Mabasi yote ya abiria nchini yatatakiwa kuwa na mikanda na abiria wote watatakiwa kujifunga mikanda hiyo muda wote wa safari wakiwa ndani ya vyombo hivyo vya usafiri, Jeshi la Polisi limetangaza wikiendi hii.

Kamanda wa Trafiki nchini, Afande James Kombe, amesema hatua hiyo inakuja katika jitihada za kupunguza vifo na majeraha makubwa yanayosababishwa kila itokeapo ajali.
Sheria kama hii imekuwa ikitumika nchini Kenya ambako inasemekana imesaidia sana katika kupunguza maafa kwa abiria wakati wa ajali.

Amesema sheria ya mikanda imo katika kanuni za Mamlaka ya usafiri wa barabara na majini (SUMATRA) na kwamba abiria akikutwa hajafunga mkanda ataadhibiwa.

Kamanda huyo amesema wamiliki wa mabasi wameshajulishwa juu ya hatua hiyo na kuwataka wahakikishe kila basi la abiria litaloagizwa liwe na mikanda ya kujifunga abiria.

Amesema tayari shirika la Usafir Dar (UDA) limeshaanza kutekeleza sheria hiyo ya kuweka mikanda kwenye mabasi yake yote ya abiria, na kwamba sharti mojawapo ya kusajili basi la abiria litakuwa ni kuwa na mikanda kwa abiria.

Kuhusu abiria kusimama ndani ya basi, amesema wamiliki wa mabasi hayo inabidi wapate leseni itayowaruhusu kusimamisha idadi maalumu ya abiria wakiwa safarini, na kwamba wataosimama wawekewe mabomba ya kushikilia.
Vile vile Kamanda Kombe amesema hivi sasa wamiliki wa mabasi ya abiria hasa yaendayo mikoani wametii amri ya kuwa na madereva wawili wataokuwa wakipokezana endapo safari itazidi masaa manane. Ameongeza pia kwamba mabasi ya abiria ya masafa marefu yameruhusiwa kusafiri hadi saa sita usiku. Awali ilikuwa mwisho saa 12 jioni.

Kiasi cha ajali 16,640 za barabarani zimerekodiwa kutokea na kusababbisha vifo vya watu 2,362 na majeruhi 14,825 kati ya Januari na Oktoba mwaka uliopita pekee. Wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa kuwa na jumla ya ajali za barabarani 3,871 zilizopoteza maisha ya watu 169.

Mkoa wa Lindi ndio wenye ajali chache, ukiwa umerekodi ajali 114 zilizopoteza masiha ya watu 66 mwaka jana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. oh yeah, natamani hii sheria itumike hadi kwa waendesha baiskeli, na wao wafunge mikanda. Kuanzia sasa baiskeli zote ziwekewe mikanda na mikanda hiyo inapatikana pale dukani kwa nanihii

    ReplyDelete
  2. Anonymous hapo juu unaelezeaje umuhimu wa kufunga mkanda kwenye baiskeli? Sijui ajali ya baiskeli unaifananishaje na ya gari. Ninavyoelewa mimi, ukivaa mkanda kwenye baiskeli, utashindwa kuruka wakati ambapo ungeweza kujiepusha. Magari mara nyingi hayatoi nafasi ya kuruka. Ukiwa ndani unaumia au kurushwa kama tu kitu ndani ya chombo kingine.

    Kwa wazo la abiria kuvaa mikanda, naona serikali imefikiria kitu kizuri majeraha na vifo vingi zitokeapo ajali. Ni kwa faida zetu wananchi. Tusione kama serikali inalenga kutukandamiza.

    Mdau,
    Oregon, USA.

    ReplyDelete
  3. wilaya ya kinondoni ina haki ya kuongoza kwa ajali kwavile hata kwa idadi ya bar kinondoni inaongoza DON`T DRINK AND DRIVE, EAT AND DRIVE, DONT DRIVE WHEN YOU ARE HUNGRY OR ANGRY,

    ReplyDelete
  4. Mabasi yetu yakwenda mikoani yakipataga ajali huwa yanakatika nusu kwa nusu utadhani pick up,sasa abiria wakifunga mikanda si ndio watajihakikishia kifo kwenye siti zao kwa kusagwa pamoja na siti zao.Maana gari itakapo geuka juu chini ndo kazi itakapoanzia.(AIR MSAE)
    ahsanteni!

    ReplyDelete
  5. Mheshiwa Mbunge wa nanihii pole na kazi kaka. Sasa hii sheria ya mikanda inamaana miaka yote hiyo haikuwepo ndio imeanzaa sasa, kwa sababu kuna sehemu huyo mkubwa anasema nisheria iliyoandikwa kwenye vitabu tangu enzi hizo sasa walikuwa wapi kufuatilia hilo? Pia kwanini hawa wakubw siku zote wanakuwa wepesi sana wa kuanzisha vitu ambavyo hawawezi kufuatilia? Sasa kutakuwa na ruhusa ya magari kusimamisha abiria lakini watapewa vibali. hiyo ni pesa tayari. sasa hawa wanao simama nao watafunga mikanda kwenye hizo bomba? na hii mikinda itapatikana wapi? kama sio deal tu la mtu? maana serikali yetu bwana. kumbuka enzi za speed governer, yako wapi leo? wazo zuri lakini kwa faida ya nani?

    ReplyDelete
  6. Bongo Tambarale ,Imeshaletwa mikanda imejaa tele dukani mpaka iishe ndio patakalika mmmmm.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Oregon wewe ndo hujui nchi hii bwana.Sheria inaanzishwa kwa faida ya mtu.Si kwamba waTanganyika hawajui lakini hizi sheria ni viini macho.Mbasi mengi ni mabovu kabisa, trafiki wakija juu na kuyakamata inakuwa nongwa.Mnakumbuka kuwa mabasi karibu 80% yana chassis za malori, yalikamatwa na kupewa muda sasa muda huo ulipita zamani.Mnakumbuka speed governor=ziko wapi?
    Kwa mwendo huu tuna subiri mikanda ya pikipiki na abiria wake,indketa kwa mikokoteni na wiper za guta(baiskeli za miguu 3) , nyie subirini tu

    ReplyDelete
  8. 1. Serikali imefanya jambo la maana sana. Idadi ya watu wanaokufa kwa ajali za barabarani kubwa mno na inaweza kuzuilika.

    2. Pia kwa watumiaji wa daladala, hii itasaidia kuondoa upuuzi mfano: wa watu wanne kukalia siti ya watu watatu na pia kushindiliwa kwenye daladala kama mizigo.

    3.Kama hii amri itatekelezwa ajali zinazoleta vifo zitapungua.

    4. Hima kwa wananchi kusaidia utekelezaji wa hii sheria

    ReplyDelete
  9. hivi ni macho yangu au?daladala zetu siku hizi zinapisha waenda kwa miguu zebra crossing?
    anyway, shukrani kwa mamlaka husika kwa kufuatilia hili swala zima la usalama barabarani. it's about time..

    ReplyDelete
  10. Huu ni mfano wa kukurupuka kufanya maamuzi bila hata yakutumia common sense
    1. magari kama hiace hazifai kutumiwa kama magari ya abiria kwa sababu viti vyake vipo karibu sana na haimpi mtu (room for manouvre)nafasi hata ya kugeuka au kukaa sawasawa na kama wanataka hiace zitumike kama basi za abiria wasiruhusu watu kusimama kwenye magari hayo

    2. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha gari za Abiri hazikimbi hasa za Mjini mfano dar-es-salaam na msongamano wote ule wa magari gari za daladala zina bidii ziwekewe kiwango maalum cha kukimbia (speed Limit)

    3.kama hiyo sheria ilikuwepo siku zote ni kwanini haikufwata tangu zamani na wanakuja kuanzisha kipindi hiki, hii ikiwa na maana isije ukawa mradi wa watu kuuza hiyo mikanda ya magari,kwani ukizingatia hiace nyingi ni modification na zinapoingia nchini huwa mara nyingi zinaingia bila viti.

    Mfano mwingine wa maamuzi ya zima moto kwani mikanda hiyo haitazuia hajali kama hakuna hatua zitakazotumika kuwaelimisha madereva kutokuendesha magari kwa speed na kama serikali haitaweka sheria kali kwa madereva wote ambao wanaendesha kwa kasi.


    Seikali inatakiwa kuhakikisha inaweka speed limit kwenye barabara na kuhakikisha sheria zinafatwa kuhusu speed limit, vinginevyo ni kama kuwaambia madereva waendesha kwa kasi kwa sababu tu abiria wote wamefunga mikanda na wapo salama.

    mjusi

    ReplyDelete
  11. Mh. Balozi
    Hii ya UDA na mabasi ya ruti za ndani ya miji abiria kuvalishwa mikanda ni kali ya kuanzia mwaka.

    Maana hapa jijini London hakuna basi linalotoa huduma ya kusafirisha ndani ya jiji la London lenye mikanda ya abiri hata yale ambayo ni mabasi ya ghorofa.

    Ila itakuwa jambo zuri kuweka kiwango cha abiria wa mjini wanao weza kusafiri ndani ya basi wakiwa wameshika bomba chapa konyagi.

    Kwa mabasi ya safari ndefu abiria wasiruhusiwe kusimama wakiwa ndani ya usafiri na pia abiria wote waliokaa ni muhimu na lazima wafunge mikanda ya usalama.

    ReplyDelete
  12. Hakuna ki2 hapo,mradi wa kuuza seat belts za PSV waja huo,kama speed governor vile.

    ReplyDelete
  13. Hicho ni chanzo cha bei za daladala kupanda. Unadhani watatengeneza faida kwa mtaji huo? Watalazimika kupandisha bei ili kila mtu akae. Kwa maana nyingine nikuwa "hakuna kushika bomba tena"...matokeo yake tutayaona muda si mrefu.
    Mdau, CA-USA

    ReplyDelete
  14. Mdau wa Oregon,

    Mimi nilishafika huko Portland, Oregon, lakini sijaona yale mabasi ya abiria pa mjini yana mikanda ya abiria. Sasa hii ya kuweka mikanda kwenye daladala itakuwa mpya na itaingia kwenye kumbukumbu za Generators, Speed Gorvenor nk. Kumbuka kuwa walaji smart wanaoogopa Kisutu hutumia mianya kama hii wakatfsiri mambo kwa kupata manufaa.
    Ulaji wa namna hii bongo haukuanza kwa Kombe tu bali na yeye ametafuta wapi anaweza kutengeneza bila ya mikwaruzo.

    ReplyDelete
  15. MNAO ISHI MAMTONI CHANGIENI KUHUSU HABARI HII KWA UNDANI ZAIDI. MAANA SHERIA NYINGINE HAZIELEKEI HATA.!!JE HUKO MNAKOISHI MABASI YANOKWENDA MIKOANI YANAKUA NA MIKANDA, JE MADALADALA YENU ABIRIA PIA HUFUNGA MIKANDA??? LABDA. TUELIMISHANE KWENYE HILI.NA MADALALA YENU HULIPWA KWA KILOMETRE NA SERIKALI, YA KWETU KASHESHE. MDA FUNGA FUNGUA MKANDA UPO WAPI KWA WANO HESABU KICHWA?(ABIRI)? NDIO MAANA KUNA UKOSEFU WA USAFIRI DAR.

    ReplyDelete
  16. Ninapenda kuipongeza idara ya usalama kwa kuamua kufikiria mikakati tofautitofauti ya kuweza kupunguza majeruhi, hata hivyo suluhisho hapa ilikuwa sio kupunguza watakaoumia bali ni kuzuia au kupunguza ajali sisitokee.
    Hapa inaonyesha ajali ni truksa zitokee ila tujaribun kuzuia idadi ya majeruhi kwa kutumia "safety belts". Mikanda ya usalama inapunguza uhumiaji kwa asilimia fulani ninakubali ila kipaumbele iwe ni kuzuia ajali kwa mambo tofauti tofauti mfano
    -Upunguzaji mwendo kasi hasa kwa magari ya abiria. Hili linawezekana kwa ushirikiano wa wadau wote kuanzia shule zinazofundisha madereva hawa, askari wa usalama barabarani ambao watakuwa wana reinforce sheria na wala sio kuchukua rushwa na kuwafanya madereva waendelee na kiburi cha kufurusha magari, na mwishi abiria na wananchi kwa ujumla wawe mstari wa mbele kuwakemea madereva wanaoenndesha kwa mwendo wa kasi.
    Vile vile kungekuwa na systerm kama za wenzetu wa ugaibuni wa kuwa na traffic cctv ingesaidia kwani askari akiwa control room anaweza kuona mwendo kasi wa gari x na kuwatuma wanaofanay control ya maeneo hayo na kulifukuzia gari husika, hii ingesaidia sana.

    Vile vile uimara wa gari ni moja ya vitu vinavyozuia gari kupata ajari kiurahisi, sina uhakika kama nchi yetu inamfumo madhubuti wa ukaguaji wa magari na vyombo vinavyotambuliwa kisheria na mamlaka ya usafiri,Huku UK kuna kitu wanaita MOT test huu ni ukaguzi wa gari kugundua lipo madhubuti kiasi gani,gari linakaguliwa na mamlaka ambazo huwezi kutoa hongo na gari lisipopasi basi huruhusiwi kuliweka barabarani mpaka umelitengeneza tatizin lililogundulika. Ninaakika kwa Bongo kama tungekuwa na MOT kam za huku ugaibuni basi asilimia zaidi ya 70 ya magari yangeonekana hayafai kuendeshwa.

    Kuhusu mikanda ninawasiwasi utumikaji wake utakuwa na utata kwa sababu ya swala zima la usafi. sijui ni kwa kiwango gani wenye gari wataakikisha mikanda inakuwa safi kwa matumizi ya abiria vinginevyo hamna atakaekubari kutumia mkanda wenye mavumbi, pia magari yanayopita maeneo yenye vumbi mikanda hii itakuwa mara kwa mara inachafuka na kuwafanya abiria wasite kuitumia. kwa hiyo hapa isisitizwe wenye magari wahakikishe mikanda inakuwa safi.

    Kuhusu madaladala ya mtoni mimi nipo London huku mabasi yanayotumika kama madaladala hayana mikanda, ila ya kwenda safari za mbali nje ya mji ie national express huwa kuna mikanda.

    Mdau London

    ReplyDelete
  17. Hakuna ubishi Bongo ni tambarare!!!
    1. magari yanayotoa huduma za usafiri mijini hayahitaji mikanda. kwanza kabisa serikali ingetafuta wawekezaji, wawe wa ndani au nje, wa kutoa huduma hiyo kwa magari makubwa kama ilivyokuwa ikurus kumbakumba, na hatimaye kupiga marufu vipanya. UDA inaweza kuwezeshwa kama nia ingekuwepo! vipanya ni magari yakutumiwa kifamilia au kikazi.
    2.Juzi nimesafiri na basi kutoka dar hadi bukoba, na kutoka bukoba hadi kampala. uendeshaji wa mabasi unatisha. madereva wana overtake magari makubwa na madogo hata kwenye sehemu zisizoruhusiwa (ambazo hata mtoto wa darasa la nne atakwambia hapa mtu huwezi ku overtake) kama vile kwenye kona na milima, nk. Inatisha!!!! Bila kutafuta njia za kubadilisha utamaduni mzima ulojengeka wa uendeshaji magari si Tanzania tu bali afrika ya mashariki yote, hili agizo au sheria ya mikanda itabakia ze comedy tu!!!

    ReplyDelete
  18. Anonymous wa January 05, 2009 12:39 AM

    Kama ulifika Portland, Oregon utaona hakuna mikanda kwenye mabasi ndani ya mji (mfano wa daladala Dar). Lakini, kama pia ulienda nje ya Portland kwa kutumia mabasi ya masafa marefu (Greyhound lines), bila shaka uliona mikanda. Na ni lazima dereva ahakikishe abiria mmefunga hiyo mikanda.

    Naungana nawe watu wanapata ulaji kupitia mradi huu, lakini pia kumbuka kuwa usalama wa daladala za Bongo kuwa bila mkanda ni mdogo, mara itokeapo ajali. Si kwamba USA ajali hazitokei kabisa, lakini kusema ukweli sijawahi kusikia basi la ndani ya mji limepata ajali na kuua. Hii inatokana na matengenezo wanayofanya kila mara. Mfano, gari ikienda mara kadhaa, lazima ipelekwe matengenezo kila siku. Nani anafanya hayo Bongo, wakati hesabu hajaifikisha?
    Kwasababu hiyohiyo ya matengenezo, ndio maana mabasi ya masafa yanawekewa mikanda sababu gari inaweza kuharibika sababu ya umbali na watu wakaumia au kufa. Sasa kwetu Bongo, ajali hata za vipanya ni nyingi, karibu kila siku watu wanaumia. Je, tuache mikanda sababu tunahisi watu wanajifaidisha kama mradi? Wakati kwa kufunga mikanda tutaokoa maisha yetu? Tuchague.

    Mdau,
    Oregon.

    ReplyDelete
  19. Nilivyokuwa nakwenda Iringa na my beloved Scandinavia, basi lilikuwa na mikanda na nikafunga kwa tahadhari yangu japokuwa Scandinavia haina historia ya mwendo wa kasi au ajali za kuua abiria.

    Ila kwa daladala sijaona zina seat belt kote nilikopitapita hapa duniani.

    Gaborone, Botswana: minibus zao lazima abiria pamoja na konda wakae kwenye viti! Hakuna konda kusimama na kuchungulia dirishani wala abiria kusimama, period!

    Mombasa, Kenya: daladala zao hakuna pia kusimama, abiria wakae wote kwenye viti ndipo gari liondoke.

    Sasa hii biashara ya seat belts ndani ya daldala zetu inatoka wapi? Kuna mtu mmoja, nadhani Robert Kiyosaki, alisema "do what the rich people do" kwenye personal finance na hakuna haja ya kure-invent the wheel towards personal financial success.

    In this case, we do not need to reinvent the wheel, and why not us do what the successful people have done? Gaborone and Mombasa here are the successful ones so why are we in Dar-es-Salaam reinventing our own rule of taking care of an ongoing problem?

    Ushauri wangu ni kwamba ujumbe ulioundwa na Tanzania traffic police, umoja wa wenye daladala etc uende study tour and/or fact-finding mission katika miji hii ya Afrika na kujionea wenyewe nini wenzetu wanafanya kutatua tatizo hili.

    ReplyDelete
  20. I'm lost! Mabasi yote nchini ni pamoja na daladala siyo? Yaani, abiria WOTE, wakiwamo wale wa G/Mboto-Sinza; Mbagala Rangi Tatu; Posta-Kimara (jioni pia) na kwingineko tutafunga mikanda kwenye mabasi? P'se nielewesheni kama kuna aliyeelewa barabara huu mradi (project) ya mikanda.

    Mwaka jana pia tumekuwa na zoezi la kuweka milango ya dharura mabasi yote nchini. Enhe! Tusikejeli hatua zinazolenga kupunguza ajali, bali jaribu kufikiria mtu anataka kukata/kukausha mti lakini anaanzia na majani; moja baada ya jingine, then matawi ilhali muda unakwenda na rasilimali nyingi na tofauti zinatumika.

    ReplyDelete
  21. minakaa UK daladala zetu hazina mikanda hiyo bongo sheria sijui imetoka wapi labda na UK watatuiga sio kila siku tuwaige wao teh!teh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...