CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Kwa: Wanachuo na Wafanyakazi Wote,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
UTARATIBU WA KUINGIA NA KUTOKA ENEO LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM 18 – 23 JANUARI 2009
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawaarifu wakazi wa Chuo Kikuu na wafanyakazi, wote kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitafunguliwa tarehe 19/01/2009.
Ili zoezi la kusaili wanafunzi waliotimiza masharti na kuruhusiwa kurudi
Chuo lifanyike kwa ufanisi na kwa usalama, uongozi wa Chuo umeweka
utaratibu maalumu wa kuingia na kutoka Chuoni hapa kutoka tarehe 18 mpaka
23 Januari 2009. Utaratibu huo ni kama ifuatavyo:
•Kuingia Chuo – Lango la Ubungo karibu ya Chuo cha Maji cha Rwegarulila tuu.
•Kutoka Chuo – Lango la Upande wa Chuo Kikuu cha Ardhi tuu.
•Milango mingine yote itafungwa na haitatumika kwa kuingia au kutoka, na
hii ni pamoja na:
oLango la kutoka Changanyikeni/ Msewe/ Makongo
oKupita Hall VI
oKupitia Savei.
•Njia nyingine zote ambazo sio rasmi zitadhibitiwa ipasavyo.
•Wale wote wanaotoka Changanyikeni, Jeshini, na Chuo cha Takwimu wanaombwa watumie njia ya Msewe na kuelekea Ubungo au Makongo kuelekea Mwenge.
•Wafanyakazi wa Chuo wanaombwa kutembea na vitambulisho vyao vya kazi, ili wavitumie kuingilia langoni. Kwa wafanyakazi wake/waume na watoto wakubwa wa wafanyakazi wasio na vitambulisho wanaombwa wawasiliane na Wakuu wa vitengo vya wafanyakazi husika ili wawapatie barua za utambulisho.
•Watoto wa shule za Sekondari na Msingi wanaruhusiwa kupita sehemu za Chuo wakiwa na sare za shule tu.
•Huduma za daladala zitaishia langoni. Kwa wanachuo na wafanyakazi,
kutakuwa na usafiri wa ndani ya Chuo kutoka lango la maji mpaka lango la
Chuo Kikuu cha Ardhi.
Chuo kinawaomba uvumilivu na radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea.
IMETOLEWA NA MENEJIMENTI
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Januari 16, 2009
Hiki Chuo au gereza! au Kituo cha kijeshi chenye mitambo ya Nyukilia. Fanyebni mamabo ya maendeleo na si kupoteza muda kwa urasimu wa akili finyu!
ReplyDeleteThis is crazy!,sometimei wonder a about the managment at UDSM, more than ten thousand students using the same gate!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHee...mna wazimu au?watu wenyewe mmesomeshwa bure halafu mnaleta nyodo...sasa kuna nini cha jabu huko yaaani maproffessor wote na madoctor hicho ndio mlichofikiria kufanya....tusiwaone mnagombea ubunge kumbe bure tu...hamna lolote ndio maaana mkiwa mawaziri utafikiri ni form 4 leavers...shame on u...think broadly and not like a chicken...hehehe...sikuwa nawajua kumbe ndivyo mlivyo duuuuuh kaaazi kweli kweli
ReplyDeleteHayo maamuzi yana nafuu, fungua link hii uone maamuzi yalivyo magumu kwa wanafunzi husika
ReplyDeletehttp://udsm.ac.tz/UDSM%20PROCEDURES%20FOR%20REGISTRATION%20OF%20READMITTED%20STUDENTS.pdf
Hapo ktk link hiyo utaweza soma masharti kwa wanafunzi jinsi ya kurudi (wale tu waliolipa hela), ni hatari hii.Hivi hii serikali ya CCM inafaa kuwa baba wa watanzania kweli au?Maana hana upendo, hawatakii mema watoto wake, hajali hatma ya wanatoto wake...inanipa wakati mgumu kupata mstakabali wa taifa la Tanzania miaka 20 ijayo.
MAKULILO Jr,
Damu zilipomwagika darasani watu walilaumu usalama mdogo. Usalama umewekwa, watu wanalalamika. Job true true
ReplyDeleteAIBU TUPU! AIBU TUPU!! maprofesa, maprofesa na usomi wenu wote mnarejesha CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM kwenye karne ya 19!!!! Nani atawakomboa watanzania?????? AIBU! AIBU! AIBU! AIBU! na kuna siku mtaueleza umma uliowapa elimu na madaraka hayo kama mlifanya maamuzi haya mkiwa mmevuta bangi au la!!!!
ReplyDeletekila chuo lazima kiwe na control ya watu wanaoingia na wanotoka sio jela wala nini but in future hiki chuo ina bidi kila mfanya kazi na mwanafunzi awe na id card na wafunge mageti auto yakufungua kwa id card hapo ndio itakuwa mwisho wa usumbufu watu hawawezi kupita chuoni tu kama mbuzi lazima ujulikane we nani na unafanya nini ndani ya chuo
ReplyDeletemichuzi upo biased.wewe ni mwoga.mdau uholanzi
ReplyDeletemy udsm!!!!!!
ReplyDeletesafi sana lazima tuheshimu jumuia ya "vyuo vikuu"
sasa izo contacts twazipataje ili tuingie tupate huduma zetu apo???kwa sie tusio staff apo na madenti
Mimi nasema alichofanya Mukandara na utawala wa chuo ni sawa. Na hao viongozi wa DArUSO hio kiburi wanayopewa na CHADEMA ndiyo inawaponza. Serikali na polisi msiwaonee huruma. Mtu akileta ffujo peleka FFU na wakoge maji ya kuwashawasha. Ingekuwa eNZI YA mWALIMU THUBUTU!!!......MTUPU11
ReplyDeleteHuu ni upuuzi wa karne! Ni uvivu wa kufikiri walionao ma Professor/doctors wa udsm coz of desas walizotumia kufika hapo. Prof Mukandala ulikuwa unasema Luhanga anatumia maguvu! ulikuwa unataka sifa tuu kumbe ulikuwa unataka hicho cheo. Luhanga alikaa hapo more than 15 yrs hatukuwahi kusikia huu upuuzi. Usione aibu nenda um consult akupe siri ya mafanikio yake. Naona sasa hiki chuo kinaanza kuwa ile sifa iliyofanya kiitwe Chuo cha Manzese!! Ndio maana walimu kibao wamekimbilia University of Dodoma coz of this upuuzi!
ReplyDeleteCCM ni mabingwa wa propoganda. Badala ya kushughulikia kiini cha tatizo wanaeneza propoganda eti wanafunzi wanachochewa na CHADEMA. Watanzania wengi wameishafumbuka macho, sidhani kama kuna watu wenye akili wanaozinunua hizo propoganda za enzi za usoshalisti!!! Yale yale ya Mugabe eti wapinzani wanachochewa na wazungu!!!
ReplyDeleteMukandara tuna wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri,sioni hekima ya ki-profesa ndani ya akili yako.sisi wengi ni wanafunzi wa chuo chako lakini we feel shame of you babaa.
ReplyDeleteMhhh jamani hayo masharti mbona yanatisha?? Je akina Misupu na wenzie hawajaelezwa kwamba watapataje habari pale wakati wanafunzi wanaripoti maana sijasikia wao wataingilia geti gani. Misupu kupitia uongozi wa waandishi wa habari nendeni mkaombe na ninyi mpangiwe geti na utaratibu wa kupata habari pale maana pia ni haki yenu kupata habari na kuzitoa kwa jamii ili ijue kinachoendelea hapo chuoni. Maana marti ni makali kiasi cha kwamba yanatisha.
ReplyDeleteMdau
SASA HII NI LEBANON!!! POSSIBLY NI BAGDADI
ReplyDeleteAtakayebahatika kufika Chuoni leo ni shahidi yangu, Mkandala na washirika wake nashindwa kuwa-define, ni wAoga ni jeuri au WAshindani. Kwa wale wasiojua vizuri mazingira ya UDSM, hapa ndani huwa kuna kituo kidogo cha polisi wanaofanya kazi bega kwa bega na Auxilialy polisi (yaani polisi walinzi wa ndani). Haikutosha kuwatumia hao katika zoezi lililoanza leo la udahili; likaletwa Jeshi la kutuliza fujo (FFU). Hapa linaonekana kupoteza maana kabsaaa!!! maana haiingii akilini kuleta jeshi hili mahali pasipo fujo, bahati mbaya zaidi hawakuja peke yao bali wamesindikizwa na Maji ya Upupu (WASHAWASHA). Mkandala hakutosheka bado, akalileta Jeshi la kujenga taaifa lisaidiane na Auxilialy polisi katika uangalizi wa wanafunzi kuingilia (MLANGO MMOJA pale Geti Maji). Na hawa sielewi kama wanaujuwa wajibu wao sawasawa! napata mashaka.
Cha KUkera zaidi ni kwamba vikosi hivi vyote vinatumia gharama Ama za Chuo au ya Taifa. Gharama ambayo kwa hesabu ndogo ingeweza walau kuwasomesha wanafunzi mia moja. Hivi Dr. Hosea (TAKUKURU) unaifanya kazi yako sawasawa! Kwanini kikosI chako kisije hapa Mlimani kuchunguza Ufisadi huu, Au unasubiri Msukumo wa Magazeti? Jamani kweli Watanzania tumefikia Hatua hii kuwekeana Ulinzi mkubwa na Kwa gharama kubwa kama vile kuna kiwanda cha kutengeneza Nyukilia. Wako wapi wanasiasa Wetu wanaokwea majukwaani kila kukicha na kuitangaza Tanzania kuwa Nchi ya Amani na Utulivu na hawaishii hapo wanaiita Nchi yenye kufuata misingi ya Uhuru na Demokrasia. Je huyu mwanafunzi anajengwa katika uzalendo upi??? wa Kidemokrasia! Wa kimabavu! Au Kinyonyaji! Kwakweli mimi sina majibu ya haraka ila watanzania Wenzangu mnisaidie kutoa Mitazamo.
Mbona sisi wazazi wenu tunagongwa virungu na ffu na wagambo kwenye maandamano,mikutano ya siasa na ya kidini.nyinyi wanafunzi huwa hamjishughulishi na mateso ya wazazi wenu tunayoyapata hapa kwetu tanzania kwenye machimbo na migodini,sasa jueni yafaa sasa msome kwa malengo ya kutukomboa nyie mjue hatuwezi kupata maendeleo kwenye dola inayokandamiza,jifunzeni elimu ya kuliknmboa taifa ili demokrasi ya watu wachache muing'owe mpande demokrasia ya wengi ili wananchi tuseme na vingozi wetu watujibu ipasavyo siyo kutishana, someni kwa malengo mshike madaraka muwanyooshe.mlalahoi.
ReplyDelete