BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeviagiza vyama vya sanaa kote nchini kuwasilisha ripoti ya utendaji ya mwaka 2008 na kalenda ya mipango ya mwaka 2008.
Agizo hilo limetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego alipokuwa akizungumza na viongozi wa vyama vya sanaa uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Baraza hilo .
Hatua hiyo imetokana kuwa vyama vingi vya sanaa kuwa vinajiendeleshea mambo bila mipango maalum na vingi kuwa vimekufa. “Kwa kuanzia ifikapo Februari 15, 2009, vyama vyote vilivyosajiliwa na BASATA viwe vimeleta ripoti ya Utendaji kazi ya mwaka 2008, na pia kalenda na mpango kazi wa mwaka 2009,” alisema Ghonche.
Alisema kuwa pamoja na hivyo pia Baraza linalazimika kuhakiki uhai wa vyama vyote vya sanaa vilivyosajili pamoja na hadhi yake kwa kuwa imedhihirika kuwa baadhi ya vyama haviko hai na vingine vimesajiliwa kwa hadhi ya kitaifa wakati ukweli hauko hivyo.
Katika mkutano huo, BASATA iliwataka viongozi wa vyama kutoa mapendekezo juu ya usajili wa vyama vya kitaifa vya sanaa ambapo viongozi wengi walitoa mapendekezo ya kuvunjwa vya vyama vyote vilivyo na hadhi ya kitaifa ambavyo havitekelezi majukumu yake kitaifa.
Viongozi hao walitoa mapendekezo kya kuwepo kwa vyama vikuu vya aina nne ambavyo vingine vitajumuisha vyma vyingine vidogo vya fani. Kwa mujibu wa mapendekezo hayo viongozi hao walipendekeza kuwepo vya vyama vikuu vitatu vya kitaifa katika fani za Sanaa za maonesho, Sanaa za Ufundi na Muziki na pia kuwepo na nafasi ya vyama vya fani maalum ambazo haziingiliani na sanaa zilizo katika makundi hayo matatu.
Pia katika mkutano huo viongozi wa vyama waliitaka BASATA yenyewe kuwa mfano wa kuigwa kwa kuanza kutanua shughuli zake hadi katika ngazi za Wilaya kwa kuwa utendaji wake wa sasa unaekana kuwa wa Dar es Salaam zaidi wakati baraza hilo lina hadi ya Kitaifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...