Serikali imetoa Sh bilioni 2.5 kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ikiwa ni fedha za awali za kuendesha kampuni hiyo na kulipa baadhi ya madeni kati ya Sh bilioni 3.3 zilizoombwa na kampuni hiyo kama mtaji wa haraka.


Sambamba na hilo, Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa ameunda Tume na kuitaka ifanye kazi kwa siku 21 tangu Desemba 29, mwaka jana ili kubainisha kiini cha matatizo ya ATCL baada ya ripoti ya Bodi ya kampuni hiyo kutotoa maelezo ya kutosheleza.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ya watu saba ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrissa Mshoro na wajumbe wengine sita, alisema Dk. Kawambwa.

Kuhusu mtaji huo wa Sh bilioni 2.5, Dk. Kawambwa aliwaambia waandishi wa habari jana Dar kuwa serikali imeamua kuibeba ATCL kuanzia mtaji mpaka ulipaji wa madeni kwa kuwa ni mmiliki wa kampuni hiyo na kwamba itatoa fedha kwa awamu kulingana na mahitaji ya wakati ya kampuni hiyo.


HABARI KAMILI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. HIVI PESA ZA NCHI HII AZINAGA KAZI??? ATCL NI MAJUZI TUU TUMEELEZWA WAMEINGIA MIKATABA MIBOVU YA UKODISHAJI NDEGE,NA KUPATA TATIZO LA PILI LA KUFUTIWA LESENI HAYA BADO AYAJAPOWA NA KUELEZWA KIUNDANI NINI TATIZO LEO MNAWAPATIA TENA 2B ZIYEYUKE MUUNDE TUME.AYA WEEEE

    ReplyDelete
  2. Kwanza wajaribu kucut costs kuanzia kwa utawala na bodi all the way to the bottom of the organization. CEO, board etc can do without the unnecessary perks that have hampered ATC for decades.

    Cutting costs should also mean layoffs, unfortunately. The company should be streamlined to almost a skeleton crew so that they can reap the benefits of a smaller, streamlined workforce - the remaining workforce should then be able to work diligently and industrially. Now, losing jobs is almost unheard of in Tanzania, and nobody likes to see someone out of a job, but hey, its cut-throat competition out there and only the strong survive.

    If it is to lease other planes, go for regional jets an/or quieter turbo-props - those who know the industry should understand me on this. The regional jets would boost the internal routes as well as the neighboring country routes. To add money streams to the company, maybe get an older version of Boeing 737 and convert it into a cargo plane shuttling between Dar and the southwest Asia regions of Dubai, Qatar, Bahrain etc, far east regions of Honk Kong, China and India and southern Africa, specifically RSA. Ever heard of Mojave Desert graveyard for airplanes? Ever heard of DeHaviland of Cananda and Brazil's Embrear?

    And, yeah, get some airline industry people on board instead of these old, tired-ass, do-me-a-favor, recycled CEOs, DGs and board members!

    My two cents......

    ReplyDelete
  3. Kweli sisi ni wadanganyika, inatia aibu sasa!

    ReplyDelete
  4. Bailout !!
    Nilifikiri ni Marekani tu wana uwezo wa ku-bailout makampuni yaliyo hoi, kumbe hata bongo tuna jeuri, si mchezo.

    ReplyDelete
  5. Sababu za timu ya ATCL kushushwa daraja na chama cha timu za ndege duniani - IATA.


    1. kukodisha wachezaji (ndege) mbovu +

    2. kufutiwa leseni na IATA baada ya kupewa notisi kwa mwaka mmoja kuwa wachezaji wake hawakupita kwenye fitness (airwortness) test

    SABABU NA DAWA

    Kocha hana ujuzi wa kutosha, mpira unachezwa bila mpangilio hakuna dira wala mwelekeo aidha kocha na wasaidizi wake wameshazeeka hawana uzoefu wa mpira pamoja na uwezo wa kumudu kasi za ligi (business in capitalist environment) za siku hizi!! Mheshimiwa Waziri, ajiri kocha mpya ili timu isizidi kushushwa daraja hadi la 6, makocha siku zote vigumu kungatuka!

    ReplyDelete
  6. Hawa viongozi (watawala) wetu kweli vichwani mwao hamna kitu kabisa. Kwa nini tuendelee kuwa na shirika amabalo kila siku linakomba pesa ya walipa kodi wa nji hii.Yaani wanawapa tena mbwa mwitu wanakondoo wakiamini kuwa mara hii hawatawararua!? huu nao ni ufisadi mwingine. Mataka na wenziyo Mungu awape nini tena hayo mabillioni yamekuja tena yatafuneni kama hamna akili nzuri (ambazo ni kweli hamna) Kijua ndo kinazama hivyo chukueni mihela hiyo.

    ReplyDelete
  7. Leeman brothers Bank imeachwa ifilie mbali na ATCL bado inafanywa kama yai likidondoka litapasuka na nchi nzima itatokomea.
    Come on ! Wake up acheni kuchezea visenti vyenu.Imarisheni mashule na huduma za tiba kwa walala hoi.
    Ex TZ

    ReplyDelete
  8. "Five vehicles now held by the bank include Toyota Land Cruisers - SU 37079, SU 37081, SU 37082, SU 37083 and 37084 which were bought from Dubai and another three vehicles. But the only working vehicle is the Toyota Land Cruiser SU 37085 which is used by the Chief Executive Officer, Mr David Mattaka".wadau tafuteni kwanini huyo CEO kapata kazi ATCL wakati alifukuzwa PPF. naomba usiibanie hii tena kaka hataka CEO nindugu yetu

    ReplyDelete
  9. MLIAKUVANA nimekukubali lakini ndo kwanza serikali imeunda Tume ya kuchunguza 'kiini cha tatizo'.

    ReplyDelete
  10. Biashara ya usafiri ya ndege ni ngumu sana duniani kote. ATC ina wafanyakazi wengi mno ukilinganisha na biashara yake. Hauwezi ukategemea kampuni kuendesha biashara kwa faida kwa kutumia ndege nne au tano lakini ina wafanyakazi zaidi ya elfu. Wenzao marekani wanafilisika na wana ndege mia moja na zaidi.

    Kama serikali inataka ATC iendeshe biashara yake kwa faida inabidi ipunguze wafanyakazi, inunue ndege kama kumi zaidi. Kuendelea kama ilivyo sasa ni kupoteza fedha za wananchi hasa ukizingatia ATC haina sifa ya kutoa huduma nzuri kwa abiria, watu wengi wanajua kuwa "ATC ni ANY TIME CANCELLED" kwa jina lingine.

    ReplyDelete
  11. Jamani jana nilivyokuwa mnasikiliza Mustafa Nyanganyi Mkiti wa Bodi ya ATCL kwenye TBC nilipata kichefuchefu. Yaani huyu mzee hata haya hana maana aliyokuwa anayazungumza ni siasa tupu tena za enzi za mwalimu. Jamani jamani. Aah!!Uwizi Mtupu!!

    ReplyDelete
  12. Ni lazima ATC ije na kaulimbiu mpya! Ni lazima kuitangaza kitaalam !

    Ilipozinduliwa kutoka kumezwa na Afrika Kusini, nilishauri kaulimbiu mpya iwe:

    Air Tanzania
    Soaring to New Heights!

    Hii inaendana sawia na huo mkia wa ndege yetu pamoja na kufufuka kwake:

    Kilimanjaro - a soaring mountain, the Peak of Africa!

    The Giraffe - a soaring neck to reach higher twigs!

    ATC inafufuka kutoka the deep of performance doom!

    Born Again Pagan

    ReplyDelete
  13. Petro,

    Pole na kichefu chefu, eti ndio mmoja wa mawaziri walioperform vizuri sana wakati wa nyerere,.... amesoma havard school of government, balozi mzuri usa, uae, ....blah blah, wakati wake umekwisha ni spent force, he seemed to be good during socialism.., socialism is over....now we are in capitalism era..

    you need to deliver, vinginevyo una wajibika, siasa na ufanisi havichanganyiki...kwa pembeni yuko bwana mataka...proven track record ya PPF si nzuri..inanukia ufisadi...basi naona hapo ndio utatapika kabisa...pole petro!

    ReplyDelete
  14. uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kaaazi kweeeeeli jaman wa-Tz

    ReplyDelete
  15. Haya wale mnao bwabwaja kuhusu balozi Nyanganyi, sasa serikali imeishatoa tamko na pesa, what were your points????? TATIZO SI UONGOZI BALI NI FWEZA! HUWEZI KUWAPA SHIRIKA LENYE MADENI YA BILIONI NA MTEGEMEE WAONDERS WITHIN A YEAR! Kama unazungumzia socialism is a problem then kuanzia RAIS WAKO NA MAWAZIRI WAKE NAO WAMEPITWA NA WAKATI MAANA WOTE NI WANAFUNZI WA NYERERE! PLEASE BRING YOUR POINTS KUHUSU ATC NA ACHA KASHFA KAMA UNA ISSUE ZAKO BINAFSI ZIWEKE KAPUNI THIS IS THE ERA YA WASOMI WANAOSHUSHA POINTS KUHUSU VITU NA SIYO KUANDIKA LUGHA ZA MATUSI NA KUITA WATU MAMBUMBU! wewe ndiyo mbumbumbu maana yote yaliyosemwa na uongozi wa ATC hukuyasikia, mbon ahuiulizi serikali yako nani aliyesaini mikataba na Afrika Kusini na kuiua ATC WAS IT MATAKA OR NYANGANYI? MBONA HAMUWATAJI WALIOIFILISI ATC NA BADALA YAKE MNAWASAKAMA HAO WALIOMBWA KUJA KUIFUFUA.

    ReplyDelete
  16. Kichefuchefu hicho mkakitoe kwa serikali yenu iliyoifilisi ATC. Mataka na Balozi Nyanganyi wamepewa shirika lililokwisha kufa kwa sababu ya mikataba mibovu iliyosainiwa na viongozi waliopita na Afrika Kusini. Ufinyu wa fikra zenu ndiyo zinawafanya muandike maneno machafu na matusi, Nani wa kuona haya? Balozi Nyanganyi anayeeleza ukweli au Viongozi waliosaini mikataba mibovu. Umeona sahihi ya mataka au Nyanganyi kwenye hiyo mikataba ya Afrika kusini? Acheni Nyodo, andikeni vitu vya ukweli na kuelimisha jamii than kuandika PUMBA

    ReplyDelete
  17. HAYA WAOSHA VINYWA SOMA HIYO HABARI HAPO CHINI KAMA UNA MAJIBU YATOE KAMA HUNA KAIULIZE SERIKALI YAKO ITOE MAJIBU:



    Na Leon Bahati
    MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Balozi Mustafa Nyang’anyi amesema kuwa yupo tayari kujiuzulu iwapo itathibitika kuwa, bodi yake ndiyo chanzo cha ndege zake kuzuiwa kuruka.

    Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na Mwananchi Jumapili kufuatia wafanyakazi wapatao 200 wa ATCL kuazimia kwenye mkutano wao jijini Dar es Salaam juzi kuwa, wataishinikiza bodi na menejimenti kujiuzulu kwa kuwa walishindwa kukabiliana na dosari ndani ya shirika hadi kulazimishwa kusimamisha huduma za safari.

    Hasira za wafanyakazi hao zilitokana na hatua iliyochukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA) ya kuzuia shirika hilo kwa siku kadhaa baada ya kugundua dosari 482 ambazo ni kinyume na kanuni za Umoja wa Mashirika ya Ndege ya Kimataifa (IATA).

    “Kama bodi ndio tatizo, hata leo niko tayari kujiuzulu,” alisema Balozi Nyang’anyi ambaye aliwahi kuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Pili katika wizara ambayo wakati huo ilikuwa inajulikana kama Mawasiliano na Uchukuzi mwaka 1985 hadi 1989.

    Vilevile alisema kuwa, yupo tayari kujiuzulu iwapo watajitokeza watu ambao wakichukua mamlaka ya bodi wataweza kuiendesha ATCL bila matatizo yoyote katika mazingira ambayo shirika lipo kwa sasa.

    Alipotakiwa kueleza kiini cha matatizo ya ATCL, Balozi Nyang’anyi alisema kuwa ni uwezo mdogo wa fedha unaoikabili serikali ambao umekwamisha mipango ya kulisuka upya shirika hilo baada ya kuvunja ndoa na shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mwaka jana.

    Alifafanua kuwa baada ya kuvunja ndoa hiyo, shirika hilo lilikuwa na deni la Sh19 bilioni na serikali ikaahidi kuwa itabeba jukumu la kulilipa na hadi hii leo bado halijalipwa.

    Kwa mujibu wa Nyang’anyi ahadi hiyo ilitolewa na serikali kupitia Wizara ya Miundombinu Machi 2007 na pia iliahidi kulisaidia shirika hilo mtaji wa kuanzia kutokana na hali mbaya ya kifedha iliyokuwepo baada ya kuachana na SAA.

    Katika kutekeleza hilo, alisema serikali iliiagiza bodi kufanya kikao haraka ili kufanya tahmini ya kufufua shirika na kulirejeshea hadhi yake, jambo ambalo walilifanya na kabla ya kufika mwisho wa Aprili 2007, wakawa wamewasilisha mchanganuo ulioonyesha ATC itafufuliwa kwa dola za Marekani 60 milioni sawa na Sh76.2 bilioni, kwa ajili ya kukodisha ndege.

    Alifafanua kuwa hadi leo serikali haijalipa deni kama ilivyoahidi na wala haijatekeleza maombi ya fedha hizo kulingana na mchanganuo waliowapeleka na mara kadhaa wamewakumbusha lakini wameambulia patupu.

    “Mpaka sasa deni waliloahidi kulipa bado. Mtaji wa dola 60 milioni bado. Sasa katika mazingira kama hayo, unadhani shirika litajiendesha vipi,” alihoji Balozi Nyang’anyi akielezea kuwa suala hilo walishalifanyia kikao na mawaziri wa Fedha na Uchumi na wa Miundombinu ikashindikana.

    Baadaye, alisema walimwendea Waziri Mkuu ambaye aliagiza wakutane na Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Katibu Mkuu Miundombinu, lakini vile vile ikashindikana.

    Alipotakiwa kueleza hali ya ATCL wakati wanaipokea kutoka kwa SAA na hali halisi ilivyo ndani ya ATC kwa sasa, Balozi Nyang’anyi alisema yeye amekuwa karibu na shirika hilo kwa muda mrefu na kwamba miaka ya 1980, lilikuwa ni shirika imara lakini walipolipokea kutoka kwa SAA lilikuwa katika hali mbaya.

    “Wakati nikiwa namaliza kipindi changu cha uwaziri wa Mawasiliano na Uchukuzi mwaka 1989 nililiacha likiwa linamiliki ndege 13, lakini tulipolipokea Machi 2007 tulilikuta bila ndege hata moja,” alifafanua.

    Alibainisha kuwa kwa sasa limeshindwa kununua ndege zake lenyewe kutokana na kutokuwa na fedha na badala yake linajiendesha kwa kukodisha.

    Kwa sasa alisema kuwa ATC ina ndege tatu za kukodi, ambazo ili ziweze kuruka mara moja kwa siku inabidi watumie Sh84 milioni wakati fedha za nauli za abiria zinakuwa hazijapatikana kwa kuwa makusanyo hayo hukamilika baada ya wiki mbili kutoka kwa mawakala wanaouza tiketi.

    Ucheleweshaji huo, aliuelezea kama moja ya matatizo katika kuendesha shirika hilo lenye mtaji mdogo na lisiloweza kukopeshwa na benki kutokana na kuwa na deni kubwa la fedha.

    Kwa sababu hiyo, alisema kuwa hasira za wafanyakazi hao zinatokana na hofu juu ya ajira zao kutokana na shirika kujiendesha katika mazingira magumu, hivyo akawataka wawe na subira kwa sababu mambo yatakuwa mazuri katika siku chache zijazo.

    Alisema kuwa bodi inatarajia kukutana wiki ijayo, ambapo pamoja na mambo mengine itaainisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na msimamo wao kuhusu hali ilivyo sasa ndani ya shirika.

    ReplyDelete
  18. Sasa Hii inakaaje? Waziri wa Miundombinu na waziri mkuu mbona mmenyamaza kama haya yanayodaiwa ni ya uongo? kama watu wanavyosema hapo juu? Kwamba uongozi umelifilisi shirika?? Hata bubu atasema. Huu urasimu wa nchi hii utatupeleka kubaya. Wenzenu developing countries hakuna kulalia mafile. File likiingia lazima utoe jibu within 24 hours au utakuwa accountable ulikuwa unafanya nini masaa 8 uliyokalia kiti chao. This is the mentality we need to build in this country. Nothing moves. Nilinunua kiwanja last year, nikaambiwa kuwa nikiishalipa it will take three months kupata offer sijui au cheti cha umiliki. I was lke three months after cashing my moni? Na bado nakisubiri maana hata kuuliza tena nimeishachoka. Kuna madaktari wanataka kuja kufanya uchunguzi kuhusu kansa ya kizazi kwa kina mama. Wamejitolea kuwafanyia uchunguzi wa vizazi "pelvic test" for free wakinamama watakaojitokeza na kuwatibu wenye matatizo bure. Guess what, wameambiwa itachukua miezi 6 kwa approval of the project. Madaktari from USA na wenye vifaa vya kisasa they just need data for research and publication purpose. Yaani niliposikia I felt so bad about the whole thing. JAMANI CAN'T WE GET BETTER WITH TIME? THIS IS 2009. HATA MASUALA YA AFYA ZETU INAKUW ANI ISSUE KUYAAPROVE?

    ReplyDelete
  19. Well .. a bit convinced ...a buck is now with the siri - kali... both ATCL management and the siri-kali share the blame....every side is now speaking ..........communication muhimu ....unacounter rumours.....hasa yanapokuja masuala ya fedha au mali za wananchi....tushazoea kusikia ndege mbovu, mahujaji etc...but the bottom line is ATC is now very sick an d without wings....ok let us wait and see whether the package will give ATCL new wings or ......graveyard?

    ReplyDelete
  20. bila ela hamna kitu - stori nyiiiingi. wa TZ tutabaki kuwatamani Kenya air/ethiopian air na wenginewe! weka capital mpasue anga!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...