WIZARAya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia inatarajia kupeleka bungeni Muswada wa Sheria ya Mawasiliano ambapo mtu atanunua kadi ya simu na kupata namba ya simu kwa kitambulisho, badala ya utaratibu holela unaotumika sasa.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alisema hayo jana wakati akielezea mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Alisema muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano ujao wa Bunge la Jamhuri utakaoanza mwishoni mwa mwezi huu. Sambamba na hilo, wizara hiyo inatarajia kuanzisha rejesta ili kubaini matumizi mabaya ya simu za mkononi yakiwamo ya watu kutukanana au kutishana.
Akizungumzia wingi wa minara ya simu, alisema, “tumezishauri kampuni za simu zishirikiane kutumia minara kwa kila mtu kuweka antena yake katika mnara mmoja, hasa iliyo maeneo ya makazi ya watu; Vodacom na Zantel wameshaanza kushirikiana”.
Alisema jumla ya watumiaji wa simu nchini hivi sasa ni 11,719,000 na kati yao 163,300 ni wa simu za mezani na 11,555,700 za mkononi.
Hata hivyo alisema takwimu hizo zinatokana na kadi za simu zilizouzwa mpaka sasa. Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wamefanikiwa kuondoa simu za kukoroga na kuanzisha huduma za simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya ‘Code Division Multiple Access’.
Alitaja mafanikio mengine kuwa ni kukamilisha ujenzi wa mitambo mipya ya kupitisha taarifa za intaneti katika manispaa za Arusha, Dar es Salaam na Mwanza.
Ujenzi wa vituo vingine vya Dodoma na Zanzibar unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. dili hilo.sasa wata control vipi vitamburisho kama hawawezi kucontrol vitu muhimu kama leseni za kuendesha gari?

    ReplyDelete
  2. Itakuwa vizuri zaidi kama kampuni za simu ndio zitakuwa zinauza kadi za simu kuliko kuwapa kina mangi wanaouza kiholela holela tu..!! Kama wataweza kucontrol through ID basi itakuwa pia ni rahisi kumtrack mtu ambaye atapiga call ya Matusi au Vitisho..!! Pia watoe hii system yao ya Private number maana kila mtu in TZ ana private number for what? Nani anataka kukuvamia wewe au akuibie mpaka uwe una private number? Na huu ununuaji wa Vocha kila siku unaboa sana..!! Waweke contract kwamba kwa mwezi Unalipa kiasi fulani, unatuma message kiasi fulani na kuongea kiasi fulani na kama hutolipa wana-deactivate yor number inakuwa huingizi call wall hutoi..!! Unajua kwa mwezi sometime mtu unaweza ukatumia hata laki moja kwenye vocha tu..!! Wakifanya hivyo makampuni yataleta ushindani mzuri sio ushindani wa kurahisisha bei ya kadi kufikia mpaka sh. 100 maeneo kama ya Mwenge, Kariakoo, Ubungo na kwingineko..!! Zimekuwa kama pipi bwana..!!
    They Have To Do Something about it...

    ReplyDelete
  3. Huyo mdau wa kwanza kaongea point..!! Hivi kwa nini kunakuwa na ufojaji wa License..!! Yaani kamatumeweza kutengeneza passbort zenye barcode ambazo zinasoma kwenye mashine, inakuaje kitu kidogo kama leseni tunatengeneza kwa mikono? Kitu ambacho ukitoa 20,000 tu maeneo fulani unapata ngoma brand new..!! Ndio maana Ajali za kiholela holela ni nyingi..!! Serikali naomba ifanyie kazi hili..!!

    ReplyDelete
  4. Ebufikirieni mambo ya muhimu ukoh!!! ninyi mnapangapanga vijimambo vyenu ya ajabu badala kushughulikia mambo muhimu zaidi, ilo litakuwa dili tuu kama ndugu yangu wa hapo juu.
    mdau kutoka kijitonyama.

    ReplyDelete
  5. UFISADI KWANZA,richmond,EPA,vitalu vya kitalii,ATCL,TTCL,radar,mikopo universities za Tanzania nk
    msituzuge aisee msipoteze habari za msingi
    eti oooooh kadi za simu khaaaaa ili nalo akili???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...