
WIMBI LA MAUJI YA ALBINO TANZANIA,
JE WADAU MLIO UGHAIBUNI MNASEMAJE?
Kumekuwa na wimbi kubwa la mauaji ya maalbino katika nchi yetu kwa muda mrefu hadi nchi tajiri duniani kama uingereza kuanza kuizungumzia hii swala kwenye bunge lao, kwani kama mtakumbuka mwaka jana mbunge mmoja aliuliza swala hili.
Kwa watanzaia tulio ughaibuni tutaisaidiaje serikali yetu kutokomeza hili wimbi la kipumbavu la kuwaua wenzetu kwa sababu tu za kiutajiri,madaraka nk?
Toa maoni ya kiutaalamu ukizingatia kwa walio UK wana kitu wanaita CHILD PROTECTION AND PROTECTION OF VULNERABLE ADULTS FROM ABUSE(POVA) na pia nitayafikisha kwa wahusika maoni yenu.
Kama mtakumbuka wiki hii wamezindua kampeni kabambe ya kutokomeza jili wimbi.Leteni maoni zaid tazameni hiyo katuni inasikitisha sana. Je, huyu rafiki yetu ataendelea kukaa kibandani mpaka lini?Baadhi ya wafanyabiashara wametoa simu je itasidia ?
TOA MAONI
Blog:www.musoma-tanzania.blogspot.com
Blog:www.musoma-tanzania.blogspot.com
Email:-bchisumo74@ yahoo.com
Kaka Misupu, katuni huwa zinachekesha lakini hii hapa imenitoa chozi maudhui yake yamezidi imani yangu. Jamani huu uuaji umezidi tuache ukatili huu!
ReplyDeleteKUNA MITI IKIKATWA SHINA, ILE MIZIZI INAYOSALIA INAANZA KUTENGENEZA MMEA BAADA YA MUDA. TATIZO LINALOENDELEA LA KUDHULUMU AU KUHUJUMU MAISHA YA HAWA NDUGU ZETU, KAKA ZETU, DADA ZETU, WADOGO ZETU, AMA WATOTO WETU WALIO KATIKA KUNDI HILI LA ALBINO, NI WAGANGA WA KIENYEJI.
ReplyDeleteWAKATI JUHUDI KUBWA ZINAFANYIKA ZA KUWAKAMATA WATU WANAOJIHUSISHA NA DHAMBI HII, AU WALIOWAHI KUHUSIKA. UFANYIKE MSAKO MKALI KABISA WA KUFA NA KUPONA KUTAWATAFUTA NA KUWACHUKULIA HATUA KALI KABISA WAGANGA WA KIENYEJI WANAOTUMA WATEJA WAO WAFANYE VITENDO HIVI.
ENDAPO NGUVU ZITAELEKEZWA KWA WATENDA MAOVU PEKE YAO NA KUWASAHAU WALIOWATUMA (WAGANGA), UPO UWEZEKANO WA TATIZO HILI KUENDELEA. TUKATE MITI NA KUHAKIKISHA KUWA TUNACHIMBUA MIZIZI YOTE BILA KUACHA HATA CHEMBE.
INASIKITISHA SANA KUONA KUWA SASA HABARI HII IMESHAINGIA HATA KWENYE VYOMBO VYA KIMATAIFA. JUZI-JUZI NIMESOMA HABARI HII KWENYE MSNBC.
NI DHAMBI KUBWA SANA KWA WATU WANAOJIHUSISHA NA UKATILI HUU.
ZIPO NJIA NYINGI NA ZA HALALI KABISA ZA KUTAFUTA MITAJI KULIKO KUHUJUMU MAISHA YA BINADAMU WENZETU.
MDAU,
LONDON.
Tanzania was never in a sad and shameful situation than it is right now.After CNN reported this dreadful ritual,the whole world began to imagine how primitive we Tanzanians still are!.I strongly put the blame on President Kikwete& the government for failing to curb the killing escalation.I read The President was condeming the killers but to my amazement there was no hard and concrete plans laid to stop the killing!I had the feeling everyone spoke softly about this tragic and very sad indeed situation.I love Kikwete,he has done so much for this country but this here is an emergence situation.Put Police,military and all sectors involved to find the responsible people for these murders...the government can do this!.I must honestly say I too almost cried at the sight of that drawn cartoon.Put yourself in Albino's shoes and look at that cartoon,if you wont get emotional then theres something wrong with your "human nature".God bless Tanzania? only you can answer that!
ReplyDeleteHABARI KAKA MICHUZI,ILI SUALA LA ZERUZERU(KUNRADHI KAMA SIJATUMIA JINA SAHIHI) NAONA BADO TUNALIFANYIA UTANI.MIMI NAPENDEKEZA UMWOMBE MTU WAKO WA IT AFANYE 'UJANJA' POSTING ZA KUHUSU MAZERUZERU ZISIWE ZINATOKA HARAKA KWENYE PAGE,YAANI UKIONGEZA POSTING ZINGINE POSTING YA ZERUZERU IBAKI,ISIONDOKE NA KUPOTEA ILI TUPATE MAWAZO MENGI SANA.JUZI ULIWEKA YULE DADA YETU ZERUZERU WA NGARA ALIYEKATWA MIKONO LAKINI BAADA YA SIKU TANO ILE TOPIC IKAPOTEA IKIWA NA MAONI YA WATU 47 TU KUTOKA KWENYE WATU KARIBU MIL.5 WANAOSOMA BLOG YAKO.HIYO,KWANGU MIMI,NI "BIAS SAMPLING".KUNA WANABLOG WENGINE WANAKUWA MBALI NA INTERNET WAKATI MWINGINE WAKIRUDI HAWAIONI HIYO POSTING.LEAVE IT FOR TWO WEEKS UPATE COMMENTS ZA KUTOSHA.WADAU MNASEMAJE
ReplyDeleteKwakweli jamii imrudie mungu jamani! Mimi naona hili suala la ndugu zetu Wenye ulemavu wa ngozi ALBINO, Serikali bado haijatilia mkazo! Ebu fikiria watu wanakamatwa, lakini hukawii kusikia ushahidi haujakamilika, ushahidi upi tena? Yule dada aliyekatwa mikono alimtaja jirani yake ndiye aliyemkata, na walimkuta amelowa damu! wanataka ushahidi upi jamani!
ReplyDeleteANGALIZO: Serikali wawakamate, kisha wanyongwe hadharani ili hata wale ambao wamesalia wawaone wenzao wakimalizwa. Pia zipigwe kura za siri kwa waganga wote, na hao wateja wao, mtaa hadi mtaa, kitongoji hadi kitongoji watakamatwa tu.
Poleni ndugu zetu, MUNGU AWALAANI HAO WOTE WANAOJIHUSISHA NA UHARAMIA HUU.
Katika kulipa nafasi suala zima la mauaji ya MA-ALBINO, gazeti la Udaku la Uingereza liliandika makala ndefu yenye mahusiano na Michezo kwa maana ya kulielezea suala hili. fuata hii Link hapa chini http://www.tanzaniasports.com/index.php?s=Albino
ReplyDelete