Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe anayesomeshwa na Zain Tanzania, Noel Mazoya (wa pili kulia) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kumpata mshindi wa fedha taslimu sh. milioni 1 wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania jijini Dar jana (Desemba 18, 2008). Kushoto ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein, Meneja Masoko wa Zain Tanzania (Kitengo cha Wateja), Kelvin Twissa na kulia ni Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya.

Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania imeongeza zawadi za fedha taslim katika promosheni yake ya Endesha Ndoto 2 na itatengeneza milionea mmoja kila siku ya wiki kuanzia Alhamis 18, 2008 ambapo mkazi wa Mwanza Wifred Baltari (24) ameibuka mshindi wa Tshs milioni moja ya kwanza.


Meneja Masoko wa Zain Tanzania Kelvin Twissa alisema jijini Dar es Salaam kwamba zawadi za fedha taslim ilikuwa ni zawadi kwa wateja wa Zain katika kipindi hiki cha siku kuu na washindi wanapatikana katika droo ya kila siku.


“Zain imeongeza zawadi za fedha taslim katika promosheni yetu ya Endesha Ndoto 2 kuwawezesha wateja wetu kufurahia msimu huu wa siku kuu na kuweza kijununulia mahitaji mbali mbali. Tunawazawadia wateja wetu kwa uaminifu wao na kwa kuichagua Zain kuwa mtandao wao wa mawasiliano,’’ alisema Twissa.


Kushiriki katika droo ya zawadi za fedha taslim mteja wa Zain anapaswa kuwa amejiunga na promosheni ya Endesha Ndoto 2 kwa kutuma neno NDOTO kwenda 100.


“Wateja wa Zain waliojiunga na NDOTO wanapaswa kuendelea kutumia huduma za ZAIN ili kujiongezea nafasi za kushinda,’’ alisema Twissa. Aidha alisema licha ya zawadi ya fedha taslim wateja wa Zain bado wataweza kujishindia zawadi kubwa katika promosheni ya Endesha Ndoto 2 ambayo ni gari Jipya aina ya Toyota Land Cruizer pamoja na zawadi nyingine za muda wa maongezi na simu za mkononi,’’ alisema Twissa na kuongeza kwamba kadri mteja atakavyotuma sms nyingi ndivyo anavyojiongezea nafasi ya kushinda zawadi hizo.

‘’Zain inarudisha kwa jamii. Licha ya zawadi ya fedha taslim, bado tunatoa zawadi za muda wa maongezi, gari la Toyota land cruizer pamoja na simu mpya za kisasa ikiwemo simu aina ya Blackberry na nokia,’’ Twissa alisema.

Mshindi huyo wa kwanza wa fedha taslim alichaguliwa katika droo iliyoendeshwa Makao Makuu ya Zain mbele ya waandishi wa habari na wawakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Zain pia ilimchagua mshindi wa muda wa maongezi wa Tsh 100,000 ambapo mkazi wa Buguruni Rachel Zakaria aliibuka mshindi.
Wateja wengine wa Zain wapatao 1,100 pia watapata muda wa maongezi katika droo ya wiki hii, ambapo 100 watapata muda wa maongeai wa 25,000, na wateja 1000 watapata muda wa maonegezi wa Tshs 5000 kila mmoja.

Zain imekuwa ikitoa gari moja aina ya RAV 4 kila mwezi tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika promosheni ya kutoa zawadi ya magari kubwa kuliko zote katika historia ya Tanzania. Mshindi wa RAV 4 ya nne atachaguliwa wiki ijayo wakati mshindi wa zawadi kubwa katika promosheni hiyo ya Toyota Land Cruiser atachaguliwa December 31 mwezi huu.

“Zain siku zote inajizatiti kuboresha maisha ya Watanzania ikiwa ni sehemu ya wajibu wetu kwa jamii na kwa kutoa zawadi hizi zote tunataka wateja wetu wanufaike kwa kuwa sehemu ya Zain, na kuwa sehemu ya Ulimwengu Maridhawa wa Zain,’’ Twissa alisema.


Zain ilizindua Endesha Ndoto Yako 2 mwanzoni mwa mwaka huu ili kuwazawadia wateja wa Zain kwa kuichagua Zain kwa kuwa mtandao wao wa mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. "Kubonyeza kitufe" ni msemo unaotumika sana hususan katika mtandao huu. Najiuliza siku zote hicho kitufe kinachobonyezwa kwenye laputopu kiko sehemu gani? Kwa maana ya "kitufe" natarajia kitakuwa ni kitu chenye kufanana na kimpira kidogo na siamini kwamba kipo na hata kama kipo siamini kwamba ndicho ambacho hubonyezwa.

    ReplyDelete
  2. Hakuna cha kuboresha maisha hapo. Wizi mtupu... Voda, Zain, TTCL, na wengine ISIPOKUWA TIGO ni wezi watupu. Michuzi kama wewe ni mkali pachika hii uone ubalozi wako utakavyokuwa matatani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...