
Picha no. 10 Baadhi ya wananchi na wadau mbalimbali wakifuatilia kwa karibu mjadala wa wazi leo kuhusu udhibiti wa bei ya mafuta nchini katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar.

Baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta wakifuatilia kwa karibu mjadala wa wazi leo kuhusu udhibiti wa bei ya mafuta nchini katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini Mh.William Ngeleja akiongea na waandishi wa habari leo kuhusu udhibiti wa bei ya mafuta nchini nje ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar leo mara baada ya kufungua mjadala wa wazi.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Haruna Masebu (aliyevaa suti nyeusi). Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Lazima kieleweke kama pipa lemeshafika $42 kwa nini mafuta yazidi kuwa juu hivyo?
ReplyDeleteWote Magabachori... hao wakiwa na mamilioni hamuulizi akipata mtu mweusi kelele nyingiiiiiii mmh! Wabongo bwana.
ReplyDeleteUdhibiti wa bei za mafuta ni muhimu sana hawa wafanya biasha wa kiachiwa hawawezi kupunguza bei hata kama soko la dinia bei itashuka mfano hapa south africa serikali inadhibiti bei pia ndo sababu mafuta mwezi uliopita bei ilikuwa R 10 per litre na sasa hivi ni R 7 per litre ne next week itashuka mpaka kufikia R 6 na ni kwasababu wadhibiti wanawapangia bei watu wa visima kutoka na bei ya Dunia iwapo hakuna mdhibiti inakuwa vigumu mno kwa hawa wafanyabiasharakupunguza bei wanachotaka wao ni faida tu sidhani kama wangeweza kupunguza bei kufikia kiassi hicho this is my opinion
ReplyDeleteWote wanatuzeveza tu.
ReplyDeleteTatizo lilianza pale tulipopotoka kuwaachia watu binafsi watupangie bei ya mafuta. Hivi kweli tujiulize, unamwachia ndugu yangu mwarabu akuletee mafuta, akupangie bei poa????? Ajaab kwel kweli. Unamwachia ndugu yangu mhindi akuagizie kisha akupangie bei ya mafuta,unategemea nini hapo.
ReplyDeleteKumradhi kama nimegusa hisia kwa yeyote, ila kama mzalendo ninayeipenda nchi yangu inanibidi niseme.
Kuna jambo moja linanitatiza, labda ndugu zangu wadau mtanisaidi. Nakwazika kidogo na huenda nikawa na jazba lakini kama binadamu ninamadhaif na naomba samahani tena enadapo nionesha jazba.
Hivi kwele serikali yetu ilishindwa kabisa kuliendesha shirika la mafuta na kuamua kukiua kiwanda cha usafishaji mafuta "TIPER" pale kigamboni!?????.
Hawa hawa TIPER wakawa na mikakati ya kujenga jengo la mafuta house (SASA BEN MKAPA HOUSE, ni kweli hili shirika lilishindwa kujiendesha???
Ninachojua mimi, lile jengo MAFUTA HOUSE lilikuwa "limedizainiwa" kuwe na maabara kubwa tu ya uchunguzi wa mafuta, lakini ati wakashindwa kulimalizia na NSSF au sijui wadau gani ndo wakapewa kulimalizia na likabatizwa jina tulionaloliona leo. Hivi kweli, kweli walishindwa kabisa kulimalizia hadi likabinafsishwa!!!! Wakati wana design kulijenga wlifikiri kitu gani na nini kilichopelekea wakashindwa???
Ni kwa nini serikali ilijitoa ghafla katika kudhibiti bei ya bidhaa hii muhimu na kuwaachia ndugu zetu wenye asili ya kiasia kuagiza na kisha kudhibiti bei ili hali fika serikali ikitambua ya kuwa mafuta ndo mhimili wa mambo yote.Mfano: unapopandisha bei ya mafuta japo kwa shilingi moja, umeshaathiri mfumo mzima wa uchumi.Kumbuka, mfumuko wa bei kwa bidhaa utakuja juu, nauli kwa ajili ya kusafirisha mazao toka vijijini tunakojisifia ya kuwa asilimia 80 ya walalahoi wanaishi huko zitapanda kwa kasi, nauli itapanda hasa kwa wananchi hasa wasio na kipato au wenye kipato cha chini itawawia vigumu kuja mijini kupata huduma muhimu ambazokwayo huko waliko vijijini ni ndoto kuzipata.
Kama kweli serikali ya awamu ya nne imepania kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania, lazima iliangalie suala la udhibiti wa uagizaji na upangaji wa bei ya mafuta kwa jicho mujarab.
Mpiga Box (Mzalendo)
Mimi sielewi sera za uchumi Bongo maana bei ya mafuta imepunguwa kwa zaidi ya nusu kufikia Dola 42 kwa pipa lakini hakuna nafuu yoyote kwa mwananchi.
ReplyDeletePia bei ya fedha ya 'madafu' yaani Tz Shillingi imeimarika thamani kulinganisha na US$/UK£ lakini hakuna faida au nafuu kwa mwananchi.
Mi nauliza hivi Tanzania haipo ktk sayari ya duniani(earth)? Nchi yetu ipo sayari ya Pluto? wachumi tupeni darasa, mambo haya vipi?!*
Bongo tambarare.....summer tulilia gas ilivyokua $4.05 sasa hivi tunajimwaya tu na &1.47 per gallon....regulation plus competition ndio jawabu tu
ReplyDeleteInabidi kuwe na chombo cha kuangalia hili jambo
Pia kuangalia hizo gauge zao ni kiasi gani cha gas wanawapa watu kwa hela yao?
Wahindi wnakamchezo kakuuza au kuadd hewa kwenye gas. Huku ilikua ndio biashara yao kila muhindi alikua ana gas station sasa hivi hawazitaki kabisa. Kila mmoja anataka kuiuza lakini wateja hamna...Siku hizi kuna mystrey shoppers kila siku kwenye magas station yao na hao watu wanavifaa vyao kiboko...ukiuza hewa tu fine hiyo unayoipata ni ya kufa mtu.....
Wangefuatilia na hilo isijekua price ipo juu na pia watu wanapata gas kidogo tu na nyingine ni faida nyingine juu baada ya kurip off watu