MDAU NASIBU KANOLE WA ILALA FLATS, DAR, AKIWA NA NDUGU ZAKE BAADA YA KULA NONDOZZZ KATIKA CHUO CHA UHASIBU KURASINI, DAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hongera sana mdau kwa kumaliza chuo. Asante kwa picha nzuri ya familia

    ReplyDelete
  2. Brother Michuzi huyu jamaa (Mdau aliyekula nondozz) mbona anaonekana kachoka sana pamoja na wapambe wake. Hizo nondozz ndiyo zimemchosha kiasi kile?? Je hawa wapambe nao kilichowachosha ni nini? Jamani kweli wanahitaji concelling vinginevyo naona kama hali sio nzuri.
    Mdauzzzzz

    ReplyDelete
  3. Hii ndio NONDOZZZ ya kihalali haswa...sio zile za kununua ughaibuni na pesa za ufisadi!!!

    ReplyDelete
  4. Hongera ndugu yetu,
    Mdau,
    Gothenburg, Sweden

    ReplyDelete
  5. A WAY TO GO. Congaratulation

    ReplyDelete
  6. WANAFUNZI WAHUNI WANAOFANYA UUAJI WA RAIA WANAOISHI KARIBU NA BAADHI YA VYUO VIKUU TANZANIA!

    Mwenyekiti nimepokea kwa masikitiko uhuni wa wanafunzi wa Chuo KIkuu cha Waislamu MOrogoro kwa kuwapiga na dhahiri kuwataka kuwaua vijana wawili ambao hawana hatia,kwa kuwazushia ni wezi.Kama wengine miongoni wa wanafunzi,raia wa Morogoro na wapenda haki tumeshikitishwa sana na kitendo hiki.Na Tunalaani kwa nguvu zote.Inasikitisha sana kuona chuo kikuu cha Waislamu Morogoro kinasomesha wahuni.
    Kijana mmoja wao aliyepigwa yuko katika hali mahututi sana,na wanafunzi walioshikwa wameshindwa kuonyesha ushahidi wa huo wizi.
    Hii sio mara ya kwanza hapa Morogoro imewahi kutokea Chuo cha Mzumbe kwa wanafunzi kujichukulia sheria mkononi na kuwasingia na kuwaona vijana wote wanaoishi maeneo ya karibu na Chuo ni wezi.
    Daima sheria itachukua mkondo wake na hamna mtu aliye juu ya sheria,ni matarajia hao Wanafunzi waliofanya kitendo hicho cha kikatili watashughulikiwa kisawasa

    ReplyDelete
  7. Anony 2:10 AM umesema kweli wote waliozaidi ya umri wa miaka 12 wanaonekana kuchoka sana ktk picha hiyo.

    Watoto hawaelewi umasikini wa nchi na wa kifamilia lakini wakifika umri wa miaka 12 vichwa vyao huanza kujiuliza maswali na majibu huyajua kuwa ni umasikini, hivyo huanza kunyong'oyea kwa msongo wa mawazo.

    Na ndio maana vijana wote ktk hiyo picha wamechoka kwa kuwaza wafanye nini ilikujinasua na hali ya umasikini. Je wasome sana, Je wafanye kazi kwa bidii, Je wazamie meli maana hao ni watoto wa Ilala Kota~Flati
    Kweli Tanzania ni pagumu sana.

    ReplyDelete
  8. We anon wa January 03, 2009 6:46 AM

    inaonekana si msomi au hujawahi kukaa kampasi au wewe ni mdini. Walichofanya wanafunzi hao kiko vyuo vyoote na hata mitaani.

    Wanafunzi wa vyuo vikuu ni watu wanajijali ki mavazi na chakula. Vijana wengi jirani ya vyuo hasa kwenye vigenge vya madrafti nk. huwa wanavizia weak point ili waibe. Wanafunzi wa vyuo huibiwa simu, computa, nguo, hata fedha wakienda hata kujisaidia. Vijana wengine huenda kubaka mademu wasomi.

    Kibaya ni kujichukulia sheria mkononi na siyo eti wanawasingizia. Kwa nini mtu usome kwa hofu? eti vibaka wengi, tia kiberiti kwa sababu sheria/polisi wameshindwa!

    ReplyDelete
  9. huyo mjomba mweupe mweupe hapo katikati leo atakunywa sana dengelua na chimpumu, inavyoelekea leo kilabuni watamkoma huyo, wakimchekea wanaweza kuyakuta kayatinga hayo majoho ya mjomba aliokula nondo huku anayakata mandomboloyasolo utadhani nondo kaila yeye vile

    ReplyDelete
  10. Swali huyo mjomba wetu mweupe mweupe aliyetajwa na anony wa 04,2009 12:48AM mbona mie si muoni?? ama nikabadilishe tena mawani yangu??

    ReplyDelete
  11. Hata mimi nimejaribu kuosha matongo nimuone huyo mjomba mweupe mweupe lakini wapi. mweupe mweupe nimuonae kati ya wote ni dogo mwenye tishirt ya white, blue na red stripes.ngoja nivae miwani.

    ReplyDelete
  12. waislam mnakuja kwa kasi na nondozi ila huyu mwenzenu kachoka sana.kwenye huo mtanange hata biscut au juice kuwapoza watoto?najua uwezo wa kununua keki hana. hata kashata na kahawa mmeshindwa waislam kumchangia ndugu yenu?
    all in all mnajitahidi sana.michuzi weka tu nondoz ni motisha.
    Mdau Japan

    ReplyDelete
  13. Michuzi, please please, mimi ni mkristo ila sipendi ubaguzi wa dini wa aina yeyote ile. Huyu jamaa anayejiita ''Mdau Japan'' naona anachochea mgawanyiko wa kidini. Michuzi lengo lako ni kujenga jamii na sio kuigawanya, so comments kama hizo hazifai kuona mwanga wa jua. I have relatives and friends who are muslims so lets respect each other.
    Mdau,
    Gothenburg,
    Sweden.

    ReplyDelete
  14. jamani mweupe ni huyo mjomba alieokolea rangi ya lami yaani mweusiiiiiiii ti

    ReplyDelete
  15. sina nia ya kugombanisha jamii.mdau aliyekula nondoz ni muislam na hakuna hata kashata na kahawa, maana keki imemshinda.
    mdau-JAPAN

    ReplyDelete
  16. Mwanangu hapo amemiss Sox na Baker walikua wapi? Maana najua wanangu wenyewe mpo pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...