Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuacha kuchukua maamuzi makubwa kuhusu uendeshaji wa Reli ya Kati bila kuishirikisha Serikali, kwa sababu Reli hiyo siyo mali ya kampuni hiyo bali mali ya Serikali ya Tanzania na ya Watanzania.
Rais amesema kuwa maamuzi yote makubwa kuhusu Reli hiyo lazima yafanywe kwa kuishirikisha Serikali ya Tanzania ambayo inamiliki asilimia 49 ya hisa katika TRL. Kampuni ya RITES ya India inamiliki asilimia 51 ya hisa katika kampuni hiyo.
Rais Kikwete ametoa msimamo huo leo, Ijumaa, Januari 16, 2009, wakati wa kikao kati yake na uongozi wa Wizara ya Miundombinu pamoja na uongozi wa TRL katika mfululizo wa mikutano yake na Wizara mbalimbali za Serikali yake kufuatilia utendaji wa Wizara hizo.
“Sisi kama Serikali ya Tanzania ni mbia-mwenza na siyo mshirika mdogo katika makubaliano ya kuendesha Reli hii. Nyie hamna haki na hamwezi kutoa maamuzi yenu peke bila kuishirikisha Serikali. Reli mali yetu. Njia ya kudumu ya reli ni ya kwetu. Sisi ndiyo wamiliki wa Reli hiyo kwa asilimia 100. Nyie tumewaajiri tu kama waendeshaji tu,” amesisitiza Rais Kikwete katika mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
“Sisi tuko katika ubia, na kila yanapotakiwa kuchukuliwa maamuzi makubwa kuhusu Reli ni lazima tuwasiliane na kukubaliana kwa pamoja. Msichukue maamuzi peke yenu. Hii siyo Reli yenu. Reli ni yetu,” amesema Rais katika kikao hicho.
Rais amelazimika kutoka msisitizo huo baada ya kuwa amepata maelezo kutoka kwa uongozi wa TRL kuhusu mipango ya uendeshaji wa Reli hiyo katika mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mali za Reli (RAHCO).
Miongoni mwa mipango hiyo ni kujaribu kupata mkopo mkubwa wa kuendesha shughuli za Reli hiyo bila ridhaa ya Serikali, mipango ya kuacha kutoa huduma kwenye baadhi ya vipande vya Reli kwa madai kuwa havina faida, hali ya usalama ya Reli yenyewe, maombi ya TRL kuzidi kupungizwa kodi, na hata kutaka mipango ya kung’oa kipande cha reli kati ya Tanzania na Kenya kwa madai kuwa hakina faida.
TRL inasema kuwa haipati faida kwenye njia za reli za Tanga-Moshi-Arusha, Kahe-Taveta, Kidatu-Kilosa na Dodoma-Singida.
Rais Kikwete amesema: “Kama ni mkopo lazima upatikane baada ya kuwa tumekubaliana sote wawili na wala siyo nyie kuchukua maamuzi pekee yenu kwa sababu mikopo yenyewe inalipwa na Serikali ya Tanzania. Na kama unataka msimamo wetu kuhusu maombi ya mkopo bila kutushirikisha, sisi basi ni kwamba hatuukubali mkopo huo.”
Kuhusu mipango ya uongozi wa TRL kuacha kutoa huduma kwenye baadhi ya vipande vya reli hiyo kwa sababu hakuna faida, Rais amesema:
“Tumekodisha Reli nzima, siyo kwa vipande. Mlifanya uhakiki na kujua hali ya Reli nzima. Mlijua tokea mwanzo kwamba baadhi ya sehemu za Reli hiyo zilikuwa haziingizi faida. Hamwezi sasa kubadilika leo na kuweka msimamo tofauti.”
Kuhusu usalama wa Reli, Rais Kikwete amesisitiza: “Kuna uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo ya Reli. Hali ya usalama wa Reli inaonekana kuwa hatarini kwa sababu nyie mnaonekana kama hamjali.”
Kuhusu ombi la kuzidi kupunguziwa kodi, Rais Kikwete ameuambia uongozi wa TRL: “ Hivi mnataka tuwaondolee kodi zote, ili sisi Watanzania tupata nini? Hivi mnataka tupate nini katika ubia huu? Sisi ndiyo tunakopa, ndio tunalipa madeni, na sasa mnataka hata tuwaondolee kodi.”
Ameongeza: “Mnataka tuwaondolee kodi zote ili tupate nini? Hivi mnaweza vipi kuhalalisha mpango wa namna hii kwa walipa kodi wetu? Tukifanya hivyo tuwaambie wananchi wetu nini? Kwamba nyie mpo hapa nchini kufanya nini hasa?”
Kuhusu hisia za kutaka kung’oa Reli kwa sababu ya kutokuwa na faida, Rais amesema: “Hili litachukuliwa kama hujuma. Kama hiyo ndiyo aina yenu ya fikra basi mtaiweka nchi yetu mahali pabaya, mtashindwa kuusaidia uchumi wetu kukua. Kung’oa sehemu yoyote ya Reli ni kutuambia kuwa hamuijali nchi hii na kwa kweli hatuwezi kuwa na washirika wa namna hiyo. Haya ni mawazo ya kushangaza kabisa. Msiondoe hata kipande kimoja cha Reli.”
Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Tanzania kuendelea kuwa na njia za reli zinazoungana na nchi nyingine za jirani. “Tunahitaji mahusiano na nchi nyingine. Hatuwezi kufanya jambo la ovyo kiasi hicho.”
Kuhusu maelezo ya uongozi wa TRL kuwa imepeleka injini mbili ili zifanyiwe ukarabati nchini India kwa sababu za kiufundi, Rais amesema kuwa Serikali inataka kuona ukarabati wa mabehewa unafanyika katika karakana ya Reli iliyoko Morogoro na siyo kwingineko.

Hakika hapo lazima niseme kuwa TRL wanakera ingekuwa ni amri yangu ningesitisha mkataba ingawa najuwa yawezekana ni kitu kigumu ila nahakika kinawezekana yani babu zetu waumiee kujenga reli hizo halafu yeye aseme anataka kung'oa hata haya haoni yeye asimamiee na aboreshe mambo tuonee maana mpaka sasa shida ndio kma zimeongezeka ukitumia usafiri huo badala tufurahie wao kuja twatamani waondoke
ReplyDeleteWATANZANIA WENYEWE NDO WANAIUA NCHI YAO.sio MAFISADI PEKEE.Kila MTANZANIA ANAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE.akila michuzi,ohh!awe impeached.KWANIN WATANZANIA TUSIBADILIKE,TUWE WAZALENDO NA UCHUNGU NA NCHI YETU.tuache tabia ya kuonyoshean vidole maana ni upotevu wa muda tu.Nyinyi mnaonyosha vidole ni kwavile hawakupata nafasi kma zao hao mafisadi.Ona kuhusu mazunguzo na TRl.yanatisha!
ReplyDeleteThanks to JK, leo mheshimiwa Rais ameongea vitu ambavyo naweza kusema nilikuwa natarajia tangia ameingia ofisini ile siku ya kwanza japokuwa ni kama amechelewa kwani 2010 naona imekaribia lakini ni mwanzo mzuri. Ni vyema akaendelea na utaratibu huu wa kukutana na viongozi wa mashirika na makampuni mbali mbali yaliyo chini ya serikali kama alivyofanya hivi. Kusikiliza mipango yao moja moja na kutolea maoni yake kama alivyofanya hii leo. Ni vyema akapunguza safari za nje na kuendelea na huu mpango wa kukutana na waendeshaji mbali mbali na kuwasikiliza wana mipango gani na hii nchi kwani maamuzi mengi yanaonekana huwa yanachukuliwa na kikundi kidogo tu cha watu ambao wanaamua vitu vikubwa vinavyokuja kuwaathiri wananchi.
ReplyDeleteEndelea na utaratibu huo huo..
Mdau
Kwa kweli hapa lazima nipongeze JK. Nimefurahi kuona kwamba ameosha kujali waTZ wote bila kujali hao wabia. Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Rais Wetu JAKAYA KIKWETE.
ReplyDeleteHongera JK ingawa umechelewa kuyasema haya ila kwa kuwa umeyasema, NIMEFURAHISHWA kama mpiga kura wako. Ninachokuomba ni kufuatilia msimamo wako ili hao jamaa wa RITES wasizidi kufanya hujuma kwa visingizio mbalimbali.
ReplyDeleteNadhani watu wengi watakubaliana nami ya kwamba usafiri wa Treni ni sehemu kubwa sana katika nchi zilizoendelea, mfano zipo mpaka treni za mijini ili kuondoa msongamano. kwa nchi kama TANZANIA ambayo ni kubwa, uimara wa usafiri wa RELI ndiyo suluhisho la matatizo ya usafiri nchini kwani tunaweza kuunganisha mikoa na wilaya kiurahisi kwa njia hii kuliko barabara. Lakini ikumbukwe pia treni inabeba mzigo mkubwa kuliko gari. HAWA RITES ni kama walivyokuwa NET GROUP SOLUTION, wanafaidika wao, nchi yao (INDIA) pamoja na makampuni yao yaliyopo india. Haiwezekani kila kitu kitoke india, kipelekwe india kwa matengenezo n.k.
USHAURI KWA WADAU: Watanzania sasa tuanze kuyaongoza wenyewe mashirika yetu kwani nia aibu nchi kuwa na wasomi wa kila aina ambao tunawapongeza kila siku lakini tunaongozwa na watu kutoka nje na sisi tumeachiwa siasa tu. Kibaya zaidi hawa jamaa wamekuja kwa ajili ya uongozi tu lakini hawatoi hata shilingi, serikali ndiyo inakopa na wao kazi yao kuzipangia matumizi. WE CAN, LET IT BE, Tuache ushabiki wa kwamba watu wa nje ndiyo wanaweza kuongoza mashirika. (NB: VIONGOZI wa ATCL kuweni mfano bora wa uongozi ili uaminifu kwa wazalendo uongezeke, acheni visingizio kwa kukosa mtaji wakati hamna mikakati madhubuti ya kuongeza mtaji, ni aibu kwani hata kile kidogo mlichokuwa nacho mmeshindwa kukiendeleza)
JK KWA KAULI TUU UJUE UNA KULA YANGU KATIKA UCHAGUZI UJAO
ReplyDeleteRais nakupa five , naona sijui kama unamawaziri Mawazo ulio toa yalitakiwa kutolewa mapema na waziri wako,ao ndio mafisadi wenyewe wamewapa michoro hao waindi.MUNGU TUSAIDIE WATANZANIA
ReplyDeleteBaada ya maneneo hayo makali, Rais awape "siku saba"! Na kama hawatajirekebisha, wafukuzwe: hawa wa reli yetu wenye 51% na wanaokula nao!
ReplyDeletemkuu, kwa mada ya hpo chini nakupa heko,sichanii hii ya jk, ni nzuri .naomba kukupa heko kwa ushauri kwa uliyoyaacha yaonekana kulingana na walivyoandika ,ilimradi ni mawazo yasiyo na matusi,kama ni ya kijinga ,mwandishi akijisoma atajipuuza.hata mkuu mwenzako mjengwa hufanya hivyo.HONGERA SANA,NA POLE KWA MJADALA,UKUBWA JALALA.
ReplyDeleteAchani ujinga jamani wa kusifia kila kitu msiwe wajinga. Nyie hamuoni kuwa hapa JK ameanza kampeni za 2010? Inakuwaje mambo haya ameyakalia kimya muda wote huo? Tutakuwa tunachangua viongozi wanaofanya kazi mwaka unafuatia uchaguzi mpaka lini? Mbona tunakuwa wepesi wakusahau kiasi hiki?
ReplyDeleteKwa hili la TRL, JK nimekukubali. Better late than never. Hawa wahindi wanatuburuza kweli! Una habari hata kulipa mishahara ya wafanyakazi ni issue! tangu Aug 08 wanakopa serikalini, hii ni hadi lini? Ushauri wa bure, hawa Rites waondoke hawana sifa! Kaza buti JK wapige teke hawa.
ReplyDeleteHata kama JK angesema siku ya uchaguzi 2010 bado msimamo wake juu ya rasilimali za nchi yetu lazima tuupongeze! Kila jambo na wakati wake, na sasa hilo la reli ndio JK kapata muda wa kulisema, kesho atasema lingine, mpaka mtondogoo. Uchaguzi utafanyika tu hata kama asingezungumzia reli. Kuna mangapi Tanzania yapo tu hayaeleweki? Big up kwa JK kwa kuwaambia bayana hao wawekezaji, wanataka kung'oa, walijenga wao???
ReplyDeleteMdau, UK
kutoka kwa Shigongo.
ReplyDeletemara chache sana nimetoa maoni yangu kupitia mitandao,leo nimejisikia kusema jambo hili ambalo mi ndio sheria yangu ya maisha;KILA SIKU UKIAMKA SALAMA MSHUKURU MUNGU KISHA PAMOJA NA MAMBO MENGINE ULIYONAYO TAFUTA JAMBO JIPYA UJIFUNZE AU KUFANYA,HATA KAMA WATU WOTE WATAKUCHEKA NA KUKUAMMBIA KUWA HUWEZI,USIKILIZE MOYO WAKO.
Watu woyt waliofanikiwa duniani walifanya hivyo baada ya kufanya mambo mapya,walichekwa,wakabezwa lakini waliendelea na leo hii wapo mahali walipo.
Kwa pamoja tukiyafamya mambo haya,tukatimiza wajibu wetu basi miaka michache ijayo nchi yetu itakuwa katika hatua nyingine. wajukuu zetu watafurahi kwa sababu sisi tuliishi.
Ahsanteni,sisi ni ndugu.
kama kweli haya yamekemewa na JK tena kwa ukali bila kucheka cheka, basi tunaelekea kuzuri asanteni nyote ambao kwa njia moja au nyingine mmechangia kumrudishia sauti Rais wetu kwa kumkosoa anapochemka, maana alikuwa anaboa.kusifiwa sifiwa kulitaka kumlevya.... Welcome again mheshimiwa Rais!thats a spirit of true Tanzanian
ReplyDeleteHapa naona Mheshimiwa anatafuta asifiwe na magazeti na wale wasiojua kama wengi wanavyofanya hapa bila hata kuonyesha tunamsifia kwa kipi alichokifanya.
ReplyDelete1. Kwanza si kazi yake au amfukuze waziri mhusika. Na waziri si kazi yake bali wakurugenzi aliowateua kwenye Bodi kwa hiyo awafukuze kama wamehindwa.
2. Kisheria ya makampuni unapokuwa unamiliki 51%(Majority votes) ya kampuni (Voting rights) wewe ni mmiliki mkuu hivyo hao 49% ni mmiliki mdogo(minority rights)
Hivyo hata wakiishirikisha Serikali wakati wa maamuzi kura watashinda hivyo JMK alitakiwa alijue hilo kabla hajaingia huo mkataba. Hakuna aliyetulazimisha kuingia huo mkataba.
3. Kusema walijua kuhusu hali ya Reli waliposaini mkataba nalo halina maana maana kibiashara inabidi uangalie sasa na baadae sio yaliyotokea jana na juzi. Hivyo kama mambo yamebadilika inabidi ufanye mabadiliko kwenye mipango yako. Business Plan sio kitabu kitakatifu au katiba. Kuwalaumu ni kutokuelewa kwani hakuna anaefanya biashara huku akipanga kupata hasara.
4. Kama sisi tumewaajiri tu kuendesha kwa nini tuwape 51% ya kampuni?? si wangelipwa tu gharama za uendeshaji?? Hapo JMK labda atueleweshe.
5. Jambo la msingi linaloonekana hapa ni wanasiasa kutokuelewa misingi ya biashara.
Kimantiki hapa kuna mgongano wa malengo. Muwekezaji lengo lake ni Faida(Maximisation of shareholders' wealth) wakati Serikali lengo lake ni huduma
(Huduma bora na "Value for money"). Sasa hapo serikali inabidi ikae chini iweze kuyatenganishe hayo mawili la sivyo tutaendelea tu kulumbana wakati wenyenchi tunapata hasara pamoja na kukosa huduma.
Sasa tusishangilie tu bali tujiulize tunashangilia nini
Ningeshauri uanzishwe mjadala kuhusu watendaji wa JMK yaani mawaziri maana mengi anayojaribu kuyafanya JMK ni ya mawaziri ni aibu kwa Taifa kuona Rais hana Waziri. Sijaona hata mmoja anaefaa hata hao vijana wa juzi nao ndio wanatia huruma kabisa.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu iokoe Tanzania
Mzawa
For the First time I feel like wavuja jasho wa Tanzania wana mtu anayewapigania haki zao. Congrat's your Excellency President JK.
ReplyDelete