweze kutambulika kwa jina lake wakati suti zake zimetundikwa madukani pamoja na suti za watengenezaji wengine. Na huo zinakuwa rahisi kuchomolewa kwani hawamtazamii mvaaji kubakisha hiyo label katika matumizi.

    Mnaotazama cinema au taarifa ya habari toka nchi nyingine yeyote, hamtakuwa mmeona wavaaji wa suti yenye hiyo label. Ni utamaduni uliopo hapa Tz tu, na ni muafaka kabisa kuukemea kwa bidii.

    ReplyDelete
  29. Jamani asante. Mimi nimeshagombana na ndugu zangu wote kwa ajili ya Labels. Wanasema mimi ndiye mshamba..Lol..yaani siwaelewi kabisa hawa ma "karigabagaho"...!!

    ReplyDelete
  30. nadhani makubaliano ya wengi ni kuwa wewe uliyetoa maombi ndiye mshamba. Hukumbi bijana wanakunja mikono ya suti? je wazungu wanafanya hivyo? umesikia maoni ya lable ya jeans? Je kwenye gari, huoni mengine lable zao hakuna? kwa mfano huyo bwana anauza mercedez, ina lable, 55AMG. Ukitaka wasiiweke unalipia, yaanai kama unununua gari mpaya. Huyo bwana labda aliamua iwepo, na aiinigie gharam ya kipuuzi. Suti unaweza kuacha lable au ukatoa, ni utashi sio ushamba.

    ReplyDelete
  31. Ni ushamba!!!!! Watembee na mifuko yake kabisa.

    ReplyDelete
  32. Ubishi wote huu unatokana na kutokua na vazi letu wenyewe la kitaifa, ndio maana hata uvaaji wa mavazi ya wenzetu unatushinda, hapa mtabishana sana lakini suti hazikuanzia kwetu hivyo hatujui masharti yake. kama alivyosema mdau hapo juu JK na wajua pamba wengine hawavai na lebo, hawa wenye kuparamia ndio lebo hazitolewi. lebo zenyewe ukizichunguza zimeshikizwa tu ikiwa na maana ondoa wakati wa kuvaa.

    ReplyDelete
  33. Nina SUTI nyingi sana kwenye kabati langu la Mbao (black only are about 6), So.. nina acha labels ili wakati wa kuvaa it doesn't take me time to figure which is which Does that make sense to you fools....!!?

    ReplyDelete
  34. Kuacha Label ni Ushamba. Full stop.

    Ni kwamba hujiamini kuwa quality ya suti yako inajidhihirisha. Kwamba ni mtu wa kujshow-off unataka kila mtu aone umevaa "Versace" hata kama ni Versace ya China au imeshonwa Mwenge Mlalakuwa

    ReplyDelete
  35. Acheni uhsmba that's a brand label mbona hubandui label ya Toyota kwenye gari yako!

    ReplyDelete
  36. janami mambo mengine yanashangaza!!! mpaka uone wewe huko ulaya ndio watanzania wataruhusiwa kufanya? ina maana hao watu wanaokuzunguka wewe ndio wanaomake fashion zote? Kwa taarifa yako huwa wanaiga pia.
    Ujue pia fashion haina mipaka. Siku hizi kila mtu hata wewe unaweza kuanzisha style, kama kunwa watu wanakutamania muonekano wako.
    Inasikitisha sana kuwa huna role model mtanzania hadi uchukue wa huko!!
    Huo ni ulimbukeni.
    Kama kweli nyi watu mngekuwa najua fashion, msingesema haya, inaonyesha jinsi mlivyo rigid.
    Suti imkae mtu aone raha, kama anataka kujionyesha, basi ajionyeshe hadi lebel, wenye kuiga tutaiga, waliobakia watatunga mpya au wataiga wengine!!
    Nakumbuka zamani mrema alivaa raba nasuti watu walisema saaaana, hadi walipomuona bekham na will smith eti ndo wakashtuka!! kumbe ni fashion!!!
    Kwa taarifa tu, hakuna nchi zilizo nyuma kwa kupendeza kama marekani na uingereza, kazi kuiga tu designers wengine na kupromote kwa kutumia media zao ambazo watu kama nyie mnazi idolize!
    any way, pole sana manake watu kama nyie hamna dawa!!!

    ReplyDelete
  37. Kwa kweli ni ushamba haswa. Halafu inakuwa ni uchafu kwani label huanza kuchakaa na kupauka kabla ya jacket lenyewe. Sasa nyie mnaotetea uvaaji huo mna akili kweli nyie? Mie huwa nakereheka kwa sababu uzuri wa suti wote wapotea. Acheni ushamba huo.

    ReplyDelete
  38. Walioona Twanga Pepeta walipokuwa wanashoot video kwa suti za Kuazima HS Amon ha ha ha

    ReplyDelete
  39. Walioona Twanga Pepeta walipokuwa wanashoot video kwa suti za Kuazima HS Amon ha ha ha

    ReplyDelete
  40. he he he he .......huu ni mchosho tu ....... vaa unavyotaka wewe!!!

    ReplyDelete
  41. Nimeingia maduka makubwa ya suits na outlets za kwa manufactures, wakati wanakukatia zile nyuzi zilizoshikizwa ktk mipasuo ya suit (huitoa wakiwa na uhakika unainunua) huwa pia wanatoa na ile lebo ya mkononi, tena bila kukuuliza kama watoe au wasitoe. So, naamini kama washonaji/wauzaji wanatoa, na sisi wavaaji tutoe.
    Usifananishe lebo ya gari na ya nguo

    ReplyDelete
  42. Bekham, P-Diddy na huyo supastaa wa bongo aliyetolewa mfano hapo juu wanaweza kuwa matajiri ila hamna shule kichwani.
    angalia CNN au TV yoyote wanayoonyesha mikutano mikubwa mikubwa duniani uone kama utaona hata mtu mmoja ktk hiyo mikutano ana lebo mkononi, ukimuona ujue ni Mzaire au Mbomgo. Exposure matters jamani

    ReplyDelete
  43. Mitumba imezidi barabarani. Hivyo wanaoweka lebo wanajaribu kujitangaza kwamba wao hawajavaa mitumba.

    ReplyDelete
  44. "USHAMBA SI MZIGO KILA MTU ANAO........." nimekazimia hako kamsemo

    somo naona limeshika hatamu nimesoma maoni ya wadau nikaona mmoja anahoji kwanini kama lebo zastahili kunyofolewa zisipachikwe mgongoni au pembeni ya kola coz ni rahisi kuonekana na mnunuzi kuliko huko mkononi ilipo

    Na je mlishaona wanamuziki kadhaa wakiwa wamevaa nguo zina lebo zile za mabox kabisaa zinang'inia...mwanzo nilijua wanaazima dukani na zinahitajika kurudishwa dukani ila nilikuja ambiwa ni fashion...na wapo wananchi wanakatiza na nguo mpya zenye lebo hizo mjini...hiyo nayo mmeionaje??!!

    ReplyDelete
  45. YAP BAADA YA KUCHEKI COMMENTS ZA WATU HAPO JUU, MI NAFIGURE OUT KWAMBA KINACHOKOSEKANA KWA WATU HAPA NI EXPOSURE TU. KUVAA NGUO NA LEBO SIO TATIZO SANA ILA INATEGEMEA NANI KAVAAA JAMANI. LITERATE KUVAA NA LEBO!!! MH, HAIPO.

    ReplyDelete
  46. we anony unaye ongelea mkulima umenichosha kwani babako alitokea wapi nyambafu weeeee mpaka ukafika huko au ndo fidadi wa ssa kwani enzi za jukius wengi wa wazazi walikuwa sawa nyambafu kudadadeki natamani nikutie ngumi ya makkkkkkkk

    ReplyDelete
  47. jamani kazu je ? haina umaarufu teh teh teh

    ReplyDelete
  48. Mimi naona hiyo label is so small kiasi kwamba haiwezi kumchefua mtu. Inasikitisha sana mabishololo unapokuatana na mtu unamuona anakukagua, kuanzia juu mpaka chini umevaa nini. Hapo hapo mimi naku-dis maanake akili zako ni finyu. People are different wakati wengine mnapenda nguo, wengine wanapenda nyumba, magari, elimu, familia, kazi au biashara zao. Hata wazungu takuta mtu amevaa tu ovyo lakini nenda kwenye account yake au hata nyumbani kwake. Please naomba kwa mtanzania yoyote mwenye akili timamu msibabaishwe na huu upuuzi, maanake leo imeanza label kesho watahamia kwenye kiatu. La maana have confidence as long as elimu, pesa na maisha mazuri unayo waache waendeleze majungu

    ReplyDelete
  49. JAMANI MIE NAINGIA KIVINGINE KIDOGO MBONA SIE WABONGO TUNA VINENO NENO SANA (GUBU)SUTI KAIVAA MWENGINE WEE WAWASHIWA NINI?YAANI MWENZIO AKAJIPINDE KUNUNUA SUTI YAKE BEI MBAYA HUKO(VERSACE) WEE MKALAKALEMWA UNAWASHWA NA LEBO YAKE KWANINI ASIINGÃ’FOE ETI!!!MWEEE!! NA WEE MDAU KULE MWANZO MWANZO SIKUHIZI BLACK PEOPLE WENZIO HAWAVAI BIDHAA ZA TOMMY HILFIGER AU HUJAMSIKIA KWENYE OPRAH WINFREY SHOW ALIVYODAI YEYE BIDHAA ZAKE SIO KWA MANIGA????KWAHIO UKISEMA UNAVAA TOMMY UTACHEKESHA NDUGU USIJIKOMBE...

    ReplyDelete
  50. Teh teh! Toeni hata lebo zilizoko kwenye jeans na suruali nyingine zifananazo na hizo.

    ReplyDelete
  51. Jamani wewe mtoa hoja, kuvaa koti likiwa na lebel yake ya dukani au kuitoa inategemea na msimamo wa mtu. Sioni haja ya kujadili suala hili. Ni sawa na mtu kuvaa shati akachomekea na mwingine asichomekee halafu unasema tujadili kuwa ni yupi yuko sawa. Hivyo ni uhuru wa mvaa suti kuamua either avae na lebel yake au aitoe lakini isije ikawa nongwa.
    Mdau

    ReplyDelete
  52. Jamani eeh msing'ang'anize watu kuchana mikono ya suti zao bure kisa tu kwa kuwa nyie hampendi labels. Je kama hiyo labels imeshonewa hapo na nzuri ngumu kabisa, mtu afumie suti yake? Na kama ilikuwa ni kwa ajili ya kuondoa hao watengenezaji wangeweka maneno au alama kuwa iondolewe au nao washamba pia kama sisi? Mbona vitu vingi vina maelezo kuwa kabla ya kufanya hivi fanya vile.

    Hizi suti sio zile zinazoshonwa kwa mafundi wa kichaga mjini jamani. Zimekuja na labels zake kutoka huko huko nje, je kama walitaka kuficha labels na sio fashion si wangeweka ndani kama zamani? Kwani hakuna suti siku hizi zenye labels ndani?

    Wala siwashangai walio nje ya nchi, kwanza wao fashions wanazozijua ni za kuona kwenye TV sio kuvaa, si tunawaona kina mama wanaotoka nje wakija kwenye maharusi wanavyochekesha na nguo zao, pengine wamenunua bei mbaya lakini kwa Bongo hakuna kitu.

    Hebu nunua yako halafu tafuta kiwembe uanze kufumua hiyo labels, ingekuwa yakuitoa ingetoka kirahisi tu, ingewekwa gundi na si kushonewa kabisa! Saa nyingine kujitia sana kujua kumbe hujui kitu, kwani hamuwezi kujifunza kitu kutoka kwa watu walio Bongo? Huko ulaya na US wenye kuhangaika na fashions ni watu wenye pesa na waafrika wenye kupenda kujionyesha the rest wala hawana mpango, sasa mpaka muwaone masupastaa au malord wamevaa labels ndio mjue zinavaliwa!

    ZINGEKUWA ZA KUTOLEWA WANGEANDIKA TOA LABEL HII!

    ReplyDelete
  53. This issue is very controversial so far, the only right people to tell will be the designers themselves, what they wanted when they put those labels that way. Found this article, nice to read.
    http://www.askmen.com/fashion/fashiontip_150/158_fashion_advice.html

    DESIGNER LABEL EXPOSED
    Hi Chris,

    I just returned from a weeklong sales convention and had a question regarding a disturbing trend that I observed among some of the male attendees. I spotted a handful of guys donning suits with designer labels on their sleeves. Am I missing out on a new trend?

    Peter Stanios -- Rochester, NY

    I'll give it to you straight; sporting a suit with labeled sleeves is tacky. I recall that this phenomenon was in style a few years back among "voguish" people who took pleasure in flaunting where their paychecks went. You can easily compare it to wearing your shoes and shirts with the price tags still on, or your tie inside out.

    Every time I spot a guy wearing a jacket with a labeled sleeve (usually near the cuffs), I wonder if he gets paid to promote his favorite designer or is planning on returning the suit for a full refund the next day. Bottom line: when you purchase a suit, don't forget to cut off the label before wearing it.

    ReplyDelete
  54. Hii inaonyesha jinsi gani wabongo tunafuatilia mambo ya kipuuzi badala ya kufuatilia mafisadi. Jamani kuna suti za aina nyingi pia fashion inalenga pia kundi la watu wasomi, vijana mabishoo na kadhalika sasa wewe ukiona suti yenye lebo haikufai nunu ambayo haina lebo lakini kusema kwa sababu mwenzako kapendelea suti ya lebo ni ushamba basi kwa taarifa yako wewe ndo mshamba suti za siku hizi hasa zenye majina kama armani, Gucci lebo ni kwa nje. Halafu mambo ya kulinganisha kikwete naona mnapotea yeye ni raisi havai vizuti vya kwenu madukani anashonewa na fundi special sehemu kama london kama una pesa zako unaenda unapimwa unashonewa suti yako bila lebo ni exclusive kwa ajili yako. sasa nyie watoa comment kidogo mfikirie kabla ya kutoa comment

    ReplyDelete
  55. WABONGO MNAPENDA SANA KUINGIZA UFUNDI WENU NA NYIE, SUIT MNATAKA KUZINGÃ’FOA LEBEL NDIO MAANA HATA ZILE CHUPA ZA MAJI SAFI MNAZICHOMA SINDANO KUJAZA MAJI YENU, NA VICHUPA VYA PAFYUM MNAVIJAZA PAFYUM ZENU MNGEKUWA KWELI WAJUAJI MSINGETUMIA MIKONO CHOONI BADALA YA KARATASI KISHA MIKONO HIOHIO NDIO MNYOITUMIA KUKAMULIA JUICE NA KUCHUJIA NAZI PAMOJA NA KULA MBONA HILO HAMLISEMI??????michuzi usibane

    ReplyDelete
  56. Kuna lebo/nembo iliyokusudiwa iwepo, ivaliwe na ndio raha yake. Huwa inakuwa ndogo na sio 'consipiquous'Hii huwa katika shati, suruali, au jacket.

    Lebo zingine hata katika suti kwenye mkono aghalabu ni alama ndani ya duka inatofautisha kati ya aina moja ya suti na aina ingine. Hutolewa ukitaka kuivaa suti

    ReplyDelete
  57. Hivi Donald Trump ana clothing line jamani toka lini acha kuwadanganya wenzio we zuzu

    ReplyDelete
  58. KILA MTU NA AVAE ANAVYOTAKA. KUVAA NI KUSITIRI MWILI TU

    ReplyDelete
  59. Anon wa Dec 20, 2008 3:16 AM
    Mkuu, Ni kweli Mr. Trump pamoja na nywele zake mbaya mbaya ana clothing line pamoja na fragrance line na iko very selected (meaning fewer outlets). Kama unaishi U.S.A ukienda duka lolote la T.J. Maxx utaona hizo nguo.

    ReplyDelete
  60. Fasheni ya labels haikuanza leo ilikuwepo wakati nyie hampo, ikaishia, sasa imerudi tena. Hapo kwenye picha ya hilo koti kuna label 2 mmoja mkononi na nyingine hiyo nyeusi inayoning'inia hapo mbele ya koti. Yakutoa ni hiyo ya karatasi maana imewekwa special ka ajili ya kutoa na ni rahisi kuitoa na ina bei, hiyo label ya kwenye mkono si ya kutoa kwa sababu ni label ya nguo iliyoshonewa.

    Sasa nyie wajuaji tuambieni na labels gani nyingine za nguo tutoe. Mi najua kama unataka kuuza nguo kwenye duka la charity au la mtumba ili hiyo nguo isiende uzwa kwa bei kubwa au dukani tena ndio label iliyo ndani inachanwa kwa minajili hiyo tu. Sasa nyie mshachana labels ngapi za mashati, suruali na suti. Isije kuwa mnanunua nguo zilizokisha chanwa labels tayari kutoka maduka ya charity sasa mnaona kila nguo yenye label lazima ichanwe!

    ReplyDelete
  61. Wakuu bila kukashifiana na kuitana washamba..naomba kusema kitu kimoja. Kwenye fashion za nguo kama ilivyo katika dancing, there's no formula. There's no right and wrong. Hii ni kwenye fashion, mapishi, etc. Kwa mfano inawezekana watu tunaopika palau leo hii tunaikosea kinoma kwa sababu pilau Original haikuwa inapikwa inavyopikwa ya siku hizi. But what the hell, its all about the taste si ndio? Kama ambavyo tukicheza rhumba kila mtu anakatika kivyake vyake ili mradi kuwe na rhythm. Nini ninataka kusema hapa?
    Ninachotaka kuongea ni kuhusu suala la lebo kwenye koti. Mimi nilikuwa mmoja wa hao wavaa lebel nilipokuwa TZ na baada ya kufika U.S. na kuona kuwa watu hawavai nikaona shut, I should go with the flow. Sitadhubutu kuwaita wavaa labels eti ni washamba kwa sababu I was one of them, but nimebahatika kutoka nje kidogo na kupata exposure. Ni kweli nikivaa suti yenye label nikaenda kwenye interview ya Ernst & Young ninaweza kunyimwa kazi. Lakini kuna bias-ness inayoendelea katika huu ulimwengu wetu. Hivi si mnamkumbuka MC Hammer na zile suti zake ambazo kipindi flani zilikuwa very popular kwa mafundi wa barazani? Zile suti collar less? Halafu mikono mifupi? Mbona hatukupiga kelele kuwa ni ushamba kwamba MC Hammer anavaa suti isiyo na shingo na badala ya tai akawa anavaa cheni nzito ya gold? Ukimwangalia waziri mkuu wetu wa zamani Mheshimiwa Lowassa ana nguo za aina hiyo kama za MC Hammer. Je hawa nao ni washamba? Mbona hatuongelei suala la suti za mikono mifupi (short sleeves)? Maana huku Marekani hakuna...Hazipo, period! Nafikiri tusitoane macho na tusitukanane na kukashifiana. The truth of the matter is suti halisi ile original itabakia kuwa jinsi ilivyo regardless ya desire ya wana mitindo kudesign alternatives ya vazi hilo. Japokuwa siku hizi nikinunua suti huwa ninabandua label, ila sijawahi kumkomalia ndugu au rafiki aliyeko nyumbani (TZ) anayevaa koti lake lenye label aondoe. Kwa hiyo ninashuri tuwe flexible au dynamic. Mimi nimeangalia nikaona wazungu wanavaa makoti plain na mimi nikaanza kuyavaa that way, na kuna watu wengine wameona koti linapendeza zaidi likiwa na lebo so they decided to leave it on. Sioni shida yeyote...there are bigger issues kuliko hii issues ya labels za makoti.
    Time ya kulala...Phatlorenzo-MN

    ReplyDelete
  62. TUWE MACHO KUNA MAMBO YA KUIGA KWENYE MAENDELEO NA YASIOFAA KUIGWA
    HUO NI USHAMBA WA KUTUPWA NA NI WACHINA NDIO WAMELETA HIVYO MAANA HUWEZI PATA PIERRE CARDIN AMA GUCCI AMA GIORGIO ARMANI FROM ITALY YENYE LABEL MKONONI HIZO ZENYE LABEL NI KUTOKA CHINA,THAILAND,MALAYSIA YAANI NI SOKO LA WACHINA a.k.a BIDHAA FEKI
    KWA HIO NI USHAMBA

    ReplyDelete
  63. wewe uliye marekani,
    basi soma hii uone hata huko hakuna la sahihi. nadhani yule aliyetoa mfano wa upikaji wa pilau leo au zamani, au jnsi hahrusi zinavyofanyika leo na miaka ya 80 nitofauti..na maana yake ni kuwa mtu anaamua anavyoona.
    http://www.askandyaboutclothes.com/forum/archive/index.php?t-52479.html

    ReplyDelete
  64. Jamani tuondoe neno USHAMBA. Basi wavaa LEBO ondoeni hazipendezi kwenye mkono wa koti. toa weka nyuma ndani kwenye kola kama umeipenda

    ReplyDelete
  65. Watetezi wengi wa hii comment bado hawataki kubadilika.Lakini naomba tena kuwaambia, jambo ulisilolijua ni kama usiku wa kiza... NENDA KATOE LABEL NDIO UVAIE HIYO SUTI HATA KAMA UMESHAVAA NENDA KAONDOE UKWELI NI KUWA HAIPASWI KUVALIWA IKIWA NA LEBO

    ReplyDelete
  66. Watetezi wengi wa hii comment bado hawataki kubadilika.Lakini naomba tena kuwaambia, jambo ulisilolijua ni kama usiku wa kiza... NENDA KATOE LABEL NDIO UVAIE HIYO SUTI HATA KAMA UMESHAVAA NENDA KAONDOE UKWELI NI KUWA HAIPASWI KUVALIWA IKIWA NA LEBO

    ReplyDelete
  67. Watanzania wenzangu.
    Tufikie wakati tunapoeleweshwa kuhusu jambo fulani tusiwe wabishi sana ila tukae na kutafakari ikiwezekana Mithupu atusaidie kuongea na wataalamu kuondoa kero zetu. Ukweli ni kwamba lebo hutolewa. Huvai suti na ile lebo hapo mkononi na ndo maana imeshikizwa kidogo.

    ReplyDelete
  68. Nimegundu wadau wengi wa Ughaibuni hawajajua kero ya hizi LEBO. Jamani zinakera hata kama haipo mwilini kwako. Naomba muelewe kwanza yaani acha tu.... Halafu inauma zaidi mtu anapotetea hilo bila kuwa na sababu ya maana kero.

    ReplyDelete
  69. hahahhahah JAMANI RAHA ..... RAHAAAAAAAAAAA. Mheshimiwa sana Mkuu wa wilaya ya Tegeta ambaye pia ni Balozi wa Zain. Hongera sana kwa hii POST kweli umenipa wakati mzuri sana wa kufrahia
    KURA YANGU MIE NI KUWA LEBO IONDOLEWE KAMA IPO MKONONI.

    ReplyDelete
  70. If its like the picture above; the truth is, you have to remove the label before wearing

    ReplyDelete
  71. You have to remove before wearing it.Please

    ReplyDelete
  72. ushamba unakuja pale unapoambiwa halafu unabisha. Ila kama ulivaa suti ikiwa na lebo bila kujua sio ushamba kwa sasa kama wewe umesoma hii blog katoe na kama una rafiki wako mweleze.

    ReplyDelete
  73. Kweli maisha bila kusoma Michuzi blog huwa yananiwia magumu sana. Nimekuwa busy kwa wiki sasa sikuwa na muda wa kusoma hii blog. Leo nipo night hapa ofisini nimefungua na kusoma kweli nimecheka sana sana. Mimi kweli sifagiliii kabisa hizo lebo kaka Michuzi asante kwa habari

    ReplyDelete
  74. LEBO NOMA JAMANI DU. Na print naenda kubandika kwenye notice board ofisini wale wasiojua wajue kabisa na hizi post na print.

    ReplyDelete
  75. Kuna aliyesema kwamba pilipili usiyokula yakuwashia nini na mwingine akasema nguo ni za kusetiri mwili. Hawa walikuwa sahihi. Nafikiri sisi watanzania tuchukue fursa hii tuchangie kwenye ufisadi badala ya kuchangia hoja ndogo ndogo namna hii. Ukibishana na mtu mwenye upenyo mfupi na wewe utaonekana una upenyo mfupi. Basi tukubali upande wowote ukubali kushindwa yaishe ILI tujadili yenye maendeleo kwa jamii yetu.

    ReplyDelete
  76. Ukweli wa mambo label ya mkononi hutolewa.Wengi wenye asili ya utamaduni wa kuva suti wa nchi za magharibi hutushangaa wafikapo hapa na kuona baadhi yetu tukivaa suti na label ingali mkononi. Tukubali 'kuishi shule' na si lazima kila mtu ajue kila kitu; kuna siku ya kujifunza. Wala si lazima tuitane majina kama 'mshamba' na kadhalika, ili kuelekezana. Tunaathiri kukubalika kwa hoja zetu tukitumia lugha ya kejeli, dharau au matusi.Kujifunza ndiyo faida moja kubwa ya blog hii. Ndugu Mkuu wa wilaya na Balozi wa nanhii, nawasilisha hoja hii, kwa nia njema kabisa.

    ReplyDelete
  77. LMAO...umeniacha hoi kweli eti bngo watu wanaomba wawekewe labels na mafundi!!!!!!!!!!!
    Waambieni ni ushamba, kama mambo yako ni ya Armani ama Gucci ama versace utajulikana tuu, maana vitu vyao vimetulia, na kama wewe ni mwenzangu na mimi wa dollar store utajulikana tu hata kama uki-magnify labels zisomeke from 10 feet away!

    ReplyDelete
  78. Hivi mshawahi sikia kuhusu watu wanaoitwa LABEL HOES? Hawa ni watu wanaonunuaga nguo esp. designer clothes zenye maandishi makubwa ya hao ma-designer all over just so ujuw wamevaa nguo za bei ghali...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...