Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya Sikia Kengele inayoendeshwa na Tanzania Marketing and Communication (T-Marc) kwa kushirikiana na Zain, Dar leo. Zain ilitoa simu selula kwa washindi wanne na muda wa maongezi kwa washindi watano huku T-Marc ikitoa mshindi wa pikipiki ambao watakabidhiwa zawadi Desemba 12, mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa Selcom Gaming, Juma Mgori na Meneja Mawasiliano wa T-Marc, James Chialo.

Meneja Mawasiliano wa Tanzania Marketing and Communication (T-Marc), James Chialo (katikati) akimpigia simu mmoja wa washindi wa promosheni ya Sikia Kengele inayoendeshwa na T-Marc kwa kushirikiana na Zain Tanzania, Darleo Zain ilitoa simu selula kwa washindi wanne na muda wa maongezi kwa washindi watano huku T-Marc ikitoa mshindi wa pikipiki. Kushoto ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe na kulia ni Meneja Masoko wa Selcom Gaming, Juma Mgori.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hizi habari za Zain ziko too much katika blog hii. hivi hii ni nini?? na inasaidia nini kusikia wanachokifanya kila siku? Hawa wanalamba hela za watu tu. Promosha habari zinazolenge mabadiliko au kinachoendelea kimaendeleo kwa wananchi walio asilimia 95 chini kiwange cha maisha bora.
    Dar na yoote yatokeayo hapo sii Tanzania hiyo. Lazima nchi nzima na miji yoote iwe inasemwa jamani.

    ReplyDelete
  2. The last time we checked hii ni blog spot na sio gazeti la serikali. Its all about publicity in this capitalist world sasa mtu anapo lalamika ati zain is always here, its more of a personal issue.stop hating! sio kila sehemu tuoneshwe habari za masikitiko we need to know that our industries are excelling.to me hawa watu wa zain wanafanya kazi nzuri sana keep it up!!

    ReplyDelete
  3. kweli kabisa anon. wa hapo juu.
    halafu mimi nampenda sana huyu dada aitwae tunu kavishe yani anaonekana ni no nonsense woman, na anaipenda kazi yake. mara nyingi unakuta wasomi wengi wana vipaji ila hawana passion katika kazi.

    ReplyDelete
  4. Kaka mithupu eeh, najua kwamba weye ni ambasada wa Zain kwa hiyo ni sahihi kutoa malalamiko yangu kwako ili uwafikishie wahusika.

    Mie mdau nipo huku udhunguni kwa mzee Kichaka ambapo siku si nyingi Mjaluo Mmarekani (Obama) anajiandaa kuchukua nchi.

    Sasa ndugu yangu, hapo zamani wakati wa Celtel, mie na wenzangu wengi wa huku udhunguni tulikuwa tunatuma text-meseji zetu kwa urahisi sana kwa ndugu zetu wa huko bongo waliokuwa wanatumia Celtel. Pia tulikuwa tunawapata kiurahisi mno tulipokuwa tukiwapigia kwa maongezi. Lakini siku za hivi karibuni, imekuwa shida-bin-shida kuwapata hao wamatumbi wenzetu wa bongo si kwa meseji wala kwa maongezi. Kila tukipiga tunapata ujumbe kwamba "circuits at destination are busy" ikiwa inamaana mitambo ya Zain inacheua. Sasa, imekuwaje tena huko? Wamepunguza bajeti ya mafundi mitambo na kuwaongezea hawa watu wa promosheni au? Au wamepata wateja wengi kwa mkupuo na walikuwa hawajajiandaa kimitambo.

    Naomba unifikishie huo ujumbe.

    Mdau wa Udhunguni

    ReplyDelete
  5. Huyu juma mgori meneja, afadhali ameenda bongo tulikuwa tunabeba nae mabox ya walmart huku wichita, marekani .kweli bongo tambarare, na mimi nitarudi bongo nikimaliza shule yangu te te te te yaani juma ameiva kishenzi.

    ReplyDelete
  6. Kweli kabisa anon wa mwanzo kabisa umesema la kusema.Kila ukifungua humu zain, zain, zain.Manaake kamawana ubia fulani na michuzi.

    ReplyDelete
  7. m naungana na anon. wa 7:39a.m huyo dada bwana anaonekana yuko decent sana.ok kazi njema dada yangu ni hayo tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...