KILIMANJARO STARS LEO IMEICHAPA BURUNDI BAO 3-2 KATIKA MECHI YA KUSAKA MSHINDI WA TATU WA KOMBE LA CHALENJI, NA KUJIHAKIKISHIA KULAMBA DOLA 10,000 KAMA ZAWADI YA MSHINDI WA NAFASI HIYO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. MICHUZI WEE KWELI SOO NAONA TUKO WOTE KWENYE PC ZETU KILA NIKISOMA HABARI INAINGIA NYINGINE MUMO KWA MUMO BIG UP SANA MAN NAAPRESHIET KAZI ZAKO BIG TAIM

    ReplyDelete
  2. Asnte kwa habari motomoto brother Misupu!! Nasubiri matokeo ya Watani zetu na Waganda Chalenji nani kamnywa mwenzake! Wote vipofu wameona mwezi hao! Kili Starz ndio yenyewe!
    Mdau toka Oslo

    ReplyDelete
  3. mdau wa oslo acha ushabiki wa kijinga. tumefungwa angalia jinsi ya kuja wafunga tena next time. Sio kukashifu

    ReplyDelete
  4. Hongera Kili Stars,

    Sasa mrudi kwenye timu zenu na muanze kujifua kwa nguvu zenu zote ili tuende Ivory Coast tukiwa na nguvu moja.

    Mashindano haya ya CHAN ndio saizi yetu kwa sasa kwa sababu hatujawa bado na wachezaji wakupambana na wachezaji wakubwa wa afrika magharibi na kaskazini, tuendelee kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na wadau wenye timu za vijana nchi nzima, kwa sababu timu imara ya taifa haijengwi ndani ya miaka miwili au mitatu, wenzetu wa afrika magharibi na kaskazini wametumia zaidi ya miaka mitano kuandaa timu zao za taifa na wako very serious katika suala zima la nidhamu za wachezaji.

    Mdau Kisiju japo katika hali ya unafiki wape hongera wachezaji wa kili stars, japo humpendi Maximo lakini kiunafiki mpe hongera yeye pamoja na wachezaji wetu.

    ReplyDelete
  5. Michezo Uingereza:
    FA Cup 3rd Round half-time results
    Southend United 1 Chelsea 1. Timu ya daraja la chini ilitangulia kuona nyavu za Chelsea ktk dakika ya 16 baada ya Barrett kuunganisha kichwa mpira wa kona mbele ya Alex , Anelka ndani ya box la chelsea. Chelsea walisawazisha ktk dakika ya 44 kupitia kwa Ballack aliyewahi mpira uliomtoka kipa wa Southend.

    Premier League halftime results:
    ManUtd 1 Wigan Athletic O. Mfungaji ni Wayne Rooney, ManUtd wakitoka na ushindi watafikisha pointi 44 na kuwa nafasi ya pili nyuma ya Liverpool, hata hivyo ManUtd watakuwa wamecheza mechi 20 wakati liverpool yenye pointi 46 imeshacheza mechi 21 katika ligi ya premier.

    ReplyDelete
  6. Michezo Uingereza:
    Matokeo baada za mechi kuisha:

    Premier League:
    ManUtd 1 Wigan Athetic O. Wayne Rooney ameiwezesha ManUtd kushinda mchezo huo na kufikisha pointi 44. Hivyo msimamo Liverpool pointi 46, ManUtd pointi 44 na Chelsea ya tatu pointi 42. Wayne Rooney majeruhi na atakuwa nje ya viwanja kwa angalau wiki 3.

    FA Cup Raundi ya Tatu:
    Southend United 1 Chelsea 4. Mabao ya Chelsea yalifungwa na Michael Ballack, Solomon Kalou, Anelka na Lampard. Chelsea itaenda kupambana na Ipswich baadaye ktk FA Cup.

    Wakati huo huo Drodga hakuongozana na Chelsea kwenda Southend katika kile kilichoelezwa inaweza kuwa mechi yake ya mwisho kuchezea Chelsea.

    Hayo yameelezwa ktk gazeti moja la Ufaransa na kuwa sasa menejimenti ya Chelsea inaanza kufikiria kumsaini mshambuliaji Adriano kuongeza makali ya Chelsea.

    Mchezaji Kaka amewekewa ndoano kitita cha paundi Milioni 100 akubali kujiunga na klabu tajiri ulimwenguni Manchester City toka AC Milan. Ukifanikiwa mkakati huo ataungana na nyota nyingine ya Man city toka Brazil Robinho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...