Ndugu wadau,
Napenda kutoa salamu za kipindi hiki cha siku kuu (Holiday Seasons), Heri ya Siku kuu ya Noeli na Mwaka Mpya 2009.
Blog ya SCHOLARSHIPS www.makulilo.blogspot.com inashukuru kwa ushirikiano wa wadau wote hadi kufikia hatua hii (sasa ina miezi 7). Blog inaahidi mambo mengi mazuri, na inatoa wito kwa wadau kufanya applications zaidi khs masuala yetu ya NONDOZZZ KWA WADAUZZZ.

Note: Nimeambatanisha na picha yangu, hapo nilikua vekesheni nje ya mjengo wa kaka Barry Obama (WhiteHouse) Washington DC.
MERRY CHRISTMASS & HAPPY NEW YEAR 2009
MAKULILO Jr,
makulilo@marshall.edu
scholarships101@aol.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Bro kata nywele

    ReplyDelete
  2. Ama kweli mshamba ni mshamba, ata aende mjini, kibanda cha simu atakinona kama choo. Waosha vinywa siyo krismasi, changamkieni hii

    ReplyDelete
  3. Mzee huko kwa Obama si ungemtafuta hata Joni mashaka akupe ujanja wa mjini, ww unaenda kichwa kichwa tu, subiri utakiona cha moto mtu wangu pole sana. waenga Walisema Jogoo wa shamba hawiki mjini
    Krismasi njema

    ReplyDelete
  4. mshikaji ww umechemsha, mbona unatuletea kamera ya mwaka 2037, au ndo kumaanisha umefika kwa Obama?

    Hiyo geti so ndo ile ya pale mikocheni kwa mkuu wa naniiiiiii?

    ReplyDelete
  5. Anony nyote hapo juu, stop your backwardness. Basically kaka Makulilo anafanya kazi nzuri sana ku'summarize opportunities for scholarships available for Tanzanians huko majuu. There are dozens of Tanzanians in higher educations institutions abroad who are fully funded and lack the motivation to communicate such opportunities to their fellows back in Tanzania. Tabia ya umimi umejaa sana waTanzania. Changamoto ni kwa waTanzania wengine walio vyuoni ulaya na marekani ku'publicize nafasi za scholarship kwa wenzao, na kuacha 'utapiafikra' uliokithiri. Huo umoja wa waTanzania tuoimba are just blind lyrical claims. Hongera sana kaka makulilo.
    Mdau,
    Kamachumu

    ReplyDelete
  6. Jamani ushauri wa bure unaponunua camera hasa digital usikimbilie tu kufotoa fanya active setting hasa kalenda, ona sasa jamaa yetu huyu anaonekana kukurupuka tu sijui ushambaa au anataka kuchekesha jamii,

    Kama kucheza na settings za digital huwezi ungewaomba hata hapo dukani uliponunua wakurekebishie hiyo kalenda au hata ungalimtafuta kwa ushauri mfotoaji kaka Michuzi lol!!

    Hili onyo kwa wengine wote wenye hivi vijitabia vya uzembe na ushamba!!!

    Nawasilisha!!

    ReplyDelete
  7. HAMNA KASORO YOYOTE NA EITHER HIYO PICHA YAKE OR UJUMBE WAKE LAKINI BADO MMELETA KEJELI, MHHHH MNANISHANGAZA NA FIKIRA ZENU, ZINANIPA WASIWASI, IT SEEMS YOU ARE STILL NOT THINKING FORWAD HOLISTICALYY, YOU ARE STILL THINKING INSIDE THE BOX. KWA HALI HIYO HATOFIKA KOKOTE KWANI INAWEZA KUWAFUNJA MIOYO WENGINE KULETA HABARI ZITAKAZOSAIDIA WATU AMA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE

    ReplyDelete
  8. Huyu jamaa ni mtu miaka ya mbele kuliko sisi nadhani. Sisi tuko mwaka 2008 tukienda 2009 bali yeye ni wa 2037. Good job

    ReplyDelete
  9. Bwana Makulilo hongera kwa kupanda Time Machine. Sie wengine huwa tunazionaga kwenye movies tu tukadhani ni uongo kumbe kweli zipo.

    Hebu tupe michapo ya 2037 maisha yatakuwaje?

    ReplyDelete
  10. Mshikaji asante kwa msaada wako kwa jamii, kwa hili ninakushukuru sana. Ila vazi lako na hiyo hairstyle mwanangu imekaa kama wale ma-actor wa 1970s; kina Nani wale walikuwa wakiitwa? I think, Fred Williamson. Yaani hapo watu hawakawii kukuomba autograph.. he he he!!

    ReplyDelete
  11. Anaweza akawa mshamba, au hajui mambo, lakini tumpe sifa kwa kuwa Mtanzania mwenye kupenda maendeleo ya wengine. Ubinafsi Watanzania hautatufikisha popote. Huyu kijana hana sababu ya kusakamwa, ana mambo ya maana kuliko wengi wetu ambao hatuna lolote la maana zaidi ya kuropoka kwenye blogu. Makuliko jitahidi kujenga nchi yako, majirani zetu wanatupita kwa sababu ya ujinga wetu, usijali kelele za mlango, hazimzuii mwenye nyumba kulala.

    ReplyDelete
  12. MMESHIKILIA MWAKA 2037, HIVI MNAUHAKIKA KUWA HUO NI MWAKA? TAREHE ZA WAPOI HIZO. ZA U.K. ZINGESOMEKA HIVI 10/09/2037 ZA U.S.A. ZINGESOMEKA HIVI 09/10/2037 U.K. WANAANZA NA TAREHE, MWEZI ALAFU MWAKA. NA U.S.A. WANAANZA HIVI MWEZI, TAREHE NA MWISHO MWAKA. HIYO HAPO KWA PICHA 2037 NI PICHA YA NGAPI IMEPIGA HIYO KAMERA TAREHE HAPO NI HIZI MBILI ZA MWISH TU. HIYO HAPO NI SAWA KABISA NI PICHA HYA 2037 YA TAREHE 10 MWEZI WA 09 KI-U.S.A.

    ReplyDelete
  13. We anon wa December 27, 2008 6:35 AM hebu toa pumba zako.

    Kama huna na/au hujawahi kutumia digital camera sema usaidiwe.

    ReplyDelete
  14. Mdau wa December 26, 3:01 Pm, yaani umeniacha hoi sana. Nilikuwa nacheka kama mwehu kama nusu saa hivi. Balozi ambassador-extraorninary na pleni-potentiary Michuzi (cheo cha juu cha ubalozi) anatusaidia sana kupunguza stress zetu hapa ughaibuni. Shukurani sana sana. Time machine HA! Ha! HA! yaani kweli kabisa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...