pichani si mwingine ila kijana mbunifu mwenye roho ya paka, bob sankofa, ambaye ndiye mwanzilishi wa tovuti inayokuja juu kwa kasi ya fotobaraza (bofya hapa uione).
ni tovuti simpo lakini imeweza kujipatia umaarufu na wanachama lukuki kwa kipindi kifupi, wengi wao wakiwa ni vijana ambao awali walikosa pahala pa kusalimiana, kubadilishana mawazo bila kusahau vibawagizo vya mambo ya taswira, huku wakijidai na teknohama.
nachukua nafasi hii kumpigia saluti bob sankofa kwa mafanikio hayo, na pia wanachama wote wa fotobaraza ambao kwa kweli wameleta mapinduzi ambayo vijana wengi wanatakiwa kuungana nao.
kama utavyoona kwenye http://fotobaraza.ning.com/ ni kweli wa kwamba INAWEZEKANA na si uwongo kwamba ITAWEZEKANA na hatimaye kuwa kama tovuti pevu za kimataifa za jamii kama vile myspace, Hi5, youtube na kadhalika.
Uwongo mbaya, nikiwa mmoja wa wanachama wa awali wa fotobaraza, najisikia fahari na furaha kuwa miongoni mwa kina bob sankofa kwani libeneke wanaloendeleza hakika litakuja kuwa kubwa kuliko ibavyodhaniwa.
na mimi nathibitisha kwamba yeyote atayejiunga, hasa vijana wa umri kati ya miaka 10 hado 30, hapa ndipo mahali pao.
haya tena shime vijana msifanye ajizi, jiungeni na fotobaraza ili muendeleze libeneke hili la teknolojia ya habari (teknohama) ambayo inaelekea kutuingia damuni kisawaswa wengi wetu.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hihi Aminia babuuuuuuuu safi sana mwili haujengwi kwa tofali,
    Nasikia ulionja tu wala hukula.

    ReplyDelete
  2. mzee naona uliviziwa ukiwa unatengeneza shavu,haha ahaa ahahah ahaha ahah,safi sana kaka.

    ReplyDelete
  3. mnaotaka kuonja kabla hamjauliza kwanza kama ni nyama ya nini nyie ni wapagani au wauchu?????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...