katika kuadhimisha miaka miwili ya mafanikio ya gazeti la kiswahili la serikali HabariLeo, wafanyakazi tisa wa magzeti ya Daily News na HabariLeo walipanda Mlima Kilimanjaro ambapo wawili, Deudatus Sagamiko (koti bluu) na Innocent Mfumu (koti jekundu) walifanikiwa kufika kileleni na kupeperusha bendera za magazeti hayo huko.
Picha zaidi na habari za msafara huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwanza hongereni sana tena sana wafanyakazi wa Habari leo kufika ktk kilele cha mlima wetu kilimanjaro.

    Kufika kwenu huko na kutupatia hizi picha kwa kweli tumefarujika sana.Lakini mimi nilikuwa na wazo moja kwa serikali kuhusu hizo mbao walizoandikia maelezo ya kuwa hicho ni kilele cha uhuru na mlima huu upo Tanzania pamoja na urefu wake ni mita 5895.

    Mbao hizo kwa kweli zimechoka sana ninaona ni bora kama wangeweza kuzirekebisha kwa kuweka bango la kudumu la chuma ambali litakuwa likipakwa rangi ili kupendezesha mahali hapo maana sehemu hiyo ni muhimu sana kwa taifa letu.Ukikumbuka mwenge wa uhuru alipandisha na kuwasha sehemu hiyo na hayati Nyirenda.

    Kama hili mtalipuuzia basi lakini jueni tu kuwa wenzetu wanaweza wakachukua advantage hiyo .Kwa mfano chukulia ikatokea watani zetu wakaandika tangazo zuri ktk pande yao na wakasema mlima ni wao kama ambavyo huwa wakitangaza kupitia mitandao ,hili litakuwa kosa la nani.Maana huwa ukiwauliza wanasema watanzania wana resource nzuri sana lakini hawaitumii ipasavyo.Baadhi ya mifano ni kama hii ya kupuuzia upambaji na kuupdate matangzao.Hii ni kwa sababu pengine wapo watendaji wengi wazembe hata vitu vidogo kwetu ni shida.Tusaidiweje sasa kama hili la kilimanjaro ambapo ni rasilimali inayotuingizia mapesa kibao tunashindwa kuutunza kiasi hicho.

    Ukila na kipofu usimshike mkono,wahenga walisemaa..

    ReplyDelete
  2. wadau
    ivi kupanda mt.kilimanjaro ufike kileleni yakupasa ufanye mazoezi ya aina gani???au yaweje jamen
    BREAKING NEWS
    KUNA MOVIE JANA NILIWATCH YAITWA "TOMB RAIDER 2" ya angelina jolie jaman wameactia adi Africa na wameongea kabisa mt.kilimanjaro ambacho sijaelewa IVI WALE WABONGO WALIOACT NAE PALE ALIPOENDA UKO AFRICA KTK mt.kilimanjaro NI KABILA GANI WA NCHI GANI?"YAN WANAONGEA KISWAHILI KABISAAAA NA mchad yule anaeact hollywood km anatafsiri,,,wasiwasi wangu pale si kama wakenya wamechukua na kusema mt.kilimanjaro km kawida yao kuuiba???je angelina alipitia Tz au ule ni upande wa kenya???
    kweli ilinisumbua saaaana yan adi nilikaa saa 8 usiku nione mwisho,,SIJAELEWA BADO,,wadau ifatilien hii movie tuone je Tz tumelala adi watu watuntangazie mlima toka hollywood au vipi,,mana me nimeona ni kitu kikubwa sana (very serious)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...