Na Mdau E. Shahidi, Morogoro
WATU watatu akiwemo mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)wamekufa katika matukio tofauti yaliyotokea katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwakaMkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Kamanda wa Polisi Mkoani humoThobias Andengenye aliitaja tukio la kwanza ambalo limetokea Januari 3, majira yasaa 9:30 usiku katika Kijiji cha Kididimo Wilaya ya Mvomero,ambapo uliokotwa mwili wa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Dkt.Rashid Kidunda(55).
Andengenye alisema taarifa ya kifo hicho ilitolewa kwenye kituo cha polisi Mkoanihumo na Mhadhiri Mwandamizi Dkt. Peter Mtakwa (54). Alisema taarifa hiyo ilieza kuwa kabla ya kifo hicho marehemu alianguka kwenyekorongo baada ya kuteleza kwenye barabara yenye mteremko mkali,wakati akiwa kwenyematembezi ya jioni.
Tukio lingine limetokea januari mosi, majira ya saa 4 usiku, ambapo mwanamke mmojaaliyetambulika kuwa ni Vumilia Banzi (26) Mkazi wa Modeco A alikufa baada ya kushika kamba ambayo ilikuwa imeshika kwenye nyaya za umeme na kufa wakati akiwa njiani kuelekea hospitali.
Alieleza kuwa taarifa juu ya kifo hicho zilitolewa na mfanyakazi wa kiwanda chaCanvas Mwinyi Baka (62). Katika tukio la tatu lililotokea januari 2, majira ya saa 10:00 jioni katika mtaa waMzinga Manispaa ya Morogoro,uliokotwa mwili wa Rajab Peleleza, ukiwa karibu nashamba lake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Masikini Dr. Kidunda, pole kwa wanafamilia na wasuaso wote hasa wa Department ya Animal Science and Production. Alikua mtaratibu sana na kicheko kikavu akiwa class. Some people walikua wanasema mkuu ni mtu wa bwax koz of some family problems, whatever make you to slide and fall down, Mungu akurehemu na akupe pumziko la milele. Utakumbukwa sana na wapendwa wako pamoja na wanafunzi wako.

    DASP student 2001-04 SUA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...