Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya muziki wa dansi na reggae, Ras Nas aka Nasibu (pichani), yuko tayari kufanya vitu vyake katika jiji la Trondheim, Norway, usiku wa Ijumaa tarehe 12 Desemba.

Kwa wabongo mliopo huko msikose kuhudhuria onyesho hilo la mwaka ambapo Ras Nas ametayarisha kikosi kikali chenye wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory Coast na Sweden.

Kwa tahadhari, asiye na mwana itabidi abebe 'fatuma.' Shoo itaanza saa nne na nusu usiku. Kabla ya hapo ma-DJ Roar Lund na Kristin Kjervold watakuwepo kufyeka nyasi ukumbini.

Kwa maelezo zaidi

www.rasnas.kongoi.com (kwa kiinglishi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Karibu kaka tuko wa tz kukuunga mkono.Hongera sana kwa juhudi zako.Karibu sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...