The family of Mr. and Mrs. William Makere, his daughter (Fatuma), uncles Arn Ndeale Juul Nielsen and Carl ndeale Tirsvad Nielsen would like to thank God for all his blessings and guides throughout this hardest time ever, since the loss of our beloved son (Ndeale William Makere).
He was a father, brother, uncle, in-law, and friend. It´s now five years since he left us in a car accident, though it´s sometimes hard to believe that it has already been so long time without seen, talk, or even laugh with him.
We loved him but God loved him more. His love, support, care, contribution and tendered heart will always be remembered and cherished for the rest of our lives. May his soul rest in eternal peace.
We would also like to express our sincere gratitude to all family members, co-workers, friends and everyone else around the world, who in one way or another participated and help us during his funeral. We highly appreciate all your support, comfort, and contribution. May GOD bless each and every one of you.
Kind regards
Makere’s family.
Makere’s family.
RIP Ndeale. Nakukumbuka sana pale nyumbani Kinondoni (karibu na kumbukumbu bar)miaka ya mwanzoni wa themanini..bado siamini kama umetutangulia.
ReplyDeleteHivi mdogo wake "Shikeni" yupo wapi siku hizi?
oh! Ndeale namkukumbuka sana, alikuwa mcheshi, sana! Nakumbuka tulikuwa naye National Service Makutupora Camp Dodoma, B-Coy Operation Kambalage, aisee, masikini wee! na hasa ile miwani yake aliyokuwa anaivaa na kamba looo! masikini Stella upo! Ndeale hatunaye duniani. Mungu amlaze mahali pema peponi. Poleni sana wafiwa. Kazi ya mungu haina makosa.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa. Ndugu mtoa maoni wa kwanza mbona unamuuliza marehemu, sijui nani yupo wapi? sio vizuri namna hii. Tumuombea rafiki na ndugu yetu.
ReplyDeleteHe had a strong and loving spirit!One of the best friends in our childhood. It's sad that you departed at a young age, but GOD love you most. We lived in the same neighborhood. R.I.P, Hope to meet again in eternity!
ReplyDeletenakukumbuka sana ndugu yangu Ndeale, tulishi wote kinondoni shamba tukapoteana lakini tukaja kukutana mbeya siku moja, nilipohamishiwa tena Dar kikazi siku moja nikapigiwa simu na brother Moses toka kinondoni kuwa umefariki kwa ajali!!! Loh nilishangaa na kushtuka sana, lakini sote njia yetu ni moja tu wewe umetangulia nasi tutakufuata.
ReplyDeleteMdau alielizia habari za mdogo ake yule aliekuwa anaitwa Shikeni kwa mara ya mwisho nilisikia yupo Denmark na dada zake Anna na Ndeshi
du ndio njia yetu.... jamaa tuli school nae pale hana-nasif kinondoni moscow..palikuwa na mdogo ake pia anaitwa shikeni walikuwa na mdogo wao wa kike pia sikumbuuki jina lake...du big loss! tulisakata ball pale uwanja wa berlin siku hizi kuna makaburi (mwembe jini)mungu amrehemu..amin
ReplyDeleteI didnt know Ndeale was gone..RIP man! we were together at IFM ...He was a good man!
ReplyDeleteRIP. ndugu wa marehemu tunawatakia kila heri na nguvu ya kukabiliana na pengo alilowaachia ndugu yenu. Lakini pia ninawaomba msiwe mnatubagua sisi ambao kiingereza hakipandi ili tuweze kushiriki kikamilifu katika lego zima la kumbukumbu kama hii!!!! tuwekee kumbukumbu ya kiswahili, Mwenyezi Mungu huwa anasikia lugha zote!!!!!
ReplyDeleteMaskini ndugu yangu ndeale jamani, my cousin brother, sikuyaamini macho yangu nilipoiona hii picha na memory imenipauchungu mkubwa sana. mama yako analia anakukumbuka kila siku ndeale mbona ulituacha angali tunakupenda hivyo. Nakumbuka ulivyokuwa unanitoa auti kwenda kucheza njenje yaani ni vigumu sana kuamini kwamba itabakia kuwa kumbukumbu na kwenye maisha haya haupo tena. Ee Mungu tunakushukuru kwa sababu kazi yako haina makosa, na roho ya kaka yetu italala mahali pema peponi daima. Shikeni siku hizi anakaa Denmark.
ReplyDeletePoleni sana kwa pengo aliloacha kaka yenu. Mungu atazidi kuwafariji, wote tuko njia moja. Ndeshi na Anna tumepoteana muda sasa, tulikuwa wote Zanaki ningefurahi kama ningepata contact ya ndeshi. Kundi
ReplyDeleteRIP jamani Ndeale.. Nakumbuka Makutupora JKT jamani bustani.. I miss you Ndeala kwa ucheshi wako. Wanafamilia poleni sana endeleeni kumuamini mungu na atawapa amani na uvumilivu. May the Lord be with him always.
ReplyDeleteR.I.P Ndeale, mshikaji tuliishi wote kinondoni kila jioni tuko kijiweni na kina Kenedy,jacki,sister zako Ana na Ndeshi na mdogo wako Mzee shikeni wa milupo lol! Ebwana tulizipoke kwa maskitiko sana habari za msiba wako na nakumbuka wakati huo ulikuwa unatafuta chuo USA.Lakini mambo ya mungu tutakutana huko uliko mkuu .
ReplyDeleteNdiale!
ReplyDeleteRIP !, I remember him back in the days, ofcourse we used to play soccer at leaders club. At the beginning in the years 1982 - 1986
we used to have St. Peters young soccer players! with one of the young Fathers who used to sponsor the team with soccer balls, jerseys and such. We have watched Simba sports club practicing at leaders club before the matches season starts. We used to meet at many different party's and of course praying at St. Peter's Church. Oohhh! so many memories!
May the almighty rest you in peace
This confirmed to me that Cherish all the Good times with your friends, enjoy any moment you meet a friend you've known since childhood, because life is short and no one knows when the will be departing the earth!
Peace!
Ndugu wafiwa poleni sana kwa kumpoteza ndugu yenu mpendwa. Yote hii ni mapenzi ya mwenyezi Mungu, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Amen.
ReplyDeleteKwako mtoa maoni namba 3, unaposema anamuuliza marehemu nami ngoja nikuulize kwani marehemu ndo amejiweka kwenye blog hii au ni ndugu zake. kwa kumtetea anayeuliza swali anawauliza ndugu zake waliotuma picha hii kwa kumbukumbu.
Dada J.
Jamani samahanini sana nilighafirika kidogo nikasahau kuandika tarehe aliyofariki marehemu Ndeale. Alifariki tarehe 04/01/03 na kwasababu niliiandika ndani ya 2008 hivyo akili ikanituma ni miaka mitano(5) tangu atutoke kumbe ukweli ni miaka 6. Naona akili haitaki kukubaliana na ukweli tuu. Kwa niaba ya familia napenda kuwapa pole sana wale wote waliuguswa na msiba huu kwa njia moja au nyingine. Mungu awabariki sana.
ReplyDeletekwa wale watakaotaka kuwasiliana na sisi ndugu wa marehemu tafadhali tutumie barua pepe kwenye ndeale@hotmail.com ili muweze kupata mawasiliano yetu.
wasalamu
Aika
RIP Ndiale may lord be with his family in this difficult time.
ReplyDeletea message yako upo wapi na marafiki wengine wa zanaki naomTunashukuru kwa wote ndugu na marafiki mlioguswa na ambao mlikuwa hamna taharifa za kumpoteza mpendwa kaka yetu,kesho ndio siku yenyewe tangu tulivyokupoteza tarehe 04/01/03, bahati mbaya siku hiyo ndio tarehe ya kuzaliwa mtoto wako fatuma,naomba mungu ampe nguvu za ujasiri katika siku ya majonzi kama hii.Nimesoma mesegi na kuzirudia zinanikumbusha sana nyumbani Tanzania na marafiki wote wa zamani,Kundi mpenzi asante kwba tuwasiliane pamoja na wengine wote tuliopotezana kwa email ndeale@hotmail.com. Na vile vile napenda kumshukuru kaka Michuzi na kumpa pongezi kwa kutuunganisha na kutupa habari mbalimbali nyumbani na nje ya nchi.
ReplyDeleteAsanteni tunaomba mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen, Ndeshi.
Napenda kutoa asante kwa wote waliokuwa pamoja na sisi katika kipindi hiki kigumu kwa namna moja ama nyingine.
ReplyDeleteMpendwa Kaka ndeale, maisha yako hapa duniani yalikuwa mafupi lakini umeacha nyayo nyingi njema ambazo tungependa kuzifuata. Ulikuwa kama Mtoto, kaka, Baba pia best friend katika maisha yetu.Pengo ulilotuachia hatuwezi kuliziba kamwe
(WE MISS YOU BROTHER)
mungu ailaze roho yako mahali pema peponi pamoja na ndugu na marafiki wote walio tutangulia
BWANA ALITOA BWANA ALITWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE AMEN
ANNA
Kwanza napenda kutoa shukrani kwa kaka Michuzi kwa mtandao wake huu ulio bora kwa kuweza kutuunganisha ndugu,jamaa na marafiki.
ReplyDeleteBwana ametoa na bwana ametwaa,akupenda tuendelee kula raha na kuinjoye na kaka yetu mpaka mda huu bali tumuombee amweke mahali pema peponi...
Nitaendelea kuwashukuru ndugu,jamaa na marafiki mliokuwa pamoja nasi ktk msiba huu,naamini ya kuwa bado mko pamoja nasi kwani mchango wenu ulikuwa ni mkubwa kiasi hausemeki.
Nilikuwa sijalala siku 3 baada ya kupata taarifa ya msiba wa kaka na rafiki yangu mpendwa ndeale lkn suprise mliyonipa nilivyotua pale TZ dar airport sikuamini macho yangu kama kaka yangu alikuwa na upendo na watu hivyo,majonzi yote yaliisha ikabaki mimi ndio niwafariji watu.
Kuna mengi ya kusema lkn siwezi kumaliza yote ila natoa shukrani kwa wote waliokuwa pamoja nasi ktk msiba huu kimawazo,kipesa,nguvu na gharama zozote Mungu awabariki sana.
Mnaweza kunipata kwa email hii:shikeni@yahoo.com
Tunaomba mungu ailaze roho ya marehemu kaka na rafiki yangu mpendwa Ndeale mahali pema peponi Amen.
Shikeni.
polen wafiwa
ReplyDeletesamahani wadau,,,mbona majina ya hao uncles sielewi-elewi so much kidhungu au vipi??
Jamani neighbor Ndeale! 2mekuwa wote mtaani, Its real SAD! Poleni sana wanafamilia, 2ko pamoja kisala. Tumekuwa wapweke kimtaa. Poleni mama Makere, Mzee Makere, Ndeshi, Shnike, Anne & Haika. "The Lord gave and the Lord has taken away, blessed be the name of the lord." May God almight be with u.
ReplyDeleteR.I.P. Ndeale. From (Leah, Lily & Glory)
Habari za msiba huu nilizipokea na butwaa. Ana , shikeni, ndiale poleni sana na msiba wa ndiale. Nilikuwa mdogo sana kaka ndiale alikuwa ananibeba saa nyingine alikuwa kaka wa mtaa maskini hata ulivyohama hapa kinondoni ulikwa unakuja kama unakaa hapa . Tunakukumbuka saana kaka ndiale Alex gondwe
ReplyDeletewewe hapo juu unaesema ndeale alikuwa anakaa kijiweni ni muwongo huyu kaka alikuwa ni mfano wa kigwa kwa wanavijiwe . shikeni na wenzake kennedy na kaela wa ada estate walikuwa wa vijiweni umenishangaza sana wewe hapo juu kaaaaaaaaaa. kila mzazi pale mtaaani alikuwa anamjua ndeale . mlibakia mtaani mwenyewe kwa juhudi zake alikwenda ifm nasijui kama alikuwa na muda wakuja kubeba mabox kwa sababu alifanikiwa masi mapema sana . You need to apologise to the family
ReplyDeleteNDIALE MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI HULIKUWA RAFIKI WA KWELI MIMI NA MKE WANGU TUNAKUOMBEA KWA MUNGU AKUPE PEPO NZURI SABABU NI ULIKUWA MWEMA SANA NA MKWELI, KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA.
ReplyDeleteC.M
Mimi naona huyu tumsamehe ameshidwa kutofautisha kijiwe ama jirani, ama anataka kuonyesha anamjua kupita vilivyo,mimi kama rafiki najua alikuwa akiongea na kila mtu, awe mdogo,mkubwa, kijana ama mzee,kwenye shida na raha labda ndio maana kasema tulikuwa wote kijiweni pamoja na watu wengine aliowataja, mda wa kijiwe kama kijiwe halikuwa hana.He had alot of goals at the same time be normal as everyone else.
ReplyDeleteNdeshi jifunze bwana kuumba sentensi vizuri unachoandika hata akieleweki bwana, vipi ndugu miaka yote uliyokaa denmark ukwenda shule au ulikimbilia tu kuolewa na wazungu uchwala, umezidiwa hata na aika mdogo wenu wa mwisho, anewai jitahidi dada Mungu awatie nguvu wote kwa kumpoteza kaka yenu mpendwa kwani he was a real gentleman and very hendsamu. hi ndeshi bado uko mzuri kama ulivyokuwa zamani?
ReplyDeleteUmenichekesha mpaka mbavu zinaniuma, nani wewe lakini? sorry kwa wote ambao hawakunielewa nilichoandika, niliandika comment kama mara tatu kila nikitaka kutuma zina frizi naandika tena upya, kwa kifupi niliingiliwa na virus hivyo sentensi kujichanganya juu chini chini juu, huyo mtu alionitumia nilimuona baadaye,lakini siwezi kumtaja, sentensi ilikuwa inaanze kama hivi,
ReplyDeleteTunashukuru kwa wote ndugu na marafiki mlioguswa na ambao mlikuwa hamna taharifa za kumpoteza mpendwa kaka yetu,kesho ndio siku yenyewe tangu tulivyokupoteza tarehe 04/01/03, bahati mbaya siku hiyo ndio tarehe ya kuzaliwa mtoto wako fatuma,naomba mungu ampe nguvu za ujasiri katika siku ya majonzi kama hii. Nimesoma mesegi na kuzirudia zinanikumbusha sana nyumbani Tanzania na marafiki wote wa zamani,Kundi mpenzi asante kwa message yako upo wapi pamoja na marafiki wengine wa zanaki naomba tuwasiliane kwenye email ndeale@hotmail.com. Na vile vile napenda kumshukuru kaka Michuzi na kumpa pongezi kwa kutuunganisha na kutupa habari mbalimbali nyumbani na nje ya nchi.
Asanteni tunaomba mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen, Ndeshi.
Hayo maswali mengine tafadhali ujijibu wewe mwenyewe. Cause is none of your business.