Ndugu wadau,
Kwanza kabisa natanguliza shukurani zangu za dhati kutokana na jitihada zenu za kutuhabarisha jamii yetu kila siku ziendavyo.Mimi, kama mtanzania wa kawaida, nasikitishwa sana na kukerwa na vitendo vya rushwa na ufisadi vilivyokithiri katika jamii yetu.
Imefika mahali inabidi kujiuliza kama kweli ni serikali pekee ndio yenye nguvu za kisheria mahakamani kupambana na rushwa na ufisadi.
Kwa mantiki hiyo naomba kufungua mjadala wa ushauri yakinifu wa kisheria kutoka kwa wanataaluma wa sheria kuhusu maswali yafuatayo:
1. Sheria inasema nini kuhusu mwananchi wa kawaida kuifungulia serikali yake kesi ya jinai au madai kutokana na serikali yake kuingia mikataba yenye utata na isiyo na maslahi kwa taifa.
2. Sheria inasema nini kuhusu serikali kuzifungulia kesi za jinai au kesi za madai makampuni ambayo imeingia nayo mikataba ambayo imebainka kuwa ina utata na haina maslahi kwa taifa.
3. Sheria inasema nini kuhusu kusitisha mikataba ambayo serikali imeingia na makampuni kama ikibainika kuna kasoro na mikataba hiyo haina faida kwa taifa.
4. Bunge kama chombo cha kidemokrasia ambacho hakifungamani na serikali wala dola kina nguvu ipi katika kutatua utata pindi ikibainika kuwa mikataba ambayo serikali imeingia na makampuni ina utata na haina maslahi kwa taifa.
5. Je sheria inaipa nguvu za kisheria ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, DPP, peke yake kuwa ndio yenye uwezo kufungua kesi za jinai ua kesi za madai kwa maslahi ya taifa inapobainika kuwa mikataba ambayo serikali imeingia na makampuni ina utata.
Natanguliza shukurani zangu za dhati kwa wachangiaji wote katika mjadala huu na nataraji mchango wenu wa mawazo utasaidia kutoa dira katika kupambana na rushwa na ufisadi katika jamii yetu.
Mdau,
Mkude Koba.


Wadau mnaofahamu sheria(Lawyers) changieni bac wengine tusome ,tuelimike.Ni moja ya kazi ya blog(Kuelimisha)
ReplyDeleteMdau, mimi nakushauri kwamba ukitaka kuingia kwenye hizi anga, ongea na wataalamu kama Jonh mashaka ili wakupe siri zao.
ReplyDeletekwa maana jamaa akiposti kitu tu, yaani wakishaona tu jonh mashaka, michuzi mwenyewe anafurahi kwa sababu hizo comments hadi machizi wanajifanya kucomment
, hadi na jini US blogger kaingia kwenye utaalamu wakati anauza ticketi kwenye ofisi ya utalii wakati hana elimu yoyote inayohusiana na uchumi, wabongo bwana, kweli bongo tambarare. US blogger ni muuza tiketi kwenye ofisi ya utalii eti
Mdau swali lako zuri sana sema unajua watu hawapendi mambo kama haya ya uwazi na ukweli wanapenda mambo ambayo wanaweza kubishana kama kijiweni. mimi sio mwanasheria lakini naweza kutoa maoni yangu jinsi ninavyo fikiri kwanini haya mambo ya rushwa na ufisadi yanaweza kukandamiza nchi yetu miaka nenda rudi.
ReplyDeletemajibu kwa maswali yako kwa maoni yangu,
1. Kwa kifupi mwananchi hana nguvu kwenye nchi yetu ya kuweza kuifungulia kesi serikali yetu kutokana na hukosefu wa demokrasia.kama mwananchi hawezi kuandamana je unafikiri ataweza kuifungulia kesi serikali?
Nguvu uliyopewa mwananchi ni ya kupiga kura kumchagua yule unayeona anafaa kuongoza nchi yako.hilo nalo ni gumu kwani choices ziko ndogo sana za viongozi nchini kwetu.
2.hata kama sheria inaruhusu serikali kuifungulia kesi za jinai kampuni ilioingia mikataba, sasa watamshitaki nani? hauoni kama hapo watajifunga na wao? ni kuulize swali dogo, je unaweza kumshitaki mtu ambaye umepiga nae dili la wizi? sasa serikali nivigumu kuyashitaki hayo makampuni ambayo hayana maslahi kwa taifa kwa vile wao wenyewe wali saini mikataba hio na walisoma kila kipengele cha mkataba lakini walifocus sana kwenye masalahi yao binafsi kuliko ya nchi na ndio maana unakuta leo hata makampuni mengine kwenye ufisadi wenye makampuni hayo wanafichwa kwa majina.
3.swali lako la tatu jibu ni kwamba serikali imekuwa nzito sana kusimamisha mikataba yote hiliotajwa kwa vile wao wenyewe ndio wahusika wakubwa na kusimamaisha hio mikataba ni lazima watajwe wahusika walio tuingiza kwenye mikataba mibovu.lakini hili swala naona litafikia mwisho tuwe na subira kidogo manake hasara tunayopata ni kubwa mno.
4.bunge ndio linatakiwa liwe na nguvu kubwa sana kwenye maswala haya lakini bunge letu limejaa wabunge wa chama kimoja kwahio ni vigumu mno kazi kufanyika. kesi ya serikali ikipelekwa bungeni ni sawa sawa na ule msemo " kesi ya nyani kapewa tumbili".
5.swali lako la tano ni kwamba kila chombo ambacho kina husiano na serikali hakina nguvu yoyote nchini kwetu kwa ajili ya wote ni kitu kimoja kama sio uoga.ndio maana DPP alishindwa kusema wamiliki wa kagoda wakawa wanatupiana mpira tu.
hayo ndio maoni kwa vile sio mwanasheria lakini ni majibu nimetoa kwa mtazamo wangu.naomba kaka michuzi hakuwekee na wadau wengine wachangie zaidi.wasalaam.
na pia nisameheni kama nimekosea kuandika kiswahili sehemu yoyote ndio lugha ninayo jua na ndio uwezo wangu umefikia hapo.
Mdau "cha mtu mavi"
Anon wa 3:46 Sasa mbona unamtisha mtu kauliza maswali tu!!Ingawa ni out of topic, ningependa kuongeza kwamba nyie ndio mnaoendeleza mjadala wa kina Mashaka na USBlogger na kuwapa u-celebrity fulani, Tujiunge pamoja na kuwaambia Mashaka na usblogger kwamba Watanzani hatutaki mshindi wa mjadala wao, tunahitaji wajiunge pamoja na kuchanga mawazo yao ili kuchangia direct kwa maendeleo ya watanzania, sio kutangazana DEBATES, NA KUTAFUTA VIWANJA KAMA BONGO RADIO NK. NA NYIE AKINA KIJIJI MNATANGAZA UREFA , BADALA YA KUWAOMBA HAWA NDUGU ZETU ,WENYE ELIMU NA UJUZI , KUJIUNGA KWA KUSAIDIA NCHI YETU KUJIKOMBOA KUTOKA KWENYE MAJANGA YANAYOKABILI JAMII ZETU.MNASEMA SIO WANASIASA LAKINI KILA MTU ANAVUTIA UPANDE WAKE ANAETOKA KAPA NI MTANZANIA, WEWE BLOGGER MWENYE LATEST DATAS , TUMIA UJUZI WAKO KWA KUIUZA VEMA SERIKALI YETU NA KUWAELIMISHA WANANCH YA KWAMBA BALI YA UGONJWA MKUBWA WA UFISADI ULIYOIKUMBA NCHI YETU NDANI NA NJE YA SERIKA, KWAMBA KUNA WATUMISHI WA SERIKALI WANAOJITAHIDI KUFANYA KAZI KWA MANUFAA YA WANANCHI, KWELI MAENDELEO NI MACHACHE, LAKINI YAPO. NA NDIO HAPO MNAPATA HIZO STATISTIC MNAZOTOA HAPA UWANJANI ,MASHAKA YOU ARE HUMBLE !LAKINI MARA UNAPANDA JAZBA NA KUTUMIA MANENO MAKALI KAMA WEAPONS NK AS IF UPO VITANI ,UKIWA NA LENGO LA KUELIMISHA BASI WACHA MLANGO WAZI WATU WAKOSOE NA KUCHANGIA KWANI WENGI WETU TUNAKUSAPOTI.BADALA YA KUZOMEANA NA KUSHINDANA, MASWALI HAYO KUTOKA KWA MDAO, TUWE POSITIVE KWA WENYE UWEZO WA KUYAJIBU KWA NIA YA KUELIMISHANA, NA MH "CHA MTU MAVI" NIMEFURAHISWA NA MAJIBU YAKO HASA UKISISITIZA NI MAONI YAKO BINAFSI, LAKINI UNGEMALIZIA KWA KUTOA ANGALAU MCHANGO WA SOLUTION. SASA MBONA BADO TUNATAFUTA UTATUZI NA BAADA YA MAJIBU YANAYOELEZA SABABU ZINAZOSABABISHA HAYA MATATIZO HAKUNA ANGALAU MCHANGO WA UTATUZI!!! TULIKUWA HATUJUI? SASA TUNAJUWA!!,
ReplyDeleteWADAU WHATS NEXT????
MDAU NYUTRO
Kwa kuongeza katika mjadala huu swali lingine la sita.
ReplyDeleteSHERIA YA UHUJUMU UCHUMI INASEMA NINI KIHUSIANA NA SERIKALI KUINGIA MIKATABA MIKATABA AMBAYO HAINA MASLAHI KWA TAIFA.
Mdau.
Mkude Koba.
sheria za nchi nyingi hazifatwi,,,
ReplyDeletefull stop