TIMU YA TAIFA YA BARA KILIMANJARO STARS IMETINGA KWENYE NUSU FAINALI ZA KOMBE LA CHALENJI, BAADA YA KUITANDIKA RWANDA BAO 2-O KWENYE UWANJA WA
BAO LA KWANZA LILIFUNGWA NA MSHAMBULIAJI WA KULIA MRISHO NGASSA NA BAO LA PILI DAKIKA 37 KWA ATHUMANI IDDI CHUJI.
UGANDA IMEMPIGA SOMALIA 4-0 NA KUCHUKUA UONGOZI WA KUNDI A
MSIMAMO KATIKA KUNDI A:
1. UGANDA POINTI 7
2. BARA POINTI 6
3. ZENJI POINTI 4
4. RWANDA POINTI 3
5. SOMALIA POINTI 3 (samahani awali nilikosea kuwaka 0 )
IJUMAA KILIMANJARO STARS WATAZIPIGA NA UGANDA KUPATA WASHINDI WA KWANZA NA WA PILI WATAOCHEZA NA WASHINDI WA KUNDI B


Kaka si bado hatujawa na uhakika tunahitaji droo mechi ya mwisho kupita? Kuna mechi ya zenji na rwanda kama sikosei, sasa hao mmoja wao akishinda na sisi tukafungwa inaweza kuleta hali nyingine. halafu somalia si wana pointi tatu walitufunga?
ReplyDeleteduh mbona tunalishana sumu,haya matokeo ni sahihi?na pia hizo point za timu mbona hazieleweki kwa baadhi kama somalia si walishinda?
ReplyDeleteHellow Mzee Michu...!!!
ReplyDeleteHappy New...! Una huhakika Somalia ina point Zero.???!!!!!.So ilipoilaza Kili stars haikupewa point tatu au nini,kulikoni ikwa haina point tena....!!!!!.
Mdau ,
MN,
USA.
kwani somalia waipomfunga Bara hawakupata point? au ndo majungu unawawekea zero! au ndo unajifanya unachukia maharamia? hao jamaa wanatoza tu kodi kwa mataifa kutumia bahari.
ReplyDeleteasante kwa taarifa. ina maana Somalia baada ya kuifunga Bara haikupata point hata moja? mbona imepewa zero point?
ReplyDeleteBalozi naona mnakosea kusema kuwa Kilimanjaro Stars imefuzu kucheza nusu fainali. Ikumbukwe kuwa Karume Boys wana mechi moja mkononi na wakishinda wanafikisha ponti saba na Kilimanjaro wakifungwa out.
ReplyDeleteVivyo hivyo ruanda ina nafasi ya kufuzu ikiifunga Karume Boys
safi sana vijana mapambano mbele kila ataka kaa mbele yenu mnafunga tu kwani mlitukatisha tamaaa kabisa na somalia lakini ni part ya mchezo naona starz ni kama gari la Diesel likichochea usikae mbele hahah keep it up
ReplyDeleteInakuwaje nchi yetu Somalia haina point wakati waliibamiza Kilimanjaro Stars 1-0?naomba jibu plzz.
ReplyDeleteMichuzi rekebisha ujumbe wako,Kili Stars haijatinga nusu fainali.Matokeo ya mechi za Ijumaa ndiyo yataamua nani kapita kwenye hilo kundi.Isipokuwa Somalia,timu zote zilizobaki kwenye hili kundi zina nafasi ya kuendelea kwenye nusu fainali.
ReplyDeleteKaka nina wasiwasi na msimamo. Somalia wametufunga wanakuwaje na point 0?
ReplyDeleteKweli aliyeweka hii kakosea kabisaaaaaaa! Tanzania Bara bado hatujapita sababu ni hizi. Tanzania inacheza na Uganda na Zanzibar inacheza na Rwanda Game ya mwisho Zanzibar ikishinda Point ni 7 Tanzania Bara ikifungwa Point Bado 6 tumia akili,
ReplyDeleteZanzibar na Rwanda zitoke Draw ndio Result nzuri.
Somalia hawana 0 Point waliwafunga Tanzania Bara Goal 1 kwa 0 kwahiyo Somalia wana Point 3 wamemaliza Game wao Out.
Rwanda na Zanzibar bado wapo in Uganda ikiifunga Tanzania Bara alafu Rwanda Ikashinda kwa mabao mengi ya kuzidi Tanzania Bara then Rwanda wanapita.
Tanzania Bara wanahitaji ushindi au draw ya mabao.
Somalia itakuwaje na pwenti zero wakati walikwapiga bao Kilimanjaro?
ReplyDeleteKisiju natinga kama kawaida.
ReplyDeletemdau usiekua na jina nitakuita MDAU WA MAXIMO NA TFF.Ile homa waliokua nayo kwa uchovu wa kucheza mechi nyingi imekwisha?? Ama inakua kwenye mechi moja tu? Mbona tuna shangilia kijinga? kama tumefungwa tukubali tu tusitoe sababu zisizoeleweka.Na kama tunashinda ni jukumu la kila mmoja kupongeza. HONGERA KILIMANJARO!!!!
Mdau wa MAXIMO NA TFF, huyu teknisheni wenu angekua kwenye vilabu vyetu tungemtimua maana si kocha kama hao waliokuja wakatimuliwa. Mjomba unafikira za kitumwa. Na upeo wako mdogo.Afadhali ya mwanakatwe wa 1980 kuliko hawa viongozi waliokueko sasa. Yeye aliweza kuipeleka timu African Cup ya kweli si ya Maximo. Mashindano tulioqualfy nimetambaa kwenye mitandao mingi tu hamna mtu anefagilia.Kwa hiyo si ishu.
TFF imechukua majukumu gani ya mchezaji wa simba kumpiga kocha wake hadharani? Ama si kazi yao??
Simba na Yanga ziwe za kisasa vipi? Kama uongozi mzima wa mpira ni mbovu. Mjomba huna habari kwamba FA ya uingereza kwa mfano hutoa maelekezo wa HOW vilabu vinatakiwa kua?? Hii ni kuanzia timu zote zinazoshiriki ziwe ni zaina gani. kama hawamiti critiria hawazisajili? jiulize hizi gaidensi TFF wanazo? Na kama wanazo mbona sijaziona kwenye website yao ama siri kama kawaida? hichi ni chanzo za rushwa tu.
Kwani ni kazi kuseti misingi kwa mfano kuanzia 2015 timu zote zinazoshiriki premia ziwe PLC. ziwe na kakiwanja kidogo hata cha kushea na timu nyingine kwa mazoezi, si lazima kiwe na majukwaa. Hivi itawezeha timu kuanza kujitegemea na kuunda miundo mbinu yao ya kujiendeleza.
Ama TFF wako bizi kuomba misaada na kutumia wenyewe badala ya kufikisha kunakohusika? Yaani vilabu? Jamani amkeni. Angalieni pesa za wagombea wapya wa TFF walizotumia kwenye kampeni kuna faida gani?? Amkeni
Eti TFF imechagua viongozi vijana, Nasibu ana sifa gani ya kua kiongozi tena umakamu wa raisi? Eti ametuahidi kuichukua timu ya taifa Uingereza. Nimefuatilia timu aliotuahidi. Ana bahati ina kiwango kulinganisha na zile tulizocheza nazo Denmark na Uswiss. Ila tuone kama ile ahadi itakua ya kweli...
jamani hebu someni alichoandika mdau wa Tarehe January 08, 2009 1:50 AM, sijamuelewa... HEBU KAJIFUNZE KUSOMA NA KUANDIKA.. EBO!
ReplyDeleteNanukuu...
"Somalia itakuwaje na pwenti zero wakati walikwapiga bao Kilimanjaro?"
tehe tehe tehe
Issa Michuzi, Unahitaji kuongeza Mke Sheikh michuzi au Umefunga nini week hii? Saumu kali kama kuna mtu anakuletea za kuleta wadau tupo bwana tuje kukusaidia. Bw Michuzi unachanganya mambo je Bwawa la maini likija kuharibu vibay vibaya kweli tutapata Habari za Michuzi Blog? siutaifungia kwa miezi Sita. tupo pamoja na wewe michuzi hatuendi sehemu, Somalia Sifuri hahaahahah kwakwakwkawkakwa kweli kipigo walichotupiga wasomali kimemchanganya Issa Michuzi. Kimoja tu. haha. Ndosi.
ReplyDeleteJana katika mechi ya Carling Cup England, wababe wa soka ulimwenguni Man Untd ilizabwa bao moja kwa sufuri na timu ndogo ya Derby County.
ReplyDeleteSir Alex wa ManUtd alijaribu mbinu zote kurudisha bao kwa kuwachezesha mastaa Ronald, Rooney, Vidic, Tevez na wengine lakini haikusaidia.
Katika mahojiano Sir Alex(Manager) alikubali timu ya Derby County iliwazidi kimchezo na wangeweza kuadhiriwa mabao kama manne, lakini kwa bahati mungu amewanusuru na aibu hiyo. ManUtd watacheza mechi ya pili na timu ya daraja la chini Derby County January 15 2009 katika kugombea kombe la Carling Cup ambalo linashikiliwa na Tottenham Hotspurs ya jijini London.
Kwahiyo unataarifu a unafurahia, unafiki huo.
ReplyDeleteMdau Kisiju unaendekeza ubishi wa kipuuzi kwenye mtandao na tabia hiyo haikusaidii..hiyo hongera kilimanjaro uliyoisema wewe ni ya kinafiki kwa sababu wewe binafsi ni mnafiki..niliposema inawezekana ni fatigue iliyowafanya wafungwe na somalia nilikuwa natoa maoni yangu binafsi..ukumbuke kuwa kwenye mechi dhidi ya somalia tulipiga kona karibu ishirini na wachezaji wetu walikosa magoli mengi..ndio mpira ulivyo..kuna mdau katueleza kuwa jana Man Utd walifungwa na Derby..ukumbuke kuwa derby ni timu ndogo sana ukilinganisha na Man Utd, ina maana kwa sasa Man Utd wafikirie kumfukuza mzee Ferguson?, halafu eti unajifanya unaujua mpira!!..kama unaona Maximo hafai nenda TFF na jina la kocha ambaye wewe kwa upeo wako unaona anawafaa wachezaji wetu..lakini hata huyo kocha wako ataonekana mbaya siku timu yetu itakapofungwa!!!...badilika achana na huo ushabiki wa kishamba..unatetea upuuzi wa simba na yanga!!..TFF pamoja na kuwa ndie msimamizi mkuu wa soka hawana wajibu wa kuzifundisha timu zetu umuhimu wa kuwa na viongozi wa wabunifu , unaweza usinielewe namaanisha nini kwa sababu wewe ni sehemu ya majungu ya soka la nchi hii..timu ikifungwa kocha hafai..timu ikishinda mnashangilia kinafiki kama unavyofanya sasa!!..watakuja makocha wengi sana nchi hii tena wenye kiwango na uelewa mkubwa kuhusiana na soka lakini kwa bahati mbaya watakuta na na aina ya wadau kama wewe Kisiju..fikra za kitumwa unazo wewe ambae unaangalia mabaya tu..ndio maana simba na yanga hazina maendeleo..TFF hata wakitoa miongozo simba na yanga hawaifuatii..walishaambiwa tangu mwaka jana kila timu ya ligi kuu lazima iwe na timu ya vijana lakini mpaka leo hakuna lolote la maana walilolifanya!!..ninawaonea huruma sana makocha wenye taaluma kubwa ambao wanakuja kukuza mpira wetu lakini wakifika hapa wanakutana na akina Kisiju wengi kwenye timu zetu..upeo na uelewa wako kuhusiana na mpira wa miguu ni mdogo sana..vilabu vyetu vinaweza kabisa kuwa vilabu tajiri katika ukanda huu kwa sababu vina mtaji mkubwa ambao ni idadi kubwa ya mashabiki ..lakini akili za akina dalali , madega na kaduguda ziko sawasawa na za kwako Kisiju.. ndio maana bado una mawazo ya kimasikini sana..mawazo ya kutegemea pesa za wafadhili wakati timu zenyewe zinaweza kabisa kujifadhili..ninapozungumzia uwanja wa kufanyia mazoezi sio lazima eti viwanja hivyo vifanane na ule uwanja mpya..simba ina eneo kubwa kule bunju..inaweza kabisa ikatengeneza uwanja wa kufanyia mazoezi ambao ni wa kisasa bila kushughulika na suala la majukwaa makubwa na ikaachana kabisa na huu upuuzi wa kuhamahama kila siku kwa sababu ya ukosefu wa uwanja wa kufanyia mazoezi..nimejitahidi kukueleza kwa kirefu kwamba safari ya soka letu bado ni ndefu na haina njia za mkato lakini kwa sababu una uelewa mdogo umeishia kufikiri kwamba Maximo ndio tatizo la soka letu..hatukuwa na wachezaji wakupambana na akina Essien kule Ghana kwa sababu hatukuwandaa..bado hatujafikia kiwango cha kupambana na akina Tunisia , Nigeria na Ivory Coast wakiwa na vikosi vyao kamili..miaka mingi tuliipoteza katika kuendekeza majungu na vurugu wakati wa FAT, huu upungufu mkubwa wa wafungaji na upungufu mkubwa wachezaji wenye stamina ya kutosha ni kielelezo cha madudu yaliyokuwa yakifanyika kwenye miaka mingi ya themanini na tisini..Kisiju endeleza chuki zako dhidi ya Maximo lakini haikusaidii zaidi ya kuonyesha ni jinsi gani wadau kama wewe bado ni kikwazo cha maendeleo ya kweli ya soka.
ReplyDeleteKwanza nitoe pongezi kwa Kili Stars kwa kufanya kile ambacho watanzania tunahitaji.
ReplyDeletePili naomba nitoe angalizo lifuatalo : Kwa waliosikiliza matangazo ya mechi ile kwa makini mutakubaliana nami kwamba mtangazaji wetu maarufu wa TBC Taifa Bw Juma Nkamia alitueleza kuwa mfungaji wa mabao yote mawili ni Athumani Idd na kwamba mchezaji huyo ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliopachika mabao matatu kwenye michuano hiyo , cha kushangaza jioni kwenye kipindi cha michezo TBC Taifa hiyo hiyo ambayo chanzo chake kikuu kule ni huyo huyo Nkamia tukaambiwa magoli yamefungwa na Mrisho Ngassa na Athumani Idd , ivi Mrisho Ngassa na Athumani Idd wanafanana? au Nkamia ana matatizo gani maana hii si mara ya kwanza , kwa wale wanaokumbuka Burkinafaso alifanya kosa kama hili likazua mtafaruku mkubwa uliopelekea mfungaji halisi wa goli kultoa ufafanuzi kwenye vyombo vya habari, ivi Nkamia haelewi kwamba goli ni haki miliki ya mtu aliyefunga ambayo haifutiki daima.
Binafsi naamini kwamba huwa anapitiwa lakini kinachotia shaka ni kwamba huyu bwana amekuwa mstari wa mbele kuwakandia waamuzi pale wanapokosea na kudiriki nyakati fulani kusema kwamba Afrika hasa ukanda wetu huu hauwezi kuendelea kisoka kwa sababu waamuzi wengi ni wabovu hasa pale timu anayoishabikia inakuwa imebanwa, sasa kama yeye yupo jukwaani amekaa anafanya makosa kama haya inakuwaje kwa mwamuzi ambaye anakuwa anakimbia asifanye makosa?
Ningemshauri awe makini anapotangaza mpira hasa kwa wakati huu wa utandawazi ambapo watu wana fursa za kuona kila kitu kwa wakati ule ule , atangaze matukio halisi aache kutangaza kinazi
Mbona waandishi wanatuchanganya? kuna wanaoripoti kuwa mabao yote mawili yamefungwa na Chuji, wengine mmeripoti kuwa bao moja limefungwa na ngassa na la pili limefungwa na chuji. Tushike lipi hapo?
ReplyDeletendugu zetu wa chenga twawala mpira bado; ingawa ngebe nyingi;
ReplyDeletenadhani kili star itapata hiyo point inayohitajika ili icheze semi final;hii inatoka na kuwa na kiwango kizuri; mpira unadunda ;hakuna yakini katika mpira.
inayetaka kubisha na abishe;kuhusu brother michuzi kukosea hilo si la kushangaza ;kila mwanadamu hukosea ndiyo ukamilifu wamwanadamu;
Christiano Ronaldo amenusurika ktk ajali ya gari katika barabara iliyo ndani ya handaki(Tunnel) jijini Manchester.
ReplyDeleteRonaldo alikuwa akiendesha gari lake la kifahari aina ya Ferrari ndipo gari hilo lilipogonga barriers za handaki hilo na kuharibika vibaya, gari limekuwa written-off. Gari la Ronaldo lilikuwa linaongozana na gari la kipa nambari moja wa ManUntd Van de Sar aina ya Bentley wakielekea vitongoji vya mabwanyenye jijini Manchester.
Polisi wa usalama barabarani wali- mpima pumzi kuona kama alikuwa kapata 'kilaji' lakini matekeo ya kipima-pumzi kikawa safi(negative).
Ronaldo aliruhusiwa na anaendelea na mazoezi na timu ya ManUtd kama kawaida.
Kisiju naingia.
ReplyDeleteHili linakua tatizo espeshiali wale waliozoea kutawaliwa. Mtu ukilonga ukweli unaitwa mpuuzi na hoja hazina misingi!! hata kama watu wanachemsha tunyamaze? wakati ule umepitwa na wakati ndugu yangu MDAU WA MAXIMO NA TFF.
Nilichosema timu ikifungwa tukubali kama fundi ambae ni MAXIMO na wachezaji wamezidiwa tusitoe sababu zisizoeleweka. ohh wachezaji wamechoka ohh sijui nini ohh sijui KISIJU lete kocha wako. Kaka mbona hueleweki? Derby ilipoifunga Man U mwalimu ambae ni Ferguson alikubali alizidiwa. Kumbuka walikua wanaweza kutoa sababu nyingi tu za kiufundi kuhusiana na kufungwa. Lakini si huyu Teknishiani wetu. Tukifungwa hatupi sababu za kiufundi kwa mfano tulizidiwa kwenye dipartment hii ama ile. Anakua kimya maana hajui anachokifanya.
Si unaona anaengoza soka la nchi hii ni SIMBA na YANGA umekiri hilo sasa kama mwili una amrisha kichwa itakua vipi ndugu yangu Mdau wa Maximo na TFF???
Kama TFF ndio wanaloliongoza wangeakikisha kwa nguvu zao hadi za dola wanachokiimposi kinafuatwa. Lakini hilo aliewezekani hata kidogo. kama walitaka lazima timu iwe na timu ya vijana nani atakaewalipa wachezaji posho? Na hela zote zitokazo FIFA kwa ajili ya kuchangia kuinua soka hapa nchini hao ndugu zako wa tff wanakula wao?? Amka MDAU WA MAXIMO NA TFF. hata huyo Maximo ingekua TFF wanamlipa wangeshamtoa baru. Hiyo TFF yenyewe inategemea wafazili ijekua Simba na Yanga?? Ama hujui hilo?
Kaka sikatai safari yetu ya kuiunua soka bado iko kweye hatua za mwanzo kabisa ila sii elewi kwa nini timu inapokua kempu na tatizo kama ulivyo lisema ni umaliziaji kocha hilo ni jukumu lake kulitatua ama kulipnguza. Lakini tatizo linakua na kocha anatupi lawama kwa nchi hali ya kua hilo ni jukumu lake. Lakini hataki kuelewa maana kuna watu kama nyinyi mnamfanya MTUME.
MAXIMO ni kocha wa mwanzo duniani kumsikia hadharani kusema nimekuja weka misingi na si kushinda. Nasisi kwa sababu tunababaika na rangi yake na Ubrazili wake tunakenua meno tu AMKA NDUGU huyu bwana ana lipwa hela nyingi na ni lazima adelive standard ya kile tunachomliapa. Ama tutafute makocha wa rahisi hata watano kwa kila levo yaani vijana china ya 12,16,18,21 na mwingine wa timu kubwa.
Sijasikia hivi karibuni kama kuna kocha yeyote mzawa amepelekwa nje kwa ajili ya masomo labda Mdau wa Maximo Na TFF unajua tueke sawa.mwisho tusubire hio hapo raisi atakaposema simlipi tena huyo tuone hicho kichwa cha soka nchini kitatoa wapi hela za kumlipa.
Tatizo lako kubwa Kisiju ni upeo mdogo, narudia tena na tena kukwambia hivyo.. ndio maana unaeleweshwa lakini bado hauonyeshi dalili za kuelewa.
ReplyDeleteTulikuwa kwenye nafasi ya 167 wakati Mximo anawasili nchini , sasa hivi tuko kwenye nafasi ya 99, hiyo inatosha kukuonyesha Maximo alikuwa sahihi siku ile alipowasili pale airport aliposema kwamba amekuja kujenga msingi wa soka , hatukuwa na misingi imara ndio maana tulikuwa kwenye nafasi ya 167!!.
Maximo hakukuta mendelezo wowote ule wa soka la vijana..aliwakuta wachezaji waliojilea wenyewe ambao hawakuwa na misingi ya soka..kumbuka hata wale mastaa wa zamani kina athumani juma chama , zamoyoni mogella , khalid abeid na wengi wengineo walikuwa na misingi iliyojengwa miaka mingi kabla ya wao kuanza kujulikana..hawa wachezaji aliowakuta Maximo hawakuwa na misingi ndio maana siku zote anasema itachukua miaka mingi kutengeneza timu, wewe huwezi ukayaona mabadiliko aliyoleta Maximo kwa sababu ndani ya akili yako ni mtu unayeishi na fikra za kushindwa tu!. sio kweli kwamba Maximo hawezi kuongelea kiutaalam matokeo ya mechi tunazocheza..akwambie wewe sababu za kiutaalam ukiwa kama nani?..mpira umeujulia wapi mpaka yeye akueleze sababu za kiutaalam..ndio maana kila siku nasema aina ya watu kama wewe ndio wameshiriki kuua mpira wa bongo..tulipiga kona zaidi ya kumi na tano , muda wote wa mchezo tulikuwa tuko kwenye goli la somalia lakini wao wakatufunga full stop..unataka uelezwe department gani ilipwaya!?
Siku zote nakueleza si kazi ya Maximo kumpa mafunzo ya awali mchezaji wa timu ya taifa..anatakiwa awe amefundishwa jinsi ya kupiga mashuti, kutuliza na kuficha mpira , jinsi ya kutoa pasi akiwa kwenye timu za watoto na sio taifa stars..tatizo lako kisiju unaabudu majungu ya vijiweni..nenda kwenye mazoezi ya stars uone jinsi Maximo anavyolazimika kurudia kila siku mafunzo yale yale kwa sababu wachezaji wetu hawakufundishwa mambo ambayo ni basic.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa soka la uwanjani utagundua kuwa hata tunapocheza na timu zenye nidhamu iliyojengwa kwa muda mrefu huwa inatubidi tucheze kwa kujihami kwa muda mrefu kwa sababu wachezaji wetu kwanza wanacheza kwenye ligi ambayo ni ya kiwango kidogo sana (ambani ambaye ndie anayeongoza kwa magoli ana miaka zaidi ya 34 na anakaribia kustaafu lakini bado anawaburuza vijana wa kibongo!!), halafu hatujawa na professionals wengi wakuweza kuifanya timu yetu imiliki mpira kwa muda mrefu..mpira ndugu yangu kisiju ni taaluma kama taaluma nyingine yoyote ..inastahili kuheshimiwa..na hakuna njia yoyote ya mkato ambayo eti inaweza kutuletea mafanikio ya ghafla.
Inaonekana unapenda kuongea bila hata kufanya uchunguzi wa kile unachokiongea..Sylvester Marsh alikwenda Ujerumani miaka miwili iliyopita na akarudi akiwa na Advanced Diploma ya football..na sasa ni kocha msaidizi wa timu za taifa za vijana.
Tatizo la umaliziaji linafanyiwa kazi ndio maana kwa sasa timu yetu ya taifa inaweza hata ikafunga magoli matatu kwenye mechi moja.
Hakuna mtu anayemfanya Maximo Mtume bali wewe unashindwa kumheshimu bila kuwa na sababu zozote za msingi, unamhukumu Maximo kwa kutumia vigezo vya mitaani ambavyo bado ni vya kitoto sana.