
Kesi hiyo ya madai ya Sh. bilioni mbili itakayosikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo Mrema analalamika kuchafuliwa jina kutokana na ripoti iliyotolewa na Jukwaa la Wahariri.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Mrema alisema amewafungulia kesi wahariri hao 14 kama watu binafsi kutokana na kuwa katika ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA), hakuona majina ya wahariri hao katika usajili wa jukwaa hilo.
Aliwataja wadaiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa na Jaji Razia Sheikh ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, Jesse Kwayu, Theofil Makunga, Absalom Kibanda, Muhingo Rweyemamu, Dina Chahali, Saed Kubenea, Jamila Abdallah, Neville Meena na Apolinary Tairo.
Alisema wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti la Majira, Meneja wa Kampuni ya Uchapishaji ya Business Printers, Mhariri wa Tanzania Daima, na Meneja wa Kiwanda cha uchapishaji cha Printech; na magazeti ya Majira na Tanzania Daima ya Oktoba 15, mwaka huu kwa kutangaza habari za kumkashifu.
Alidai Septemba mwaka huu, Jukwaa la Wahariri lilijipatia jukumu la kufanya uchunguzi wa habari zilizoripotiwa katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe na kutoa ripoti iliyomchafulia jina.
Aidha, Mrema alidai kamati hiyo ya uchunguzi kabla ya kutoa ripoti yake ilipaswa kumhoji ili ajieleze kama sheria inavyotaka, lakini cha kushangaza kamati hiyo ilitoa ripoti hiyo bila kumhoji, jambo ambalo amedai amenyimwa haki yake ya asili ya kutakiwa kujieleza na kusikilizwa.
“Habari hiyo imenifedhesha na kunichafulia jina langu hasa ukiangalia mimi ni kiongozi TLP, chama chenye wanachama nchi nzima na wanachama hao wana imani na mimi kiongozi wao, hivyo habari hiyo imenivunjia heshima kwa wanachama, familia yangu na jamii kwa ujumla,” alisema Mrema.
Alisema hata baada ya taarifa hiyo kuchapishwa gazetini aliwataka wadaiwa wote waombe radhi, lakini hawakufanya hivyo, jambo ambalo ameona kwenda mahakamani ili kusafisha jina lake na Watanzania wafahamu ukweli. Oktoba 14, mwaka huu, Jukwaa la Wahariri lilitoa ripoti ya uchunguzi wa Kamati ya Wahariri iliyoongozwa na Kubenea iliyochunguza kuhusu wana habari walivyoripoti msiba wa marehemu
Wakuu hivi ni kweli Lyatonga amekuwa mzee namna hii au ni hii picha au ni mimi sijam tia machoni siku nyingi?
ReplyDeleteVipi mzee wa Kiraracha, mbona ngozi ya uso kama imepata mabakax2?
ReplyDeleteHuo ni ule ugonjwa wa m-ba au ni mega-chunusi za uso. Things are right with this mzee, hebu tufahamishane wandugu.
Duu, hivi ukigombea upuresidenti mara nyingi unaumwa mpaka ugonjwa wa ngozi.
ReplyDeleteMzee Lyatonga naona muda wake umeisha, kachoka. its about time to call it a day and let vijana take the realm.
Mimi kwanza nilifikiri alisharudi Moshi kunywa mtori, kumbe bado anangangana tu. Kweli waafrika tunapenda umwinyi.
jamani huyu mrema huu uso wake umefikwa na masahibu gani tena?jamani ujana ni moshi na ukienda haurudi
ReplyDeleteHuyu mzee atakuwa ana matatizo ya INI kuna jirani yangu alikuwa anabadilika rangi kama hivi mwili mzima na Dr walimfahamisha ana matatizo hayo mie sio DR madr wanaweza kutufahamisha zaidi lakini kwa uzoefu wangu wa kuishi nchi nyingi najua hivo. hasa south africa ugonjwa huu upo sana matatizo yanakuwa ndani ya tumbo kuna kitu hakifanyi kazi vizuri na matokeo yake ngozi inakuwa hivo ni ugonjwa mbaya sana matibabu yake yanachukuwa muda mrefu sana na posibilty ya kupona ndogo sana mungu atamsaidia mwanasiasa wetu kwa ushauri angepumzika mambo ya siasa tu akajilia maisha yake yalio baki
ReplyDeleteWanakijiji hebu muheshimuni huyo ni mwanasiasa mkongwe na ndiye aliyekua wa kwanza kumsimamia kidete mzee ruksa. Mseme msemavyo kasaidia wengi. Maradhi kila mtu yanamfika si ndio visukari vya jela zenu si afadhali huyo ngangali. Kwani walio wanyonge kuliko yeye wapo tena au hamjui?
ReplyDeleteMichuzi wajibu wadau babu anazali gani?
ReplyDeletemsiendelee kumchafua baba wa watu!
ReplyDeletekama ni maradhi...kila mtu anaweza kupata..km imeandikwa hivyo!eboh!
Mike Cape!! Acha ujinga wako huo, hata kama ungekuwa unaishi wodini haikupi uelewa wa kujua magonjwa....na hata ungehamia mochwari haikusaidii kujua sababu za vifo...ni madaktari tu tena baada ya kumpima wanaweza kueleza anaumwa nini.
ReplyDeleteHuyu mzee, ni mwanamapinduzi wa kwanza kusimama hadharani na kukemea maovu, ilikunyamanzishwa! aliwahi kuundiwa cheo serikarini ambacho hakijawahi kuwepo, cheo cha juu sana lakini haikumukataza kukemea maovu.....unaweza ukasema unavyotaka lakini kelele zake za muda huo ndizo zilifungua watanzania wengi kuanza kusema hadharani na matokeo yake ndiyo tumeweza kupata watu wanaoweza kuongea hadharani na kusaidia kupunguza uozo selikarini.
Historia yake wanaitafsiri vibaya lakini "he is a legend in opposition" tukiachana na akina maparara yeye ni mmoja wa wasisi wa mageuzi Tanzania, hata nyerere alilijua hilo...you may take it or leave but i'm sure you'll take it!
Alipokuwa wizara ya mambo ya ndani, alitenda haki na kupunguza ujambazi kwa "record" ambayo haijawahi kuvunjwa......nikipindi hicho alipowaonea huruma wakimbizi walioingia Tanzania miaka ya 1972 na kuamua kuwapa uraia ambao walishindwa kuuchukua kwasababu walikuwa hawana uwezo wa kuulipia, lakini raiti kama UN ingemuunga mkono tusingekuwa tunapata aibu za kuwapa watu uraia kwa kulazimishwa na UN baada ya kuishi Tanzania miaka 36...is disgrace na nikinyume na haki za binadamu mtu kuwa mkimbizi miaka 36 at the watch of respected country like Tanzania, lakini hili lilizimwa baada ya yeye kuanza kupata matatizo kutoka chama tawala.
Mrema is someone who has courage and conviction...hao munapenda kusikia the dark side of somebody na msiopenda kujua uzuri wa mtu ndio mnamsema huyu mwanamapinduzi na mmoja wa waasisi wa siasa vibaya kwa sababu mnasikiliza upande mmoja...uliza historia ya Mrema utajua kwanini tumeweza kuwapata akina Zitto Kabwe, alifanya mengi ilikuweza kuwatengenezea watu kama Zitto jukwaa la kuongea ukweli bila matatizo.
Mwaka 1996 alipozungumzia rushwa iliyomhusishe Rais..hata mahakama alishindwa kumshinda kwasababu alikuwa na hoja yenye ukweli, kama watanzania wangemuelewa tusingekuwa na aibu tunayoipata juu ya akina Yona, kwani walikuwa wamesha fanya kazi za taaluma zao na walikuwa na maisha mazuri lakini wameharibu historia zao kwa kipindi hiki cha miaka 10, Yona alianza siasa miaka 10 iliyopita na kipindi kichafu.
Mrema anamapungufu yake lakini hii haitufanyi tudanganyike na kuanza kumsuta hata kwa vitu vilivyopo nje ya uwezo wake. Tujitahidi kumtendea haki jamani huyu mzee wetu mwanamapinduzi.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
FREEDOM OF SPEECH . THE JOURNALIST HAS A RIGHT TO WRITE AS LONGER THEY KNOW THE TRUTH AND EVIDENCE. MREMA IS LOOKING FOR HEADLINES . THE LAST PEOPLE YOU NEED TO HURT ARE THE JOURNALIST. THEY WILL NAIL YOU TO THE THROAT . HE IS JUST DEALING WITH THE FIRE
ReplyDeleteUmenifurahisha uliyeandika hapo juu kumsifia Mrema na kukemea wanaomsema vibaya. NIlikuwa TZ kwa mwaka mmoja nikapata nafasi yakumwona tena, amedhoofika sana: kiafya na kipesa. Ukweli ni kwamba CCM na vibaraka wake wamemmaliza. Watanzania wangapi wangeweza kukubali kuachia madaraka ya juu kabisa na marupurupu yake, wakapiga vita rushwa, wizi na ufisadi mpaka kufikia hali hiyo. Wasiojua, Mrema amesema wazi atamwunga mkono kiongozi yeyote wa upinzani kuwa rais na atashiriki kunedeleza vita kwa ajili ya haki za walala hoi!
ReplyDelete