Mheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya, pole na kazi.
Naomba kutoa wazo kuwa Mheshimiwa Simba apewe fursa ya kuhojiwa tena. Mahojiano yake na Mwanakijiji yameleta zogo kubwa, wengi wakionyesha kutoridhika kabisa.
Fursa ya kuhojiwa tena ni muhimu kwake na kwetu. Itatusaidia kwa mengi, kama vile kudhihirisha kama aliteleza tu au la kwenye yale mahojiano ya mwanzo. Kwa vile ni kiongozi, anao wajibu wa kujieleza mbele ya wananchi. Kwa hivi, pendekezo langu ni suala la kujaribu kumtendea haki na pia suala la wajibu wake kama kiongozi.
Tena ingekuwa bora kama viongozi wote wangekuwa wanahojiwa mara kwa mara.
Mdau JM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Any public leader who is not going along with people is not a good leader, as a leader you should accept and accomodate other peoples' differences, if you don't do just like that, HUFAI KUWA KIONGOZI WA UMMA, KWANI MADARAKA YA UMMA NI DHAMANA, SI MALI YA MTU ALIYEPEWA NA UMMA KUWASIMAMIA MAMBO YAO, NI MALI YA UMMA WOTE, we need to re-engineering our society as it was long time ago. "SOCIAL RE-ENGINEERING" I don't think Sophia IS FIT FOR THE PURPOSE.

    ReplyDelete
  2. wewe mdau JM pendekezo lako halina maana yeyote. Tumeshamsikia huyo Bi Simba na tumeshatoa judgment zetu. Labda unaundugu naye, kashachemsha na hilo halitabadilika kumsafisha kuhojiwa tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...